Josep Maria Bartomeu ajiuzulu

Rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu amejiuzulu kutokana na shinikizo kubwa, lakini amesema anaunga mkono pendekezo la klabu hiyo kujiunga na ligi mpya ya Ulaya inayoitwa European Super League.

Mashabiki walikuwa wakijaribu kumwondoa Bartomeu, ambaye alikua rais tangu 2014 na baadae kukosana na Lionel Messi.