Sarafu ya miaka ya 1066 yauzwa katika mnada

Sarafu (peni) ya kipekee ya mfalme Harold wa pili ambalo linakisiwa kuwa la mwaka wa 1066 iliyopatikana na kijana mmoja sasa imeuzwa kwenye mnada kwa pauni elfu 4,000 .

Reece Pickering, kutoka eneo la 'Great Yarmouth' Uingereza alipata sarafu hiyo eneo la Norfolk, mwezi wa Agosti alipokuwa anaokota vyuma na baba yake.

Tupe maoni yako bbcswahili.