Virusi vya corona "The Rock" asema familia yake ilipata Covid-19

Muigizaji maarufu Dwayne "the Rock" Johnson anasema kuwa yeye na familia yake yote walipata ugonjwa wa Covid-19. Mwanamieleka huyo wa zamani ambaye pia ni muigizaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani ameelezea kuwa walishangaa kupata virusi hivyo licha ya kuchukua tahadhari. The Rock amepata umaarufu kwa filamu hii ya Moana.