Donny van de Beek: Manchester United kulipa pauni milioni 40

Manchester United inakaribia kumsajili kiungo wa Ajax, Donny van de Beek baada ya vilabu hivyo viwili kukubaliana ada ya pauni milioni 40. Meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer anasemekana kumpenda sana mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi aliye na miaka 23.