Kwanini programu ya video ya Tik Tok inapata upinzani Marekani?

Rais Trump amesaini agizo la ikushughulikia kile alichokiita tishio linalosababishwa na programu maarufu, inayomilikiwa na China, ya TikTok. Marufuku ya shughuli za kampuni mwenza ya, ByteDance, yataanza baada ya siku arobaini na tano. Rais Trump amesema imebidi achukue hatua kali za kulinda usalama wa kitaifa wa Marekani.