Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tamasha la "Together At Home" lafana sana Marekani
Zaidi ya nyota mia moja wa muziki wameshiriki katika tamasha la Together At Home nchini Marekani. Lady Gaga alipanga tamasha hilo kwenye mitandao ya kijamii ili kuwasherehekea wahudumu wa afya walio msitari wa mbele kupamabana na virusi vya corona. Baadhi ya matukio hayo yalionyeshwa na BBC One. Miongoni mwa waliotumbuiza ni Taylor Swift aliyeimba wimbo wa "Soon You’ll Get Better".