Je, Wabunge wa Kenya watakubali kukatwa mishahara yao?

Wabunge nchini Kenya wanatarajiwa kuonekana kufuata mfano wa Rais Uhuru Kenyatta kukubali kupunguzwa kwa mshahara wake kwa muda mfupi kuchangia katika kushuhulikia maambukizi ya virusi vya corona.

Wabunge hao ni miongoni mwa wabunge wanaolipwa zaidi barani Afrika.

Rais Kenyatta alitangaza Jumatano kwamba yeye na makamu wake watapunguziwa asilimia 80% katika mshahara wao.

Alihimiza hatua hiyo ichukuliwe na viongozi wengine serikalini. Unadhani wabunge nchini Kenya watafuata mfano wa Rais Kenyatta?