Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Usambazaji wa mipira ya kondomu wasimamishwa Utah
Gavana wa jimbo la Utah huko Marekani Gary Herbert amesitisha mpango wa kugawa bure Kondomu elfu mia moja kutokana na ujumbe tata ulioandikwa kwenye vifungashio vya kondomu hizo. Ameomba radhi kwa matumizi ya lugha isiyofa – lakini akasisitiza kuwa kampeni hiyo itaendelea hilo litakaporekebishwa kwani kampeni hiyo ni yenye lengo la kuzuia uenezaji wa virusi vya ukimwi. Je, juhudi za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Ukimwi zinafanyika vipi katika eneo lako? Wasiliana nasi kwenye ukurasa wa Facebook, BBCSwahili