Raia wa Congo nchini Israel: 'Tumekimbia vita na kujikuta katika vita vikubwa zaidi'

Maelezo ya video, Raia wa Congo nchini Israel: "Tumekimbia vita na kujikuta katika vita vikubwa zaidi"
Raia wa Congo nchini Israel: 'Tumekimbia vita na kujikuta katika vita vikubwa zaidi'

Mtangazaji wa BBC Focus on Africa, Waihiga Mwaura, alizungumza na Tonton Amisi Chalupa, raia wa Congo ambaye amekuwa akiishi Israel kwa miaka tisa.

Anaishi Bat Yam, jiji lililo karibu kilomita 10 kutoka mji mkuu wa Israeli, Tel Aviv, ambalo limekuwa likilengwa na makombora mabaya ya Iran katika wiki iliyopita.