Ney wa Mitego: Wakati mwingine sipewi vibali hata nikiandaa matamasha yangu
Ney wa Mitego: Wakati mwingine sipewi vibali hata nikiandaa matamasha yangu
Mashabiki wake hupenda kumuita 'rais wa kitaa', Emmanuel Elibariki, maarufu Nay wa Mitego ni miongoni mwa wasanii wa muziki nchini Tanzania ambaye tungo zake mara kadhaa zimemtia matatani kutokana na mamlaka za udhibiti wa maudhui kutoridhishwa na tungo zake.
Mwandishi wa BBC Veronica Mapunda amekutana na msanii huyo na kuzungumza naye masuala mbalimbali ikiwemo kwanini hutunga mashairi yanayomuweka matatani mara kwa mara?




