Afcon 2023: Kichapo cha Morocco kwa Tanzania kitawafanya kubeba ubingwa?

Hh

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Romain Saiss akishangilia na wachezaji wenzake baada ya goli la kwanza dhidi ya Tanzania

Morocco imeanza kampeni zake katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 kwa ushindi mnono dhidi ya Tanzania, mabao 3-0 katika mechi za makundi. Simba wa Atlas walipata bao la kuongoza dakika ya 30 ya mchezo likifungwa na nahodha Romain Saiss baada ya kipa wa Tanzania kutema mpira wa adhabu uliopigwa na Hakim Ziyech. Timu ya Morocco ilitumia fursa ya upungufu wa wachezaji wa Tanzania baada ya mchezaji wake kutolewa kwa kadi nyekundu Novatos Mirushi, dakika 20 kabla ya mechi kumalizika, kuongeza bado la pili kupitia Azzedine Onahi. Youssef Al-Nusairi alihitimisha mabao hayo kwa kufunga la tatu kupitia mpira wa krosi kutoka kwa Ashraf Hakimi.

Morocco ndio itabeba ubingwa?

Morocco ilishinda katika Kombe la Dunia dhidi ya timu kubwa kama vile Ubelgiji, Uhispania na Ureno, wakisaidiwa na mashambulizi yao ya kushtukiza. Ilifanikiwa kutwaa taji lake la pili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1976, na inachukuliwa kuwa miongoni mwa timu zenye nafasi kutwaa ubingwa katika michuano inayofanyika kwa sasa nchini Ivory Coast baada ya kuingia katika nusu fainali ya kihistoria katika Kombe la Dunia 2022. Simba wa Atlas walitawala mechi dhidi ya Tanzania katika mechi hiyo ya ufunguzi ya Kundi F kwenye Uwanja wa Laurent Poco katika jiji la San Pedro nchini Ivory Coast, na kipa wa timu ya taifa ya Morocco, Yacine Bounou, hakufanyiwa mashambulizi makubwa.

Tanzania bila historia ya ushindi

Tanzania haikupata ushindi katika mechi tatu ilizocheza katika mashindano yaliyopita ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na bado inasubiri kupata ushindi wake wa kwanza, lakini mechi yake dhidi ya Morocco ilizidi kuwa ngumu baada ya Mirushi kutolewa. Miroshi alipokea kadi ya njano ya kwanza baada ya kumchezea rafu Onahi nje ya eneo la hatari katika kipindi cha kwanza, kisha akapokea kadi ya pili baada ya rafu nyingine kwa Onahi yuleyule. Ndani ya kundi hilo, Congo ilitoka sare na Zambia bao 1-1, huku kila timu ikipata pointi moja na Morocco inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi tatu. Mechi za mzunguko wa pili wa kundi hilo zitafanyika Jumapili ijayo.

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah