Ifahamu safari hatari zaidi inayofanywa na Mabilionea kutalii anga za mbali

f

Chanzo cha picha, SPACEX

Maelezo ya picha, SpaceX kujaribu vazi jipya la mpya EVA
Muda wa kusoma: Dakika 5

Chombo cha anga za juu cha kibinafsi Polaris Dawn kiliondoka duniani Jumanne hii kutoka Florida kwa usaidizi wa roketi ya SpaceX Falcon 9.

Miongoni mwa wasafiri katika chombo hiki ni bilionea Jared Isaacman, mwanzilishi mwenza wa kampuni ya malipo, Shift4, ambaye anatarajia kufanya safari ya kwanza ya kibinafsi inayofadhiliwa katika siku zijazo.

Pia ndani ya chombo hicho yumo Scott "Kidd" Poteet, rubani mstaafu wa Jeshi la Anga la Marekani, na wahandisi wawili wa SpaceX, Anna Menon na Sarah Gillis.

Chombo hicho cha anga za juu, kiitwacho Resilience, kitaingia katika mzunguko wa kilomita 1,400 juu ya Dunia. Hakuna binadamu aliyesafiri hadi sasa katika eneo hilo tangu mpango wa Apollo wa NASA ulipomalizika miaka ya 1970.

Wanaanga hao watapita katika eneo la anga za juu linalojulikana kama Van Allen Belt, lenye viwango vya juu vya mionzi, lakini wafanyakazi watalindwa na chombo hicho chenye vifaa vyao vya kisasa vya anga za juu.

Kupita kwenye ukanda huo mara chache kutakuwa ni sawa na miezi na kupigwa na mionzi kwa miezi mitatu uzoefu walionao wanaanga kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga, ambacho kiko ndani ya mipaka inayokubalika.

Lengo la safari ni kujifunza madhara ya muda mfupi lakini salama ya mionzi iliyonayo kwa mwili wa binadamu.

Katika siku ya pili ya safari yao ya anga za juu wanaanga hao watafanya kufanya majaribio hadi 40, ikiwa ni pamoja na mawasiliano kati ya chombo cha anga za mbali. cha Dragon na nyota ya setilaiti Space X.

Unaweza pia kusoma:
f

Chanzo cha picha, SpaceX

Maelezo ya picha, Ujumbe huo ulifanikiwa kuondoka katika jimbo la Florida.

Itavunja rekodi

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ikiwa mambo yote yatakwenda kama ilivyopangwa, siku ya tatu ya safari yao, Isaacman na Sarah Gillis wanatarajiwa kujaribu safari ya kwanza ya kibinafsi inayofadhiliwa, ambayo itadumu masaa mawili.

Hii itafanyika wakati watakapokuwa kilomita 700 (maili 430) kwenye mzunguko.

Wanaanga watajaribu mavazi mapya ya anga au suti za (EVA), ambazo, kama jina linavyoeleza, zimeboreshwa kulingana na shughuli za ndani za Space X (IVA) ili kufanya kazi nje ya chombo cha anga, wanaanga hao watakapohitaji kufanya shughuli hizo.

Mavazi yao yamebadilishwa kwa ajili ya kuhimili ombwe la angani. Matanki ya ziada ya nitrojeni na oksijeni yamewekwa ndani ya chombo hicho na wanaanga wanne wanavaa mavazi mapya ya EVA, ingawa ni wawili tu watakaotoka nje ya chombo hicho kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Kwa hivyo ujumbe huo wa wanaanga utavunja rekodi ya idadi kubwa ya watu kuwahi kufika katika eneo la ombwe la anga za juu kwa wakati mmoja.

Wanaanga hao watafanya vipimo juu ya athari za ugonjwa wa decompression, pamoja na hali ya wanaanga kushindwa kuona vizuri, hali ambayo wakati mwingine huipata wanapokuwa katika anga za juu, inayoitwa ugonjwa wa neuro-ocular syndrome.

Vipimo vya athari za mionzi ya Van Allen Belt vinakusudiwa kuweka msingi wa safari za anga za juu zaidi katika sekta ya kibinafsi ya anga za juu kwa siku zijazo, labda kwa kwa safari za Mwezini au katika sayari ya Mars.

f

Chanzo cha picha, SPACEX

Vazi Jipya

Vazi la EVA linajumuisha kofia ambayo hutoa habari juu ya suti wakati iponavaliwa. Vazi la EVA ni zuri na rahisi kutosha kuvaliwa wakati wa kuondoka na kutua, duniani kwani kuondoa hitaji la vazi jingine tofauti la IVA.

Katika mahojiano yaliyofanyika wakati wa mafunzo kwa ajili ya safari ya anga za juu, Gillis alielezea kuwa vazi hili ni sehemu muhimu ya mipango ya Space X ya kupeleka watu kwenye sayari nyingine.

"Hadi sasa, ni safari za kitaifa tu ambazo zimeweza kufanya safari ya anga za juu. Space X ina matarajio makubwa ya kufika katika sayari ya Mars na kufanya maisha kuwa ya aina nyingi.

Ili kufanikisha hili, tunapaswa kuanzia mahali fulani. Na hatua ya kwanza ni kujaribu mwingiliano wa kwanza na nafasi ya EVA ili tuweze kuboresha zaidi nafasi na miundo ya suti ya baadaye."

Isaacman alirudia hisia hii: "Nafasi X inajua inahitaji uwezo wa EVA ikiwa inataka kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya siku moja inayojitokeza sayari nyingine."

Lengo ni kutengeneza vazi la anga za juu si kuwa vazi tu , l bali ni kihakikisha vazi moja linakidhi mahitaji mbali mbali ya shughuli zinazofanyika angani, ili kupungua gharama ya kutengeneza mavazi mbali mbali kwa ajili ya shughuli mbali mbali zinazotarajiwa kufanyika angani

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ujumbe wa Polaris Dawn utafikia kiwango cha juu zaidi juu ya Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

"Hatari kubwa"

"Kunahisia kuwa kuna hatari nyingi zinazohusika," Dkt Adam Baker, mtaalamu wa roketi katika Chuo Kikuu cha Cranfield nchini Uingereza, aliiambia BBC.

"Wamejiwekea malengo mengi ya kutamani na matamanio mengi huku chombo chenyewe kikiwa ni kidogo . Kwa upande mwingine, wametumia masaa elfu kadhaa kuiga kwenye eneo linalolengwa. Kwa hivyo wanafanya kila wawezalo kupunguza hatari," mtaalamu huyo alisema.

Ikiwa safari hiyo itafanikiwa, baadhi ya wachambuzi wanaamini kuwa itachochea kufanyika kwa safari nyingine za sekta binafsi zenye gharama ya chini ambapo watu wengi wataweza kusafirishwa zaidi kuliko mashirika ya anga za juu ya serikali ambayo yamewahi kufanya hivyo.

Lakini Beker ana mawazo tofauti: "Mpaka sasa sekta binafsi imetumia fedha nyingi, imefanya matangazo mengi, lakini idadi ya watu ambao wamesafiri kwenda anga za juu na kurudi (kwenye misheni hizi) imekuwa chini ya 100."

"Safari ya anga za juu ni ngumu, ghali na hatari, kwa hivyo kutarajia kuona idadi kubwa ya raia matajiri wanaoruka angani wakati wowote hivi karibuni, au kuwa miongoni mwao, haiwezekani."

f

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kutoka kushoto kwenda kulia: Anna Menon, Scott Poteet, Jared Isaacman na Sarah Gilli.

Suala la matajiri

Kwa wengine, wazo la mabilionea kulipa kwenda anga za juu ni la kusikitisha, na linaibua maswali mengi

Simeon Barber, mwanasayansi wa anga za juu katika Chuo Kikuu Huria nchini Uingereza ambaye anatengeneza vyombo vya kisayansi kwa ajili ya chombo cha anga za juu katika miradi inayofadhiliwa na serikali pekee, anasema sio suala la ubatili.

"Isaacman ni mwanaanga mwenye uzoefu zaidi - yeye ndiye pekee ambaye amekuwa angani hapo awali, kwenye safari nyingine inayofadhiliwa na SpaceX, ambapo pia aliwahi kuwa kamanda. Katika muktadha wa ujumbe huo, yeye ni chaguo la asili," aliiambia BBC News.

"Kwa upana zaidi, faida kutokana na uuzaji wa tiketi hii ya daraja la nyota itabaki duniani: pesa zitanunua vifaa na huduma, kulipa mishahara, na kwa upande wake kuzalisha kodi. Bila kutaja fedha za uhisani ambazo ujumbe utaongeza."

Anasema wengi katika sekta ya anga za juu wanaamini kuwa ushiriki wa watu matajiri ni jambo jema .

"Kama wanataka kujitosa kwenye mtandao, na siku moja kwenda mwezini au hata Mars, hiyo itatengeneza fursa za kisayansi. Na sababu tofauti zaidi za kuchunguza anga za juu, mpango huo utakuwa na nguvu zaidi."

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Yusuf Jumah