Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Gabriel Jesus hana mpango wa kuhamia Napoli

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester City wamemtambua Manu Kone wa Roma kama mchezaji wanayeweza kumsajili; kiungo huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 pia amehusishwa na wapinzani wao, Manchester United, katika dirisha hili la usajili la majira ya joto. (Mail)

Gabriel Jesus wa Arsenal hana mpango wa kuhamia Napoli licha ya klabu hiyo kuonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Brazil, mwenye umri wa miaka 29. (Mirror)

Aston Villa inataka kumsajili beki wa Chelsea, Tosin Adarabioyo (28), ili kuziba pengo la Ezri Konsa, baada ya Arsenal kuonyesha nia ya kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports)

Benfica pia wameanza mazungumzo na Chelsea kuhusu uwezekano wa kumsajili Adarabioyo. (Sun)

Barcelona wanafuatilia mazungumzo ya mkataba wa Harry Kane na Bayern Munich, huku mshambuliaji huyo wa Uingereza, aliye umri wa miaka 33, akiwa katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa. (Mail)

Sunderland inaweza kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kulipa kipengele cha kuachiliwa cha euro milioni 60 ili kumsajili winga wa Sporting na Msumbiji, Geny Catamo,25. (Teamtalk)

Everton inavutiwa na winga wa klabu ya Como na Senegal, Assane Diao, aliye na umri wa miaka 20, ambaye anaweza kugharimu kati ya pauni milioni 50 na milioni 60. (Teamtalk)

Tottenham iko katika mazungumzo ya kuwasajili wachezaji wawili wa Manchester City: winga wa Brazil, Savinho (22), na mshambuliaji wa Misri, Omar Marmoush (27). (Athletic - usajili unahitajika)

Juventus imeungana na Napoli katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Joshua Zirkzee (25), lakini klabu zote mbili zitalazimika kuwauza wachezaji kwanza kabla ya kufanya jaribio la kumsajili mchezaji huyo raia wa Uholanzi. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Hull City wako karibu kufikia makubaliano na Real Betis kuhusu winga wa Kihispania mwenye umri wa miaka 20, Pablo Garcia. (Sport - kwa Kihispania)

Hull, Ipswich Town na Al-Ittihad wanajitahidi kumsajili kiungo wa Morocco, Azzedine Ounahi (26), kutoka Girona. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Arsenal wanafanyia kazi mipango ya kuwasajili winga wa Gibraltar, James Scanlon (19), na beki wa Kiingereza, Habeeb Ogunneye (20), kutoka Manchester United. (Telegraph - usajili unahitaji )

Barcelona imesitisha kwa muda mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Julian Alvarez (26), kutoka Atletico Madrid. (ESPN)

Atletico Madrid inalenga kuipiku Manchester United katika usajili wa beki wa Uhispania, Jorge Salinas (19), kutoka Racing Santander. (Teamtalk)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi