Karim Mandonga: 'Katika watoto wangu wote huyu Shariff ndiye atakayekuwa mtu kazi'

Maelezo ya video, Karim Mandonga: 'Katika watoto wangu wote huyu Shariff ndiye atakayekuwa mtu kazi'
Karim Mandonga: 'Katika watoto wangu wote huyu Shariff ndiye atakayekuwa mtu kazi'
Mandonga

Bondia wa Kitanzania Karim Khalid Saidi maarufu kama Mandonga Mtu Kazi, amefahamika kwa kupigwa nchini kwao Tanzania na kumpiga bondia wa nchi jirani ya Kenya kwa Technical Knock out hivyo kutoa funzo kubwa la jinsi ya kutoa hamasa katika mchezo wa ngumi uliokosa hamasa miaka ya hivi karibuni.

Amekuwa akishiriki mapambano mfululizo bila ya kupumzika vya kutosha jambo lililoibua taharuki kwa wanafamilia na wataalamu wa afya.

Mwandishi wa BBC @frankmavura amemtembelea @k_mandonga nyumbani kwake Morogoro nchini Tanzania.