Tanzania yachukua hatua kupambana na mitandao ya ngono
Tanzania yachukua hatua kupambana na mitandao ya ngono
Tanzania inatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kupambana na mitandao ya ngono.
Tanzania inasema picha hizo ni kinyume cha maadili ya nchi hiyo, hivyo inatengeneza mfumo utakaoweza kuchuja na kuzuia utumiaji ama kupakua au kurambaza katika mitandao hiyo.
Nchi kadhaa duniani pia zimechukua hatua za udhibiti kutokana na sababu mbalimbali.
Mamlaka zimetaka watu wanaotumiwa picha za ngono kuzifuta mara moja.
Waziri wa Habari nchini Tanzania amezungumza na mwandishi wa BBC Salim Kikeke.





