Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Tanzania 2020: Lissu asimulia jinsi alivyokamatwa
Polisi nchini Tanzania wamewaachia huru viongozi wote wa upinzani ambao walikuwa wamewakamata kwa mashtaka ya kupanga maandamano yasiokuwa halali .
Kiongozi wa chama cha upinzani Tundu Lissu amezungumzia matukio ya kukamatwa kwake huku akitoa wito kwa mbunge mmoja na madiwani 15 wa chama cha chadema walioshinda katika Uchaguzi mkuu uliopita kutoshiriki katika shughuli za kuapishwa.