Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kitendo cha Cristiano Ronaldo chaisababishia kampuni ya vinywaji hasara ya mabilioni
Kwanza ilikuwa Cristiano Ronaldo na sasa ni Paul Pogba.
Siku moja tu baada ya Ronaldo kugonga vichwa vya habari kwa kuondoa chupa mbili za Coca-Cola kwenye mkutano wa waandishi wa habari na kisha kuwahimiza watu kunywa "agua!" (maji) badala yake, Pogba ameenda naye pia ametamba mitandaoni baada kuondoa chupa ya bia ya Heineken.
Mfaransa huyo wa miaka 28, ambaye ni Mwislamu hakutoa maoni juu ya jambo hilo - kwa busara alihamisha bia isiyo na kileo na kuiweka chini ya meza wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi.
Tukio hilo lilijiri baada ya Pogba kushiriki katika mechi ya Ufaransa waliopata ushindi katika Kundi F kwa kuifunga Ujerumani bao moja kwa nunge katika mechi za kombe la Euro na kupewa tuzo ya Heineken ya 'nyota wa mechi'
Inafahamika Uefa haioni vitendo vya wachezaji hao kama suala kubwa , licha ya visa vinavyohusisha wadhamini wao wawili wakubwa .
Thamani ya soko ya kampuni kubwa ya vinywaji ya Marekani Coca cola ilipoteza karibu $ 4bn baada ya kitedo cha Ronaldo. Kampuni hiyo, ambayo ina thamani, karibu $ 240bn, ilipepezea chini athari za kitendo hicho na Ronaldo
"Kila mtu ana haki ya kupenda kinywani kinachomfaa’ ilisema Coca-Cola katika taarifa fupi, na kuongeza kuwa kila mtu ana "ladha na mahitaji" tofauti.