Carlo Ancelotti atua Everton

aNCELOTTI

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 1

Ni rasmi - Everton wamemteua Carlo Ancelotti kuwa kocha wao mpya.

Ancelotti anatua Everton siku chache baada ya kutimuliwa katika klabu ya Napoli ya nchini kwao Italia.

Anachukua nafasi iliyoachwa wazi katika uga wa Goodison Park na kocha Marco Silva ambaye alitimuliwa Disemba 6.

Ancellotti ni moja ya makocha wenye mafanikio makubwa barani Ulaya, amenyakua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya (Champions League) mara tatu.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Anarejea England miaka nane na nusu toka alipotimuliwa na klabu ya Chelsea.

"Kuna maono ya wazi kabisa kutoka kwa mmiliki kuwa anataka kuleta mafanikio klabuni," amesema Ancelotti.

Everton wamemtangaza Ancelotti saa chache kabla ya mchezo wao dhidi ya Arsenal ambao Ijumaa walimteua Mikel Arteta kuwa kocha wao mpya.

Mechi yake ya kwanza kuiongoza timu hiyo itakuwa dhidi ya Burnley Disemba 26.

"Hii ni klabu nzuri na yenye utajiri wa historia na mashabiki wenye mapenzi ya juu," ameeleza kocha huyo wa zamani wa AC Milan, Real Madrid, Bayern Munich na Paris St-Germain.

"Nina furaha isiyo na kifani kwa kupata nafasi ya kufanya kazi hapa na kuffanya ndoto zetu zitimie."

Katika miaka yake 24 ya ukocha, Ancelotti mwenye miaka 60 ameshinda mataji 15, na ni moja kati ya makocha watatu tu ambao wameshinda Champions League mara tau sawa na kocha nguli wa zamani wa klabu ya Liverpool Bob Paisley na kocha wa sasa wa Real Madrid Zinedine Zidane.