Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hassan Mwakinyo: Bondia Mtanzania asema maisha magumu yamechangia ushindi wake
Bondia Hassan Mwakinyo aliwashangaza wengi katika ndondi, baada ya kumchapa mpinzani wake Sam Eggington wa Uingereza katika pambano lililochezewa Birmingham.
Mwakinyo, anayetokea Tanga, alicheza pambano la mwisho la utangulizi lililokutanisha bondia maarufu wa Uingereza Amir Khan dhidi ya Samuel Vargas.
Siri yake ya kufanikiwa ilikuwa nini?
Nassor Rashid, meneja wa bondia huyo, anasema alikuwa na matumaini asilimia 95 kwamba angefanikiwa.
Promota huyo anasema video ya ukalimani wake ambayo imesambaa sana mitandao ya kijamii imesaidia sana kumvumisha na kwamba ndoto ya kupambana na kelly Brook na Amir Khan bado ipo, na baadaye Floyd Mayweather.