Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mafanikio ya mwanariadha Beatrice Chepkoech hutokana na nini?
Beatrice Chepkoech anasema tofauti na miongoni mwa wanariadha wenzake wa Kenya ambao kwa siku za hivi karibuni wamepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu, yeye anategemea nguvu zake za kuzaliwa, vyakula na mazoezi kufanya vyema.
Chepkoech mwezi jana aliweka rekodi mpya ya dunia mbio za mita elfu tatu kuruka vizuizi na maji, dakika nane sekunde 44, nukta tatu-mbili, na kuvunja ya zamani iliyokua inashikiliwa na mzaliwa wa Kenya anayekimbilia Bahrain kwa sasa, Ruth Jebet, ambaye anashukiwa kutumia dawa za kusisimua misuli......John Nene amezungumza na Chepkoech huko Kericho eneo la bonde la ufa...