Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Wachezaji waliosajiliwa dakika za mwisho England

Kandarasi zote mpya kabla ya dakika ya mwisho ya dirisha la uhamisho England

Moja kwa moja

  1. Tottenham yamsaini Giovani Lo Celso

    Tottenham imethibitisha kumsajili kiungo wa kati Giovani Lo Celso kutoka klabu ya Uhispania ya Real Betis kwa mkopo wa muda mrefu kukiwa na uwezekano wa kumsaini kwa mkataba wa kudumu.

  2. Habari za hivi punde, Mbwana Samatta akosa kujiunga na Klabu ya England

    Mshambuliaji wa klabu ya Genk nchini Ubelgiji na nahodha wa timu ya taifa Stars ya Tanzania Mbwana Samatta amekosa kujiunga na klabu ya England baada ya dirisha la uhamisho la taifa hilo kufungwa rasmi.

    Samatta ambaye kulingana na gazeti la The Sun la England ana thamani ya pauni milioni 12 bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake na mabingwa wa Ubelgiji KRC Genk pia amezivutia klabu za Roma ya Italia na Lyon ya Ufaransa.

    Klabu nyengine za England ambazo zinamuwania Samatta ni Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley.

  3. Habari za hivi punde, Caroll arudi Newcastle

    Mshambuliaji wa zamani wa England Andy Carroll amerudi katika klabu yake ya utotoni miaka minane baada ya kuondoka.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 , aliachiliwa na kuwa mchezaji huru na klabu ya West Ham msimu huu kufuatia kandarasi ya miaka sita iliokumbwa na majereha.

    Ametia kandarasi ya mwaka mmoja.

  4. Dirisha la uhamisho lafungwa

    Dirisha la uhamisho hatimaye limefungwa .

    Hatahivyo haimaanishi kwamba hakutakua na matangazo yoyote.

    Mikataba kadhaa huenda imeidhinishwa na tutaisikia saa moja lijalo.

    Mashabiki wa Arsenal wanasubiri kwa hamu habari kuhusu uhamisho wa David Luiz.

  5. Habari za hivi punde, Kieran Tierney ajiunga rasmi na Arsenal

    Sasa ni rasmi beki wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney atajiunga na Arsenal

  6. Andy Caroll kurudi Newcastle?

  7. Grady Diangana aelekea West Bromwich Albion

  8. Eddie Nketia ajiunga na Leeds kwa mkopo

  9. Habari za hivi punde, Romelu Lukaku ajiunga na Inter Milan

    Inter Milan wametuma ujumbe wa twitter ulio na kanda ya video ya Lukaku akiwa amevalia jezi ya timu hiyo akisema ''Inter sio ya kila mtu ndio sababu niko hapa''

    Romelu Lukaku ametia kandarasi ya hadi tarehe 30 Juni 2024.

    Lukaku sasa atakuwa mchezaji wa tatu aliye ghali zaidi kusajiliwa na ligi ya Serie A kufuatia uhamisho huo wa dau la £74m move to Inter Milan.

    Wachezaji wengine waliosajiliwa kwa dau la juu zaidi ni Cristiano Ronaldo (£99.2m) aliyejiunga na Juventus na Gonzalo Higuain (£75.3m) .

  10. Watford wametangaza kumsaini winga Ismaila Sarr, kutoka klabu ya Stade Rennais

  11. Sio vyema jinsi Real Madrid inavyomuhangaisha Bale

  12. Austin kuelekea West Brom

    West Brom imemsajili mshambuliaji wa Southampton Charlie Austin kwa dau la £4m.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anaelekea katika ligi hiyo baada ya misimu mitatu na nusu akiichezea St Mary, ambapo aliichezea mara 81 na kufunga magoli 20.

  13. Burnley yakaribia kumsajili Drinkwater kutoka Chelsea

  14. Habari za hivi punde, Tottenham yamsajili rasmi Sessegnon

  15. Crystal Palace kutafuta mchezaji atakayechukua mahala pake Zaha

    Crystal Palace imewasilisha ombi la kumsaini mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Jean-Kevin Augustin iwapo mktaba wa siku ya mwisho itaafikiwa kumnunu winga wake Wilfried Zaha, kulingana na Sky Sports.

  16. Habari za hivi punde, Djibril Sidibe ahamia Everton kutoka Monaco

    Everton imeafikia makubaliano na beki wa Ufaransa Djibril Sidibe kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Monaco.

    Everton ina mbadala ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa mkataba wa kudumu mwisho wa msimu huu.

    Sidibe alishinda taji la ligi ya daraja la kwanza na Monaco katika msimu wa 2016-17 na alikua miongoni mwa kikosi cha Ufaransa kilichoshinda kombe La dunia nchini Urusi mwaka uliopita.

    Amefunga magoli sita katika mechi 114 akiichezea Monaco tangu ajiunge na lille 2016.

  17. Mchezaji wa zamani wa Tottenham Jermaine Jenas anasemaje?

  18. Everton inamtaka Rojo

  19. Herrera apata pigo!

    Ander Herrera atalazimika kusubiri kwa muda zaidi ili kuanza kuichezea PSG.

    Mchezaji hyo wa zamani wa Man Uniuted ametuma ujumbe wa twitter wa picha yake akipokea matibabu ya jeraha la mguu alilopata katika mazoezi siku ya Jumatano, ambalo litamweka nje kwa wiki nne au tatu.

  20. Mario Mandzukic hataelekea Man United - kunani?