Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Tanzania na Kenya zawekwa kundi moja AFCON 2019

Mataifa manne kutoka Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi kushiriki michuano hiyo.

Moja kwa moja

  1. AFCON 2019: Watanzania mitandaoni waonesha matumaini

  2. AFCON 2019: Je Wakenya waliopo katika mitandao walikuwa na yapi ya kusema?

  3. Droo ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2019

  4. Nani kucheka, nani kulia?

    Hatimaye makundi sita ya mchuano wa Kombe la Mataifa ya Africa, Afcon 2019 yamepangwa.

    Kwa ukanda wa Afrika Mashariki, kwa vyoyote vile habari kubwa kwa sasa ni Kundi C ambalo linaundwa na mataifa jirani ya Kenya na Tanzania.

    Mataifa hayo, yanaungana pamoja na vigogo wa mpira wa Afrika mataifa ya Senegal na Algeria.

    Kwa upande wa Uganda wao wapo Kundi A pamoja na wenyeji Misri, DR Congo na Zimbabwe.

    Burundi wapo kwenye Kundi B pamoja na Nigeria, Madagascar na Guinea.

  5. Kundi F

    • Cameroon,
    • Ghana,
    • Benin,
    • Guinea-Bissau
  6. Kundi E

    • Tunisia
    • Mali
    • Mauritania
    • Angola
  7. Kundi D

    • Morocco,
    • Ivory Coast,
    • South Africa,
    • Namibia
  8. Kundi C

    • Senegal
    • Algeria
    • Kenya
    • Tanzania
  9. Kundi B

    • Nigeria
    • Guinea
    • Madagascar
    • Burundi
  10. Kundi A

    • Misri
    • DRC
    • Uganda
    • Zimbabwe
  11. Sherehe bomba! Muda je?

    Watu mbali mbali barani Afrika wamekuwa wakiimwagia sifa Misri kwa sherehe kemkem zinazoendelea kwenye Mapiramidi ya Giza.

    Misri imechukua jukumu la kuandaa mashindano hayo dakika za mwisho baada ya Cameroon ambao ndio walikuwa waandaaji kufeli dakika za mwisho.

    Hata hivyo, ilitangazwa kuwa droo hiyo itapangwa saa 3 usiku kwa saa za Afrika lakini mpaka baada ya saa moja na nusu baadae, bado droo ilikuwa haija pangwa.

    Hali hiyo imeoneka pia kuwaudhi baadhi ya watu.

  12. Timu moja katika kila chungu itaunda kundi la timu nne

  13. Mara ya mwisho Ghana kushinda kombe hilo

  14. Droo ya AFCON inaendelea kwa sasa

  15. Harambee Stars ya Kenya kuzawadiwa ksh.250,000 kwa kila ushindi AFCON

  16. Burundi yafuzu kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza

    Burundi ilifuzu katika kombe la mataifa ya Africa AFCON kwa mara ya kwanza baada ya kumzuia mshambuliaji wa Gabon na Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang wakitafuta droo ya 1-1.

    Huku Burundi ikihitaji droo ya 1-1, wageni Gabon walioandaa fainali za kombe la 2017, walihitaji kupata ushindi ili kujiunga na washindi wa kundi C Mali katika kinyang'anyiro hicho kilichopanuliwa na kushirikisha timu 24 nchini Misri kuanzia mwezi Juni na Julai.

    Mshambuliaji wa klabu ya Stoke City nchini Uingereza Saido Berahino aliiongoza miamba hiyo ya Afrika mashariki.

    Burundi inajiunga na Madagascar pamoja na Mauritania miongoni mwa mataifa yatakayoshiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza huku ufanisi wao ukizua sherehe katika taifa hilo.

    Katika kipindi chote cha mechi hiyo Burundi ilizuiliwa na kipa wa siku nyingi wa Gabon Didier Ovono kabla ya Cedric Amissi kufunga bao la pekee dakika ya 75.

    Hatahivyo sherehe hizo zilizuiliwa hadi katika kipenga cha mwisho wakati Gabon ilipofuzu baada ya beki wa Burundi kujifunga.

  17. Nyota wa kandanda wamiminika Misri

    Mambo yameiva nchini Misri na muda wowote kutoka sasa droo itaanza kupangwa.

    Wachezaji nyota wa zamani barani Afrika wakiongozwa na Yaya Toure, Didier Drogba, Elhadji Diouf na Mustafa Hajd wote wamefika katika ukumbi itakapofanyika shughuli hiyo.

    Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano ya Afcon kuongezwa idadi ya timu shiriki toka 16 mpaka 24.

  18. Kocha wa Tanzania 'aongea kiarabu'

    Emmanuel Amunike ni moja ya wachezaji maarufu wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria.

    Ameongeza umaarufu wake barani Afrika baada ya kuipeleka Tanzania kwenye michuano ya Afcon baada ya makocha wengine kushindwa kwa miaka 39.

    Lakini je unajuwa gwiji huyo anaambulia lugha ya kiarabu?

    Michuano ya Afcon ya mwaka huu inafanyikia Misri, na Amunike alishawahi kuishi nchini humo toka mwaka 1991 mpaka 1994 akichezea klabu kongwe ya Zamalek.

    Mtizame mwenyewe kwenye video hiyo chini 'akimwaga' kiarabu.

  19. Uganda yafuzu mara ya pili mfululizo

    Tofauti na Tanzania ambao walitupwa nje kwa miaka 39, Kenya waliosubiri kwa miaka 15 ama Burundi ambao wamefuzu kwa mara ya kwanza, hii ni mara ya pili mfululizo kwa Uganda kushiriki michuano ya Afcon.

    Uganda walishiriki michuano hiyo miaka miwili iliyopita (2017) nchini Gabon na kutolewa kwenye hatua ya makundi.

    Kabla ya 2017, Uganda nao walisubirikwa miongo mitatu kufuzu.

    Uganda ilifuzu katika nafasi ya kwanza kwenye kundi L ikufuatiwa na Tanzania katika nafasi ya pili.

  20. Habari za hivi punde, Hivi ndivyo timu zilivyopangwa kabla ya droo