Biden atangaza vikwazo zaidi ya 500 dhidi ya Urusi
Vikwazo hivyo vinawalenga watu waliohusishwa na kifungo cha Navalny na taasisi zinazoongoza vita vya Urusi dhidi ya Ukraine Rais Joe Biden alisema.
Moja kwa moja
Kifungo cha jela au faini yatolewa kwa wamiliki wa baa ambako vijana walifariki Afrika kusini
Wamiliki wa baa moja nchini Afrika Kusini, ambapo vijana 21 walifariki wakati wa tafrija mwaka wa 2022, wameagizwa kulipa faini kila mmoja au kukaa jela kwa siku 100.
Wanandoa hao walipatikana na hatia ya kuuza pombe kwa watoto wa chini ya miaka 18.
Vifo vyao katika jimbo la Eastern Cape vilisababisha ghadhabu na kuzua wito mpya wa kutaka umri halali wa kunywa pombe uongezwe.
Ripoti kiwango cha sumu katika miili yao ilifichua walikufa kutokana na kukosa hewa kutokana na msongamano.
Pia iliibuka kuwa chembechembe za kemikali yenye sumu, methanoli zilipatikana katika miili yao.
Uchunguzi rasmi bado haujafanyika.
Ubakaji wa watoto na mauaji ya kikabila yafichuliwa nchini Sudan - UN
Chanzo cha picha, AFP
Ripoti ya Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeweka wazi ukiukaji wa kutisha unaofanywa na pande zote mbili katika vita nchini Sudan.
Ripoti hiyo inahusu miezi minane baada ya mzozo huo kuzuka mwezi wa Aprili mwaka jana na ina ushahidi kutoka kwa mamia ya watu.
Inapendekeza maelfu ya watu wameuawa katika mashambulizi ya kikabila katika eneo la Darfur na inajumuisha madai ya watoto kubakwa.
Picha za satelaiti zinaonyesha kuenea kwa matumizi ya vilipuzi vizito kwenye maeneo yenye watu wengi, na kuua idadi kubwa ya raia.
Ripoti hiyo inajiri baada ya kanda za video kuibuka wiki hii za wanafunzi wakikatwa vichwa na wanaume waliovalia sare ambao baadaye waliviweka vichwa vilivyokatwa kwenye vijiti barabarani.
Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na mazungumzo jumuishi kuelekea serikali ya kiraia nchini Sudan.
Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu aweka wazi mpango wa Gaza baada ya vita
Chanzo cha picha, Reuters
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa mpango wake kuhusu Gaza baada ya vita.
Chini ya mpango wake Israel itadhibiti usalama kwa muda usiojulikana, na Wapalestina wasiokuwa na uhusiano na makundi yanayochukia Israel watasimamia eneo hilo.
Marekani, mshirika mkuu wa Israel, inataka Mamlaka ya Palestina yenye makao yake Ukingo wa Magharibi (PA) kuitawala Gaza baada ya vita.
Lakini waraka huo mfupi - ambao Bw Netanyahu aliwasilisha kwa mawaziri jana usiku - hauitaji PA.
Hapo awali ameondoa jukumu la baada ya vita kwa mamlaka hiyo inayoungwa mkono kimataifa.
Anatarajia Gaza "isiyo na uwezo wa kijeshi";Israeli itakuwa na jukumu la kuondoa uwezo wote wa kijeshi zaidi ya ule unaohitajika kwa utulivu wa umma.
Kutakuwa na "Kufungwa kwa mpaka Kusini" wa eneo hilo na Misri ili kuzuia magendo ya chinichini na ya ardhini.
Biden atangaza vikwazo zaidi ya 500 dhidi ya Urusi
Chanzo cha picha, Getty Images
Marekani imetangaza vikwazo vipya zaidi ya 500 dhidi ya Urusi
kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine na kifo cha kiongozi wa upinzani Alexei Navalny.
Vikwazo hivyo vinawalenga watu waliohusishwa na kifungo cha Navalny na taasisi zinazoongoza vita vya Urusi dhidi ya Ukraine Rais Joe Biden alisema.
Vikwazo vya kuuza bidhaa nje vitawekwa kwa karibu makampuni 100 au watu
binafsi.
EU pia ilitangaza vikwazo, ambavyo Moscow ilijibu kwa kupiga
marufuku maafisa wa EU kuingia Urusi.
Haijulikani ni athari gani vikwazo hivyo vitaleta kwa uchumi wa
Urusi.
Katika taarifa yake, Rais Biden alisema vikwazo hivyo
"vitahakikisha" Rais wa Urusi Vladimir Putin "analipa gharama
kubwa zaidi kwa uvamizi wake nje ya nchi na ukandamizaji nyumbani".
Vikwazo hivyo vinakuja wiki moja tangu Navalny kufariki ghafla
katika jela ya Arctic Circle. Bwana Biden amesema "hakuna shaka"
rais wa Urusi ndiye anayefaa kulaumiwa .
Vikwazo hivyo pia vinakuja katika mkesha wa kuadhimisha mwaka wa
pili wa uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine.
"Miaka miwili iliyopita, alijaribu kuifuta Ukraine kwenye
ramani. Ikiwa Putin hatalipa gharama ya kifo na uharibifu wake,
ataendelea," Bw Biden alisema katika taarifa hiyo.
Rais wa Kenya Ruto awaahidi pesa wanariadha
Chanzo cha picha, KTN News
"Sasa tumerejesha hazina ya michezo ili kushughulikia masuala [ya] pekee ya michezo," amesema Rais wa Kenya William Ruto, akiongeza kuwa vifaa vyote vilivyoombwa wakati wa mazishi ya Ijumaa ya mshindi wa rekodi ya mbio za marathon Kelvin Kiptum vitatolewa.
"Tutarekebisha mfumo wetu wa zawadi - kwamba pia ziwe pesa kwa siku zijazo," pia ameahidi wakati wa hotuba yake kwa waombolezaji - akimaanisha maisha mafupi ya kikazi ya wanariadha wa juu ikilinganishwa na kazi zingine na matatizo ya kifedha wanayokabiliana nayo.
"Pesa zitawekwa katika mfumo wa pensheni kusaidia wanariadha baada ya kustaafu," rais aliongezea, akiitaka wizara ya michezo kutekeleza hili.
“Roho ya Kelvin ipumzike mahali pema peponi,” alimalizia.
Vita vya Gaza: Ujumbe wa Israel kushiriki mazungumzo ya Paris ili kupata muafaka kuhusu Gaza
Chanzo cha picha, Getty Images
Vvyombo vya habari vya Israel na vyanzo vya
kidiplomasia vilithibitisha kwamba Israel itashiriki katika mikutano ya Paris
katika siku zijazo ili kufikia makubaliano ya kudumu ya kusitisha
mapigano.
Majadiliano hayo
yanajumuisha wajumbe kutoka Misri, Qatar na Marekani.
Vyombo vya habari vya Israel vimesema kuwa serikali ya mrengo wa
kulia imekubali kutuma ujumbe mjini Paris kushiriki katika
mazungumzo hayo.Msemaji wa Ikulu ya White House alithibitisha Alhamisi kwamba
mazungumzo yanayoendeshwa na mjumbe wa Rais Joe Biden kuhusu kuachiliwa kwa
mateka na mazungumzo yanayoendeshwa na mjumbe wa Rais Joe Biden
kuhusu kuachiliwa kwa mateka na kusitisha mapigano huko Gaza
"yanaendelea vizuri."
Vikosi vya
Israel vililenga maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza usiku wa kuamkia Alhamisi,
na kusababisha makumi ya vifo.
Zaidi ya Wapalestina 23, wengi wao wakiwa watoto
na wanawake, waliuawa, na wengine kujeruhiwa, kutokana na mashambulizi ya ndege
za kivita za Israel kwenye makazi ya raia katikati mwa Ukanda wa
Gaza.
Ofisi ya habari ya
serikali ya Hamas huko Gaza ilithibitisha kuwa nyumba katika eneo la Deir
al-Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza zililengwa na kusababisha vifo vya
zaidi ya watu 40 na wengine takriban 100 kujeruhiwa.
Kiptum alitarajia kufanya harusi mwezi Aprili - mjane
Chanzo cha picha, NTV
Maelezo ya picha, Wanandoa hao wana watoto wawili
Mkewe Kelvin Kiptum alilia wakati wa kutoa heshima zake kwa mwanariadha huyo, ambapo alifichua kwamba wangefunga ndoa mwezi Aprili.
Wanandoa hao walikuwa na harusi ya kitamaduni mnamo 2017, lakini bado hawajafunga ndoa rasmi ya kanisani.
"Tumekuwa tukipanga kwa siku kuu ya kufunga pingu za maisha katika sherehe ya harusi ya kupendeza mnamo Aprili 2024, lakini mipango ya Mungu ni mikubwa zaidi," Asaneth Rotich alisema, baada ya kutulia kwa muda wakati hisia za majonzi na huzuni zilipozidi.
"Bado nitafanya viapo vyangu vya mapenzi hata katika mapumziko yako...Umekuwa mume na baba bora kwa watoto wetu," Bi Rotich alisema.
Wakfu wa Kelvin Kiptum utaundwa
Wakfu utaundwa ili kumuenzi Kelvin Kiptum kwa kuendeleza kazi yake ya kibinadamu, Jack Tuwei, rais wa bodi inayosimamia riadha nchini Kenya amesema.
Bw Tuwei alibasema kuwa Kiptum amekuwa akiwalipia karo baadhi ya watoto katika kijiji chake.
"Ili kuweka kumbukumbu ya Kelvin Kiptum hai na kusaidia familia na jamii yake, Golazo anazindua Wakfu wa Kelvin Kiptum. Hazina hiyo itatoa msaada wa kifedha kwa elimu na miundombinu," Bw Tuwei alisema katika mazishi ya Kiptum.
Galazo ni wakala wa masoko ambao ulikuwa ukifanya kazi na Kiptum.
Wakfu huo utaungwa mkono na bodi ya utawala ya Riadha Kenya, Bw Tuwei alisema, akiongeza kuwa bodi hiyo itahakikisha malipo yote yanayosubiri kulipwa kwa Kiptum yanafanyika.
Jaji wa Texas aunga mkono kusimamishwa shule kwa mwanafunzi mweusi kwa sababu mtindo wake wa nywele
Jaji wa jimbo la Texas ameamua kuwa wilaya ambako kuna shule ya mwanafunzi huyo haikumbagua mwanafunzi mweusi wa shule ya sekondari ilipomuadhibu kwa mtindo wake wa nywele.
Wilaya ya Shule ya Kujitegemea ya Barbers Hill ilimsimamisha kazi Darryl George, 18, Agosti mwaka jana, akisema mtindo wake wa nyweleuilikiuka kanuni zake za nywele.
Jaji aligundua kuwa shule hiyo iliyoko eneo la Houston haikuvunja sheria ya serikali inayopiga marufuku ubaguzi wa rangi kuhusu nywele.
Wakili wa familia alisema wanapanga kukata rufaa.
Wakati huo huo, mwanafunzi ataendelea kusimamishwa masomo na kuondolewa kwenye madarasa ya kawaida ya shule.
Jaji wa Kaunti ya Chambers Chap Cain III aliamua kuunga mkono shule hiyo baada ya takriban saa tatu za kutoa ushahidi siku ya Alhamisi.
Bw George alizungumzia "hasira, huzuni, kukatishwa tamaa" kwake nje ya mahakama baada ya uamuzi huo.
Mahakama: Wafungwa sasa wako huru kuhudhuria maziko ya wapendwa wao Kenya
Maelezo ya picha, Wafungwa nchini Kenya
Wafungwa waliohukumiwa wana haki ya kuhudhuria maziko ya
wanafamilia wa karibu isipokuwa kama kuna sababu za msingi za kukataa kibali
hicho, Mahakama Kuu imetangaza.
Jaji Lawrence Mugambi alisema wafungwa wote waliohukumiwa na
wafungwa wanaoshikiliwa chini ya ulinzi wana haki ya kutendewa utu.
Haki hii alisema ni pamoja na kuwaruhusu
kuhudhuria mazishi ya wanafamilia wao wa
karibu isipokuwa kuna sababu za msingi.
Alitoa maagizo hayo kufuatia ombi lililowasilishwa na Moses
Dola, mfungwa katika Gereza la Kiambu GK.
Dola aliambia mahakama kuwa kufuatia kifo cha mamake mnamo
Julai 12 2021, hakuruhusiwa kuhudhuria mazishi yake na idara ya Magereza.
Alidai kuwa kunyimwa huko ni unyama na kukiuka haki yake ya
utu sio yeye tu bali pia wafungwa wengine wa kabla ya kesi na wafungwa walio
katika mazingira kama hayo.
Rais wa Senegal asema ataondoka madarakani tarehe 2 mwezi Aprili
Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Senegal Macky Sall amesema ataondoka madarakani tarehe 2 Aprili
wakati muhula wake utakapokamilika, lakini bado haijafahamika ni lini uchaguzi
utafanyika ili kumchagua mrithi wake.
Alisema tarehe ya uchaguzi itategemea mdahalo wa kitaifa
uliopangwa kuanza Jumatatu, ambao unajumuisha mashirika ya kiraia, vyama vya kisiasa
na wagombea.
"Tarehe 2 Aprili 2024 dhamira yangu kama mkuu wa
Senegal inafikia kikomo...ningependa mjadala huu utatuliwe kwa uwazi,"
alisema wakati wa mahojiano ya televisheni.
Tangazo lake linapunguza hofu kwamba alikuwa akipanga
kuongeza muda wake, huku kukiwa na mzozo wa kisiasa.
Bw Sall amekuwa chini ya shinikizo la kutangaza tarehe ya
uchaguzi tangu kujaribu kuuchelewesha mapema mwezi huu.
Alikuwa akitaka kuahirisha uchaguzi hadi Desemba ili mizozo
kuhusu kustahiki kwa wagombea wengine iweze kutatuliwa.
Lakini mahakama kuu ya nchi hiyo ilisema kucheleweshwa huko
ni kinyume cha katiba, na kutaka uchaguzi ufanyike "haraka
iwezekanavyo".
Akina mama wa Uganda wahukumiwa kwa kupeleka watoto kuomba
Chanzo cha picha, Getty Images
Mahakama nchini Uganda imewahukumu zaidi ya wanawake 100
kifungo cha mwezi mmoja kila mmoja kufanya huduma za jamii baada ya kukiri kuwatuma
watoto wao kuomba omba katika mji mkuu wa Kampala.
Mahakama pia imepiga marufuku wanawake hao kurejea mjini na
kuamuru warudishwe katika wilaya yao ya Napak kaskazini mwa Uganda, gazeti la
kibinafsi la Daily Monitor liliripoti.
Wanawake hao waliomba kuhurumiwa, huku wengine wakisema ni
wajane na wengine ni mama wasio na wenza, gazeti la serikali la New Vision
liliripoti.
"Nimesikiliza
kilio chao na hukumu [jela] haitakuwa sawa. Ni lazima nitekeleze adhabu ya
kuzuia... nitawahukumu kufanya kazi za kijamii. Bila malipo, utatumikia kifungo
cha mwezi mmoja," hakimu katika mahakama hiyo Edgar Karakire, alinukuliwa
akisema na Daily Monitor.
Kutuma watoto
kuomba au kuomba msaada ni kinyume na sheria za ulinzi wa watoto za Uganda na
adhabu yake ni ya juu zaidi ya miezi sita.
Wanawake hao
walikuwa wamekamatwa mwezi uliopita wakati wa msako mkali wa kuwaondoa ombaomba
kutoka mji mkuu, kabla ya mikutano mitatu ya kimataifa ambayo iliandaliwa huko.
Watoto hao
walipelekwa katika Kijiji cha Watoto cha Masulita katikati mwa Uganda, ambacho
ni mwenyeji wa watoto waliookolewa.
Kwa Picha: Mshindi wa mbio za marathon za Kenya Kiptum anatarajiwa kuzikwa
Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon za
wanaume, Kelvin Kiptum, anatarajiwa kuzikwa baadaye Ijumaa nyumbani kwake Eldoret
magharibi mwa Kenya.
Rais wa Kenya William Ruto ataongoza waombolezaji katika
kumuenzi mwanariadha mahiri ambaye aliweka na kuvunja rekodi katika maisha yake
mafupi ya mbio.
Kiptum alifariki
katika ajali ya gari, akiwa na umri wa miaka 24 pekee, wiki mbili zilizopita.
Maelfu wametoa
heshima kwa Kiptum katika mji wake wa asili.
Umati wa watu
ulikusanyika njiani mjini Eldoret huku gari la maiti likiendeshwa hadi kijijini
kwake kabla ya mazishi.
Kazi yake kama
mwanariadha ilikuwa inaanza tu.
Katika miaka miwili,
angekimbia marathoni tatu kati ya saba za kasi zaidi katika historia, akavunja
rekodi ya dunia na kuweka rekodi ya mbio za London.
Alikuwa
amejiwekea malengo ya kukimbia mbio fupi za saa mbili za marathon huko
Rotterdam mwezi huu wa Aprili.
Chanzo cha picha, bbc
Vikwazo vipya dhidi ya Urusi kutangazwa siku ya Ijumaa kuhusiana na vita na kifo cha Navalny
Marekani inapanga kuweka vikwazo kwa zaidi ya mashirika 500 na watu binafsi waliohusika katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.
Vikwazo hivyo, ambavyo vitawekwa siku ya Ijumaa, vitaikumba "Urusi, washirika wake na chombo chake cha vita," Idara ya Hazina ya Marekani ilisema.
Vikwazo vitawekwa na Hazina na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Kulingana na Wizara ya Fedha, vitakuwa vikwazo vilkubwa zaidi tangu kuanza kwa uvamizi wa Putin nchini Ukraine.
"Baada ya Urusi kuanzisha vita kamili dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022, Washington na washirika wake waliweka vikwazo kadhaa vinavyolenga mapato ya Moscow , jeshi na viwanda.
Hatua hizi ni pamoja na ukomo wa bei ulioanzishwa na Marekani na washirika wake, unaolenga kupunguza mapato ya Moscow kutokana na mauzo ya nje ya mafuta na bidhaa za petroli.
Wakati huo huo, wakosoaji wanaona kuwa licha ya idadi na sauti kubwa ya vikwazo vilivyowekwa, bado hawajaweza kufikia malengo yao: uchumi wa Urusi sio tu haujapata mkataba tangu mwanzo wa vita, lakini umeendelea kukua ingawa kwa kasi ndogo), na bajeti imepokea mamia ya mabilioni ya dola kutokana na kupanda kwa bei ya nishati.
Urusi yaikasirisha serikali ya Guinea baada ya serikali kuvunjwa
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Mtawala wa kijeshi Kanali Mamady Doumbouya hajatoa sababu za kuvunja serikali yake
Wanajeshi wa Guinea wameandamana hadi kwa balozi wa Urusi baada ya ubalozi wake kuripotiwa kuonya kuhusu uwezekano wa machafuko katika mji mkuu wa Conakry.
Onyo hilo lilitolewa baada ya kiongozi wa junta Kanali Mamady Doumbouya kuvunja serikali siku ya Jumatatu, na kuamuru kufungwa kwa mipaka yote.
Balozi Alexey Popov aliomba msamaha kwa junta kwa kile alichokiita kutokuelewana, vyombo vya habari vya Guinea viliripoti.
Kanali Doumbouya alichukua mamlaka baada ya mapinduzi ya 2021.Alivunja serikali yake siku ya Jumatatu bila kutoa maelezo yoyote.
Pia aliamuru kukamatwa kwa pasipoti za mawaziri waliofutwa kazi, na akaunti zao za benki kufungiwa.Vyombo vya habari vya Guinea viliripoti kuwa uamuzi wa Kanali Doumbouya ulipelekea ubalozi wa Urusi nchini Guinea kuwashauri raia wa Urusi kuwa waangalifu kwani kunaweza kutokea machafuko katika mji mkuu wa jimbo hilo la Afrika Magharibi, Conakry.
Junta ilijibu kwa hasira, na afisa katika wizara yake ya mambo ya nje kumwita Bw Popov kwenye mkutano.
"Nilieleza kuwa ilikuwa ni kutoelewana, tafsiri ya uongo ya kile kilichochapishwa. Tangazo hilo lilichapishwa kwa Kirusi pekee kwa raia wa Urusi," Bw Popov alinukuliwa na televisheni na redio inayomilikiwa na serikali ya Guinea.
Serikali ilikubali msamaha huo, huku Bw Popov akisema kisa hicho hakitaathiri uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.
Guinea ni mojawapo ya makoloni kadhaa ya zamani ya Ufaransa huko Afrika Magharibi ambayo yamekumbwa na mapinduzi katika miaka ya hivi karibuni.Wanajeshi, ambao walichukua mamlaka katika Mali, Niger na Burkina Faso wameegemea kwa Urusi, huku wakiwa na chuki dhidi ya Ufaransa na kambi ya kanda ya Afrika Magharibi, Ecowas.Lakini Kanali Doumbouya amejaribu kudumisha uhusiano mzuri na pande zote.
Ameahidi kufanya uchaguzi ili kurejesha utawala wa kidemokrasia ifikapo mwisho wa 2024.Utawala wa kijeshi ulipiga marufuku maandamano yote mwaka wa 2022 na umewaweka kizuizini viongozi kadhaa wa upinzani, na wanachama wa mashirika ya kiraia.
Kanali Doumbouya alimpindua Rais Alpha Condé mnamo Septemba 2021, akisema jeshi lilikuwa na chaguo dogo ila kunyakua mamlaka kwa sababu ya kukithiri kwa rushwa, kutozingatia haki za binadamu na usimamizi mbovu wa kiuchumi.
Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha mazungumzo cha Marekani Wendy Williams apatikana na tatizo la ubongo
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wendy Williams
Nguli
wa kipindi cha mazungumzo cha mchana nchini Marekani, Wendy Williams Hunter,
aligunduliwa mwaka jana kuwa na aphasia inayoendelea na matatizo ya ubongo ya
frontotemporal (FTD), timu yake ya utunzaji imefichua.
Timu
hiyo ilisema ilikuwa ikitoa habari hiyo "ili kurekebisha uvumi usio sahihi
na wa kuumiza kuhusu afya yake".
Bi
Williams, 59, alikuwa mwenyeji wa kipindi cha Wendy Williams Show kilicho na
umaarufu mkubwa kilichhokwenda hhewani nchini Marekani kwa zaidi ya muongo
mmoja.
Lakini kiliisha
mnamo 2022 huku kukiwa na shida za kiafya ambazo amekuwa akizikabili.
Habari
za kugunduliwa kwa matatizo hayo zinakuja siku moja baada ya jarida la People
Magazine, ambapo jamaa walisema Bi Williams yuko katika kituo cha utunzaji
katika eneo lisilojulikana na amekuwa katika hali ya kushangaza ya kiafya.
"Kama
mashabiki wa Wendy wanavyofahamu, siku za nyuma amekuwa wazi kwa umma kuhusu
mapambano yake ya kimatibabu na Ugonjwa wa Graves' na Lymphedema pamoja na
changamoto zingine muhimu zinazohusiana na afya yake," timu yake ya
utunzaji iliandika katika taarifa Alhamisi.
"Katika
kipindi cha miaka michache iliyopita, maswali yaliibuka wakati fulani kuhusu
uwezo wa Wendy wa kuchakata taarifa na wengi wamekuwa wakikisia kuhusu hali ya
Wendy, hasa alipoanza kupoteza maneno, kufanya mambo yasio ya kawaidda wakati
fulani, na kuwa na ugumu wa kuelewa miamala ya kifedha."
Alexei Navalny: Mamake mkosoaji wa Putin anasema ameonyeshwa mwili wa mwanawe
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Lyudmila Navalnaya mamake mkoajia mkubwa wa rais Putin Alexei Navalny
Mamake
Alexei Navalny amesema ameonyeshwa mwili wa mwanawe, lakini mamlaka ya Urusi
inamshinikiza kuruhusu mazishi ya "siri".
Katika
anwani ya video, Lyudmila Navalnaya alisema alipelekwa kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti ambapo alitia saini cheti cha kifo.
Katibu
wa waandishi wa habari wa kiongozi huyo wa zamani wa upinzani alisema ripoti ya
matibabu iliyowasilishwa kwa Bi Navalnaya ilisema alikufa kwa sababu za asili.
Mjane
wa Navalny amesema aliuawa na mamlaka ya Urusi.
Lyudmila
Navalnaya alisema sheria inawataka maafisa kukabidhi mwili wa mwanawe, lakini
alikuwa "akidanganywa" kwani walikataa kufanya hivyo. Alidai mamlaka
ilikuwa ikiweka masharti ya mazishi ya mtoto wake, ikiwa ni pamoja na mahali,
wakati na namna ya maziko yake.
Akasema:
"Wanataka kunipeleka nje ya makaburi ya umma na kunioneysha kaburi ambalo
mwanagu amezikwa .
Bi
Navalnaya alisafiri hadi mji wa kaskazini mwa Urusi wa Salekhard kufuatia
habari za kifo cha mwanawe katika jela la karibu la adhabu siku sita
zilizopita.
Hapo
awali alinyimwa uwezo wa kuuona mwili wa mwanawe, Jumanne akiomba binafsi Rais
wa Urusi Vladimir Putin amruhusu azike.
Katika
hotuba ya Alhamisi, Lyudmila Navalnaya alisema alikuwa akitishiwa na mamlaka.
"Wakinitazama
machoni mwangu, wanasema kwamba ikiwa sitakubali mazishi ya siri, watafanya
kitu na mwili wa mwanangu."
Alisema
aliambiwa na wachunguzi: "Wakati unakwenda na maiti inaharibika."
Mashine Intuitive: Kampuni ya Marekani yaweka historia kwa kupeleka chombo chake mwezini
Chanzo cha picha, Intuitive machine
Maelezo ya picha, Mchoro: Ilichukua dakika chache kabla ya kuanzisha mawasiliano
Kampuni
moja ya Marekani imeweka historia kwa kuwa ya kwanza kuwasilisha chombo chake
cha angani kwenye Mwezi.
Mashine
za Intuitive za Houston ziliwasilisha roboti yake ya Odysseus karibu na ncha ya
kusini ya mwezi.
Ilichukua
dakika kadhaa kwa vidhibiti kubaini kuwa chombo kilikuwa kimewasili, lakini
hatimaye ishara ilipokelewa.
"Tunachoweza
kuthibitisha, bila shaka, ni vifaa vyetu viko kwenye uso wa Mwezi na
tunapata ishara," mkurugenzi wa ndege Tim Crain alitangaza.
Wafanyakazi
wa kampuni hiyo walishangilia na kupiga makofi kwa habari hiyo njema
Ilikuwa
wakati muhimu, sio tu kwa ushindani wa kibiashara lakini pia kwa mpango wa anga
wa Marekani kwa ujumla.
Intuitive
Machines imevunja historia ya kutokuwepo kwa Marekani kwa zaidi ya nusu karne
kwenye uso wa Mwezi.
Mara ya
mwisho kwa Marekani kuwasili mwezini ni mwaka 1972 wakati chombo cha Apollo
kilipowasili kwenye sakafu ya mwezi.
Marekani yaionya Iran dhidi ya kuisambazia Urusi silaha
Chanzo cha picha, Tasnim
Serikali ya Marekani imeionya Iran kwamba ikiwa itapeleka makombora ya balistiki kwa Urusi, itakabiliwa na majibu ya "haraka na makali" kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.
Haya yanajiri baada ya shirika la habari la Reuters kuripoti mapema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilituma aina hizo za silaha nchini Urusi.
John Kirby, msemaji wa Baraza la Usalama la Ikulu ya White House, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Alhamisi kwamba Marekani bado haijaona ushahidi wa kuthibitisha kuhamishwa kwa makombora hayo kutoka Iran hadi Russia.
Shirika la habari la Reuters liliripoti siku ya Jumatano, likinukuu vyanzo sita, kwamba Iran ilituma idadi kubwa ya makombora yenye nguvu ya balestiki hadi Urusi.
Bwana Kirby alisema: "Ripoti inasema kwamba Wairani wanaonyesha wazi kwamba watatuma makombora ya balestiki nchini Urusi. Hatuna sababu ya kufikiria kwamba hawatachukua hatua juu ya hili."
Ameongeza kuwa: "Sisi kwa upande wetu tunalizungumzia suala hili katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Tutaweka vikwazo vipya dhidi ya Iran na tutazingatia chaguzi zaidi kama jibu kwa uratibu wa washirika wetu barani Ulaya na kwingineko duniani."
Katika ripoti yake, shirika la habari la Reuters, likinukuu vyanzo vitatu vya habari nchini Iran, liliandika kuwa Iran imetuma takribani makombora 400 kwa Urusi, yakiwemo idadi kubwa ya makombora ya masafa mafupi ya Fateh-110, kama vile mfumo wa rununu wa Zulfiqar, unaoweza kuangazia eneo kati ya kilomita 300 na 700.
Shirika la habari la Reuters liliandika kuwa, shehena ya silaha hizo ilianza kusafirishwa mapema Januari, yaani baada ya makubaliano kukamilika mjini Tehran na Moscow mwishoni mwa mwaka jana kati ya jeshi na mamlaka ya nchi hizo mbili.
Bwana Kirby alisema kuwa Iran imeuza nje idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani, mabomu ya kuongozwa na risasi za kivita kwa Urusi, ambazo nchi hiyo ilitumia katika vita vya Ukraine.
Amesema: "Katika kukabiliana na Iran kuendelea kuunga mkono vita vya kikatili vya Russia, tutaweka vikwazo zaidi dhidi ya Iran katika siku zijazo, na tuko tayari kuchukua hatua hiyo.
Unaweza pia kusoma
Je, Marekani inafanya nini kuipa Iran inachotaka bila vita vya moja kwa moja na Israel?
Je, Iran inapanga nini juu ya mashambulizi ya Marekani dhidi ya wapiganaji wake nchini Syria, Iraq na Yemen?