Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Iraq yaonya juu ya athari mbaya kikanda baada ya shambulizi la Marekani
Pentagon inasema imeshambulia maeneo lengwa zaidi ya 85 kujibu shambulizi la ndege isiyo na rubani ambayo iliua wanajeshi watatu wa Amerika.
Moja kwa moja
Asha Juma
Kwa nini Marekani imechukua muda kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya wanajeshi wake?
Mashambulizi haya yalitarajiwa kuanza ndani ya siku chache, tena ya hatua kwa hatua, utawala wa Biden ulianza kukabiliwa na maswali na ukosoaji kutoka kwa Republican kuhusu muda na nguvu ya vile Marekani itakavyojibu.
Lakini wataalam wa masuala ya uhusiano wa kigeni wanaamini kuwa mbinu hii ya kuchelewesha ya Marekani iliiruhusu Iran kuwaondoa watu wake kwenye vituo ambavyo vingeweza kushambuliwa na kwa vitendo kuzuia mzozo mkubwa kati ya Iran na Marekani.
"Hii itawaruhusu kupunguza uwezo wa wanamgambo hao wanaoungwa mkono na Iran kushambulia vikosi vya Marekani, lakini sio kuongezeka," Mick Mulroy, naibu katibu msaidizi wa zamani wa ulinzi wa Mashariki ya Kati, aliiambia BBC.
"Ingawa haitawezekana kuwa kizuizi kwa mashambulizi ya siku zijazo."
Faida kuu, alisema, itakuwa "kuepusha vita vya moja kwa moja" kati ya Marekani na Iran. Anasema kwamba faida kuu ya kazi hii ni kwamba pengine itazuia "vita vya moja kwa moja" kati ya Iran na Amerika.
Katika mashambulizi yake ya kulipiza kisasi, Marekani iliilenga Jeshi la Quds la Revolutionary Guards Corps (IRGC) na makundi tanzu katika vituo saba tofauti vya Iraq na Syria.
Kulingana na maafisa wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, wapiganaji wa nchi hii walilipua jumla ya maeneo lengwa 85 katika vituo hivyo.
Rais wa Marekani Joe Biden alisema baada ya mashambulizi hayo: "Wajulishe wale wote ambao wangetaka kutudhuru: Ukimdhuru Mmarekani, tutajibu."
Maafisa wa Marekani walilaumu kundi la wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran kwa shambulizi la Jordan.
Shirika hili linajumuisha makundi kadhaa ya wanamgambo, ambayo yanasemekana kupewa silaha, fedha na mafunzo ya kijeshi na Iran.
Hata hivyo, Iran imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na shambulio la ndege zisizo na rubani kwenye kambi ya Marekani huko Jordan.
Maafisa wa ulinzi na usalama wa Marekani wanasema kuwa hali ya hewa ilifanya isiwezekane kuanza mashambulizi mapema, hadi Ijumaa, waliposema hali ya hewa bora zaidi iliwezesha kutekeleza mashambulizi hayo.
Ingawa Ikulu ya Marekani zimesema mara kwa mara katika siku za hivi karibuni kwamba ilijiepusha kutoa "ujumbe" kabla ya mashambulizi, wataalamu wanaamini walifanya hivyo kwa lengo la kuepusha vita kamili na Iran.
Hussein Arish, mtafiti na mtaalamu wa masuala ya kisiasa mjini Washington, alisema kwamba ucheleweshaji huo kwa hakika ulikuwa na ujumbe kutoka kwa Marekani kuhusu "kile ambacho hawatafanya, ambalo ni kushambulia ndani ya ardhi ya Iran."
Bw Mulroy aliiambia BBC kwamba kuna uwezekano kuwa Marekani iliruhusu wanajeshi wa kikosi cha Revolutionary Guard cha Iran "kuondoka kwenye vituo ambavyo vitashambuliwa".
Wataalamu walibainisha kuwa Marekani lazima awe makini kati ya kuzuia nchi kama Iran bila kuzua mzozo mkubwa zaidi.
Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa John Kirby alisema Ijumaa kwamba Washington haita "kuzungumza kuhusu shughuli za siku zijazo" lakini alithibitisha "kutakuwa na hatua za ziada za kujibu shambulizi hilo katika siku zijazo".
Soma zaidi:
Marekani: Kijana mmoja adaiwa kumpiga risasi na kumkata kichwa baba yake kabla ya mzozo wa kisiasa wa YouTube
Waendesha mashitaka wametoa maelezo mapya ya kutatanisha kuhusu kukatwa kichwa kwa mwanamume na mwanawe katika nyumba ya kitongoji cha Philadelphia.
Justin Mohn, 32, alidaiwa kumpiga risasi babake, mfanyakazi wa serikali, kabla ya kutumia kisu na panga kumkata kichwa.
Kisha aliweka video hiyo kwenye mtandao wa YouTube akitetea kuteswa na kuuawa kwa wafanyakazi wa serikali ya Marekani.
Video hiyo ilikuwa kwenye tovuti kwa saa kadhaa kabla ya kuondolewa, mamlaka ilisema.
Wakili wa Wilaya ya Bucks Jennifer Schorn alisema wakati wa mkutano na wanahabari Ijumaa kwamba Bw Mohn alikuwa na "mpango dhahiri" alipomuua babake - Michael Mohn mwenye umri wa miaka 68 - kisha akaendesha gari hadi kituo cha mafunzo cha Walinzi wa Kitaifa saa mbili kutoka hapo. Alikuwa na matumaini ya kuchochea uasi huko, alisema.
"Mtu huyu alikuwa akifanya yote haya akiwa na akili timamu, akijua matendo yake na kujivunia matokeo yake," aliwaambia waandishi wa habari.
Kwenye video ya mtandao, alionekana akisoma maandishi kabla ya kuchukua kichwa cha babake kilichokatwa na kuonesha kwa kamera, kulingana na ripoti ya polisi.
Kijana huyo aliwahimiza watu wanaotazama kuwatesa na kuwaua maafisa wa serikali. Pia alimwita babake "msaliti" na alionyesha hasira juu ya "makundi ya watu wa mrengo wa kushoto", wahamiaji na jumuiya ya LGBTQ.
Polisi walisema video hiyo ilitazamwa moja kwa moja kwenye mtandao kwa takriban saa tano na watu zaidi ya mara 5,000.
Mlipuko wa gesi Nairobi: William Ruto aamuru kufutwa kazi na kukamatwa kwa maafisa walioidhinisha leseni
Rais William Ruto wa Kenya ameamuru kufutwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa maafisa wa serikali waliohusika na utoaji wa leseni kwa kampuni ya gesi iliyosababisha mlipuko mkubwa katika eneo la Embakasi jijini Nairobi.
Akizungumza kuhusu mkasa huo aliouhusisha na ufisadi na uzembe uliofanywa na baadhi ya maafisa serikalini, Ruto alisema:
‘’Kuna watu wenye leseni katika maeneo ya makazi na wanahatarisha maisha ya raia. Nimeagiza wizara husika kwamba wale wote waliohusika na utoaji wa leseni mahali ambapo haikustahili wafutwe kazi na kupelekwa mahakamani. Hawa watu wanajua kuwa waliambiwa hawatapewa leseni lakini kwasababu ya ufisadi na kukosa uaminifu, walipewa leseni na kuendelea na shughuli zao.’’
Mlipuko huo ulisababisha vifo vya watu watatu huku wengine karibu 300 wakijeruhiwa.
Soma zaidi:
Iraq yaonya juu ya athari mbaya kikanda baada ya shambulizi la Marekani
Msemaji wa waziri mkuu wa Iraq amesema mashambulizi ya Marekani ni "ukiukaji" wa uhuru wa Iraq, kulingana na shirika la habari la AFP.
Jenerali Yehia Rasool anaongeza kuwa mashambulizi hayo yataleta "athari mbaya kwa usalama na uthabiti wa Iraq kikanda," AFP inaripoti.
Marekani ilishambulia maeneo 85 nchini Syria na Iraq usiku wa kuamkia leo kujibu shambulizi la ndege zisizo na rubani Jumapili iliyopita kwenye kambi ya kijeshi ya Marekani na kuua wanajeshi watatu.
Soma zaidi:
Kwa nini kuna kambi za kijeshi za Marekani Mashariki ya Kati?
Kambi iliyoshambuliwa katika shambulio baya la ndege zisizo na rubani kaskazini-magharibi mwa Jordan ni mojawapo ya zaidi ya 10 ambapo wanajeshi wa Marekani wanafanya kazi kote Iraq, Jordan na Syria.
Katika miezi ya hivi karibuni, kambi hizi - kuanzia ukubwa wa kijeshi kama vile Tower 22, hadi kambi ya jeshi la anga ya Al Asad magharibi mwa Iraq - zimeshambuliwa na wanamgambo waliofunzwa, kufadhiliwa na kupewa vifaa na Iran.
Kuna takriban wanajeshi 3,000 wa Marekani walioko Jordan, mshirika mkuu wa Marekani, na 2,500 nchini Iraq - wako huko kwa mwaliko wa serikali ya Iraq kama sehemu ya muungano unaoongozwa na Marekani ili kuzuia kuibuka tena kwa kundi la kijihadi la Islamic State, ambao bado wapo.
Pia kuna takriban wafanyakazi 900 wa Marekani nchini Syria, rasmi wapo kwa ajili ya kumuunga mkono mshirika wake anayepinga IS, Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria vinavyoongozwa na Wakurdi katika eneo lenye uhuru nusu kaskazini-mashariki mwa Syria.
Serikali ya Syria inapinga uwepo wa Marekani katika nchi yake, ikiiita hilo kuwa uvamizi. Marekani pia ina kambi nyingi zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati, zikiwemo kambi tatu kuu za anga katika Ghuba na bandari nchini Bahrain ambayo inatumika kama makao makuu ya Kamandi Kuu ya Kikosi cha Wanamaji cha Marekani.
Soma zaidi:
Maeneo saba ya Syria na Iraq yameshambuliwa na Marekani kwa dakika 30
Maafisa wa Marekani wanasema wanaamini kuwa mashambulizi hayo yamefanikiwa - lakini bado wanatathmini uharibifu.
Walisema maeneo saba yalishambuliwa - manne nchini Syria na matatu nchini Iraq.
Katika maeneo hayo saba kulikuwa na walengwa 85 watu binafsi - ikiwa ni pamoja na vikundi vinavyohusishwa na kuungwa mkono na Jeshi la Walinzi la Revolutionary Guard la Iran.
Marekani imerudia kusema kwamba haitafuti mzozo na Iran yenyewe. Maafisa wanasema kuwa mashambulizi hayo usiku wa kuamkia leo yalilenga kudhalilisha uwezo wa kijeshi na kukomesha mashambulizi dhidi ya kambi za Marekani katika eneo hilo.
Walisema ndege zote za Marekani zilizohusika katika mashambulizi ya usiku wa leo sasa zimetoka katika maeneo hatari.
Marekani ilitumia silaha 125 kwa muda wa dakika 30.
Afisa mkuu wa Marekani aliongeza "hii haitaisha usiku wa leo".
Soma zaidi:
Rais Biden: 'Ukimdhuru Mmarekani, tutajibu'
Rais wa Marekani Joe Biden ametoa taarifa kuhusu mashambulizi ya kulipiza kisasi.
"Leo mchana, kwa maelekezo yangu, vikosi vya kijeshi vya Marekani vilishambulia vituo vya Iraq na Syria ambavyoJeshi la Ulinzi la Iran la Revolutionary Guards Corps (IRGC) na wanamgambo washirika hutumia kushambulia vikosi vya Marekani," alisema.
Aliongeza kuwa hapo awali alihudhuria "kurudi kwa heshima kwa Wamarekani hawa wajasiri" na alizungumza na familia zao.
"Hatua yetu imeanza leo. Jibizo hili litaendelea katika nyakati na maeneo tunayochagua."
Biden alisema Marekani "haitafuti mzozo katika Mashariki ya Kati au popote pengine duniani" lakini alitoa onyo.
"Wacha wale wote ambao wanatafuta kutudhuru wajue hili: Ukimdhuru Mmarekani, tutajibu."
Soma zaidi:
AFCON 2023: Penalti ya Wissa yasaidia Congo kutinga nusu fainali
DR Congo ilitoka nyuma na kuifunga Guinea 3-1 na kutinga nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023.
Mohamed Bayo aliifungia Guinea kwa mkwaju wa penalti dakika ya 20 baada ya fowadi huyo kufanyiwa madhambi na Chancel Mbemba, ambaye alipiga shuti kali kutoka upande wa pili na kusawazisha dakika saba baadaye.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walipata penalti yao pekee katika kipindi cha pili pale Julian Jeanvier alipoanguka nyuma ya Silas na fowadi wa Brentford Yoane Wissa akafunga na kuwapa Leopards uongozi zikiwa zimesalia dakika 25.
Wenyeji hao wa Afrika Magharibi hawakuwa na jibu baada ya kurudi nyuma na ukurasa huo kufungwa baada ya mkwaju wa faulo wa Arthur Masuaku kutoka nje ya upande wa kushoto kumchanganya kipa wa Guinea Ibrahim Kone na kuingia kwenye wavu karibu naye.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa imetoka sare katika mechi zote nne za awali nchini Ivory Coast, ikiifunga Misri kwa mikwaju ya penalti katika hatua ya 16 bora, na sasa inajiandaa kwa mchujo wa nusu fainali ya kwanza tangu kumaliza wa tatu mwaka 2015.
Kikosi cha Sebastien Desabre kitamenyana na washindi wa robo fainali Jumamosi kati ya Mali na wenyeji Ivory Coast (17:00 GMT) katika mechi nne za mwisho Jumatano.
Pia unaweza kusoma:
Marekani yashambulia maeneo yenye uhusiano na Iran nchini Iraq na Syria
Marekani imeanza mashambulizi ya anga dhidi ya makundi yanayoungwa mkono na Iran nchini Syria na Iraq, maafisa wawili wa Marekani waliiambia CBS News.
Mashambulizi hayo yanafuatia shambulio la ndege isiyo na rubani iliyolenga kambi ya kijeshi ya Marekani huko Jordan, ambayo iliua wanajeshi watatu wa Marekani na kujeruhi makumi ya wengine.
Baadhi ya maelezo yaliyothibitishwa na BBC kutoka kwa Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) ni kuwa vikosi vya Marekani vilianzisha mashambulizi ya anga nchini Iraq na Syria dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Iran la Revolutionary Guards Corps (IRGC) vikosi vya Quds na makundi ya wanamgambo tanzu saa 16:00 EST (21:00 GMT).
- Zaidi ya malengo 85 yalilengwa.
- Ndege nyingi zikiwemo za masafa marefu zilizorushwa kutoka Marekani, zilihusika.
- Zaidi ya risasi 125 za usahihi zilitumiwa.
Maeneo yaliyolengwa yalijumuisha oparesheni za amri na udhibiti, vituo, vituo vya kijasusi, roketi, makombora, maeneo ya kuhifadhi ndege zisizo na rubani, vifaa vya usambazaji wa silaha za vikundi vya wanamgambo na vinginevyo.
Soma zaidi:
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 03/02/2024.