Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Pakistan yalaani shambulizi baya la makombora la Iran katika ardhi yake

Iran imefanya shambulizi la kombora ambalo linaonekana kulenga vituo vya wanamgambo magharibi mwa Pakistan na kusababisha vifo vya watoto wawili, maafisa wa Islamabad wamesema.

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Dinah Gahamanyi

  1. Afcon 2023: Morocco 3 - 0 Tanzania

    Na refa anapiga kipenga cha mwisho kuashiria kukamilika kwa mechi hiyo

  2. Afcon 2023: Morocco 3 - 0 Tanzania

    Licha ya kufunga magoli matatu bila Morocco wanatafuta goli la nne kwa udi na uvumba

  3. Afcon 2023: Refa aongeza dakika sita za majeruhi

    Morocco 3 - 0 Tanzania

  4. Afcon 2023: Kipa wa Tanzania Manula aokoa shambulizi ambalo lingezaa bao la nne

    Dakika ya 90

    Morocco 3 - 0 Tanzania

  5. Habari za hivi punde, Afcon 2023: Morocco 3 - 0 Tanzania

    Goooooooooal Morocco yajipatia goli la tatu hapa ambalo lililazimika kuchunguzwa na VAR

    Mfungaji wa goli ni Youssef

  6. Afcon 2023: Morocco 2 - 0 Tanzania

    Gooooal

    Morocco yapata bao jingine kupitia Ounahi

  7. Habari za hivi punde, Mchezaji wa Tanzania Novatus Miroshi apigwa kadi nyekundu hapa kwa kucheza visivyo

    Wachezaji wa Tanzania wabakia 10 uwanjani baada ya Novatus Miroshi kupigwa kadi nyekundu dakika ya 72

  8. Afcon 2023: Msuva na Samatta waongoza safu ya mashambulizi ya Tanzania

  9. Afcon 2023: Tanzania 0- 1 Morocco

    Dakika 56

  10. Afcon 2023: Tanzania yajipatia kona

    Tanzania yajaribu kufanya mashambulizi kutoka mbali . Wapata kona

  11. Afcon 2023: Kipindi cha pili kinaanza

    Tanzania yafanya mabadiliko Mudathiri Yahya atolewa huku Morice Abraham akiingizwa

  12. Afcon 2023: Morocco 1 - 0 Tanzania

    Hadi kufikia kipindi cha mapumziko, Morocco imeshambulia mara 8 huku Tanzania ikiwa bado haijalijaribu lango la Morocco

  13. Afcon 2023: Romain Saiss mfungaji wa goli la Morocco

    Mchezaji Romain Saiss ndiye mfungaji wa goli la Morocco baada ya kipa wa Tanzania manula kuutema mpira wa adhabu uliopigwa na hakim Ziyech

  14. Afcon 2023: Morocco 1 Tanzania 0

    Kipindi cha kwanza Morocco imetawala mchezo huku wachezaji Ziyech , Hakimi na Romain Saiss wakionesha mchezo wa hali ya juu Mbele ya Tanzania

  15. Afcon 2023: Tanzania 0-1 Morocco

    Dakika 45

    Timu zinaenda kwa mapumziko

  16. Afcon 2023: Tanzania 0-1 Morocco

    Goooooooooal Morocco yapata bao la kwanzaMfungaji bao Romain Saiss

  17. Tanzania vs Morocco: 'Taifa Stars ina wachezaji wenye uzoefu wa mechi za kimataifa' - Waziri Ndumbaro

    Kuelekea mchezo wa Tanzania na Morocco leo Jumatano utakao pigwa saa 2 usiku muda wa Afrika Mashariki.

    Mwandishi wa BBC @frankmavura amefanya mahojiano na Waziri wa Michezo wa Tanzania Damas Ndumbaro ambaye anaelezea maandalizi ya timu na jinsi Serikali ya Tanzania ilivyotoa hamasa kwa wachezaji ili waweze kulipatia Taifa hilo ushindi.

  18. Tanzania vs Moroco: Watanzania wasema Taifa Stars itamudu wapizani wake

    Wakati timu ya taifa ya Tanzania ikijianda na mchezo wao wa kwanza wa hatu ya makundi ya michuanoo ya AFCON huko nchini Ivory Coast baadhi ya mashabiki wa timu ya taifa wamezungumza juu ya mchezo wa huo unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki

  19. Ndege yarejea Japani baada ya mtu ‘mlevi’ kumng'ata muhudumu

    Ndege ya kampuni ya ANA iliyokuwa ikielekea Marekani ililazimika kurejea mjini Tokyo baada ya abiria aliyekuwa amelewa kumng'ata mfanyakazi katikati ya safari.

    Mwanamume huyo, anayeripotiwa kuwa Mmarekani mwenye umri wa miaka 55, alikuwa "amelewa chakari" alipomng'ata mkono mhudumu huyo, na kumjeruhi kidogo, msemaji wa shirika la ndege aliambia AFP.

    Vyombo vya habari vya Japan vilisema mwanamume huyo aliwaambia polisi kuwa alikuwa amekunywa kidonge cha usingizi na hakumbuki kilichotokea.

    Ni matukio ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa matukio ya hivi majuzi yaliyoathiri usafiri wa anga wa Japani.

    Ndege hiyo, ambayo inasemekana ilikuwa na abiria 159, ilikuwa juu ya Bahari ya Pasifiki wakati kisa hicho kilipotokea, na kuwafanya marubani wake kurejea Uwanja wa Ndege wa Haneda mjini Tokyo.

    Ilipotua mtu huyo alikabidhiwa kwa polisi, shirika la ndege lilisema.

    Ni tukio la pili kuathiri ANA katika siku za hivi majuzi - na la tano kuhusisha sekta ya anga ya Japani katika muda wa wiki chache.

    Siku ya Jumamosi, ndege ya ANA nchini Japan irudi ilikotoka baada ya ufa kugunduliwa kwenye dirisha la chumba cha marubani.

    Ufa huo ulionekana kwenye sehemu ya juu kabisa ya tabaka nne za dirisha lililozunguka chumba cha marubani, na hakukuwa na majeraha yoyote kwa mtu yeyote kwenye ndege.

    "Ufa huo haukuwa kitu ambacho kiliathiri udhibiti au shinikizo la ndege," msemaji wa ANA alisema.

    Matukio makubwa zaidi ya hivi majuzi yalitokea Haneda mnamo Januari 2, wakati ndege ya Japan Airlines ilipogongana na ndege ndogo ya walinzi wa pwani.

    Watu wote 379 waliokuwa kwenye ndege hiyo ya abiria walitoroka kabla ya kuwaka moto, lakini watu watano kati ya sita kwenye ndege hiyo ndogo - ambayo ilikuwa ikitoa misaada baada ya tetemeko kubwa la ardhi kupiga katikati mwa Japani - walikufa.

    Siku ya Jumanne, ndege za Korean Air na Cathay Pacific zilikatika mbawa kwenye uwanja wa ndege kwenye kisiwa cha kaskazini mwa Japan cha Hokkaido huku kukiwa na baridi kali. Hakukuwa na majeraha.

    Tukio kama hilo lilitokea Jumapili wakati ndege ya ANA ilipokutana na ndege ya Delta Air Lines katika uwanja wa ndege wa Chicago nchini Marekani, shirika la ndege la Japan liliiambia AFP, pia bila kusababisha majeraha.

  20. Pakistan yalaani shambulizi baya la makombora la Iran katika ardhi yake

    Iran imefanya shambulizi la kombora ambalo linaonekana kulenga vituo vya wanamgambo magharibi mwa Pakistan na kusababisha vifo vya watoto wawili, maafisa wa Islamabad wamesema.

    Operesheni hiyo ilishambulia maeneo mawili ya Balochistan yanayohusishwa na kundi la wanamgambo la Jaish al-Adl, runinga ya taifa ya Iran ilisema. Iran ilishambulia maeneo ya Iraq na Syria mapema wiki hii.

    Maafisa wa Pakistan walisema watoto wawili waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa.

    Islamabad ilisema shambulio hilo "halikuwa halali" na kuonya "madhara makubwa".

    Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian, akizungumza mjini Davos, alisisitiza kuwa hakuna raia wa Pakistani aliyelengwa, isipokuwa wanachama wa Jaish al-Adl.

    Shambulio la hivi punde la anga linakuja wakati hali ya wasiwasi ikiongezeka kote Mashariki ya Kati, huku vita vikiendelea kati ya Israel na kundi la Wapalestina la Hamas huko Gaza.

    Tehran inasema haitaki kujihusisha katika mzozo mkubwa zaidi. Lakini makundi katika kile kinachoitwa "Axis of Resistance", ambayo ni pamoja na wanamgambo wa Houthi nchini Yemen, Hezbollah nchini Lebanon na makundi mbalimbali ya Syria na Iraq, yamekuwa yakifanya mashambulizi dhidi ya Israel na washirika wake ili kuonyesha mshikamano na Wapalestina. Marekani na Uingereza zimeanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya Wahouthi baada ya kushambulia meli za kibiashara.

    China siku ya Jumatano ilizitaka Pakistan na Iran kuonyesha "kujizuia" na "kuepuka vitendo ambavyo vitasababisha kuongezeka kwa mvutano". Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Mao Ning aliongeza kuwa Beijing iliona nchi hizo kama "majirani wa karibu".

    Labda kwa kuumwa na mashambulizi mabaya ya hivi majuzi katika ardhi ya nyumbani, Iran inaonekana kuwa na nia ya kulipiza kisasi kwa wale inaowaona kuwa walihusika.

    Wakati wa mvutano mkubwa wa kikanda, Iran ina nia ya kuonyesha nguvu na kuonyesha kwa wakazi wake kwamba vitendo vya unyanyasaji havitakosa kuadhibiwa.