Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uhamiaji: Rwanda yapinga uamuzi wa mahakama ya Uigereza kwamba ni nchi isiyo salama
Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo, anasema ingawa huu ni uamuzi wa mfumo wa mahakama ya Uingereza, hatukubaliani na kauli hiyo.
Moja kwa moja
Maandamano Ufaransa: Afisa wa polisi ashtakiwa kwa mauaji ya kijana wa miaka 17
Afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuua kijana mwenye umri wa miaka 17 ameshtakiwa kwa mauaji na kuwekwa chini ya ulinzi.
Inakuja baada ya mwendesha mashtaka wa eneo la Nanterre, ambapo kijana huyo alikuwa akiiishi kabla ya kufariki, kusema awali kwamba afisa aliyehusika alikuwa amewekwa rasmi chini ya uchunguzi wa mauaji.
Wakati huo huo polisi wa Ufaransa wamekabiliana na waandamanaji kufuatia maandamano ya kupinga mauaji ya Nahel M.
Zaidi ya watu 6,000 walikuwa wamehudhuria mkesha huo, pamoja na mama yake, katika mji wa Nanterre ulioko magharibi mwa Paris ambako alikulia.
Picha zinazosambazwa mitandaoni zinaonyesha magari yakiungua,vurugu barabarani huku watu wakikimbia kutokana na gesi ya kutoa machozi.
Picha nyingine anamuonyesha muandamanaji akirusha mawe, huku picha zingine zikionekana kuonyesha maafisa wa polisi wakiwa wamejeruhiwa.
Vyombo vya habari vya Ufaransa hapo awali viliripoti kwamba baadhi ya watu ambao walitaka kuhudhuria maandamano hayo walikuwa na hofu ya ghasia zaidi kuzuka.
Mwanamke mmoja aliambia BBC kuwa alienda kwa sababu tukio hilo lilimfanya ahoji ni kwa kiasi gani anaweza kuamini mamlaka.
Uingereza: Serikali kupeleka uamuzi wa Rwanda katika Mahakama ya Juu
Serikali ya Uingereza itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya Rufaa ambao umesema mpango ya kuwapeleka wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda ni kinyume cha sheria, Rishi Sunak amesema.
Majaji wa Mahakama ya Rufaa walisema Rwanda haikutoa ulinzi wa kutosha kuthibitisha kuwa ni "nchi ya tatu salama".
Waziri Mkuu alisema "kimsingi hakubaliani" na uamuzi huo na kuongeza kwamba serikali itaipinga katika Mahakama ya Juu.
Shirika la kutoa msaada lilowasilisha kesi hiyo mahakani limepongeza uamuzi huo.
Msemaji wa Asylum Aid alisema uamuzi huo ni "uthibitisho wa umuhimu wa utawala wa sheria na haki ya msingi".
Lakini Bw Sunak alisema ingawa anaheshimu uamuzi wa mahakama atafanya “chochote kinachohitajika” kuvuza magenge ya wahalifu yanayoendesha vivuko vidogo vya boti.
Alisema: "Ninaamini sana serikali ya Rwanda imetoa uhakikisho unaohitajika ili kuhakikisha hakuna hatari ya kweli kwamba wanaotafuta hifadhi waliohamishwa chini ya sera ya Rwanda watarejeshwa kimakosa katika nchi za tatu - jambo ambalo Bwana Jaji Mkuu anakubaliana nalo.
"Rwanda ni nchi salama. Mahakama Kuu ilikubali. UNHCR wana mpango wao wa wakimbizi wa Libya walioko Rwanda. Sasa tutaomba kibali cha kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu kwa Mahakama ya Juu."
Maelezo zaidi:
Wagner: Picha za setilaiti zaonyesha shughuli katika kambi ya kijeshi huko Belarus
Picha za satelaiti zinaonekana kuonyesha shughuli katika kambi ya kijeshi isiyotumika huko Belarus, huku kukiwa na uvumi kuhusu vikosi vya Wagner kuhamia nchi hiyo.
Picha kutoka tarehe 27 Juni iliyopatikana na BBC Verify, na kuripotiwa kwa mara ya kwanza na Radio Free Europe, inaonyesha kile kinachoweza kuwa mahema au miundo kama hiyo inayoonekana kwenye kambi hiyo.
Picha ya awali iliyopigwa tarehe 19 Juni inaonyesha mashamba ndani ya kambi ya kijeshi kwa kiasi kikubwa yakiwa tupu.
Kundi la Wagner, ambalo linajumuisha mamluki, lilikuwa likipigania Urusi nchini Ukraine hadi mwishoni mwa juma lililopita, wakati lilipofanya uasi.
Kiongozi wake, Yevgeny Prigozhin, baadaye alisitisha mpango wa kwenda Moscow baada ya makubaliano kufikiwa kwa msaada wa kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko.
Baada ya kushindwa kwa uasi, mamlaka ya Urusi ilisema Wagner atapokonywa silaha lakini wanachama wake hawatashtakiwa.
Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema wapiganaji wake wanaweza kujiunga na jeshi la Urusi, kwenda nyumbani au kwenda Belarus.
Kambi inayoonekana kwenye picha za satelaiti iko umbali wa maili 13 (21km) kutoka mji wa Asipovichy - karibu maili 64 kutoka mji mkuu Minsk.
Eneo hilo limeripotiwa katika vyombo vya habari vya Urusi kama sehemu ambayo inaweza kuwahifadhi wapiganaji wa Wagner.
Bwana Lukashenko amejitolea kuwapa makao wapiganaji wa Wagner nchini mwake, ambako inaaminika kuwa Prigozhin amekwenda uhamishoni.
Maelezo zaidi
Nahel M: Kijana aliyepigwa risasi na polisi huko Ufaransa ni nani?
Mauaji ya Nahel M, 17, yamezua ghasia katika miji tofauti nchini Ufaransa ikiwa ni pamoja na mji wa Nanterre magharibi mwa Paris alikokulia.
Mtoto wa pekee aliyelelewa na mama yake, alikuwa akifanya kazi kama mtu wa utoaji pizza na kucheza ligi ya raga.
Elimu yake ilielezwa kuwa ya machafuko. Aliandikishwa katika chuo kimoja huko Suresnes karibu na mahali alipokuwa akiishi, ili kupata mafunzo ya kuwa fundi umeme.
Waliomfahamu walisema alikuwa akipendwa sana huko Nanterre alikoishi na mamake Mounia na inaonekana hakuwahi kumjua babake.
Rekodi yake ya kuhudhuria chuo ilikuwa mbaya. Hakuwa na rekodi ya uhalifu lakini alijulikana na polisi.
Alimpiga busu mama yake kabla ya kwenda kazini, na kumwambia "Nakupenda, Mama".
Muda mfupi baada ya saa tisa asubuhi aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani, kwa kuendesha gari wakati wa ukaguzi wa trafiki wa polisi.
"Nitafanya nini sasa?" aliuliza mama yake. "Nilijitolea kwa hali na mali," alisema.
"Nina mtoto mmoja tu, sina [watoto] 10. Alikuwa kila kitu maishani mwangu, rafiki yangu mkubwa."
Bibi yake alimtaja kama "mvulana mzuri". "Kukataa kutii amri hakukupi leseni ya kuua," kiongozi wa Chama cha Kisoshalisti Olivier Faure alisema. "Watoto wote wa Jamhuri wana haki ya kupata haki."
Mzozo wa Sudan: Kuenea kwa mapigano kwatia 'wasiwasi' Ethiopia
Ethiopia imeelezea kusikitishwa kwake na kuongezeka kwa ghasia nchini Sudan hadi maeneo ya nje ya mji mkuu Khartoum haswa katika jimbo la Kordofan huku wakimbizi wakiendelea kuvuka mipaka yake kwa wingi.
Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia, Meles Alem, alielezea mapigano kati ya kundi lenye silaha la SPLM-Kaskazini na vikosi vya serikali ya Sudan katika jimbo hilo kuwa "ya kutia wasiwasi."
"Mgogoro nchini Sudan unaharibu sio tu Khartoum lakini unaenea zaidi ya Khartoum - unaenea hadi Darfur na Kordofan kufuatia mzozo kati ya SPLM-N inayoongozwa na Abdulaziz al-Hilu na vikosi vya serikali ya Sudan.
Ethiopia inapokea wakimbizi,” Bw. Meles amesema Alhamisi. Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 50,000 wamevuka mipaka na kuingia Ethiopia tangu mzozo huo uanze mwezi Aprili kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF).
Mapigano tangu wakati huo yameenea katika maeneo ya Darfur magharibi ambako mapigano yamebadilika na kuwa ghasia za kikabila.
Wiki iliyopita, jeshi lilishutumu SPLM-Kaskazini, kundi lenye nguvu la waasi lenye mafungamano katika nchi jirani ya Sudan Kusini na ambalo linadhibiti maeneo katika jimbo la Kordofan Kusini, kwa kuanzisha mashambulizi.
Huku mvutano ukiongezeka karibu na mji mkuu wa jimbo la Kadugli wengi wamekimbia jimbo hilo. Ghasia pia zimeripotiwa katika jimbo la Blue Nile linalopakana na Ethiopia.
Umoja wa Mataifa ulisema ghasia za hivi majuzi katika eneo la Kurmuk katika Mkoa wa Blue Nile ziliwahusu sana.
Wakati huo huo Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) inasema imewezesha kuachiliwa kwa wanajeshi 125 wa Sudan wanaoshikiliwa na Kikosi cha RSF.
ICRC ilisema wanajeshi hao - wengi wao wakiwa wamejeruhiwa - walichukuliwa kwa basi kutoka mji mkuu, Khartoum, hadi mji wa Wad Madani kuelekea kusini.
Vita kati ya jeshi la Sudan na RSF vimesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu, na kusababisha karibu watu milioni tatu kuyahama makazi yao.
Rwanda yapinga uamuzi kwamba ni nchi isiyo salama
Serikali ya Rwanda inatofautiana na uamuzi wa mahakama ya Uingereza kwamba nchi hiyo si salama kwa wanaotafuta hifadhi na wakimbizi. Yolande Makolo, msemaji wa serikali ya Rwanda, alisema:
Habari za hivi punde, Uingereza: Mpango wa kupeleka waomba hifadhi nchini Rwanda ulikuwa kinyume cha sheria- Mahakama
Mahakama ya Rufaa nchini Uingereza imebatilisha uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu mpango wa serikali kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda ikisema mpango huo ni kinyume cha sheria hadi pale mabadiliko yatakapofanywa kwenye mfumo wa hifadhi huko.
Mapema wiki hii, Ofisi ya Mambo ya Ndani ilichapisha tathmini ya athari za kiuchumi ya Mswada wa Serikali wa Uhamiaji Haramu - ikiwa ni pamoja na mpango wa Rwanda.
Ilikadiria kuwa kupeleka mhamiaji katika "nchi salama" kama vile Rwanda kunaweza kugharimu pauni 63,000 zaidi ya kuwaweka nchini Uingereza.
Tulifikaje hapa?
Aprili 2022: Serikali ya Uingereza yatangaza mpango wa kuwapeleka baadhi ya waomba hifadhi nchini Rwanda, ili kuzuia watu kuingia nchini humo kwa kutumia boti ndogo kutoka Ufaransa.
Juni 2022: Ndege ya kwanza iliyobeba waomba hifadhi kutoka Uingereza hadi Rwanda iliahirisha safari dakika chache kabla ya kupaa baada ya Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu kuingilia kati.
Desemba 2022: Mahakama Kuu ilitoa uamuzi kwamba mpango huo ni halali - lakini inasema kesi za watu wanane wanaotafuta hifadhi waliyojumuishwa kwenye ndege ya Juni "hazijazingatiwa ipasavyo"
Januari 2023: Wahamiaji wanaokabiliwa na uwezekano wa kuondolewa kwenda Rwanda wapata kibali cha kupinga sera hiyo katika Mahakama ya Rufaa
Aprili 2023: Mahakama ya rufaa yabatilisha uamuzi wa awali wa Mahakama Kuu.
Maelezo zaidi:
Je Moises Caicedo anaelekea wapi?
Kiungo wa kati wa Brighton Moises Caicedo amesababisha ushindani mkali kutoka timu tatu ikiwemo Chelsea, Manchester United na Arsenal – Lakini yeye mwenyewe ameamua kujiunga na timu gani ?
Sky Sports inaripoti kwamba Caicedo anawindwa sana na mkufunzi wa United Erik Ten Hag.
Mchezaji huyo wa Ecuador aliombwa kununuliwana Arsenal wmezi Januari , lakini dau la pauni milioni 70 lilikataliwa.
Huku Arsenal sasa wakikaribia kumsajili Declan Rice kwa ada ya £105m, inazua swali iwapo wataweza kuwanunua Havertz, Rice na Caicedo wote katika dirisha moja.
Pia unaweza kusoma:
- Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 29.06.23
- Haaland, Bellingham, Vinicius, Mbappe: Nani atashinda taji la Ballon d'Or 2024?
- Kwanini ligi ya Tanzania bara inakua kwa kasi?
Morocco yamrudisha nyumbani balozi wake Uswidi baada ya uchomaji wa Kuran
Morocco imemrudisha nyumbani balozi wake nchini Uswidi kufuatia kuchomwa kwa Koran kwenye maandamano mjini Stockholm.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni mjini Rabat ilikitaja kitendo hicho kuwa cha kuudhi na kutowajibika katika wakati ambapo Waislamu walikuwa wakisherehekea mojawapo ya siku takatifu zaidi katika kalenda yao.
Mratibu wa maandamano hayo - ambaye anasemekana kuwa mzaliwa wa Iraq Salwan Momik - anachunguzwa kwa uchochezi wa chuki.
Mahakama ya Uswidi ilikuwa imeamua maandamano hayo yaruhusiwe kuendelea kwa misingi ya uhuru wa kujieleza.
James Maddison: Tottenham wakamilisha mkataba wa dau la £40m
Tottenham wamemsajili kiungo wa kati wa Uingereza James Maddison kwa mkataba wa miaka mitano kwa £40m kutoka Leicester City.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameichezea England mechi tatu na kusaidia Foxes kutwaa Kombe la FA kwa mara ya kwanza katika historia yao mnamo 2021.
Alicheza mechi 203 kwa Leicester baada ya kujiunga kutoka Norwich mwaka 2018 kwa ada ya karibu £20m.
Maddison alifunga mabao 10 ya Premier League msimu uliopita lakini hakuweza kuizuia klabu hiyo kushuka daraja.
Pia unaweza kusoma:
- Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 29.06.23
- Haaland, Bellingham, Vinicius, Mbappe: Nani atashinda taji la Ballon d'Or 2024?
- Kwanini ligi ya Tanzania bara inakua kwa kasi?
Aliyekuwa polisi wa Rwanda ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mauaji ya halaiki
Mahakama nchini Ufaransa imemhukumu kifungo cha maisha jela aliyekuwa afisa wa polisi wa Rwanda, baada ya kumpata na hatia ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.
Uhalifu wa Philippe Hategekimana ulifanyika wakati wa mauaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994, wakati wanamgambo wa Kihutu walipoua mamia ya maelfu ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani.
Waendesha mashtaka walimweleza kuwa alikuwa na sehemu kuu katika kutekeleza mauaji hayo, sio tu kuua watu lakini pia kuwachochea wengine kufanya hivyo.
Hategekimana, ambaye alifanya kazi kama jenda mkuu huko Nyanza, mji ulioko kusini mwa nchi hiyo, alikimbilia Ufaransa baada ya mauaji ya kimbari.
Alipata hifadhi ya ukimbizi na utaifa wa Ufaransa chini ya jina la Philippe Manier.
Alifanya kazi kama mlinzi wa chuo kikuu nchini Ufaransa na alikimbilia Cameroon mnamo 2017 aliposikia malalamiko yamewasilishwa dhidi yake, AFP inaripoti. Alikamatwa Yaoundé na kurejeshwa Ufaransa mwaka uliofuata ili kushtakiwa.
Ilikuwa ni kesi ya tano ya aina hiyo nchini Ufaransa kwa mshukiwa mshiriki katika mauaji ya halaiki.
Mauaji ya takriban Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani yalifanyika kwa muda wa siku 100 mwaka 1994.
Maelezo zaidi:
- Mauaji ya Kimbari Rwanda: Jinsi mauaji yalivyozaa mapenzi
- Rwanda: Manusura wa mauaji ya kimbari wanaoishi nyumba moja na 'waliotekeleza mauaji'
- Mauaji ya kimbari Rwanda:Jinsi picha iliyomuita ‘muuaji’ ilivyoharibu maisha yake na familia yake
Kramatorsk: Jasusi wa Urusi kushtakiwa kwa shambulio baya
Rais wa Ukrain Volodymyr Zelensky anasema kuwa ajenti wa Urusi anayedaiwa kuhusika katika shambulio baya huko Kramatorsk atashtakiwa kwa uhaini.
Wale wanaoisaidia Urusi kuharibu maisha wanastahili "adhabu ya juu zaidi", alisema.
Watu 12, wakiwemo vijana watatu, waliuawa katika shambulio la kombora la Jumanne kwenye mkahawa mmoja maarufu.
Ukraine ilisema mwanamume huyo, mkazi wa Kramatorsk, alituma picha za video za mgahawa huo kwa jeshi la Urusi saa chache kabla haujaharibiwa.
Dada mapacha wenye umri wa miaka 14 Yuliya na Anna Aksenchenko na msichana wa miaka 17 walikuwa miongoni mwa waliouawa.
"Makombora ya Urusi yalisimamisha kupiga kwa mioyo ya malaika wawili," idara ya elimu ya halmashauri ya jiji la Kramatorsk ilisema katika taarifa.
Takriban watu wengine 60 walijeruhiwa, wakiwemo raia wa Colombia na mwandishi mkuu wa Ukraine`.
Siku ya Jumatano, maafisa wa usalama wa Ukraine walitoa picha ya mwanamume wa eneo hilo ambayo walimkamata, wakimuelezea kama wakala wa Urusi.
Akizungumza katika hotuba yake ya usiku, Bw Zelensky alieleza kuwa idara za usalama nchini humo zilifanya kazi pamoja na vikosi maalum vya polisi kumzuilia mshukiwa huyo ambaye huenda akafungwa jela maisha.
Huduma za dharura zilisema Jumatano kwamba juhudi za utafutaji na uokoaji bado zinaendelea.
Kramatorsk, mji wa mashariki katika eneo la Donetsk, uko chini ya udhibiti wa Ukraine lakini uko karibu na maeneo yanayokaliwa na Warusi nchini humo.
Mwezi Aprili mwaka jana, zaidi ya watu 50 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulio la kombora kwenye kituo cha treni mjini humo.
Sebule ya Ria, ambayo ililengwa wakati huu, ilikuwa ukumbi maarufu unaowakaribisha mara kwa mara waandishi wa habari wa kimataifa, watu waliojitolea na wanajeshi wa Ukraine waliokuwa wakipumzika kutoka mstari wa mbele.
Soma:
- Mkuu wa Wagner aliyegeuka kuwa muasi
- Ndege ya Urusi ya II-22 iliodunguliwa na Wagner: Kipi cha kipekee kuihusu?
- Vita vya Ukraine: Urusi iliitumiaje Belarus katika vita?
Madonna aahirisha ziara baada ya kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi
Mwanamuziki Madonna ameahirisha ziara yake ya kimataifa baada ya kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) akiwa na maambukizi makali ya bakteria.
Kulingana na meneja wake, maambukizi ya mwanamuziki huyo wa kimataifa yalikuwa "mabaya" na yalisababisha "kukaa kwa siku kadhaa katika chumba cha ICU". Aliongeza kuwa afueni kamili inatarajiwa.
Katika taarifa yake, Guy Oseary alisema afya ya Madonna inaendelea kuimarika, lakini bado yuko chini ya uangalizi wa kimatibabu. Madonna anaaminika kupokea matibabu katika hospitali moja huko New York City, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.
Mwanamuziki huyo nyota wa pop alitarajia kusherehekea kumbukumbu ya miaka 40 ya wimbo wake mpya, Holiday, kwa kuanza ziara yake ya kwanza ya vibao bora zaidi. Ziara iliyopewa jina la ‘Celebration Tour’, ingekuwa ni kurejea kwa mwimbaji huyo baada ya maonyesho yake ya majaribio ya Madame X mnamo 2019 na 2020.
Baadhi ya maonyesho hayo yalisitishwa kwa sababu ya majeraha ya goti na nyonga. "Samahani ilibidi niahirishe usiku wa leo," nyota huyo aliandika kwenye Instagram baada ya kughairi onyesho la 2020 huko Lisbon, "lakini lazima nijisikize mwili wangu na kupumzika!" Ziara ya hivi punde zaidi ya Madonna ilipaswa kuanza Vancouver, Canada, tarehe 15 Julai na kumalizika tarehe 30 Januari huko Mexico City.
Lakini meneja wa mwimbaji-mtunzi huyo wa nyimbo alisema Madonna alipata "maambukizi makubwa ya bakteria" Jumamosi 24 Juni na matokeo yake, ahadi zote zitahitaji kusitishwa. Alitarajiwa kuanza ziara yake huko Uingereza na Ulaya kidogo tarehe 14 Oktoba, iliyopangwa kuanza na kumalizika huko O2 Arena, London.
Ufaransa: 77 wakamatwa katika maandamano ya ghasia baada ya polisi kumuua kijana mmoja
Takriban watu 77 wamekamatwa nchini Ufaransa wakati wa usiku wa pili wa machafuko yaliyosababishwa na tukio la dereva wa miaka 17 kupigwa risasi na polisi.
Kijana huyo, aliyetambulika kwa kija la Nahel M, alipigwa risasi katika eneo lililowazi kabisa baada ya kukataa kusimama kwenye taa za barabarani na kuondoka.
Video zilizoshirikishwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha magari yakichomwa moto na maduka yakiporwa siku ya Jumatano.
Huko Nanterre, kitongoji cha Nahel alikotoka, polisi walilazimika kujiondoa kwa kiasi, Le Monde iliripoti. Waandamanaji kote Paris walionekana wakilenga vituo vya polisi kwa fataki.
Waandamanaji pia walikabiliana na polisi katika mji wa kaskazini wa Lille. Picha zilizochapishwa mtandaoni zilionyesha watu ndani ya ukumbi wa mji wa kitongoji cha Mons-en-Barœul wakichoma moto hati na viti.
Katika mji wa magharibi wa Rennes, takriban watu 300 walikusanyika kutoa heshima kwa kijana huyo - ambao baadhi yao pia waliwasha moto na kutawanywa na polisi. Siku ya Jumanne, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kupigwa risasi kwa Nahel "hakuwezi kusamehewa".
Lakini maoni yake yaliibua hasira kutoka kwa vyama vya polisi, ambavyo vilimshutumu kwa kukimbilia kuwahukumu maafisa waliohusika. Muungano wa Polisi wa Alliance ulitaka wachukuliwe kuwa hawana hatia hadi wapatikane na hatia, huku wapinzani wa Unité SGP Police pia wakizungumzia uingiliaji kati wa kisiasa ambao ulihimiza "chuki dhidi ya askari".
Waziri wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin alisema atachukua hatua za kisheria dhidi ya kundi jingine, Polisi wa Ufaransa, baada ya kuchapisha kile alichokiita "tweet isiyokubalika na ya kutisha" ikitaka kuhalalisha mauaji ya kijana huyo.
Ujumbe wa Twitter ambao sasa umefutwa uliandikwa "bravo" kwa maafisa ambao "walimfyatulia risasi mhalifu mwenye umri mdogo" na kuwalaumu wazazi wa kijana huyo kwa kifo chake, wakidai "wameshindwa kumsomesha mtoto wao".
Natumai Hujambo siku ambayo Waislamu wanasherehekea Siku Kuu ya Eid Ul Adhaa