Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marekani yaishutumu Afrika Kusini kwa kuipatia silaha Urusi
Marekani imeishutumu Afrika Kusini kwa kusambaza silaha na risasi kwa Urusi Disemba mwaka jana.
Moja kwa moja
Afrika kusini yaijibu Marekani kuhusu madai ya kuisambazia silaha Urusi
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amejibu madai ya Marekani ya kuishtumu nchi yake kuwa ilitoa silaha kwa Urusi licha ya msimamo wake kwamba haiegemei upande wowote katika vita vya Ukraine.
Rais Ramaphosa alisema serikali yake inachunguza madai hayo.
Nchi hiyo imedumisha madai ya kutoegemea upande wowote katika uvamizi wa Ukraine.
Mamlaka ya Afrika Kusini ilikanusha kuwa ushirikiano wa mazoezi ya kijeshi uliwekwa ili kuendana na kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kuanza kwa vita na kusema kuwa nchi hiyo mara kwa mara huwa na mazoezi kama hayo na mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na Ufaransa na Marekani.
Awali Afrika Kusini haikupiga kura ya Umoja wa Mataifa kulaani uvamizi huo.
Pia ilikataa kuungana na Marekani na Ulaya katika kuiwekea Urusi vikwazo.
Akijibu swali lililoulizwa na kiongozi wa upinzani John Steenhuisen, Bw Ramaphosa aliambia bunge Alhamisi kwamba maoni yaliyotolewa na balozi wa Marekani yataangaliwa.
Rais alivitaka vyama vya upinzani kuruhusu mchakato huo ukamilike.
Bw Brigety alisema katika kikao na wanahabari mjini Pretoria siku ya Alhamisi kuwa "anaamini" kwamba meli ya Urusi ilikuwa imesheheni risasi na silaha mjini Cape Town Desemba mwaka jana "ilipokuwa ikirejea Urusi".
Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani bado haijatoa maoni yoyote kuhusu madai hayo.
Soma zaidi:
Sanna Marin: Waziri Mkuu wa Ufini atalikiana na mumewe anapojiandaa kuondoka ofisini
Waziri Mkuu anayemaliza muda wake wa Finland Sanna Marin na mumewe Markus Raikkonen wamewasilisha maombi ya talaka.
"Tunashukuru kwa miaka 19 pamoja na binti yetu mpendwa," Bi Marin alisema kwenye Instagram Jumatano.
Wenzi hao walioa mnamo 2020, wakati Bi Marin alipokuwa akiongoza nchi hiyo katika kukabiliana na janga la corona, na wamejaaliwa kuwa na binti wa miaka mitano pamoja.
Anatazamiwa kuondoka ofisini baada ya chama chake cha mrengo wa kati kushindwa katika uchaguzi mkuu mwezi uliopita.
Katika hadithi iliyotumwa kwenye akaunti yake ya Instagram, Bi Marin alisema "bado ni marafiki wakubwa" na Bw Raikkonen, ambaye ni mfanyabiashara na mwanasoka wa zamani wa kulipwa.
"Tutaendelea kutumia wakati pamoja kama familia kati yetu," aliongeza.
Bi Marin, 37, alikua waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi duniani alipoingia madarakani mwaka wa 2019.
Lakini alishindwa katika kinyang'anyiro kikali cha Chama cha Kitaifa cha Muungano, kilichoongozwa na Petteri Orpo, na chama cha mrengo wa kulia cha Finns Party, kinachoongozwa na Riikka Purra, mwezi Aprili.
Ilikuwa ni kushindwa vibaya kwa Bi Marin. Wakati aliongeza viti vya chama chake na kupata 19.9% ya kura, washirika wake wa muungano wote walipoteza idadi kubwa ya viti.
Serikali yake imejiuzulu rasmi lakini itaendelea kuhudumu kwa muda hadi pale itakapoundwa na kuteuliwa serikali mpya.
Bw Orpo amesema anatumai kuhitimisha mazungumzo ifikapo Juni.
Afrika Kusini ilitoa silaha kwa Urusi - Marekani
Marekani imeishutumu Afrika Kusini kwa kusambaza silaha na risasi kwa Urusi Disemba mwaka jana, licha ya madai yake kwamba haiegemei upande wowote katika vita vinavyoendelea dhidi ya Urusi nchini Ukraine, magazeti ya Afrika Kusini yanaripoti.
Katika maelezo mafupi kwa waandishi wa habari wa Afrika Kusini, balozi wa Marekani mjini Pretoria Reuben Brigety alisema silaha hizo zilipakiwa kwenye meli ya Urusi iliyokuwa imetia nanga katika kituo cha jeshi la majini huko Simon's Town.
"Miongoni mwa mambo tuliyoyabaini ni pamoja na kupandishwa kwa meli ya mizigo katika kambi ya jeshi la majini ya Simon's Town kati ya tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2022, ambayo tuna uhakika ilipakia silaha na risasi kwenye meli hiyo huko Simon's Town ilipokuwa ikirejea Urusi. " balozi huyo alinukuliwa na tovuti ya News24 ya Afrika Kusini akisema.
Alipoulizwa jinsi taarifa za kijasusi za Marekani zilivyokuwa sahihi kwamba Afrika Kusini ilisambaza risasi kwa Urusi, Bw Brigety alisema angeweka dau maisha yake juu yake, kulingana na News24.
Tovuti ya habari ya TimesLive ilimnukuu Bw Brigety akisema itakuwa "kosa kudharau wasiwasi uliopo Washington".
Afrika Kusini bado haijatoa maoni yoyote.
Pia unaweza kusoma:
Uingereza yathibitisha kuwasilisha makombora ya Storm Shadow Ukraine
Uingereza yathibitisha kuwasilisha makombora ya Storm Shadow kwa Ukraine
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace amethibitisha kuhamishiwa hadi Kyiv kwa makombora ya Storm Shadow, ambayo yanawakilisha uwezekano mpya wa Ukraine wa kushambulia kwa masafa marefu.
Akizungumza na wajumbe wa Bunge la Uingereza siku ya Alhamisi, Wallace aliitaja hatua hiyo kuwa kipimo na jibu sawia kwa kuongezeka kwa mashambulizi ya Urusi.
"Matumizi ya makombora ya Storm Shadow yataruhusu Ukraine kurudisha nyuma vikosi vya Urusi kutoka eneo huru la Ukraine," Wallace alisema, akizungumza bungeni.
"Hatutatazama tu huku Urusi ikiua raia," aliongeza waziri huyo. "Urusi lazima itambue kuwa ni hatua zake tu ndizo zilizosababisha ukweli kwamba mifumo kama hiyo ilitolewa kwa Ukraine."
Storm Shadow ni kombora la kusafiri kwa ndege lililotengenezwa kwa pamoja na Uingereza na Ufaransa.
Safu ya kurusha ni zaidi ya kilomita 250, ambayo inazidi kwa kiasi kikubwa umbali wa kusafiri kwa makombora ambayo washirika wa Magharibi wa Ukraine wametoa hadi sasa.
Pia unaweza kusoma:
Israel yamuua kwa kombora Kamanda wa PIJ huko Gaza
Jeshi la Israel limemuua mkuu wa kikosi cha makombora ya roketi cha Palestina Islamic Jihad (PIJ) katika shambulio la anga kabla ya alfajiri kwenye ghorofa moja huko Gaza.
Watu wengine wawili, ambao jeshi lilisema pia walikuwa wanamgambo, walikufa katika shambulio hilo katika mji wa kusini wa Khan Younis.
Ving'ora baadaye vilisikika kusini mwa Israel huku maroketi na makombora yakendelea kurushwa Gaza. Hakuna majeruhi walioripotiwa.
Siku ya Jumatano, wanamgambo walirusha makombora 507 dhidi ya Israeli na Israeli ikarusha 158 dhidi ya PIJ huko Gaza. Watu 25 wameuawa na 76 kujeruhiwa huko Gaza tangu Jumanne asubuhi, wakati Israeli ilipoanza operesheni yake dhidi ya PIJ kwa mfululizo wa mashambulizi yaliyoua makamanda wake wengine watatu, maafisa wa afya huko wanasema.
Takriban raia 10 pia ni miongoni mwa waliofariki, jambo ambalo Umoja wa Mataifa umelitaja kuwa halikubaliki.
Wakenya wamsifu mwalimu aliyeshona nguo ya mwanafunzi iliyochanika
Mwalimu anayeonekana kwenye picha iliyosambazwa sana akishona nguo ya mwanafunzi iliyochanika katika shule moja nchini Kenya amepata sifa na kupongezwa kwa kitendo chake cha fadhili.
Joyce Malit anaonekana kwenye picha akishona nguo hiyo huku mwanafunzi mwenye umri wa miaka minane akisimama kando yake, akiwa amefunikwa kwa kitambaa.
Aliambia vyombo vya habari vya ndani kwamba nguo ya msichana huyo ilikuwa imechanwa na msumari kwenye meza yake, na kufichua vazi lake la ndani.
Mwalimu mwenzake katika shule hiyo katika kaunti ya Narok alimpa msichana huyo kitambaa cha kujifunika huku Bi Malit akishona nguo hiyo kwa kutumia sindano ambayo aliibeba kila mara.
Alisema picha hiyo, ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii wiki hii, ilipigwa tarehe 7 Machi na mfanyakazi mwenza.
Alisema amepokea simu nyingi kutoka kwa watu wakimsifu.
Aliambia tovuti ya habari ya Nation kwamba alikuwa na uhusiano maalum na msichana huyo, ambaye anatoka katika malezi duni na anaishi na babu na babu yake.
“Ni msichana mwerevu. Tangu siku hiyo, yeye ni rafiki yangu mkubwa. Asubuhi hii aliniletea ua kama ishara ya shukrani, alinitoa machozi,” alisema.
Habari za hivi punde, Mwanaume akamatwa kwa kumiliki kichwa na sehemu za siri za kiume
Mwanaume mmoja amekamatwa katika jimbo la kati la Sofala nchini Msumbiji kwa kumiliki kichwa na sehemu za siri za mwanaume, polisi wamesema.
Watoto waligundua sehemu za miili hiyo kwenye mfuko wa plastiki katika wilaya ya Nhamatanda na kutoa taarifa kwa mamlaka, alisema Dércio Chacate, msemaji wa kamandi ya polisi ya Sofala.
Uchunguzi ulipelekea kukamatwa kwa mtu huyo ambaye alikiri kumuua mtu kisha kumkata kichwa na sehemu zake za siri ili aweze kuziuza, alisema.
Mshukiwa alikiri kuua na kukata vichwa vya watu wengine watatu, Bw Chacate alisema.
Uchunguzi ulikuwa ukiendelea ili kuwakamata wanaodaiwa kuwa wapangaji na wanunuzi.
Viungo vya mwili hutumiwa na baadhi ya wanaoitwa madaktari wa jadi kutengeneza dawa, ambazo kwa uwongo wanadai zinaweza kutibu magonjwa, kuondoa dalili mbaya na kuboresha maisha ya watu.
'Yesu wa Tongaren' kuchunguzwa zaidi juu ya mafundisho yake
Eliud Wekesa almaarufu ‘Yesu wa Tongaren’ ameagizwa kurejea katika kituo cha polisi cha Bungoma kwa siku ya pili huku maafisa wa upelelezi wakitafuta kuibua makosa yoyote yanayohusiana na wizara yake.
Kwa mujibu wa gazeti la The Standard nchini Kenya , Francis Kooli, mkuu wa polisi wa Bungoma, alisema uchunguzi kuhusu Wekesa utaendelea baada ya kukaa na wapelelezi siku ya Jumatano ambao walichunguza imani yake, mafundisho yake na mabadiliko ya jina lake. Wito wa Wekesa unajiri mwezi mmoja tu baada ya kisa cha Shakahola katika Kaunti ya Kilifi ambapo familia nyingi zimepoteza wapendwa wao kutokana na imani za kidini.
Akihutubia wanahabari katika makao makuu ya DCI mjini Bungoma Jumatano, Wekesa alijitenga na madai kuwa yeye ni kiongozi bandia wa kiroho.
"Tangu nilipoanzisha kanisa hili, sijawahi kuwa na tatizo na mtu yeyote lakini tangu tukio la Shakahola litokee watu walianza kuhoji kuhusu kanisa langu la Yerusalemu Mpya," alisema.
Wekesa alianza huduma yake miaka 12 iliyopita. Alionyesha imani kwamba angethibitishwa mwishowe kuwa hakuvunja sheria yoyote.
Tisa wafariki, 80 walazwa hospitali kutokana na mlipuko wa ugonjwa usiyojulikana kaskazini mwa Kenya
Watu tisa wamefariki na wengine zaidi ya 80 kulazwa hospitalini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa usiojulikana katika kaunti ya Marsabit kaskazini mwa Kenya.
Msimamizi wa eneo hilo alisema kati ya watu tisa ambao wamekufa, sita walikuwa watu wazima na watoto watatu kati ya mwaka mmoja na mitatu.
Wengi wa watu walioathiriwa walionyesha dalili kama za mafua, macho ya manjano, wengu kuvimba na maumivu makali ya kichwa, vyombo vya habari vya nchini humo vinaripoti.
Baadhi ya wagonjwa wamepatikana na kuwa na malaria lakini madaktari wanasema huenda ni leishmaniasis ya visceral-pia inajulikana kama ugonjwa wa kala-azar .
Mlipuko huo unajiri miezi miwili baada ya Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu nchini Kenya kugundua mbu washambuliaji katika maeneo ya Laisamis na Saku kaunti ya Marsabit.
Ethiopia yatoa leseni ya huduma ya mpesa kwa kampuni Safaricom ya Kenya
Ethiopia imeipatia kampuni kubwa ya mawasiliano ya Safaricom leseni ya kuendesha huduma za pesa kwa simu, kuifanya kuwa kampuni ya kwanza ya kigeni kupata kibali kama hicho katika taifa hilo lenye watu wengi.
Safaricom ilizinduliwa mwezi Agosti mwaka jana shughuli zake nchini Ethiopia, ambayo kwa miaka mingi imekuwa mojawapo ya soko kubwa lililofungwa katika bara la Afrika.
Kampuni ya simu ya Ethio inayomilikiwa na serikali ilikuwa mtoa huduma pekee wa huduma za mawasiliano ya simu na kutum ana kupokea pesa kwa njia ya simu katika nchi yenye zaidi ya watu milioni 110.
Lakini Addis Ababa ilifungua soko lake mwaka 2021 kwa wazabuni wa kimataifa, na kuupa muungano unaoongozwa na Safaricom leseni ya kufanya kazi nchini humo.
Siku ya Alhamisi, Benki ya Kitaifa ya Ethiopia (NBE) ilisema katika taarifa kwamba utoaji wa leseni ya mpesa uliakisi malengo yake yanayoendelea ya "kukuza uvumbuzi wa kifedha na kujumuishwa katika soko la Ethiopia".
Afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa alisema kampuni hiyo itasambaza huduma za kifedha kwa njia ya simu nchini kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Ethiopia imeshuhudia ukuaji mkubwa wa huduma za pesa kwa simu katika miezi ya hivi karibuni.
Wiki mbili zilizopita, mamlaka ilianzisha huduma ya pesa kwa njia ya simu kuwa njia pekee ya malipo katika vituo vya mafuta na taasisi za kifedha za serikali kwa nia ya kuwavuta watu kwenye malipo ya kidijitali.
Umoja wa Mataifa kufanya kikao cha dharura kuhusu Sudan
Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa leo litafanya kikao cha dharura mjini Geneva siku ya Alhamisi, kujadili mzozo unaoendelea nchini Sudan.
Kuna ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya raia, unyanyasaji wa kijinsia na uporaji wa hospitali.
Maelfu ya watu wamekimbia makazi yao na mashirika ya misaada yanasema hayawezi kufanya kazi kwa usalama.
Mataifa kadhaa ya Afrika, ikiwemo Sudan, yanaripotiwa kusitasita kuhusu mkutano huo unaofanyika, wakihofia kuwa unaweza kuhatarisha mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha mapigano.
Kikao hicho kiliitishwa na Uingereza, Marekani, Ujerumani na Norway.
Kaliningrad: Ghadhabu kuhusu hatua ya Poland kupendekeza kubadilisha jina la eneo lake la zamani
Urusi imejibu kwa hasira baada ya bodi simamizi ya nchi ya Poland kushauri kutumia jina tofauti kutambulisha eneo maalum lenye jina la kirusi la Kaliningrad katika pwani ya Bahari ya Baltic.
Kamati ya Poland ilisema kuwa jiji na eneo pana linapaswa kuitwa Królewiec kwani lilikuwa jina la kitamaduni la eneo hilo. Aidha ilisema kuwa, uamuzi wa kutotumia tena "jina lililowekwa" ulikuwa ni matokeo ya Urusi kuivamia Ukraine.
Nayo Urusi ilijibu na kusema uamuzi huo "unapakana vitendo vya wazimu" "na cha uadui".
"Tunajua kwamba katika historia, Poland imejihusisha mara kwa mara katika hatua hizi za chuki dhidi ya Warusi," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema.
Kwa mamia ya miaka kabla ya Vita vya Pili vya Dunia, eneo hilo lilijulikana kama Königsberg na lilikuwa sehemu ya Prussia Mashariki. Królewiec ni tafsiri ya Kipolandi yaani Königsberg.
lakini, baada ya Vita vya pili vya dunia vya dunia, jiji na eneo hilo lote liliwekwa chini ya usimamizi wa Soviet. Wanasovieti walipatia jina Kaliningrad kwa heshima ya Mikhail Kalinin, mmoja wa viongozi wa mapinduzi ya Bolshevik.
Baada ya Umoja wa Kisovieti kuporomoka, Kaliningrad ikawa sehemu ya eneo la Urusi, na kuifanya kuwa eneo ambalo limetenganishwa kijiografia na eneo kuu la nchi - lililo kati ya nchi za Poland na Lithuania.
Kaliningrad ni muhimu kimkakati kwa Moscow kwa sababu inamiliki Meli ya Baltic ya Urusi kwenye bandari ya Baltiysk na ni mojawapo ya bandari za Uropa zisizo na barafu nchini Urusi.
Siku ya Jumanne, Kamati ya Poland ya Kudhibiti Majina ya Kijiografia Nje ya Jamhuri ya Poland ilisema ilikuwa inapendekeza mara moja kwamba jiji hilo lijulikane nchini Poland kama Królewiec na eneo pana la eneo hilo kama Obwód Królewiecki.
Israel yamuua kamanda wa kundi wa Islamic Jihad huko Gaza
Shambulio la anga la Israel la mapema alfajiri limemuua kamanda mkuu wa kundi la Islamic Jihad (PIJ) na wanamgambo wengine wawili mjini Gaza.
Ndege ya kivita ilishambulia ghorofa ya tano ya jengo la makazi la Hamad , karibu na Khan Younis kusini mwa eneo hilo.
Siku ya Jumatano wanamgambo huko Gaza walirusha zaidi ya makombora 460 dhidi ya Israel.
Jeshi la Israel lilishambulia zaidi ya wapiganaji 130 huko Gaza, katika mapigano makali zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miezi tisa.
Watu 25 wameuawa huko Gaza tangu Jumanne asubuhi wakati Israeli ilipoanza operesheni yake dhidi ya PIJ, Wizara ya Afya ya Palestina huko inasema.
Waliouawa ni pamoja na raia wasiopungua 10 na makamanda wengine watatu wa PIJ.
Jeshi la Israel lilisema watu wanne, wakiwemo watoto watatu, wameuawa huko Gaza kwa roketi zilizoanguka, ingawa hii haijathibitishwa na vyanzo vya Palestina.
Tanzania yafungua kituo cha upandikizaji wa Uloto,
Tanzania imefungua kituo chake cha kwanza cha kupandikiza uloto(bone marrow) katika mji mkuu, Dodoma.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, ni hatua muhimu kwa sekta ya afya nchini na kitengo hicho kitajikita katika kuwatibu wagonjwa wa seli mundu.
Ni nchi chache sana barani Afrika zinazotoa upandikizaji wa uloto ambazo ni Algeria, Misri, Morocco, Afrika Kusini na Tunisia pekee ndizo zilizo na programu sawa za matibabu.
Seli mundu ni ugonjwa wa kurithi na kesi nyingi hupatikana katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Husababishwa na jeni mbovu ambayo huathiri jinsi seli nyekundu za damu zinavyokua na hali hiyo inaweza kusababisha maumivu makali na viungo kushindwa kufanya kazi.
Upandikizaji wa uloto hubadilisha uloto na seli zenye afya. Pia hutumiwa kutibu wagonjwa wenye saratani ya damu.
Taifa hilo la Afrika Mashariki linashika nafasi ya nne duniani kwa kuwa na viwango vya juu vya seli mundu, likiwa na takriban watoto 11,000 wanaozaliwa na ugonjwa huo kila mwaka, kwa mujibu wa Wizara Afya ya Tanzania.
Mafuriko DRC: Idadi ya waliofariki imeongezeka hadi 438
Miili zaidi inaendelea kupatikana karibu wiki moja baada ya maporomoko ya ardhi katika eneo la Kalehe mashariki mwaJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msemaji wa Serikali ya Congo Patrick Muyaya amethibitisha kwamba kufikia sasa watu 438 wamefariki, mamlaka zinasema huenda idadi hiyo ikaongezeka kwa sasabu kuna wale ambao bado hawajapatikana.
Mashirika ya kiraia yanakadiria kuwa watu 5,000 hawajulikani walipo.
Gavana Theo amesema manusura watahamishwa kwa muda katika uwanja wa ndege wa Luena.
Pia unaweza kusoma:
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo tarehe 11 Alhamisi Mei 2023