Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Malawi yatangaza mafuriko kuwa janga huku watu 200 wakifariki

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kukumba eneo la kusini mwa Afrika kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa leo

  2. Simba wa Tanzania maarufu 'Bob Junior' auawa,

    Simba maarufu Kaskazini mwa Tanzania aliyeishi katika Hifadhi ya Serengeti, ‘Bob Junior’ ameuawa baada ya kushambuliwa na kundi la Simba watatu waliokuwa na lengo la muda mrefu la kuuangusha utawala wake, Mamlaka za hifadhi nchini humo zimethibitisha kifo hicho kilichotokea Jumamosi iliyopita.

    Simba hao watatu waliowahi kujaribu kujisimika ufalme walilelewa na ‘Bob Junior’ tangu wakiwa wadogo lakini majaribio ya kufanya mapinduzi mara kadhaa ili kuuangusha utawala wa Bob Junior haukufanikiwa na badala yake walikimbizwa katika maeneo hayo, yaliyopo mashariki mwa hifadhi hiyo.

    Simba ‘Bob Junior’ akisaidiana na kaka yake, Joel walitawala kwa zaidi ya miaka mitano na kuwa miongoni mwa Simba waliotawala kwa kipindi kirefu zaidi kabla ya kufanyika mapinduzi.

    Mhifadhi Mwandamizi wa hifadhi hiyo, Fredy Shirima ameieleza BBC kuwa tukio hilo ni asilia katika uhifadhi lakini pia hutokea zaidi kwa Simba ambao hushikilia ngome dhidi ya wengine wanaoitaka ngome.

    Shirima anasema, "Bob Junior aliuawa siku ya Machi 11, akishambuliwa na Simba watatu ambao walikuwa sehemu ya kundi la simba saba waliokuwa wanapanga mapinduzi.

    “…kwa kawaida hatuwezi kuingilia maisha ya wanyama pori… hivyo kilichotokea kilipangwa miongoni mwao ikiwa ni vita vya kimapinduzi na simba huwa wana tabia hiyo ambapo mtawala anapozeeka hutolewa kimabavu,” alieleza.

    ‘Bob Junior’ alipata vipi umaarufu?

    Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, ni simba aliyejibebea sifa kwa kuwa mpole na anayekuwa na utulivu anapoona watalii.

    Shirima anasema, ‘Bob Junior’ pia alikuwa na sifa za kipekee kama vile kuwa na manyoya mengi zaidi kuliko simba wengine lakini mwenye kuvutia kwa muonekano na hutulia pale anapopigwa picha.

    Wadau wa utalii wamesikitishwa na kifo cha simba huyo, huku ikimtaja kuwa ndiyo simba bora na mtulivu kuwahi kuonekana katika hifadhi ya Serengeti.

    Kaka yake ‘Bob Junior’ adaiwa kuuawa

    Mamlaka inafuatilia kwa karibu kaka wa Bob Junior, Joel anayedaiwa kuuawa kwa kushambuliwa na washirika wa simba waliomuua Bob Junior.

    Shirima anasema, “Bado tunamtafuta Joel, alikuwa sehemu ya simba ambao walikuwa wanatafutwa na kundi hilo lililokuwa likiwinda ngome… ingawa maofisa wetu wanafuatilia, bado hatuna uthibitisho la kuuawa kwake.”

    Kuhusu idadi ya Simba, Serengeti

    Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali,Tanzania ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya simba kuliko nchi nyingine yoyote barani Afrika.

    Inakadiriwa kuwa na simba 15,000 huku hifadhi ya Serengeti pekee ikiwa na takribani simba 3,000.

  3. Malawi yatangaza mafuriko kuwa janga huku watu 200 wakifariki

    Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Tropiki Freddy kukumba eneo la kusini mwa Afrika kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja.

    Kiasi cha kutisha cha maji ya kahawia yametiririka katika vitongoji, na kusomba nyumba.

    Kitovu cha kibiashara cha Malawi, Blantyre, kimerekodi vifo vingi, 158, wakiwemo 36 katika maeneo ya maporomoko ya ardhi.

    Serikali imetangaza hali ya janga katika wilaya 10 za kusini ambazo zimeathiriwa zaidi na dhoruba.

    Wafanyakazi wa uokoaji wamezidiwa, na wanatumia majembe kujaribu kuwatafuta manusura waliofukiwa na udongo.

    "Tuna mito inayofurika, tuna watu wanaobebwa na maji ya bomba, tuna majengo yanayoporomoka," msemaji wa polisi Peter Kalaya aliambia BBC.

    Shirika la serikali la kusaidia majanga limesema idadi ya waliofariki imeongezeka kutoka 99 siku ya Jumatatu hadi 190, huku takriban watu 584 wakijeruhiwa na 37 bado hawajulikani walipo.

    Zaidi ya watu 20,00 wamekimbia makazi yao, iliongeza.

    Soma zaidi:

  4. Vita vya Ukraine: Mwanajeshi wa Urusi akamatwa 'baada ya kuwa mafichoni kwa miezi sita'

    Mwanajeshi wa Urusi anayedai kukwepa kugunduliwa katika eneo la Kharkiv nchini Ukraine kwa miezi sita amezuiliwa, polisi wa Ukraine wamesema.

    Mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 42 alizuiwa na wanajeshi wa Ukraine walipokuwa wakishika doria katika wilaya ya Kupiansk, idara ya polisi ya mkoa wa Kharkiv ilisema.

    Eneo hilo lilichukuliwa tena na wanajeshi wa Ukraine Septemba iliyopita.

    Mwanajeshi huyo aliwaambia polisi kwamba alikuwa amejificha katika majengo yaliyotelekezwa tangu wakati huo.

    Baada ya kumpata siku ya Jumatatu, polisi waligundua kuwa mwanamume huyo - aliyevalia kiraia - alikuwa askari wa Kikosi cha 27 cha Walinzi wa Kikosi cha Kujitenga cha Urusi na alikuwa mkazi wa mkoa wa Moscow.

    Mwanajeshi huyo alipelekwa katika kituo cha polisi cha eneo hilo kwa uchunguzi zaidi, taarifa ya polisi ilisema.

    Kupiansk – eneo ambalo lina makutano muhimu ya reli - limeshuhudia mapigano makali tangu vita hivyo vilipoanza mwaka jana, huku Urusi ikichukua udhibiti katika muda wa siku chache, na kuukalia mji huo kwa miezi kadhaa.

    Ingawa eneo hilo lilichukuliwa tena na wanajeshi wa Ukraine Septemba mwaka jana, linakabiliwa na tishio la majaribio ya Urusi kuliteka tena.

    Pia unaweza kusoma:

  5. Warusi hawana makombora ya kutosha - Wizara ya Ulinzi ya Uingereza

    Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imeandika katika muhtasari mfupi wa kila siku wa hali ilivyo nchini Ukraine kwamba wanajeshi wa Urusi walio vitani wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa makombora.

    "Katika wiki za hivi karibuni, ukosefu wa silaha kwa Warusi labda umezidi kuwa mbaya kiasi kwamba vikwazo vikali vya makombora vimeanzishwa katika sekta maeneo mengi vitani.

    Hakika hii ndio sababu kwa nini wanajeshi wa Urusi hawajaweza kufanya shambulio hata moja la msingi hivi karibuni," - jeshi la Uingereza limeandika.

    Kulingana na wao, kwa sababu ya uhaba wa makombora, Urusi inatumia risasi za zamani, zilizoisha muda wake.

    Soma zaidi:

  6. Tanzania: Mwanamume ashambuliwa na tembo aliyetoroka hifadhi wakati anajipiga ‘selfie’ naye

    Mwanaume mmoja raia wa Tanzania yuko katika hali mbaya hospitalini baada ya kujipiga picha yaani ‘selfie’ na tembo yaani ndovu kabla ya kumgeukia na kumshambulia.

    Ni sehemu ya kundi la wanyama waliotoroka eneo la hifadhi katika mkoa wa Manyara kaskazini na kula mazao ya shambani katika kijiji kimoja, kwa mujibu wa mamlaka.

    Kamishna wa polisi wa eneo hilo alisema tembo hao walikasirika na kuanza kuchanganyikiwa baada ya kundi la wenyeji kuwakaribia na kuanza kupiga selfie nao.

    “Mtu huyo amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kiteto na anaendelea na matibabu...hali yake imeimarika kidogo,” alisema George Katabazi.

    Migogoro kati ya binadamu na wanyamapori ni jambo la kawaida nchini Tanzania, ambapo vipindi vya ukame mara nyingi husababisha wanyamapori kukimbilia mashambani kutafuta chakula.

  7. Mkataba wa Okus: Marekani, Uingereza na Australia zatia saini makubaliano ya kuanzisha kundi la manowari za nyuklia

    Marekani, Uingereza na Australia zimefichua maelezo ya mradi wa pamoja unaolenga kuunda kundi jipya la manowari zinazotumia nguvu za nyuklia, ili kukabiliana na ongezeko la ushawishi wa China katika eneo la Bahari za Hindi na Pasifiki.

    Chini ya makubaliano ya Okus, Australia itapata manowari ya kwanza kati ya angalau tatu zinazotumia nguvu za nyuklia kutoka Marekani.

    Washirika hao pia wanafanyia kazi kuunda kundi jipya la meli ambalo litatumia teknolojia za kisasa zaidi, ikiwa ni pamoja na vinu vya Rolls-Royce vinavyotengenezwa Uingereza.

    China siku ya Jumanne ilishutumu mradi huo mkubwa wa ushirikiano, ikionya kwamba makubaliano hayo yanawakilisha "njia mbaya na hatari".

    Ujumbe wa China kwenye Umoja wa Mataifa pia ulishutumu washirika wa Magharibi kwa kutatiza juhudi za kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia.

    Beijing hapo awali ilitoa wito kwa nchi hizo tatu, kabla ya tangazo la Jumatatu, "kuachana na mawazo ya Vita Baridi na michezo ambayo haileti matokeo."

    Urusi nayo ililaani mkataba huo, ikisema kwamba yatasababisha "makabiliano ambayo yatadumu kwa miaka" huko Asia.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alisema, "Ulimwengu wa Anglo-Saxon unajenga mmikataba kama vile Okus, kuendeleza miundombinu ya NATO barani Asia, na kucheza kamari katika makabiliano ambayo yatadumu kwa miaka mingi."

    Pia, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki lilionya Jumanne kuhusu hatari ya kuenea kwa nyuklia kutokana na mradi wa manowari unaoendeshwa na nyuklia uliozinduliwa na Marekani, Australia na Uingereza.

    Hata hivyo, Rais wa Marekani Joe Biden alisema kuwa mkataba huo unalenga kukuza amani katika eneo hilo, na kusisitiza kuwa manowari hizo "zitakuwa zinaendesha nishati ya nyuklia na sio silaha za nyuklia."

    Akizungumza pamoja na mawaziri wakuu wa Uingereza na Australia, Rishi Sunak na Anthony Albanese, mjini San Diego, California, Biden alisema makubaliano hayo hayatahatarisha dhamira ya Australia ya kuwa nchi isiyo na silaha za nyuklia.

    Pia unaweza kusoma:

  8. Mwanasayansi wa Marekani atajaribu kuishi siku 100 chini ya maji

    Akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 28 kama mzamiaji katika Jeshi la Wanamaji la Marekani, Daktari wa Uhandisi wa Biomedical Joseph Dituri, mtafiti na profesa katika Chuo Kikuu cha Florida Kusini (USF), amekuwa na shauku kubwa kwa manowari.

    Akiwa amepewa jina la utani Dr. Deep Sea, Dituri, ana umri wa miaka 55.

    Wiki iliyopita, Dituri, mtaalamu wa kuzamia maji kwa kina kirefu sana, alijaribu kuchukua changamoto kubwa zaidi ya kazi yake: kuishi siku mia moja chini ya maji.

    Katika kipindi hiki, ataishi katika nyumba ya kulala ya wageni chini ya maji.

    Dituri anataka kuvunja rekodi ya dunia kwa muda mrefu zaidi chini ya maji, ambayo ilishindwa mwaka 2014 na watafiti wawili kutoka Chuo Kikuu cha Tennessee, ambao walitumia siku 73 katika makazi hayo hayo, yaiitwayo Jules' Undersea Lodge.

    "Lakini hiyo sio sehemu muhimu zaidi," Dituri alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwasilisha mradi huo ulioanza Machi 1.

    Katika uzoefu wake wote chini ya maji, atafanya utafiti wa afya, mazingira ya bahari na teknolojia mpya, huku akiendelea kufundisha Chuo Kikuu, Kozi zinazotolewa mtandaoni.

    Mradi huo utawezesha utafiti wa muda mrefu wa kuongezeka kwa shinikizo la chini ya maji kwa wanadamu.

    Athari za kimwili na kisaikolojia za kukaa kwa muda mrefu katika mazingira ya chini ya maji lazima zifuatiliwe na timu ya matibabu ya wataalamu kumi.

    Watafanya uchunguzi wa mara kwa mara na kumfanyia Dituri wingi wa vipimo, ikiwa ni pamoja na vipimo vya damu, ultrasounds na electrocardiograms, miongoni mwa mengine.

    Alipitia mfululizo wa vipimo vya kimwili na kisaikolojia. Utaratibu huo huo utafanyika mwishoni mwa kipindi chake chini ya maji ili kujua ikiwa uzoefu huo umesababisha madhara kwa afya yake ya akili na kimwili.

    Pia atatathminiwa mara kwa mara na wanasaikolojia na wataalamu wa akili, ambao watafuatilia athari ya kiakili ya kukaa kwake chini ya maji.

    "Mwili wa binadamu haujawahi kuwa chini ya maji kwa muda mrefu, hivyo nitafuatilia kwa karibu," Dituri alisema.

    "Wataalamu watachunguza madhara yote ya kukaa kwangu kwa muda mrefu chini ya maji, lakini maoni yangu ni kwamba uzoefu huu utakuwa na athari nzuri kwa afya yangu kwa sababu ya kuongezeka kwa shinikizo la chini ya maji.

  9. Wafungwa sita wa Zimbabwe watoroka kutoka kizuizini SA

    Raia sita wa Zimbabwe, wote wanaoshukiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha, wametoroka kutoka kizuizini walipokuwa kwenye usafiri siku ya Jumatatu asubuhi baada ya wenzao kuwakabili polisi wa Afrika Kusini katika majibizano ya risasi.

    Katika taarifa, polisi wa Afrika Kusini walisema wameanzisha msako wa kuwasaka washukiwa "wenye silaha nzito" ambao waliwaachilia wafungwa sita wakati wa mapigano hayo ya risasi.

    Shambulio hilo la kijasiri lilifanyika umbali wa kilomita 120 kusini mwa Beitbridge - mji wa mpakani karibu na Zimbabwe.

    "Watu wanashauriwa kutowakaribia washukiwa kwa hali yoyote ile kwani wanachukuliwa kuwa hatari badala yake watoe ripoti kwa polisi," polisi wa Afrika Kusini walisema.

    Zimbabwe ina idadi kubwa ya wahamiaji nchini Afrika Kusini huku raia wake wakiendelea kutoroka matatizo ya kisiasa na kiuchumi nyumbani.

    Serikali ya Afrika Kusini imekuwa ikikabiliana na raia wa kigeni hasa Wazimbabwe wanaohusika na uhalifu wa kutumia nguvu.

  10. Rekodi za santuri zauza zaidi kuliko za CD kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha muongo

    Mauzo ya rekodi za santuri za muziki yamekuwa ya juu zaidi kuliko rekodi za CD nchini Marekani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1987, kulingana na repoti mpya.

    Zaidi ya rekodi milioni 41 za santuri ziliuzwa katika mwaka 2022, kwa bei ya $1.2bn (£.99bn).

    Ni CD milioni 33 zilizouzwa pekee, ambazo ziliuzwa kwa $483m.

    Ulikuwa ni mwaka wa 16 mfulurizo wa ukuaji wa mauzo ya rekodi, ikiwa ni takriban 71% ya mapato ta sampuli.

    Mapato ya muziki yaliyorekodiwa nchini marekani yaliongezeka kwa miaka saba mfulurizo na kufikia $15.9bn.

    Kwa ujumla, mapato ya rekodi ya muziki katika mwaka2022 yaliongezeka kwa 6%, kulingana na ripoti iliyotolewa na Shirikisho la la sekta ya Kurekodi ya Marekani (RIAA), mapato haya yakipatikana kwa kiasi kikubwa kutokana na kusikilizwa kwa muziki mtandaoni lakini pia kutokana na mauzo ya muziki halisi.

  11. Casemiro: Manchester United yaamua kutokata rufaa dhidi ya kadi nyekundu

    Manchester United wameamua kutokata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa kiungo wa kati wa Brazil Casemiro katika mchezo wa Jumapili wa 0-0 na Southampton.

    Mwamuzi Anthony Taylor kwanza alimuacha Casemiro kwa kumchezea rafu Carlos Alcaraz, lakini akamtoa nje baada ya kwenda kwa mfuatiliaji wa televisheni kwa ushauri wa mwamuzi msaidizi wa video.

    United waliamini kulikuwa na uwezekano mdogo wa uamuzi huo kubatilishwa.

    Casemiro sasa atatumikia adhabu ya kutocheza mechi nne za nyumbani mara moja.

    Hilo linatokea ikiwa ni mara yake ya pili kufukuzwa msimu huu, kufuatia kadi nyekundu dhidi ya Crystal Palace mnamo mwezi Februari.

    Atakosa mechi ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Fulham na michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Newcastle United, Brentford na Everton.

    "Casemiro yuko katika ligi za Ulaya, katika zaidi ya mechi 500 hakuwahi kupewa kadi nyekundu na sasa ana mara mbili," meneja wa United Erik ten Hag alisema baada ya mechi ya Southampton.

    "Anacheza kwa bidii lakini anacheza kwa haki, pia katika hili anacheza kwa haki, sawa na dhidi ya Palace, hivyo hili linajadilika sana.

    "Unapositisha mtu kucheza inaonekana ni mbaya, lakini kila mtu anayejua kuhusu soka, ambaye anacheza soka la juu, anajua kipi kibaya na kipi si kibaya, kipi ni cha haki.

    "Nakwambia, Casemiro ni mchezaji wa haki. Ana mchezo mkali lakini wa haki na inajionyesha kwa zaidi ya mechi 500 kwenye ligi kubwa, hajawahi kutolewa nje kwa kadi nyekundu."

    Beki Raphael Varane aliongeza: "Ni mchezaji ambaye ni muhimu sana kwetu.

    Pia unaweza kusoma:

  12. Benki kuu ya Nigeria yaruhusu utumizi wa noti za zamani

    Benki Kuu ya Nigeria (CBN) inasema noti za zamani zitasalia kuwa pesa halali hadi mwisho wa mwaka kulingana na uamuzi uliotolewa na mahakama kuu mapema mwezi huu.

    Benki pia zimeagizwa kutii uamuzi wa mahakama ulioruhusu noti za zamani na mpya za naira kutumiwa kwa wakati mmoja hadi tarehe 31 Desemba.

    Ukosefu wa noti mpya zilizoundwa na naira ulisababisha uhaba wa pesa katika nchi ambayo 40% ya watu hawana akaunti za benki.

    Milolongo mirefu ilishuhudiwa katika kumbi za benki na mashine za kutolea pesa huku wengi wakishindwa kupata noti hizo mpya. Hii ilisababisha maandamano katika baadhi ya maeneo ya nchi.

    Mnamo Februari, baadhi ya magavana wa majimbo walipeleka serikali ya shirikisho kortini, wakipinga kutekelezwa kwa tarehe ya mwisho ya Februari 10 ya kuondoa noti za zamani.

    Rais Buhari mnamo tarehe 16 Februari aliamuru benki kuu kusambaza noti za zamani za naira 200 pekee hadi tarehe 10 Aprili, akisisitiza noti za naira 500 na 1,000 hazikuwa tena zabuni halali. Lakini uamuzi wa mahakama kuu ulipuuza agizo hili.

    Siku ya Jumatatu, ofisi ya rais ilikanusha maoni ya umma kwamba alikuwa ameagiza gavana wa CBN na mwanasheria mkuu kutotii maagizo ya mahakama.

    "Maagizo ya Rais, kufuatia kikao cha Baraza la Nchi, ni kwamba Benki lazima itengeneze pesa zote zinazohitajika kwa mzunguko na hakuna kilichotokea kubadili msimamo" alisema katika taarifa yake.

    Oktoba iliyopita, benki kuu ilibuni upya noti za juu zaidi ili kukabiliana na ughushi, uhifadhi wa fedha na ukosefu wa usalama unaochochewa na utekaji nyara kwa ajili ya fidia.

  13. Kampuni ya Kitanzania ilihamisha pesa kabla ya benki ya SVB kuporomoka

    Kampuni za Kiafrika zinafuatilia kwa karibu kuona nini kitatokea baada ya kuporomoka kwa Benki ya Silicon Valley yenye makao yake makuu nchini Marekani (SVB).

    Benki hiyo iliyobobea katika kutoa mikopo kwa makampuni ya teknolojia, ilifungwa na wadhibiti ambao walitwaa mali yake siku ya Ijumaa.

    Hata hiyo ilifikiwa baada ya SVB kuhangaika kutafuta pesa za kuzuia hasara kutokana na mauzo ya mali iliyoathiriwa na viwango vya juu vya riba.

    Benki hiyo ilikuwa mshirika na kampuni iliyoanzisha kampuni ya Y Combinator, ambayo inasemekana ina zaidi ya kampuni changa 80 za Kiafrika katika jalada lake.

    Rais wa Y-Combinator Garry Tan alitweet: "30% ya kampuni za YC zilizofichuliwa kupitia SVB haziwezi kufanya malipo katika siku 30 zijazo."

    Mwanzilishi wa Tanzania fintech NALA, Benjamin Fernandes, aliiambia Kipindi cha Redio cha BBC Focus on Africa kwamba walikuwa na benki na SVB.

    "Nilipigiwa simu na mmoja wa wawekezaji wetu akisema tutoe pesa kwani benki hii itaanguka

    Mara moja tulituma pesa hizo kwenye akaunti nyingine ya benki ambayo tunafanya nayo kazi.''

    "Sidhani kama waanzishaji wengi wa wa kampuni za Kiafrika waliathiriwa ikilinganishwa na kile tulichofikiria mwanzoni kwa sababu sio benki nyingi zinazoanza na SVB. Kampuni ya Kiafrika inayoinukia ni vigumu kupata akaunti ya benki ya Marekani,” alisema.

  14. Idadi ya vifo kutokana na Kimbunga Freddy nchini Malawi yafikia 99

    Idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Freddy nchini Malawi imengezeka hadi 99 Jumatatu, huku vifo 85 vikirekodiwa katika jiji la Blantyre pekee, mamlaka ilisema.

    Nchi inajitahidi kuzuia athari za dhoruba, ambayo imesababisha uharibifu haswa katika wilaya 10 za mkoa wa kusini mwa nchi.

    Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imeharibu nyumba, kusomba barabara na madaraja, kuharibu mashamba ya mazao na kutatiza uzalishaji wa umeme.

    Hospitali kuu ya rufaa mjini Blantyre inasema imelemewa na idadi kubwa ya miili inayopokea.

    Imetoa wito kwa familia zilizofiwa au ambao ndugu zao wamepotea kwenda hospitali kutambua na kuchukua miili kwa ajili ya mazishi kwani hospitali inakosa nafasi.

    Dhoruba imelemaza uwezo wa kuzalisha umeme huku sehemu nyingi zikikabiliwa na kukatika kwa umeme kwa muda mrefu

    Kampuni ya kitaifa ya kuzalisha umeme inasema haiwezi kurejesha nguvu kwa mtambo wake wa kufua umeme kutokana na mrundikano wa uchafu uliosababishwa na mafuriko.

    Wataalamu wa hali ya hewa wanasema mvua kubwa na mafuriko yataendelea siku ya Jumanne huku dhoruba hiyo ikitarajiwa kuanza kuondoka Malawi kurejea Bahari ya Hindi siku ya Jumatano.

    Serikali ya Malawi imetangaza hali ya maafa ya kitaifa katika wilaya zilizoathirika zaidi.Iliomba msaada wa ndani na kimataifa kwa makumi ya maelfu ya watu ambao wameachwa bila chakula na makazi.

  15. Tahadhari yatolewa kuhusu uwezekano wa mlipuko wa Volkano DR Congo

    Wataalamu wa volcano wanasema kuwa wameshuhudia kuongezeka kwa lava juu ya Mlima Volkano wa Nyiragongo mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

    Hii imesababishwa kushuka kwa lava kwenye maeneo ya wazi ya kina kuelekea kwenye shimo la creta la voklano ya Nyamulagira, kulingana na data za hivi karibuni.

    Mlipuko wa mwisho wa Nyamulagira ulitokea mwaka 2011 – ukiwa ndio mlipuko mkubwa zaidi wa Volkano kuwahi kushuhudia katika kipindi cha miaka 100.

    Nyamulagila inapatikana katikati mwa Mbuga ya Wanyama ya taifa ya Virunga, ambayo ia ni makao ya sokwe wa milimani.

    Iwapo mlipuko mpya utatokea, lava itashuka kuelekea upande wa mbuga, waangalizi wa volcano waliopo Goma wametahadharisha Jumatatu jioni.

    Kwa sasa hakuna vitisho kwa mji wa Goma, ambao unakaliwa na watu 670,000 kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.

    Lakini jivu la volcano na mawe ya kupoa kwa lava vinaweza kupeperushwa na upepo katika maeneo ya makazi, ilisema taarifa ya waangalizi.

    "Tunashauri kwamba watu wa Goma waendelee kuwa watulivu na kuendela na shughuli zao kwa uhuru ," ilisema.

    Wakazi wameshauriwa kuosha vyema mboga zao na kutumia maji yaliyotunzwa kwa muda, huku ndege zikishauriwa pia kuzingatia mwelekeo wa upepo wakati zinaposafiri juu ya eneo la Virunga.

    Mnamo mwezi Mei, 2021, maelfu ya watu walihamishwa kutoka jiji la goma baada ya kulipuka kwa mlima Nyiragongo.

  16. Iwao Hakamada: Mfungwa wa Japan anayesubiri hukumu ya kifo, apewa fursa ya kusikilizwa upya kwa kesi yake

    Iwao Hakamada, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 87, ndiye mfungwa aliyefungwa aliyeishi gerezani kwa muda mrefu zaidi huku akisubiri hukumu ya kifo, kulingana na shirika la haki za binadamu la kimataifa la Amnesty International.

    Alihukumiwa kifo mwaka 1968 kwa maujai ya bosi wake, mke wa mwanaume huyo na waoto wao wawili katika mwaka 1966.

    Mwanamasumbwi huyo wa zamani wa ndondi za kulipwa alikiri mauaji hayo baada kuhojiwa kwa siku 20 ambapo alisema alipigwa. Baadaye aliondoa ushahidi wake wa kukiri kosa mahakamani.

    Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamekosoa utegemezi wa Japan kuhusu kukirimakosa, ambapo walisema polisi hutumia nguvu mara kwa mara kuwalazimisha washukiwa kukiri mashitaka.

    Katika kesi mpya, majaji watataka kubaini iwapo vinasaba DNA kutoka kwenye madoa ya damu iliyopatikana kwenye nguo inayodai wa kuvaliwa na muuaji vinafanana na na vya Bw Hakamada.

    Mawakili wake wanadai kuwa havifanani na kwamba ushahidi dhidi yake ulitbuniwa.

    Iwao Hakamada alikamatwa na kushutumiwa kwa wizi na mauaji ya muajiri wake na familia yake katika kiwanda cha kusindika soya kilichopo Shizuoka magharibi mwa jiji la Tokyo mwaka 1966. Walipatikana wakiwa wamekufa kwa kudungwa kisu.

  17. Vita vya Ukraine: Zelensky atoa heshima kwa mwanajeshi asiye na silaha aliyechukuliwa video akipigwa risasi

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa heshima kwa mwanajeshi wa Ukraine ambaye alichukuliwa picha ya video hukiu akipigwa risasina wanajeshi wa Urusi, wiki iliyopita.

    Oleksandr Matsievskiy hakuwa na silaha wakati alipochukua video huku akivuta sigara na kupaza sauti akisema‘’Utukufu kwa Ukraine’’ "Glory to Ukraine" kabla ya kupigwa risasi hadi kufa.

    Video hiyo imepelekea Urusi kukabiliwa na shutuma mpya za uhalifu wa kivita. Jumapili , Rais Zelensky alimtunukia mwanajeshi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 42 cheo cha Shujaa wa Ukraine, ikiwa ndio heshima ya juu zaidi ya nchi.

    "Leo nimempatia cheo cha Shujaa wa Ukraine mwanajeshi Oleksandr Matsievskiy," Bw Zelensky alisema katka hotuba yake kutoka Kyiv.

    "Mwanaume ambaye Waukraine wote watamjua. Mwanaume ambaye atakumbukwa daima. Kwa ujasiri wake, kwa Imani yake kwa Ukraine na kwa ‘’Utukufu wake kwa Ukraine’’, alisema Zelensky.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  18. Wakwe 'wamtesa' mke, waiuza damu yake ya hedhi kwa Rupia 50,000

    Mwanamke mmoja nchini India ametoa madai ya kushangaza kwamba baba mkwe alimlazimisha kuuza damu ya hedhi.

    Kulingana na malalamiko yaliyowasilishwa na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 katika kituo cha polisi cha Vishrantwadi huko Pune, wakwe zake walimlazimisha kwanza kuuza damu ya hedhi mnamo Agosti 2022.

    Tangu wakati huo, mume wake na wakwe walikuwa wakimtesa kimwili na kiakili kila mara. Kulingana na malalamiko yaliyosajiliwa Machi 7, 2023, kesi imesajiliwa dhidi ya mume wa mwanamke huyo na wakwe saba.

    Kulingana na inspekta wa kituo cha polisi cha Vishrantwadi Dattatray Bhapkar, "Mwanamke huyo aliolewa mwaka wa 2019. Mwanamke huyo aliwasilisha malalamishi ya unyanyasaji wa nyumbani katika mahakama mwaka wa 2021. Hata hivyo, aliondoa kesi hiyo baada ya kushawishiwa na mama mkwe na mumewe."

    Walitaka kuuza damu hiyo kwa rupia elfu 50

    Wakati wa tamasha la Ganesh mnamo Agosti 2022, jamaa za mwanamke huyo walimwendea na kusema kwamba alikuwa akiona damu ya hedhi. Yule mwanamke aliposikia hayo, alikasirika sana, akasema, "Ichukue kutoka kwa mkeo!" Hatahivyo, mpenzi wake alimwambia kwamba alitaka damu ya hedhi ya mwanamke asiye na mtoto na atapata rupia elfu 50 sawa na zaidi ya dola 500 za Marekani kwa kumpa mtu. Hatahivyo, alikataa kwani hii haikuidhinishwa.

    Inspekta wa polisi Dattatraya Bhapkar alisema, "Shemeji kwa pamoja walichukua damu ya hedhi na kuiuza licha ya kutokuwepo kwake. Kwa hivyo, kesi imeandikishwa dhidi yao." Kulingana na polisi, hakuna mtu aliyekamatwa katika kesi hii bado. Tume ya wanawake ya jimbo imezingatia suala hilo. Rais wa Tume ya Wanawake Rupali Chakankar alisema kuwa wanafuatilia suala hilo na wanapata taarifa kila mara kutoka kwa polisi.

  19. Rais Kagame kuhusu suala la Rusesabagina: 'kuna kazi inayofanywa’’,

    Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema suala la mpinzani wa serikali ya Rwanda ,Paul Rusesabaginalinachunguzwa ili kulimaliza.

    Mwaka 2021 , Rusesabaginaambaye ni mpinzani dhidi ya serikali ya Rwandaalihukumiwa kifungo cha miaka 25 jelabaada ya kupatikana na hatia ya makosa ya ugaidiulio na misingi ya mashambulizi ya kundi la waasi la FLN ambalo ni tawi la muungano wake wa kisiasa.

    Rusesabagina alipata umaarufu kutokana nafilamu ya “Hotel Rwanda” akionyesha alivyookoa maisha ya wengi wakati wa mauaji ya kimbarinchiniRwanda 1994.

    Katika mahojiano maalum na gazeti laSemaforla nchini MarekaniRais wa Rwanda Paul Kagame, alisema kuna njia ya kusonga mbele juu ya uwezekano wa kuachiliwa kwaBwanaPaul Rusesabagina, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 25 jelamwaka2021.

    Kagame alimwambia mwanahabariSteve Clemons wa Semafor kwamba "kuna kazi inaendelea" kutatua suala hilo laRusesabagina. "Sisi si watu ambao hatutaki kukwama katika sehemu moja na kutosonga mbele," rais wa Rwanda alisema wakati wa mahojiano katika Kongamano la Usalama la dunia mjini Doha, Qatar.

    ‘’Kama unavyojua zama zetu tunapotaka kupiga hatua mbele... tulifika mahalipa kusamehewatu ambaohatamakosa yaosi ya kusamehewa,yaaniwahusika wa mauaji ya kimbari ,wengi wao tuliwasamehe ‘’ aliongezaRais Kagame.

    "Kuna mjadala unaoangalia njia zote zinazowezekana za kutatua suala hilo bila kuathiri vipengele vya msingi vya kesi hiyo na nadhani daima kutakuwa na njia ya kusongambele," alisema Kagame.

    Mwezi Disemba Kagame alihoji kwa nini nchi yake imuachilie hilie kwa sababu tu ya umaarufu wake au hadhi yake kama mkaazi wa kudumu wa Marekani, wakati ana hatia?.

    Rusesabagina, 68, ambaye alionyeshwa kama ‘’shujaa’’ katikafilamu yaHotel Rwanda kwa kuwalinda watu wa kabila la Watutsi dhidi ya mauaji ya kimbari , alihukumiwa pamoja na watuwengine 20 baada ya kupatikana na hatiayaugaidikwa misingi ya kufadhili kundi la FLN(The National Liberation Front) ambalo ni tawi la kijeshi la muungano wa kisiasa wa MRCD unaongozwa na Paul Rusesabagina.

    Yeye alijiondoa katika kesi hiyo kwa madai kuwa hawezikutendewa haki kisheria.

    Familia yake na mashirika ya haki za binadamuwanaendelea kupaza sauti wakitaka aachiliwe na kusema alifungwa kwa sababu za kisiasa, madai yanayotupiliwa mbali na serikali ya Rwanda ikisema kuwa kesi yake ilikuwa ya uwazi.

    Unaweza pia kusoma:

    • Paul Rusesabagina: Mfahamu mkosoaji mkuu wa rais wa Rwanda Paul Kagame
    • Paul Rusesabagina: Rwanda yakiri kuwa 'iliilipa ' ndege iliyomtoa Dubai na kumpeleka Kigali, bila kujua
  20. Mkataba wa Aukus :Marekani, Uingereza, na Australia zakubaliana kuhusu mradi wa nyuklia wa manowari

    Viongozi wa Marekani, Uingereza na Australia wamefichua maelezo mapyaya mpango wao wa kubuni manoari ya kizazi kipya inayotumia nishati ya nyuklia .

    Chini ya makubaliano ya Aukus Australia itapokea kwanza walau manoari tatu zinazotumia nishati ya nyuklia kutoka kwa Marekani.

    Washirika hao pia watashirikiana kwa pamoja kubuni manoari mpya ya kiteknolojia, mkiwemo vinu vya nyuklia vilivyotengenezwa na kampuni ya Rolls-Royce ya nchini Uingereza.

    Makataba huo unalenga kukabiliana na ushawishi wa Uchina katika kanda ya bahari ya India na ile ya Pacific.

    Akizungumza na viongozi wengine mjini San Diego, California, Rais wa Marekani Joe Biden alisisitza kwamba maboti hayatakuwa na silaha za nyuklia na hayatabadilisha sera ya Austaralia ya kuwa nchi isiyokuwa na nyuklia .

    Chini ya mkataba ulioainishwa Jumatatu , wanajeshi wa majini wa kikosi cha Australia - Royal Australian Navy (RAN) watafanya kazi na vikosi vya Marekani na Uingereza.

    Unaweza pia kusoma:

    • Makombora ya Hypersonic:Uingereza,Marekani na Australia kuzidisha ushirikiano wa kijeshi
    • Uingereza, Marekani, Australia kuzindua jeshi kwa jina Aukus kuikabili China