Shambulio la kombora lilikuwa tukio la bahati mbaya- Poland
Rais wa Poland Andrzej Duda amesema hakuna dalili ya shambulio la makusudi baada ya kombora kuanguka katika mpaka kati yake na Ukraine, kuua watu wawili.
Moja kwa moja
Kuondoa ukomo wa Urais ni 'ubinafsi' - Ruto

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Kenya William Ruto amelaani kauli ya mbunge aliyesema kwamba nchi hiyo inapaswa kufuta ukomo wake wa mihula miwili ya urais, akieleza kuwa ni ya "ubinafsi".
"Msitumie muda wenu kushinikiza sheria za ubinafsi na kama vile kubadilisha katiba kuondoa ukomo wa mihula, lengo langu ni kuwatumikia wananchi," Rais Ruto, ambaye aliingia afisini Septemba, alinukuliwa akisema.
Hivi majuzi, Mbunge Salah Yakub, kutoka chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA), alizua utata baada ya kutaka ukomo wa muhula wa urais uondolewe kwa sababu "unamzuia mkuu wa nchi kuendeleza taifa".
"Muhula wa urais haufai kuwa na mihula miwili, mihula mitatu au hata minne. Ikiwa rais anafanya kazi nzuri anapaswa kuongeza muhula wake," Bw Yakub alinukuliwa na tovuti ya habari ya Citizen na kuongeza kuwa baadhi ya wabunge wenzake wanashinikiza mabadiliko haya ya kanuni.
Lakini chama cha Bw Ruto cha UDA kilikanusha madai hayo.
Kwanini shambulio la kombora Poland limeleta wasiwasi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Shambulio baya la kombora nchini Poland lilizua wasiwasi mkubwa katika nchi za Magharibi.
Ilikuwa ni mara ya kwanza wakati wa vita vya Ukraine kwamba nchi ya NATO ilikuwa imeshambuliwa, na lilikuwa na uwezo wa kusababisha madhara mabaya zaid.
Hiyo ni kwa sababu kanuni ya msingi ya NATO ni kwamba shambulio dhidi ya nchi moja mwanachama linachukuliwa kama ni shambulio kwa wanachama wote - kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 5 cha mkataba wa nchi za NATO.
Iwapo makombora yaliyoishambulia Poland yangerushwa na Urusi yangezingatiwa zaidi kama shambulio la silaha, hata kama Ukraine ndiyo iliyokuwa inalengwa.
Kulipiza kisasi kutoka kwa mataifa mengine ya NATO haingefanyika moja kwa moja, lakini nchi zingelazimika kuchukua hatua zozote ambazo ziliona kuwa ni "muhimu" kuiunga mkono Poland.
Kifungu cha 5 cha mkataba wa nchi za magharibi imeanzishwa mara moja tu hapo awali - baada ya tukio la 9/11 la kushambuliwa na Marekani.
Watu kadhaa wahofiwa kukwama ndani ya jengo lililoporomoka Nairobi
Wafanyakazi wa uokoaji wanawatafuta watu 10, wengi wao wajenzi, wanaohofiwa kukwama chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Jengo hilo la gorofa saba lilikuwa bado linaendelea kujengwa lilipoanguka Jumanne alasiri katika eneo la Kasarani, viungani mwa jiji la Nairobi.
Msimamizi wa jengo hilo inasemekana alipuuza wito kutoka kwa mamlaka kusitisha kazi ya ujenzi kufuatia hofu kuhusu uthabiti wake, tovuti ya habari ya Nation inaripoti.
Kuporomoka kwa majengo yanayoendelea kujengwa ni jambo la kawaida katika jiji hilo.
Vikosi vya dharura siku ya Jumatano asubuhi vilikuwa bado kwenye eneo la tukio, huku mashine nzito zikiondoa vifaa vya ujenzi huku waokoaji wakijaribu kuwatafuta wahasiriwa waliofukiwa chini ya vifusi.
Ruka YouTube ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazoMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa YouTube ujumbe
Vita vya Ukraine: Poland yasema vifo vilivyotokana na kuanguka kwa kombora ni tukio la bahati mbaya

Rais wa Poland Andrzej Duda amesema hakuna dalili shambulio la makusudi baada ya kombora kuanguka katika mpaka wa magharibi wa Ukraine na kuua watu wawili.
Awali,Rais wa Marekani Joe Biden alisema "haiwezekani" kombora hilo kurushwa kutoka Urusi.
Wafanyakazi hao wawili waliuawa wakati Ukraine iliposhutumiwa kutokana na mashambulio makubwa ya makombora katika vita hivyo.
Kremlin ilikuwa imesisitiza kuwa haikuwa na uhusiano wowote na vifo vyao.
Poland awali ilisema kwamba kombora lililoanguka Przewodow, kilomita 6 kutoka mpakani, lilitengenezwa na Urusi.
Akishutumu mataifa ya Magharibi kwa kuibua wasi wasi, msemaji wa Urusi Dmitry Peskov alisema Warsaw ilipaswa kuweka wazi mara moja shambulio hilo limetoka kwa ulinzi wa anga wa S-300 wa Ukraine.
Wakati wachunguzi wa Poland wakipekua eneo la tukuo hilo, mabalozi wa Nato walikutana mjini Brussels kutathmini jinsi ya kukabiliana na vita vya Urusi vinavyosambaa hadi katika nchi wanachama.
Katibu Mkuu Jens Stoltenberg aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakuna dalili kwamba tukio hilo lilitokana na shambulio la makusudi au kwamba Moscow ilikuwa ikitayarisha hatua za kichokozi dhidi ya muungano wa NATO.
"Niseme wazi, hili sio kosa la Ukraine," katibu mkuu huyo alisema.
"Urusi inawajibikia tukio hilo wakati inaendeleza vita vyake haramu dhidi ya Ukraine."
Zaidi ya makombora 90 ya Urusi yalirushwa nchini Ukraine siku ya Jumanne, kulingana na Kyiv.
Ijapokuwa jeshi la Ukraine lilisema 77 zilidunguliwa, baadhi ya makombora hayo yalipiga Lviv, karibu na mpaka wa magharibi wa nchi hiyo na Poland.
Maelezo zaidi:
Winnie Odinga: 'Kuwa binti wa Raila ni hasara'

Chanzo cha picha, Winnie Odinga / Twitter
Maelezo ya picha, Winnie Odinga anawania kuwa mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki Winnie Odinga, binti wa kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga, amesema jina lake la familia limemfanya "kunyanyaswa" na "kuteswa" na halikuwa faida ya kisiasa kama wanavyodai baadhi ya wakosoaji.
Winnie Odinga, ambaye anawania kuwa mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), alipinga wazo hilo katika kituo cha Citizen TV Kenyakwamba uhusiano wa familia yake ulikuwa nyuma ya uteuzi wake.
Bi Odinga alidai kuwa wakosoaji “hawataki kuangazia ninachoweza kufanya” kwa sababu ya babake ni nani.
Hata hivyo, alikubali kwamba jina la familia yake pia lilikuwa "baraka" ambayo imemruhusu kusafiri ulimwengu na kuelewa jinsi bara la Afrika linaweza kufanya kazi pamoja.
EALA ni chombo cha kutunga sheria cha jumuiya ya kikanda baina ya serikali, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na wanachama wanawakilisha mataifa yao kwa muhula wa miaka mitano.
Soma:
Nchi 10 kushiriki mashindano ya kuogelea ya CANA Zone 3 yanayoanza kesho Tanzania

Chanzo cha picha, TSA
Mashindano ya kimataifa ya mchezo wa kuogelea ya CANA Zone 3 yataanza kutimua vumbi kuanzia kesho nchini Tanzania.
Jumla ya mataifa 10 ya CANA Zone 3, yatachuana kusaka mabingwa wa michuano hiyo ambayo washindi wanajizoea medali.
Mbali na wenyeji Tanzania mataifa mengine yatayoshiriki michuano hii ni Ethiopia, Sudan, Djibouti, Uganda, Kenya, Zambia7, Afrika Kusini, Africa, Rwanda na Burundi.

Chanzo cha picha, TSA
Maelezo ya picha, Wawakilishi wa Tanzania kwenye Mashindano ya CANA Zone 3 mara baada ya kukabidhiwa bendera Timu ya kuogelea ya Tanzania ,ilikabidhiwa bendera siku ya Jumatatu tayari kuliwakilisha taifa hilo kwenye mashindano hayo yatakayomalizika Novemba 20.
Tanzania inayopigiwa chapuo kama ilivyo kwa Uganda, ilimaliza ya pili mwaka jana kwa alama 2638, Kenya ikiwa ya tatu kwa alama 2369 huku Uganda ikiibuka kidedea kwa alama 2827.
Uteuzi wa Grammy kwa nyota wa Afrika Tems na wengine

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Tems ameteuliwa kuwania Tuzo nne za Grammy Uteuzi wa Tuzo za Grammy 2023 umetangazwa na nyota wa Kiafrika Tems, Burna Boy, Rocky Dawuni na Angélique Kidjo wote wanawania tuzo.
Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Nigeria Tems ameteuliwa kwa uandishi wake kwenye albamu ya Renaissance ya Beyonce na wimbo wa rapa Drake wa Wait For U ambao umetajwa kuwania Rekodi ya Mwaka.
Burna Boy ameshinda uteuzi wake wa tatu wa Grammy kwa mfululizo wa utendaji bora wa Muziki wa Global na pia ameteuliwa kwa albamu yake ya Love, Damini.
Mwimbaji nyota wa Benin Angélique Kidjo pia ameteuliwa kuwania tuzo kadhaa zikiwemo Albamu Bora ya Muziki ya Global na kumfanya kuwa mteule wa Grammy mara 12.
Mkali wa dancehall wa Afropop, Eddy Kenzo amekuwa msanii wa kwanza wa Uganda kuteuliwa kuwania tuzo za Grammys na wasanii wa Afrika Kusini Zakes Bantwini na Nomcebo Zikode pia wametajwa kwenye nyimbo zao za wimbo, Bayethe.
Toleo la 65 la tuzo hizo litafanyika Februari ijayo mjini Los Angeles Marekani.
Soma:
Mwanamke wa Ethiopia miongini mwa watu saba walionyongwa nchini Kuwait

Kuwait imekeleza mauaji hukumu yake ya kwanza ya kifo katika kipindi cha miaka mitano, kunyongwa watu saba wakiwemo wanawake wawili licha ya maombi ya wanaharakati wa haki za kimataifa kutaka wahurumiwe.
Kulingana na idara ya mashtaka ya umma, waliouawa ni mwanamke kutoka Ethiopia na mwingine kutoka Kuwait, mwanamume wa Syria na Pakistani, na wanaume watatu wa Kuwait.
Kuwait imewanyonga karibu watu 80 tangu miaka ya 1960, wengi wao walikabiliwa na kesi za mauaji au dawa za kulevya.
Shirika la Amnesty International limeitaka nchi hiyo ya Ghuba kushinikizwa isitishe mauaji hayo.
Maelezo zaidi:
Virginia McLaurin: Ajuza aliyecheza densi na Obamas afariki akiwa na miaka 113

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanamke wa Washington DC ambaye aliifanikisha ndoto yake ya kucheza densi na Rais Barack Obama katika Ikulu ya White House amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 113.
Virginia McLaurin alikuwa na umri wa miaka 106 alipokutana na rais wa kwanza mweusi na mke wake mwaka wa 2016.
"Wacha nikwambie, Nina furaha sana," alimwambia Rais Obama wakati huo. "Rais mweusi, yay, na mke wake mweusi."
Mwaka 2014, ajuza huyo alianzisha ombi la mtandaoni kutaka kumuona. "Jina langu ni Virginia McLaurin," aliandika, "Naishi Washington DC. Nilizaliwa mwaka 1909."
"Sijawahi kukutana na Rais. Sikuwahi kufikiria ningemuona Rais mweusi wa nilizaliwa Kusini na sikufikiri ingetokea. "Nina furaha sana na ningependa kukutana nawe na familia yako ikiwezekana."
Mshonaji huyo wa zamani aliendelea: “Nakumbuka nyakati za kabla ya Rais Hoover. "Nakumbuka hatukuwa na umeme, niltumia taa ya mafuta ya taa, nakumbuka gari la kwanza la Ford.
"Mume wangu alikuwa katika Jeshi. Nilimpoteza mume wangu mwaka wa 1941. Nimekuwa DC tangu wakati huo. Nilikuwa nikiishi hapa wakati Martin Luther King aliuawa."
Uganda yawatoa hofu watalii kuhusu Ebola

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewahakikishia watalii kutoka mataifa ya kigeni kwamba mlipuko wa Ebola katika taifa hilo la Afrika Mashariki utadhibitiwa.
Katika hotuba yake kwa nchi siku ya Jumanne, rais Museveni alibainisha kuwa watalii wa kigeni walikuwa wakighairi kuweka nafasi na mikutano ya kimataifa ilikuwa inaghairishwa au kuhamishiwa katika nchi nyingine.
Alisema janga hilolipo ndani - na kesi zinazoendelea katika wilaya sita tu kati ya 146 kote nchini.
"Uganda iko salama na wageni wa kimataifa wanakaribishwa," aliongeza.
Alisema kuwa orodha ya watu walioambukizwa virusi hivyo imetolewa kwa mamlaka ya uhamiaji ili kuwazuia kusafiri kimataifa.
Baadhi ya kesi 141 zilizo na vifo 55 zimerekodiwa tangu kuzuka kwa ugonjwa huo kuthibitishwa mnamo Septemba.
Rais Museveni alisema kuwa mafanikio yamepatikana katika kudhibiti janga hilo. Kwa siku 18, hakukuwa na kesi zilizothibitishwa katika wilaya ya Mubende, kitovu cha mlipuko huo, ingawa kisa kimoja kiliripotiwa Jumatatu, kwa mujibu wa maafisa wa afya.
Bw Museveni alisema kuwa juhudi za kudhibiti janga hilo zinatatizwa na baadhi ya wananchi wanaokataa kuzingatia vikwazo vya afya. Usafiri wa pikipiki, unaojulikana kama boda boda, ulikuwa ukikaidi sheria za kutotoka nje katika maeneo yaliyoathiriwa na kusafirisha abiria badala ya mizigo pekee.
Katika wilaya ya Kassanda, watu 10 wa familia moja walikufa kwa ugonjwa wa Ebola baada ya kufukua maiti iliyozikwa na timu rasmi ya mazishi na kuzika tena kulingana na imani zao za kidini.
Jijini Kampala, watu wawili waliohusishwa na kesi tofauti walitoroka kutoka vituoni - moja hadi mji wa Masaka na mwingine katika jiji la Jinja - na wote wawili wamefariki dunia.
Ingawa janga hili limeenea katika wilaya mbali na kitovu katika eneo la kati, maafisa wa Uganda wanaonekana kuwa na imani kwamba mlipuko huo unaweza kudhibitiwa kabla haujasambaa.
Kwa picha: Kundi la pili la wanajeshi wa kenya wakielekea DR Congo

Chanzo cha picha, Richard Kagoe/BBC
Wanajeshi wa Kenya wanaanza safari ya kuelekea mashariki mwa Congo, kundi hili ni la pili kuelekea nchini humo kulinda amani.
Wakitokea katika uwanja wa ndege wa Embakasi, Kenya, imefanyika sherehe fupi ya kubadilisha benderea kati ya nchi hizo mbili.
Wanajeshi elfu moja wa Kenya wataungana na wenzao wa Burundi waliowasili DR Congo mapema mwezi Agosti kwa oparesheni ya pamoja dhidi ya waasi.

Chanzo cha picha, Richard Kagoe/BBC

Chanzo cha picha, Richard Kagoe/BBC

Chanzo cha picha, Richard Kagoe/BBC

Chanzo cha picha, Richard Kagoe/BBC
Watu kadhaa wanahofiwa kukwama katika jengo lililoporomoka jijini Nairobi
Wafanyakazi wa uokoaji wanawasaka takriban watu 10, wengi wao wakiwa wajenzi, wanaohofiwa kuwa wamekwama kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Jengo hilo la ghorofa saba lilikuwa bado linaendelea kujengwa lilipoanguka Jumanne alasiri katika eneo la Kasarani, viungani mwa jiji.
Msimamizi anayesimamia eneo hilo mara mbili alipuuza maonyo kutoka kwa mamlaka ya kukomesha kazi ya ujenzi kufuatia wasiwasi kuhusu uthabiti wake, tovuti ya habari ya Nation inaripoti.
Kuporomoka kwa majengo yanayojengwa ni jambo la kawaida katika jiji hilo na mara nyingi husababisha vifo.
Vikosi vya dharura siku bado vipo kwenye eneo la tukio, huku mashine nzito zikisogeza vibao vya zege huku waokoaji wakijaribu kuwatafuta waliokuwa wamefukiwa kwenye vifusi.
Ruka YouTube ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazoMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa YouTube ujumbe
Jeshi la Ukraine linadai kuangusha makombora 73 kati ya zaidi ya 90 yaliyorushwa na Urusi
Uongozi wa Jeshi la Wanahewa la Ukraine umeidhinisha kwamba, kulingana na data yake ya awali, wakati wa shambulio kubwa la kombora la leo, makombora 73 kati ya zaidi ya 90 yaliyorushwa na Warusi, pamoja na dronei zote 10 za kamikaze za Shahed, zilitunguliwa.
Kulingana na ripoti ya amri ya Jeshi la Wanahewa la Ukraine, Warusi walifyatua takriban makombora 70 ya Kh-101 na Kh-555 kutoka kwa ndege 14 za kubeba makombora ya Tu-95 kutoka eneo la Bahari ya Caspian na kutoka mkoa wa Rostov, karibu makombora 20 ya kusafiri ya Kalibr kutoka kwa meli katika Bahari Nyeusi, pamoja na drones 10 za kamikaze.
Wakati wa vita, BBC haiwezi kuthibitisha mara moja madai ya wapiganaji.
Mashambulizi ya Urusi yanaashiria kuwa haitaki kumaliza vita - Zelensky

Chanzo cha picha, Ukrainian President's Office
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mashambulizi ya makombora ya Jumanne ya Urusi dhidi ya Ukraine yalikuwa ujumbe wa Moscow kwamba haina nia ya kumaliza vita.
Katika hotuba yake ya usiku, Zelensky alisema jumla ya makombora 90 yalirushwa, na kuharibu miundombinu ya nishati, pamoja na biashara na majengo ya makazi.
“Na ilitokea lini? Mara tu baada ya siku ya kwanza ya mkutano wa kilele wa G20 kumalizika nchini Indonesia," alisema, baadaye akirejelea tukio hilo kama "G19", dharau kali ya Moscow.
"Urusi inaambiwa kuhusu amani, lakini inarusha makombora kujibu. Inaambiwa juu ya machafuko ya kimataifa ambayo Urusi ilisababisha, na inazindua droni za Irani kujibu.
Zelensky alisema mashambulizi hayo yamesababisha kukatika kwa umeme kote nchini, ikiwemo katika mikoa ya Kyiv, Lviv, Kharkiv na Zhytomyr.
“Hili ndilo jibu la Urusi kwa Indonesia, India, China na nchi nyingine zote zilizozungumzia haja ya kumaliza vita. Urusi inauambia ulimwengu kwamba inataka kuendelea. Sasa ni wakati wa dunia kujibu,” alisema.
Zelensky aliongeza kuwa zaidi ya makombora 70 na ndege zisizo na rubani 10 zimedunguliwa, akiwashukuru "washirika wote wanaosaidia kulinda anga".
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alikuwa mjini Bali kama mwakilishi wa nchi yake katika G20 lakini aliondoka kwenye mkutano huo mapema Jumanne jioni kabla ya mashambulizi ya Urusi.
Kundi la pili la wanajeshi wa Kenya kuwasili DR Congo leo,

Chanzo cha picha, AFP
Kundi la pili la wanajeshi wa Kenya wanatarajiwa kuwasili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo. Wao ni sehemu ya kikosi cha kikanda kilichotumwa kwa misheni ya kulinda amani mashariki mwa nchi.
Makundi yenye silaha yameongeza mashambulizi katika miezi ya hivi karibuni na kuibua wasiwasi kuhusu tishio wanalotoa kwa usalama wa eneo hilo.
Zaidi ya wanajeshi 900 wa Kenya watakuwa na makao yao karibu na mji wa Goma katika eneo hilo lenye hali tete.
Wanaungana na wanajeshi wa Burundi ambao wamekuwa wakifanya kazi katika jimbo la Kivu Kusini tangu Agosti.
Watasaidia jeshi la Congo kupambana na waasi ambao wamefanya uharibifu katika mwaka uliopita.
Wakiongozwa na kundi la M23, wameteka maeneo zaidi katika miezi ya hivi karibuni na kuwahamisha maelfu ya watu.
Serikali ya Congo inatazamiwa kuanza tena mazungumzo na wawakilishi wa makundi mbalimbali yenye silaha baadaye mwezi huu katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Trump kuwania tena urais wa Marekani 2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza nia yake ya kugombea tena Urais na kurudi Ikulu ya White House mnamo 2024.
Trump alizindua nia yake hiyo - ya tatu ya urais - siku ya Jumanne katika eneo lake la Mar-a-Lago huko Florida, wiki moja baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula ambapo Republican walishindwa kushinda viti vingi katika Congress kama walivyotarajia.
Ni jaribio nadra sana la kiongozi wa zamani wa Marekani kutaka kutwaa tena Ikulu ya White House baada ya kushindwa katika uchaguzi.
Katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja na televisheni ya Marekani, Trump alizungumza na mamia ya wafuasi wake kwenye ukumbi uliopambwa kwa vinara kadhaa na kupambwa na bendera nyingi za Marekani.
"Ili kuifanya Amerika kuwa bora tena, leo usiku natangaza nia yangu ya kuwa rais wa Marekani," Trump alisema kwa umati wa wafadhili na wafuasi wa muda mrefu waliokuwa wakipunga simu.
"Ninagombea kwa sababu ninaamini ulimwengu bado haujaona utukufu wa kweli wa kile taifa hili linaweza kuwa," alisema. "Tutaweka tena Amerika kwanza," aliongeza.
Donald Trump anapozungumza huko Mar-a-Lago, wafuasi wanapokea simu za michango katika vikasha vyao vya barua pepe.
Rais wa Marekani Joe Biden aongoza kikao cha ''dharura",kujadili kombora lililoanguka Poland
Viongozi wa G7 katika mkutano wa G20 huko Bali wamekusanyika ili kujadili hali nchini Poland. Ikulu ya White House iliiita "meza ya dharura", na ilifanyika nyuma ya milango iliyofungwa.
Mwandishi mmoja aliuliza iwapo Rais wa Marekani Joe Biden anaweza kutoa taarifa kuhusu shambulizi la kombora lililoua watu wawili katika kijiji cha Poland karibu na Ukraine.
Biden alitoa jibu la "Hapana." Majibu kutoka kwa nchi za Nato, pamoja na Ikulu ya White House, yamekuwa ya tahadhari na hakuna lawama yoyote ambayo imehusishwa na kombora hilo bado.
Katika ujumbe wake wa Twitter, rais wa Marekani alisema amezungumza na Rais wa Poland Andrzej Duda na kutoa "uungaji mkono kamili kwa uchunguzi wa Poland kuhusu mlipuko huo".
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Poland yadai Kombora la Urusi limetua katika eneo lake na kuua wawili

Chanzo cha picha, EPA
Wizara ya mambo ya nje ya Poland imesema kuwa "kombora lililotengenezwa na Urusi" lilitua katika eneo lake na kuua watu wawili katika kijiji cha Przewodow.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lukasz Jasina aliongeza kuwa balozi wa Urusi nchini Poland ameitwa kutoa "maelezo ya kina mara moja" juu ya tukio hilo.Taarifa hiyo haisemi ni nani aliyerusha kombora hilo na pande zote mbili katika mzozo huo zimetumia mabomu yaliyotengenezwa na Urusi.
Przewodow iko kwenye mpaka wa Poland na Ukraine, na kaskazini mwa jiji la Lviv.Makombora yaripotiwa kushambulia kijiji cha Przewodow, yapata maili nne (6.4km) kaskazini mwa Ukraine, mapema Jumanne.
Raia wawili wa Poland waliuawa katika mlipuko huo, wazima moto walisema. Marekani na washirika wengine wa Magharibi wanachunguza lakini hawajathibitisha ripoti kwamba yalikuwa makombora ya Urusi yaliyopoteza mwelekeo.Urusi inakanusha kuhusika:
"Hakuna kombora tulilorusha karibu na mpaka wa jimbo la Ukraine na Poland " wizara yake ya ulinzi ilisema katika taarifa, na kuongeza kuwa ripoti hizo ni "uchochezi wa makusudi unaolenga kuzidisha hali hiyo".
Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki amewataka watu kuwa watulivu baada ya kombora lililotengenezwa na Urusi kuwaua watu wawili katika kijiji cha Poland karibu na mpaka wa Ukraine.
"Ninatoa wito kwa Wapoland wote kuwa watulivu katika kukabiliana na janga hili... Ni lazima tujizuie na kuwa waangalifu," Morawiecki alisema baada ya mikutano ya dharura ya serikali huko Warsaw.
Pia alisema kuwa Poland itaongeza ufuatiliaji wa anga yake kufuatia tukio hilo."Tuliamua kuongeza utayari wa kupambana na vitengo vilivyochaguliwa vya jeshi la Poland, kwa msisitizo maalum katika ufuatiliaji wa anga," aliwaambia waandishi wa habari.
