Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mashambulizi ya Ukraine ya kukabiliana na Urusi hayatabadili mipango ya Urusi – Putin

Mashambulio ya hivi karibuni ya kukabiliana na vita vya Urusi hayatabadili mipango ya Urusi, Vladimir Putin amesema katika kauli zake za kwanza kwa umma kuhusu sula hilo.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Raia wa China akamatwa nchini Nigeria kwa madai ya kumuua mpenzi Mnigeria

    Mwanaume mmoja raia wa China amekamatwa nchini Nigeria kwa madai ya kumuua mpenzi wake raia wa Nigeria katika mji wa kaskazini wa Kano. Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid anaripoti kutoka Abuja.

    Msemaji wa polisi katika jimbo la Kano (Abdullahi Haruna) aliiambia BBC mfanyabiashara huyo mwenye asili ya China anazuiliwa na kuhojiwa na polisi.

    Mshukiwa (Geng Quantong) alidaiwa kujilazimisha katika nyumba ya familia ya msichana huyo, na kumshambulia na kumkata koo kwa kisu.

    Madaktari katika hospitali ya eneo hilo walithibitisha kuwa alikuwa amefariki alipofika.

    Mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 22.

    Mshukiwa alikamatwa alipokuwa akijaribu kutoroka eneo la tukio.

    Haijulikani ni nini hasa kilisababisha kisa hicho Ijumaa usiku.

    Lakini wakaazi na vyanzo vya familia vinasema wapenzi hao waliokuwa wameachana walianza kuwa na matatizo wakati marehemu (Ummulkulthum Sani) alipoonyesha kwamba hakuwa na nia tena ya kuolewa na Mchina huyo.

    Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 47 bado hajatoa maoni yake hadharani.

    Mauaji hayo yameibua hasira za umma huku familia ya mwathiriwa ikitaka haki itendeke.

  3. Rais Museveni asema Uganda itamtafuta mwekezaji mwingine iwapo kampuni ya Total italisikiliza Bunge la Ulaya

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni asema nchi hiyo itamtafuta mwekezaji mwingine wa kufanya naye kazi iwapo kampuni ya mafuta ya Total Energies itachagua kusikiliza Bunge la Umoja wa Ulaya linalozitaka Uganda na Tanzania kusitisha maendeleo ya mradi wa bomba la mafuta na gesi katika nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.

    Museveni aliuambia mkutano mjini Kampala siku ya Ijumaa kuwa mradi wa mafuta utaendelea kama ilivyoainishwa katika mkataba na Total Energies na Kampuni ya kitaifa ya Mafuta ya China, CNOOC. Alisema pipa la kwanza la mafuta litatoka mnamo 2025.

    Bunge la Umoja wa Ulaya Alhamisi lilionya kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na hatari ya kijamii na kimazingira inayoletwa na mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki, EACOP.

  4. Vikosi vya Somalia vyawauwa wajumbe thelathini wa Al-Shabaab

    Vikosi vya serikali ya Somalia vimefanya mashambulio katika jimbo la Hiran, kaskazini- magharibi mwa nchi hiyo, na kuwauwa wajumbe wa kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab.

    Shirika la habari la somalia, SONNA, limeripoti kuwa vikosi vya nchi hiyo vimepigana Ijumaa usiku katika eneo lililopo karibu na Abourey Al Shabaab, ambayo iko kilomita takriban 25 mashariki mwa mji wa Beledweyne,mji mkuu wa jimbo la Hiran.

    Wanajeshi watano wamejeruhiwa katika shambulio.

    Vikosi vya serikali ya Somalia kwa ushirikiano na vikosi vya kimataifa vilivyopo nchini humo hivi karibuni vimeimarisha harakati za usalama dhidi ya makundi ya Jihadi yanayopigana katika majimbo ya kusini na kati mwa Somalia.

  5. David Beckham apanga foleni kwa ajili ya kuutazama mwili wa Malkia : Uzoefu huu ‘unafaa kuwa wa kushirikishana’

    Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya Egland David Beckham amesema ameshukuru muda aliotumia kushirikiana na umma wa watu wengine waliokuwa wamepanga msururu kwa ajili ya kumuona Malkia Elizabeth. Baada ya kusimama kwenye mstari kwa saa 12 amesema alitaka "kusherehekea maisha mazuri ya ajabu ya Malkia wetu".

  6. Malkia Elizabeth II: Ibada maalum kwa ajili ya Malkia kufanyika katika kanisa alikosali Malkia Kenya

    Nchini Kenya, ibada maalumu ya kumuombea Malkia itafanyika baadaye leokatika kanisa la ambapo Malkia Elizabeth alikwenda kabla ya kutangazwa kuwa Malkia.

    Zawadi zilizotolewa na Malkia kwa kanisa la Kianglikana la St. Philips bado zimetunzwa katika kanisa hilo.

    Chini ya Mlima Kenya kando ya mto Naro Moru, ndipo linapopatikana Kanisa la zamani la Kianglikana lenye kumbukumbu zinazohusiana na Malkia . Ni katika kanisa hilo ambako Malkia alihudhuria ibada ya Jumapili akiwa Bintimfalme mwezi Februari mwaka 1952.

    Siku chahe baadaye alipokuwa katika hoteli ya malazi -Treetops Lodge karibu na kanisa hilo, baba yakeMfalme George VI, alifariki na Bintimfalme Elizabeth akawa Malkia.

    Kwa miaka, uhusiano wake na kanisa ulihifadhiwa. Ngao yake inang’inia ndani ya jengo hilo dogo lililojengwa kwa mawe. Kipande cha zulia alilotembea juu yake wakati wa kutawazwa kwake linaonyeshwa.

    Na nje ya kanisa hili, mti alioupanda katika siku ile ya Jumapili bado umesimama.

    Leo waumini wa kanisa la kianglikana la St. Philips watafanya ibada maalumu kwa ajili ya heshima yake Malkia.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mwanaume akamatwa baada ya kulisogelea jeneza la Malkia
    • Taji la kifalme linalong'aa juu ya jeneza la Malkia
    • Nyumba gani kati ya nyingi za kifalme atakayoishi Mfalme Charles wa Uingereza?
  7. Polisi Ufaransa wawakamata washukiwa wa genge la wizi wanaovaa wigi ndani ya treni

    Washukiwa wa genge la wezi wanaodaiwa kuiba mali zenye thamani ya euro 300,000 (£260,000) kutoka kwa wasafiri wa daraja la kwanza la treni nchini Ufaransa wamekamatwa.

    Inadhaniwa kuwa waliiba mizigo hiyo baada ya kuketi kando yao katika treni za mwendo kasi nchini humo.

    Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 57, anasemekana kujifanya kama mwanamke, aliyevaa wigi.

    Yeye na wanaume wengine, mmoja mwenye umri wa miaka 47 na mwingine mwenye umri wa miaka 40, wamekiri kutekeleza wizi huo, kwa kipindi cha kati ya miaka mitano na sita, vimesema vyombo vya habari vya Ufaransa.

    Wanaaminiwa kuhifadhi mali hizo za wizi katika jengo la gorofa lililopo katika mji waMarseille.

    Mbinu ya watu hao ilikuwa ni kuiba mali wakati treni zinaposimama kwenye kituo baada ya wamiliki wa mali hizo kutoka nje kunyoosha miguu au kuvuta sigara.

  8. Mashambulizi yaUkraine ya kukabiliana na Urusi hayatabadili mipango ya Urusi – Putin

    Mashambulio ya hivi karibuni ya kukabiliana na vita vya Urusi hayatabadili mipango ya Urusi, Vladimir Putin amesema katika kauli zake za kwanza kwa umma kuhusu sula hilo.

    Katika mashambulio ya haraka ya kukabiliana na mashambulio ya Urusi, vikosi vya Ukraine vinasema viliweza kutekaeneo la kimolita za mraba 8,000 (saw ana maili 3,000 za mraba ) katika kipindi cha siku sita katika jimbo la kaskazini-magharabi la Kharkiv.

    Lakini Bw Putin alisema kuwa hana haraka, na mashambulizi ya jimbo la Ukraine la Donbas bado yanaendelea.

    Pia alisema kuwa Urusi hadi sasa haijapeleka vikosi vyake kamili.

    "Mashambulizi yetu katika Donbas hayakomi. Yanasonga mbele – sio kwa kasi sana – lakini wanaendelea taratibu kuyateka maeneo zaidi na zaidi ," alisema baada ya mkutano katika Uzbekistan.

    Mji wa viwanda wawa jimbo la Donbas uliopo mashariki mwa Ukraine unalengwa katika uvamizi wa Urusi, ambapo Bw Putin anadai ni muhimu kuuteka ili kunusuru wazungumzaji wa Kirusi na mauaji ya kimbari.

    Sehemu za Donbas zilitwaliwa na wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi tangu mwaka 2014.

    Jimbo la Kharkiv, ambako hivi karibuni Ukraine ilifanya mashambulio ya kukabiliana na uvamizi, sio sehemu ya Donbas.

    Katika kauli za Ijumaa, Bw Putin alitishia kujibu ’’vikali zaidi’’ iwapo mashambulizi ya Ukraine yataendelea.

    Unaweza pia kusoma:

    • Biden amuonya Putin asitumie silaha za kimbinu za nyuklia
    • Mzozo wa Ukraine: Jinsi Rais Erdogan anavyouma na kupuliza kwa ndimi mbili
  9. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo Jumamosi tarehe 17.09.2022