‘Urusi itakomesha mashambulizi ikiwa Ukraine itajisalimisha’- Kremlin
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mara kwa mara wanajeshi wa nchi yake hawatasalimu amri na kwamba hatimaye watakuwa washindi katika vita hivyo.
Moja kwa moja
Tanzania: Vyuo vikuu vyaonywa kuwa huenda wakatengeneza wahitimu ambao soko litawakataa
Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania kwa kwa mara ya kwanza ilitoa leseni kwa vyombo vya habari mtandao mwaka 2018 baada ya kuweka kanuni na miongozo ya kuwawezesha kufanya kazi kwa mujibu wa sheria Wakati kukiwa na mabadiliko yote haya wapo baadhii ya wanafunzi katika vyuo vya uandishi wa habari wanaiona mitandao ya kijamii kama kitovu cha upotoshaji. ‘’Kama vyuo vikuu havitabadikika kwa sasa watajikuta wanatengeneza wahitimu ambao soko litawakataa” – anasema Dotto Bulendu, Mkufunzi katika Chuo kikuu cha uandishi wa habari cha Sauti nchini Tanzania.
BBC imezungumza na wanafunzi katika Chuo kikuu cha Sauti nchini Tanzania kuhusu maendeleo ya sekta ya habari na changamoto zake hususan wakati huu ambapo upatikanaji wa taarifa za mitandao ya kijamii umekuwa rahisi:
Maelezo ya video, ‘’Kama vyuo vikuu havitabadilika kwa sasa watajikuta wanatengeneza wahitimu ambao soko litawakataa''- Dotto Bulendu Mwanaume akamatwa kwa kumzaba kofi mbunge kanisani Uganda

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ripoti moja ilisema Mbunge alikuwa katika eneo la kanisa kutoa trekta kwa wakulima (picha ya maktaba file photo) Mwanaume mmoja amekamatwa magharibi mwa Uganda na kushikiliwa katika mahabusu ya polisi baada ya kumzaba makofi mbunge katika kanisa moja Jumapili, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 39 alimvamia Waziri wa uchukuziambaye pia ni mbunge, Musa Ecweru alipokuwa akitoa hotuba kwa kusanyiko la waumini katika kanisa la kikatoliki la Mtakatifu Michael (St Michael Catholic Church) mjini Amuria.
"Hakujibu bali alimtazama tu. Wakristo na mapadre walishtuka,", chanzo kimoja ambacho hakikutajwa jina kililiambia gazeti linalomilikiwa na serikali nchini humo la New Vision
Walinzi wa Ecweru hatimaye walimzidi nguvu mwanaume huyo, wakamkamata na kumkabidhi kwa polisi, zilisema ripoti za vyombo vya habari.
Miaka 65 ya BBC Swahili: Tunakupakulia picha,sauti na mandhari ya mji wa Bukavu nchini DRC
Maelezo ya video, Tunakupakulia Picha,Sauti na mandhari ya mji wa Bukavu nchini DRC Wiki hii BBC Swahili imekuwa ikikuletea matangazo maalum ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanza matangazo yake .
Mojawapo ya maeneo ambayo wanahabari wetu wamekita kambi ili kukuleta taarifa mji wa Bukavu ,ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo .
Huu hapa msururu wa video na Picha zilizotumwa na wanahabari wetu walioko Bukavu zinaoonyesha vivutio na mengi mazuri katika mji huo

Maelezo ya picha, Shule ya Wasichana ya Lycée Wima,Bukavu 
Maelezo ya picha, Majengo yanavyoonekana kwa mbali pembeni mwa ziwa Kivu,Bukavu 
Maelezo ya picha, Ziwa Kivu,mojawapo ya vivituo vya kupendeza katika mji wa Bukavu,DRC 
Maelezo ya picha, Mnara wa wanajeshi katikati ya mji wa Bukavu, DRC 
Maelezo ya picha, Majengo katika mji wa Bukavu 
Maelezo ya picha, Ziwa Kivu linavyoonekana kwa mbali ,mjini Bukavu 
Maelezo ya picha, Shule ya Wasichana ya Lycée Wima,Bukavu Taarifa zaidi kuhusu Maadhimisho ya Miaka 65 ya BBC Swahili:
- 'Tulipata habari mtu aliyekuwa anawania urais Marekani alikuwa amezaliwa Kenya'
- Miaka 65 ya BBC Swahili: Aliyekuwa mkuu wa BBC Swahili Tido Mhando azungumza
- Idhaa ya Kiswahili ya BBC ikitimiza miaka 65
Miaka 65 ya BBC Swahili - Zanzibar: Hapa kuna milango iliyodumu kwa miaka zaidi ya 400
Moja ya miji ya kihistoria inayotambuliwa na Shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO kama urithi wa dunia, ni Mji Mkongwe, ama Stone Town, ZANZIBAR.
Moja ya sifa kubwa ya mji huu ni upekee wa Milango ya nyumba zake inayoupa umaarufu mkubwa na kuvutia wageni.
Milango hii ni mikongwe na inayoweza kudumu kwa zaidi ya miaka 200, inaitwa Milango ya Zanzibar ama Zanzibar Door.
Mwandishi wetu Yusuph Mazimu ametembelea mji huo na kukuta mlango unaotajwa kuwa mkongwe zaidi Zanzibar na moja ya milango mikongwe zaidi Afrika. Una miaka zaidi ya 400. Je nini siri ya kudumu kwa milango ya Zanzibar?
Maelezo ya video, Milango ya Zanzibar iliyodumu kwa zaidi ya miaka 400 Taarifa zaidi kuhusu Maadhimisho ya Miaka 65 ya BBC Swahili:
- 'Tulipata habari mtu aliyekuwa anawania urais Marekani alikuwa amezaliwa Kenya'
- Miaka 65 ya BBC Swahili: Aliyekuwa mkuu wa BBC Swahili Tido Mhando azungumza
- Idhaa ya Kiswahili ya BBC ikitimiza miaka 65
Urusi itakomesha mashambulizi ikiwa Ukraine itajisalimisha - Kremlin

Chanzo cha picha, Dmitry Peskov
Tumepata kusikia mengi zaidi kutoka kwa Dmitry Peskov, msemaji wa Kremlin.
Anasema Urusi itamaliza mashambulizi yake nchini Ukraine punde tu Kyiv itakapojisalimisha.
Anazitaka mamlaka za Ukraine kuamuru wanajeshi wao kuweka silaha chini.
"Upande wa Ukraine unaweza kusimamisha kila kitu kabla ya mwisho wa leo," Peskov alisema, kulingana na shirika la habari la Agence France-Presse.
"Amri kwa vitengo vya utaifa kuweka chini silaha zao ni muhimu."
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mara kwa mara wanajeshi wa nchi yake hawatasalimu amri na kwamba hatimaye watakuwa washindi katika vita hivyo.
Baada ya mkutano wa G7 kukamilika, viongozi wa dunia wanatarajiwa mjini Madrid baadaye kwa mkutano wa kilele wa muungano wa Nato, ambapo wanatarajiwa kuidhinisha mipango ya kuongeza idadi ya wanajeshi walio katika hali ya tahadhari hadi zaidi ya 300,000.
Ikizungumza kabla ya mkutano huo, Kremlin inaelezea Nato kama "kambi yenye fujo" iliyoundwa kwa makabiliano, kulingana na shirika la habari la Reuters.
Maoni ya msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov yanakuja baada ya G7 kukutana hapo awali - na kutoa kauli zake juu ya hatua dhidi ya mafuta ya Urusi, dhahabu, na mzozo wa chakula duniani.
Katika mkutano na waandishi wa habari, anasema uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine - ambayo inaiita operesheni maalum ya kijeshi – itaendelea na itafikia malengo yake.
Nato - Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini - ni muungano wa kijeshi unaojihami na wanachama 30. Wanachama wanakubali kusaidiana iwapo watashambuliwa kwa kutumia silaha.
Uswidi na Finland zimetuma maombi ya kujiunga na muungano huo kwa sababu ya vita nchini Ukraine.
Soma zaidi
Kenya ’imeaibishwa’ na biashara haramu ya watoto iliyofichuliwa na BBC
Mkurugenzi wa mashitaka ya umma nchini Kenya anasema "ameaibishwa " na ufichuzi wamakala ya BBC Africa Eye kuhusu usafirishaji haramu wa watoto walemavu wanaoletwa kutoka Tanzania hadi Kenya kwa ajili ya faida.
“Kusema ukweli nmeaibika na sio kujaribu kutoa sababu, ninaahidi kuchukua jukumu hili mimi mwenyewe lakini kitu bora zaidi ni kwetu sisi kuwa na mazungumzo kama wana Afrika Mashariki", Noordin Haji alisema Jumanne.
"Ushawishi utakuwa ndio moja ya mambo bora zaidi, ngoja tuwahusishe wanasiasa, wafanyakazi wa umma- kama tutaweza kukubalianana kuwa na lengo, ninaweza kukuhakikishia nitakuwa sehemu ya hilo na pia kuwajumuisha wenzangu katika mfumo wa sheria za uhalifu," aliongeza.
Wakati huo huo Tanzania imeelezwa ‘’kusikitishwa kwake’’ na matokeo ya ufichuzi wa BBC, na imesema kuwa tayari’’inafanya kazi pamoja ‘’ na Kenya kukabiliana na usafirishaji haramu wa watoto.
Waathiriwa wengi katika visa hivu huchukuliwa kutoka kwa wazazi wao wakiahidiwa maisha bora. Lakini mara wanapofika mjini Nairobi wanalazimishwa kuwa ombaomba kwenye mitaa huku pesa wanazopewa zikienda mikononi mwa waliowateka
Tazama uchunguzi wa BBC Africa Eye:
Maelezo ya video, BBC Africa Eye: Ufuchuzi wa watoto wa Kitanzania wanaopelekwa Kenya kuwa ombaomba mitaani Polisi wa Afrika Kusini kufanya uchunguzi kwenye mabaa baada ya vijana 21 kufariki

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, imu za uchunguzi zilichunguza kilichotokea kwenye eneo la tukio Polisi wa Afrika Kusini Jumatatu walikuwa wakifanya uchunguzi katika baa ambapo vijana 21 walifariki kwa njia isiyoeleweka huku manusura wakielezea vita vya kutoroka eneo lililokuwa limejaa msongamano wa watu huku mtu mmoja akisema kulikuwa na ukosefu wa hewa safi.
Wengi wa wahasiriwa, wengine wakiwa na umri wa miaka 13, walipatikana wamefariki ndani ya baa maarufu katika jiji la kusini mwa London Mashariki.
11 walifariki dunia ndani ya baa hiyo, huku wanne wakifia hospitalini.
Wengine 31 walilazwa hospitalini wakiwa na dalili zikiwemo maumivu ya mgongo, vifua kubana, kutapika na maumivu ya kichwa, afisa alisema.
Wengi waliruhusiwa kuondoka hospitali siku ya Jumapili huku wengine wawili wakisalia hospitalini, walisema.
Bw Cele, ambaye alitembelea eneo la tukio na kupewa taarifa na polisi wa eneo hilo, alisema waliofariki walikuwa na umri wa kati ya miaka 13 na 17 - lakini orodha ya kina ya wahasiriwa wakati huo haikuwa imetolewa.
Umri wa chini wa kisheria wa kunywa pombe nchini Afrika Kusini ni miaka 18.
Kuna ripoti kwamba watu waliokuwa wameenda kujivinjari walikuwa wakisherehekea mwisho wa mitihani ya shule.
Kundi la kwanza la wauguzi wanaokwenda kufanya kazi Uingereza liko tayari

Chanzo cha picha, ASTER GUARDIANS
Maelezo ya picha, Wauguzi wanaokwenda Uingereza waagwa rasmi Kenya Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe Jumatatu aliwaaga rasmi kundi la wauguzi 19 wa Kenya ambao wameajiriwa kufanya kazi nchini Uingereza.
Hii inafuatia makubaliano ya pande mbili kati ya Kenya na Uingereza yaliyotiwa saini na Rais Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson Julai mwaka jana.
Bw Kagwe alisema kuwa mchakato mkali ulifanywa ili kupata orodha ya mwisho kutoka kwa wauguzi 3,329 waliotuma maombi mwaka jana.
Kati ya 19 waliohitimu, 13 wataambatanishwa na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Oxford na wataondoka nchini Juni 28. Sita waliosalia ambao mahali pa kazi bado hapajatambuliwa, watasafiri hadi Uingereza baada ya wiki mbili.
Pia, wengine ni wauguzi 80 waliohitimu ambao watakuwa sehemu ya kundi la pili.
Bw Kagwe aliwataka wauguzi wengine pia kuangalia fursa kama hizo na kutuma maombi.
“Wahudumu wa afya wa Kenya wanapaswa kuwa na mawazo mapana. Ukweli kwamba ulifunzwa nchini Kenya hakupaswi kukuweka Kenya pekee. Fikiri kwa mapana na utafute fursa nje ya nchi. Hufanyi mazoezi ya maisha. Katika nafasi moja uliyonayo, panua fikra zako na ufanye kazi katika maeneo mengine,” alisema.
Alirejelea hitaji la Kenya kuwa kitovu cha utalii wa afya akisema kuwa kuajiri wauguzi hao hadi Uingereza kunaonyesha ubora wa mafunzo yaliyotolewa na taasisi zetu za ndani.
Ethiopia yaunda timu kwa ajili ya mazungumzo ya amani ya Tigray

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mchakato wa amani wa Ethiopia utaongozwa na waziri wa mambo ya nje Serikali ya Ethiopia inasema imeunda kamati ya watu saba kufanya mazungumzo ya amani na vikosi vya Tigrayan katika jitihada za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 19.
Itaongozwa na naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Demeke Mekonen.
Waziri wa Sheria wa Ethiopia Gediwon Timothios - ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo - alisema chama tawala kitakubali tu Umoja wa Afrika kuongoza mchakato wa amani.
Waandishi wa habari wanasema hiki ni kikwazo kinachoweza kuwa kikwazo kwa mazungumzo kwani vikosi vya Tigrayan vimekosoa juhudi za AU na vimesema vinamtaka Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuwa mpatanishi.
Soma:
Hatma ya wakili Paul Gicheru wa Kenya yasalia katika mikono ya majaji wa ICC

Chanzo cha picha, icc
Maelezo ya picha, Majaji wanaoamua kesi ya wakili wa Kenya paul Gicheru Mahakama ya ICC mjini the Hague Uholanzi hapo jana ilifunga kesi ya wakili Paul Gicheru kuhusu madai ya kuwahonga mashahidi ambao walitarajiwa kutoa ushahidi wao dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto kuhusiana na ghasia za uchaguzi za 2007ambazo zilisababisha mauaji ya watu 1200.
Wakili wake na waendesha mashtaka wa ICC walilumbana mwisho wa kesi hiyo ambayo ilichukua takriban miezi 19, ambapo Ruto alitajwa mara kadhaa. Jaji Miatta Maria Samba alisema mahakama hiyo itajadiliana kuhusu kesi hiyo na katika wakati ufaao itatoa uamuzi wake kuhusu iwapo atakuwa hatiani au atawachiliwa huru.
Kulingana na gazeti la Nation, ofisi ya mwendesha mashtaka ikiongozwa na wakili Anton Steyberg ilisisitiza mshukiwa huyo kuwekwa hatiani lakini mawakili waliokuwa wakimtetea bwana Gicheru walikosoa kiwango cha uchunguzi na kuiomba mahakama kumuondolea kesi mteja wake.
Wakili wa Gicheru Michael Karnavas alisema kwamba ofisi ya mwendesha mashtaka haikufanya uchunguzi katika eneo la bonde la ufa , eneo ambao uhalifu ulitekelezwa , licha ya kwamba hawakuzuiliwa na serikali ya kenya.
Ikilinganishwa na kesi ya awali , ambapo eneo linalokaliwa na watu wanaofuatilia kesi hiyo halikuwa na mtu , kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliohudhuria katika kikao cha jana ambacho kilikuwa cha mwisho.
Makumi ya watu wauawa katika shambulizi kijijini Cameroon

Maelezo ya picha, Cameroon Kuna ripoti kwamba watu wasiopungua 26 wameuawa katika shambulio lililofanywa katika kijiji kimoja katika mikoa inayozungumza Kiingereza nchini Cameroon, ambapo wanajeshi wamekuwa wakipambana na waasi wanaotaka kujitenga kwa takriban miaka mitano.
Bado haijabainika ni nani aliyesababisha vurugu hizo.
Afisa wa afya wa wilaya alisema baadhi ya watu bado hawajulikani walipo baada ya shambulio katika kijiji cha Ballin, karibu na mpaka na Nigeria.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limewashutumu wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaozungumza Kiingereza kwa kufanya ukatili mwingi katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji nyara na kuchoma shule.
Boris Johnson: Wanasayansi wa Urusi - waalikwa kuhamia Uingereza!

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Johnson alisema kuwa wanasayansi wa Urusi, waliokasirishwa na sera za Putin, wanaweza kutuma maombi ya kuhamia Uingereza na kufanya kazi hapa na wenzao wa Ukraine. Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa mwaliko wazi kwa wanasayansi wa Urusi, wasioridhika na sera za Putin na hali ya nchi, kuhamia Uingereza, kulingana na gazeti la The Guardian la Uingereza.
Ofa hii kwa wanasayansi wa Urusi, Johnson alisema, ni upanuzi wa mfumo uliopo wa ushirikiano na vyuo vikuu vya Ukraine, kuruhusu wanasayansi wa Ukraine kuendelea na utafiti wao nchini Uingereza.
"Wasomi na watafiti wa Urusi wanaotazama vurugu za Putin kwa mshangao na ambao hawajisikii salama tena nchini Urusi: jisikieni huru kutuma maombi ya kuhamia Uingereza na kufanya kazi katika nchi inayothamini uwazi, uhuru na kutafuta maarifa," Johnson alisema.
Kama sehemu ya Mpango wa Watafiti walio katika Hatari , ambao bajeti yao sasa imeongezeka kwa karibu pauni milioni 10, wanasayansi wapatao 130 wa Ukraine watakuja Uingereza, gazeti la The Guardian limesema.
Mamlaka ya Uingereza sasa inatoa usaidizi sawa kwa wenzao wa Urusi.
Soma zaidi:
Chelsea yawasiliana rasmi na Man City kuhusu Raheem Sterling

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Raheem Sterling Chelsea wamefanya mawasiliano na Manchester City kuhusu kutaka kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling.
Sterling, ambaye alijiunga na City kutoka Liverpool kwa mkataba wa £49m mwaka 2015 na ambaye amefunga mabao 131 katika mechi 339, anasakwa sana na mmiliki mpya wa Blues Todd Boehly.
Inafahamika kuwa Chelsea bado hawajawasilisha ombi rasmi la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, lakini huenda ombi hilo likawasilishwa hivi karibuni.
Sterling amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na inafahamika kuwa anakagua chaguzi zake.
Sterling, ambaye ameichezea England mara 77, hajawahi kufanya siri yoyote ya kutaka kucheza kadiri awezavyo na kuwa kiungo wa kati katika timu ambayo ina changamoto ya kupata heshima kubwa.
Habari za hivi punde, Zelensky: Urusi imekuwa 'shirika kubwa la ugaidi' duniani

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Rais Zelensky Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema nini kuhusu mlipuko wa kituo cha maduka katika hotuba yake ya kila siku jana usiku.
Kiongozi huyo ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kumaliza "ugaidi wa Urusi", akisema kwamba mashambulizi ya makombora katika eneo la Kremenchuk Ukraine yamelifanya taifa la Vladimir Putin kuwa "shirika kubwa la kigaidi zaidi duniani".
Kufikia sasa, watu 18 wanakisiwa kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa lakini Zelensky alionya kuwa kunaweza kuwa na zaidi. "Bado [bado] tunatambua idadi ya watu chini ya vifusi," alisema.
Kuhusu mkutano wa viongozi wa G7 ambao umekuwa ukifanyika, alisema kumekuwa na "matokeo muhimu yaliyokubaliwa":
‘’Demokrasia zenye nguvu zaidi ulimwenguni zitasaidia serikali yetu mradi tu itahitajika kwa ushindi wetu. Ukraine haitavunjwa! Kamwe.
Soma zaidi:
Wanajeshi wa Urusi wajiandaa kufanya shambulio dhidi ya Sloyansk

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Gari la kijeshi la Ukraine likipita kwa kasi kwenye barabara kuu karibu na Sytnyaky, Ukraine. Tuanzie na eneo la Kharkiv, ambapo adui ameweka juhudi zake kuu katika kuzuia kusonga mbele kwa wanajeshi wa Ukraine, na anaendelea kufanya shughuli za mashambulizi ili kuboresha hali yake na kuzuia vitendo vya wanajeshi wa Ulinzi vya Ukraine.
Katika eneo la Slavyansk, wanajeshi wa Urusi wanatengeneza mazingira ya kushambulio Slavyansk.
Juhudi kuu zimejikita katika kuendeleza mashambulizi kuelekea Izyum - Slavyansk.
Hakukuwa na shughuli nyingi huko Kramatorsk, isipokuwa upigaji makombora dhidi ya makazi ya Mayaki na Tatyanovka.
Katika eneo la Lisichansk, adui hajaacha tumaini la kuchukua udhibiti wa barabara kuu ya Bakhmut-Lysichansk.
Huko Yuzhnobuzh, adui ameweka juhudi zake katika kushikilia maeneo ya awali yaliyokaliwa, kuzuia mashambulizi ya Ukraine katika mikoa ya Kherson na Nikolaev.
Kama ifuatavyo kutoka kwa ripoti hiyo, hakukuwa na mabadiliko kuhusiana na vita wakati wa usiku, vita vinaendelezwa katika maeneo mbalimbali, makombora yakirushwa katika maeneo ya makazi na wanajeshi wa Ukraine.
Soma zaidi:
Rais wa Ukraine amehutubia mkutano wa G7 kwa njia ya video

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Rais wa Ukraine alihutubia mkutano wa G7 na wawakilishi wawili wa EU kupitia kiunga cha video Viongozi wa mataifa saba tajiri zaidi duniani wameahidi kuiunga mkono Ukraine "kwa muda wote ule itachukua" katika siku ya pili ya mkutano wa kilele uliofanyika nchini Ujerumani.
Katika taarifa, kundi la G7 pia lilisema kwamba Urusi lazima ikome kuzuia chakula kutoka kwa bandari za Ukraine.
Akihutubia mkutano huo kwa njia ya video, rais wa Ukraine alitoa wito wa kuongezwa kwa silaha nzito kutoka kwa washirika wa Magharibi.
Viongozi wa G7 wako chini ya shinikizo la kuwa kitu kimoja katika mtazamo wao dhidi ya kuongezeka kwa uvamizi wa Urusi.
"Tutaendelea kutoa msaada wa kifedha, kibinadamu, kijeshi na kidiplomasia na kusimama na Ukraine kwa muda wote itachukua," walisema katika taarifa yenye maneno makali siku ya Jumatatu. Tunasalia kustaajabishwa na tunaendelea kulaani vita vya kikatili, visivyochochewa, visivyofaa na visivyo halali vya uchokozi dhidi ya Ukraine na Urusi na kusaidiwa na Belarus."
Viongozi wa G7 - Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani - wameungana huko Bavaria, Ujerumani na wawakilishi wawili kutoka Umoja wa Ulaya.
Mazungumzo hayo ya ngazi ya juu yalifanyika huku vikosi vya Urusi vikizidisha mashambulizi yao dhidi ya Ukraine, ambapo maafisa walisema kituo cha biashara chenye shughuli nyingi kilipigwa na kombora katikati mwa jiji la Kremenchuk na kuua watu wasio na hatia kulingana na gavana wa eneo hilo.
Soma zaidi
Urusi yashambulia eneo la manunuzi Ukraine

Maelezo ya picha, Urusi yafanya shambulizi katika eneo la manunuzi Ukraine Takriban watu 16 wamefariki dunia katika shambulizi la kombora lililolenga sehemu ya manunuzi yenye maduka mengi katika mji wa Kremenchuk nchini Ukraine.
Raia wapatao 1,000 walikadiriwa kuwa ndani ya jumba hilo lenye shughuli nyingi wakati wa shambulio hilo linatokea mwendo wa saa 15:50 (12:50 GMT), Rais Volodymyr Zelensky alisema.
Viongozi wa kundi la G7 la mataifa tajiri zaidi - wanaokutana nchini Ujerumani - wamelaani shambulio hilo na kusema "uovu usio kubalika".
"Mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia wasio na hatia ni uhalifu wa kivita," walisema katika taarifa ya pamoja.
Urusi imelaumiwa kwa shambulio hilo ambalo pia lilijeruhi takriban watu 59, na kuna hofu kwamba idadi ya waliouawa itaendelea kuongezeka.
Picha mtandaoni zilionyesha jengo hilo likiteketea kwa moto na moshi mzito mweusi ukitanda angani.
Rais wa Ukraine Zelensky alielezea shambulio hilo kama moja ya "vitendo vya kigaidi" vya ukatili zaidi katika historia ya Ulaya".
Alisema maduka hayo hayana thamani ya kimkakati kwa Urusi, na hayaleti hatari kwa vikosi vyake - "ni jaribio tu la watu kuishi maisha ya kawaida, ambalo linawakasirisha waliowakalia."
Ni magaidi wenye wazimu kabisa, ambao hawapaswi kuwa na nafasi duniani, wanaweza kupiga makombora kitu kama hicho," aliongeza.
Kremlin bado haijazungumza lolote kuhusiana na shambulio hilo, na mara zote imekanusha kuwalenga raia.
Gavana wa eneo hilo Dmytro Lunin alielezea shambulio hilo kama uhalifu dhidi ya ubinadamu, akiandika kwenye Telegram kwamba ni " kitendo cha wazi na ugaidi dhidi ya raia."
Huduma ya Dharura ya Jimbo la Ukraine, ambayo ilitoa taarifa juu ya idadi ya vifo na majeruhi, ilisema vitengo 57 vilihusika katika kupambana na moto huo.
Ilichapisha picha zinazoonyesha eneo la juu la jengo lililokuwa limetanda weusi na kuungua. Katika video moja iliyochukuliwa muda mfupi baada ya shambulio hilo, mwanamume alisikika akisema: "Je, kuna mtu yeyote aliye hai ... mtu yeyote yuko hai? "
Kidogo gari la wagonjwa lilifika kuwapeleka majeruhi hospitali.
Lakini bado kuna watu hawajulikani walipo, na ilipofika usiku wanafamilia walikusanyika katika hoteli moja kando ya barabara, ambapo waokoaji wameweka kituo cha kusubiri habari zozote.
Soma zaidi:
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja




