Akina mama wa Urusi wanawasaidia wanao ambao hawataki kupigana

Siku ya Jumatatu mashambulizi ya mabomu ya Severodonetsk - katika jimbo la Donbas - yalionekana kufikia hatua mbaya.

Moja kwa moja

  1. na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Uchaguzi Kenya 2022: Wingu la madai ya vyeti feki latanda katika kampeni Kenya

    Wanasiasa Wakenya kadhaa wanaogombea viti vya ugavana wanakabiliwa na changamoto ya kupata idhini ya mwisho ya kugombea nyadhifa hizo kwani wanadaiwa kutumia vyeti feki vya shahada.

    Sheria za Kenya zinamtaka kila mtu anayetaka kuchaguliwa kuwa gavana au rais kw na walau shahada ya chuo kikuu.

    Katika kaunti ya Machakos, inayopakana na jiji kuu la Nairobi, wapiga kura wawili wametuma malalamiko yao katika Tume ya uchaguzi wakitaka mgombea Wavinya Ndeti azuiwe kugombea kwa madai kuwa shahada yake ya masomo ya Sayansi ya kompyuta aliyodai kuipata kuyoka Uingereza ni gushi.

    Katika mji mkuu Nairobi, Johnson Sakaja –ambaye ni mgombea wa ugavana atika chama cha mgombea aliye mstari wa mbele katika uchaguzi wa rais na Naibu rais William Ruto – pia anahangaika kuhakikisha juhudi za kutaka asigombee kiti hicho zisifanikiwe.

    Awali Bw Sakaja alikuwa ameidhidnishwa na Tume ya uchaguzi (IEBC) kugombea , lakini madai kwamba cheti chake kilipatikana kwa njia zisizo halali yalipekwa katika mahakama ya tume. Amekanusha madai yote dhidi yake.

    Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakimkejeli kwa madai ya kugushi vyeti vya elimu kuonyesha kuwa alisoma katika Chuo kikuu cha Uganda, baada ya Chuo Kikuu cha Kenya kusema alichukua kozi ya shahada palelakini hakufuzu.

    Gazeti nchini humo la Daily Nation limeripoti wagombea wengine kote nchini ambao wanakabiliwa na changamoto ya makaratasi yao ya elimu.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Wiki iliyopita, IEBC iliondoa idhini ya mchekeshaji Walter Mong’are, f kwa jina maarufu la jukwaani Nyambane, ya kugombea urais.

    Tume hiyo ilisema ilichua uamuzi huo baada ya kupata taarifa mpya kuhusu uwezo wake wa kielimu.

  3. Akina mama wa Urusi wanawasaidia wanao ambao hawataki kupigana

    TH

    Chanzo cha picha, Reuters

    Hapo awali tuliripoti juu ya ukosoaji wa Papa Francis kwa wanajeshi "wakatili " wa Urusi - na Rais Zelensky wa Ukraine akilaani vitendo vya jeshi la Urusi kama "maovu kabisa".

    Lakini pia tumekuwa tukisikia madai kwamba wanajeshi wa Urusi wanakataa kurudi vitani kwa kupelekwa kwa mara ya pili - au hawatapigana kabisa .

    Kamati ya Akina Mama wa Wanajeshi, inayofanya kazi ya “kulinda haki za wanajeshi,” inasema imekuwa ikisaidia familia za Warusi zinazopinga vita.

    Katika mahojiano na chombo cha habari cha Urusi Meduza, katibu mtendaji wa shirika hilo lisilo la kiserikali Valentina Melnikova alisema baadhi ya watumishi wanaoondoka Ukraine wameomba ushauri wa kamati ili kuepuka kurudi kwenye mstari wa mbele.

    Dk Jenny Mathers, msomi katika Chuo Kikuu cha Aberystwyth ambaye anasoma Ukraine, alisema kuongezeka kwa wanajeshi wasiotaka kupigana kunaweza kuwa na athari kubwa.

    "Uwezo wa Urusi sio usio na mwisho," alisema.

    "Tuna visa zaidi na zaidi vya wanajeshi wa Urusi ambao wamehudumu nchini Ukraine na kurudi Urusi wakikataa kurejea tena kwa kutumwa vitani.

    "Tuna mifano zaidi na zaidi ya ofisi za kuandikisha jeshi la Urusi kushambuliwa, kuteketezwa ... hadithi zaidi na zaidi za familia zilizo tayari kusaidia wana wao wanaojificha kutoka kwa jeshi."

    Ingawa BBC haiwezi kuthibitisha madai yote ya Mathers, hivi majuzi tuliripoti kuhusu wanajeshi wa Urusi waliokataa kupigana nchini Ukraine.

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  4. Ufaransa: Marufuku ya vazi la 'burkini’ yapingwa katika mahakama ya juu

    Burkini

    Chanzo cha picha, CITIZEN ALLIANCE OF GRENOBLE

    Maelezo ya picha, Wana kampeni waliwashawishi maafisa wa jiji kuruhusu uvaaji wa Burkini Campaigners katika vidimbwi vya kuogelea vya umma mwezi uliopita (picha ya maktaba)

    Jiji la Grenoble nchini Ufaransa limekwenda kwenye mahakama yajuu zaidi ya utawala ya Ufaransa kupinga marufuku iliyowekwa inayowaruhusu watu kuvaa vazi la kuogelea linalofunika mwili mzima"burkini" katika shule za umma.

    Uamuzi wa Grenoble wa kuruhusu mavazi yote ya kuogelea, ikiwa ni pamoja na burkini, uliibua makabiliano ya kisheria na serikali ya Ufaransa.

    Burkinis huvaliwa sana na wanawake Waislamu, kama njia ya kujisitiri na kuendeleza imani yao .

    Lakini kujieleza kwa dini katika maisha ya umma nchini Ufaransa kunaleta mgawanyiko.

    Burkini

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Mmoja wa raia wa Ufaransa(kulia) akiwa amevalia burkini tayari kwa kuogelea

    Kabla ya kesi hiyo Jumanne, Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gérald Darmanin alielezea sera ya jiji la Grenoble ya vazi la kuogelea kama "uchokozi usio kubalika" na kwamba ni kinyume cha maadili ya kawaida ya Ufaransa.

    Unaweza pia kusoma:

    • Ufaransa na katazo la vazi la Burkini,katika pwani zake
  5. Mpenzi wa zamani wa Britney Spears ashutumiwa kwa kumvizia katika siku ya harusi yake

    Britney

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanaume ambaye alikuwa na uhusiano na muimbaji maarufu Britney Spears, ameshutumiwa na muimbaji huyo kwa kumvizia baada ya kuhudhuria sherehe yake ya harusi bila kualikwa

    Jason Alexander mwenye umri wa miaka 40, ambaye alikua mume wa Spears kwa masaa 55, amekana mashitaka aliyoshitakiwa ikiwa ni pamoja na kuoa kwa lengo la kujinufaisha kutokana mali ya mwenzi, wizi na mawasiliano yaliyolenga kumuumiza Bi Spears.

    Alexander alikamatwa wiki iliyopita baada ya madai kwamba aliharibu lango na kusambaza video kutoka kwenye harusi ya Spears na mume wake wa sasa Wissam Asgari.

    Harusi ya Spears, mwenye umri wa miaka 40, na Asgari, mwenye umri wa miaka 28, ilifanyika katika mazingira rafiki katika jimbo la California wiki iliyopita, lakini sherehe zilivurugika wakati Alexander alipovamia eneo la harusi na polisi walikuja na kumkamata baada ya madai kuwa alikuwa amepasua lango la kuingia kwenye harusi, na kuanza kuchukua za video kutoka ndani ya sherehe kabla ya kukamatwa na polisi.

    Alexander na Britney ambao walikuwa marafiki wa utoton, na alimuoa kwa muda mfupi sana katika mwaka 2004.

  6. Habari za hivi punde, Urusi na Ukraine: Urusi yavamia eneo la Severodonetsk katika jimbo la Lugansk

    Fights for Severodonetsk have been going on since the end of May

    Chanzo cha picha, Sergei Gaidai

    Maelezo ya picha, Mapigano ya kuiteka Severodonetsk yamekuwa yakiendelea tangu mwishoni mwa mwezi Mei

    Vikosi vya Urusi vikisaidiwa na makombora , vinavamia eneo la mji muhimu wa Severodonetsk lililopo katika jimbo la Lugansk na wanajaribu kung’ang’ana kupenya hadi katikati mwa mji huo, kulingana na ripoti ya Mkuu wa majeshi ya Ukraine iliyotolewa mapema leo.

    Katika jimbo la Slavyansk, jeshi la Urusi linajaribu kupata udhibiti wa eneo la Bogorodichny ili kuweza kuutumia kujiandaa kwa shambulio dhidi ya Slavyansk.

    Katika jimbo la Kharkiv, vikosi vya Urusi vinaweka ulinzi ili kuyazuwia majeshi ya Ukraine kusonga mbele kuelekea kwenye mpkana.

    Kwa ujumla tangu vilipoanza vita, kulingana na Mkuu wa majesi wa Ukraine, Vikosi vya Urusi vimepoteza vifaru vya kijeshi 1,434 , magari ya jeshi 3,503 , mifumo , 721 ya kufyatua makombora na droni 588. Mkuu wa majeshi huyo anasema jumla ya wanajeshi wa Urusi 32,500 wamefariki katika vita vya nchi hizo.

    Kulingana na ujasusi wa Uingereza, kufuikia mwezzi Mei, Urusi ilikuwa imepoteza watu 15,000 nchini Ukraine. Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilitangaza idadi ya vifo vya wanajeshi wake mara ya mwisho mwezi Machi- ambapo walikuwa ni watu 1351.

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  7. Urusi na Ukraine: Papa akosoa matumizi mamluki wa 'kuogofya ' ya Urusi

    Pope Francis

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Papa Francis alikutana na wakimbizi wa met Ukraine katika Vatican mapema mwezi huu

    Papa Francis: ’Vita ya III ya Dunia tayari imetangazwa’

    Pope Francis ameripotiwa akisema kuwa matumizi ya mamluki wa Uusi nchini Ukraine, wakiwemo Wachechnya na Wasyiria ni "ya kuogofya" katika Makala iliyochapishwa na gazeti la kila siku la Italia, La Stampa.

    Katika kipande, ambacho huripoti mazungumzo kati ya Papa na Mhariri wa jarida la utamaduni la Jesuit European, Papa alisema kuwa Vita vya Ukraine ni vya "labda nia ya kuchokoza kwa njia moja au sio vya kuiwa".

    Aliyaelezea majeshi ya Warusi kama majeshi "makalik na katili", akiongeza kuwa Waukraine wana "pigana kwa ajili ya kuishi".

    Alipoulizwa iwapo anampenda Rais wa Urusi, Vladimir Putin, Papa Francis anasema hatapunguza ugumu wa vita kwa kutofautisha"wema na ubaya".

    Aliendelea kusema kuwa ana matumaini ya kukutana na- Mkuu wa Kanisa la Waorthodox wa Urusi Patriarch Kirill mwezi Septemba nchini Kazakhstan.

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi

    • MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  8. Maafisa wa DR Congo waishutumu Rwanda kwa uvamizi

    TH

    Chanzo cha picha, AFP

    Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamelishutumu jeshi la Rwanda kwa kuvamia ardhi yake baada ya kudaiwa kuwasaidia waasi kuchukua Bunagana, mji wa mpakani katika jimbo la Kivu Kaskazini.

    Waasi wa Kongo wa M23 waliuteka mji huo siku ya Jumatatu baada ya kuwalazimisha baadhi ya wanajeshi wa serikali kukimbilia nchi jirani ya Uganda.

    Mji huo wa kimkakati ni muhimu kwa biashara ya kuvuka mpaka kati ya DR Congo na Uganda.

    Katika taarifa, mamlaka ya mkoa wa Kivu Kaskazini ilisema "jeshi la Rwanda liliamua kukiuka uadilifu wa eneo letu na kukalia mji wa Bunagana".

    Walitaja kutekwa kwa mji huo "uvamizi wa DRC" na kuongeza kuwa jeshi "italinda taifa".

    Rwanda imerudia mara kadhaa kuuita mzozo wa mashariki mwa DR Congo "suala la ndani" na kukanusha kuwaunga mkono waasi wa M23.

    Jeshi lake halijatoa maoni yoyote kuhusu kutekwa kwa Bunagana, lakini katika taarifa yake siku ya Jumanne lilisema litahakikisha uadilifu wa ardhi ya Rwanda.

    Mvutano kati ya majeshi hayo mawili umeongezeka baada ya kulaumiana kwa mashambulizi ya kuvuka mpaka mwishoni mwa juma.

    TH
  9. Vitendo vya Urusi ni 'vya kishetani kabisa' - Zelensky

    Mwanamke wa Lysychansk ameguswa na kifo cha majirani wawili baada ya makombora ya Urusi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mwanamke wa Lysychansk ameguswa na kifo cha majirani wawili baada ya makombora ya Urusi

    Vitendo vya Urusi nchini Ukraine ni 'vya kishetani kabisa',Rais Volodymyr Zelensky alisema katika hotuba yake ya kawaida ya usiku kwa taifa.

    Wakati wa hotuba yake alisema Waukraine wamekuwa wakilipa "gharama kubwa zaidi" katika vita vinavyoendelea katika eneo la Donbas, akielezea kuwa "moja ya vita vya kikatili zaidi barani Ulaya na kwa Ulaya".

    Zelensky alikiri gharama ya vita "ni ya juu sana – na inatisha tu".

    Aliomba tena kwamba Ukraine ipate silaha zaidi za Magharibi ili kusaidia "kuhakikisha wananufaika na hatimaye kufikia mwisho wa mateso ya Urusi kwa Donbas ya Ukraine".

  10. UN: Yalaani mpango wa Uingereza wa kupata hifadhi nchini Rwanda

    Mahakama mjini London zilikataa pingamizi mbili za dakika za mwisho za mpango wa hifadhi ya Rwanda

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mahakama mjini London zilikataa pingamizi mbili za dakika za mwisho za mpango wa hifadhi ya Rwanda

    Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ame shutumu mipango ya Uingereza ya kutuma ndege ya kwanza ya waomba hifadhi nchini Rwanda siku ya Jumanne.

    Filippo Grandi alisema sera hiyo imeweka historia mbaya.

    Alisema nchi zingine ambazo zilichukua watu wanaotafuta hifadhi zaidi kama Uingereza zinaweza kuamua kufuata mfano wake.

    Mahakama mjini London zimekataa changamoto mbili za dakika za mwisho kwa sera hiyo mpya.

    Serikali ya Uingereza inasema kuwa hatua hiyo imekusudiwa kuzuia biashara haramu ya watu, lakini kumekuwa na ukosoaji mkubwa wa vyama vya upinzani na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

    Mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya Ofisi ya Mambo ya Ndani.

    Unaweza pia kusoma:

    • 'Mpango wa Uingereza wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda 'ni kinyume cha Mungu' - Welby
    • Mkataba wa wahamiaji wa Uingereza: Je, Rwanda ni nchi ya usalama au hofu?
  11. Kabuga yuko sawa kusikiliza kesi ya mauaji ya halaiki ya Rwanda dhidi yake - UN

    Félicien Kabuga alikamatwa mnamo mwaka 2020 huko Paris

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Félicien Kabuga alikamatwa mnamo mwaka 2020 huko Paris

    Mahakama ya Umoja wa Mataifa imeamua kuwa mwanamume anayedaiwa kuwa mmoja wa wafadhili wakuu wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda anastahili kushtakiwa huko The Hague, ambako anazuiliwa kwa sasa.

    Félicien Kabuga anatuhumiwa kufadhili na kuwapa silaha wanamgambo wa Kihutu ambao waliwachinja Watutsi wapatao 800,000 wa kabila la Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani katika mauaji ya halaiki.

    Mawakili wake hapo awali walikuwa wakitaka kusitisha kesi dhidi ya mzee huyo wa miaka 87 kwa misingi ya afya.

    Bw Kabuga alikuwa mtoro kwa miaka 26 hadi alipokamatwa mwaka wa 2020 mjini Paris, ambako alikuwa akiishi chini ya utambulisho wa uongo.

    Anakanusha mashtaka yote dhidi yake.

    Mwaka 1997 alifunguliwa mashtaka na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya Rwanda kwa makosa saba yakiwemo mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.

    Soma zaidi:

  12. Marquinhos: Arsenal wamsajili kinda wa Brazil kwa mkataba wa muda mrefu

    Marquinho

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Marquinho

    Arsenal imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa Brazil Marquinhos mwenye umri wa miaka 19 kutoka Sao Paulo.

    The Gunners wanasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil chini ya umri wa miaka 17 amejiunga na klabu hiyo ya Premier League kwa mkataba wa muda mrefu.

    Mchezaji huyo wa vijana wa Sao Paulo alicheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 18 Julai mwaka jana kabla ya kuwasaidia kushinda kombe la Campeonato Paulista mwaka wa 2021.

    "Bado ni mdogo sana, hivyo ni mchezaji wa siku zijazo," alisema mkurugenzi wa ufundi wa Arsenal Edu."Marquinhos alikuwa mchezaji ambaye tulikuwa tukimtazama kwa muda," Edu aliongeza.

    "Tunamtazamia sasa kuungana nasi kwa maandalizi ya msimu mpya, kutengeneza makao yake mapya, na kuendelea kukua na kukua nasi."

  13. Habari za hivi punde, Katika siku 100 za vita, Urusi imejipatia dola bilioni 100 kutoka kwa mauzo ya mafuta na gesi

    Rais Putin

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais Putin

    Kulingana na Kituo Huru cha Kifini cha Utafiti wa Nishati na Hewa Safi (CREA), Urusi ilipata takriban dola bilioni 100 kutokana na biashara ya mafuta na gesi katika siku 100 za kwanza za vita.

    Hayo yamesemwa katika ripoti mpya iliyotolewa na kituo hicho.

    Ripoti ya kituo hicho ilisema bado kuna "mashimo" mengi yamesalia katika EU na juhudi za Marekani kupunguza uagizaji kutoka Urusi.

    EU ilikuwa imepanga kwamba vikwazo vya mafuta kwa Urusi vingekuwa na athari kubwa, lakini usafirishaji wa mafuta ghafi ya Urusi kwenda India umeongezeka, wakati bidhaa za mafuta iliyosafishwa nchini India zinauzwa kwa Marekani na EU.

    Kulingana na utafiti huo, asilimia 61 ya mauzo ya nje ya Urusi yalikwenda kwa Jumuiya ya Ulaya, ambayo ilinunua mafuta na gesi yenye thamani ya dola bilioni 60.

    Kati ya hizo, dola bilioni 12.1 zilinunuliwa na Ujerumani na dola bilioni 7.8 na Italia.

    China ilikuwa muagizaji mkubwa wa mafuta na gesi ya Urusi nje ya Uropa, na tangu Februari 24, Urusi imeuza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 12 kwa Uchina.

    Mwanzoni mwa Juni, Umoja wa Ulaya uliidhinisha vikwazo ambavyo viliashiria kuachana kabisa na uagizaji wa Kirusi na kupunguza matumizi ya gesi ya Kirusi kwa theluthi mbili.

  14. Urusi na Ukraine: Kila daraja linaloelekea mji wa Severodonetsk limeharibiwa na Urusi

    Mtu akitembea Ukraine

    Chanzo cha picha, AFP

    Siku ya Jumatatu mashambulizi ya mabomu ya Severodonetsk - katika jimbo la Donbas - yalionekana kufikia hatua mbaya.

    Madaraja yote matatu kuelekea mji huo yameharibiwa, gavana wa mkoa Serhiy Haidai alithibitisha, hatua inayofanya uhamishaji wa wakaazi na usafirishaji wa bidhaa kutowezekana.

    Wanaounga mkono Urusi wanaotaka kujitenga walisema wapiganaji wa Ukraine sasa walipaswa kuchagua "kujisalimisha au kufa".

    Kutekwa kwa Severodonetsk itakuwa ushindi mkubwa wa mfano kwa Urusi. Mji huo na mwenzake pacha wa Lysychansk, ni kituo muhimu cha kikanda na kuiteka yote miwili kungeashiria hatua kubwa kuelekea lengo la Moscow la kuchukua udhibiti kamili wa Donbas.

  15. Natumai hujambo