Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Vitendo vya Urusi Donbas ni ‘mauaji ya halaiki’-Zelensky

"Mashambulizi ya sasa ya wavamizi huko Donbas yanaweza kufanya eneo hilo kutokuwa na watu," Zelensky alisema. "Wanataka kuchoma Popasna, Bakhmut, Lyman, Lysychansk na Severodonetsk kuwa majivu.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu mubashara kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Theluthi mbili ya mji wa Severodonetsk umezungukwa - Gavana

    Vikosi vya Urusi vimechukua theluthi mbili ya eneo la mji wa makabiliano wa Severodonetsk, gavana wa mkoa wa Luhansk anasema.

    Lakini Serhiy Haidai anasema mji huo haujazingirwa kabisa, akikanusha ripoti za maafisa kutoka Jamhuri ya watu wa Luhansk inayounga mkono Moscow kwamba vikosi vya Ukraine vimezungukwa huko.

    Severodonetsk ndio mji ulio na watu wengi katika eneo la mashariki unaodhibitiwa na Ukraine.

    Hapo awali tuliripoti kwamba 60% ya hisa za makazi za jiji zimeharibiwa kabisa na hadi 90% ya majengo yameharibiwa.

    Takriban watu 1,500 wamekufa katika eneo hilo tangu uvamizi huo uanze mwezi Februari.

  3. Habari za hivi punde, Urusi na Ukraine: Sehemu kubwa ya Lyman iko chini ya udhibiti wa Urusi -Maafisa wa Ukraine wathibitisha

    Taarifa za hivi punde zinaeleza kuhusu kuanguka mikononi mwa Warusi kwa mji wa Ukraine wa Lyman unaopatikana katika jimbo la mashariki la Donetsk.

    Mshauri wa rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, Oleksiy Arestovych, anaonekana pia kuthibitisha kwamba wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi wamechukua udhibiti wa mji huo.

    "Kulingana na data ambazo hazijathibitishwa, tumepoteza mji wa Lyman," Arestovych alisema katika video, akiongeza kuwa shambulio lilikuwa limeandaliwa na kupangwa vizuri.

    "Hii inaonyesha, kimsingi, kuongezeka kwa kiwango cha ujuzi wa udhibiti wa opresheni na mkakati wa jeshi la Urusi ," aliongeza.

    Kauli zake zinakuja huku gavana wa jimbo la Ukraine la Donetsk, Pavlo Kyrylenko, akiviambia vyombo vya habari kuwa Lyman "imethibitiwa kwa kiasi kikubwa na vikosi vya Urusi" lakini akasema jeshi la Ukraine lilikuwa limeweka ngome mpya katika eneo.

    Lyman ni eneo lenye leri muhimu na mji huo ukilengwa kwa muda mrefu na vikosi vinavyounga mkono Urusi.

    Unaweza pia kusoma:

  4. Mwekezaji wa Twitter amshitaki bilionea Elon Musk na jukwaa kwa bei ya hisa

    Mwekezaji wa Twitter anamshitaki Elon Musk na jukwaa hilo la mtandao wa kijamii kuhusiana na namna bei ya hisa ya Musk ya dola bilioni 44 (£34.9bn) inavyoshugulikiwa.

    Kesi hiyo inadai kuwa Bilionea Musk alikiuka sheria za kampuni kwa njia kadhaa.

    Inamshutumu mkuu wa Tesla kwa "mienendo isiyofaa" kwani "taarifa zake za uongo na njama za kujipatia soko la kibinafsi vimesababisha 'vurugu ' katika makao makuu ya twitter mjini San Francisco".

    Hisa za Twitter ni 27% kiwango hiki kikiwa ni cha chini ya bei inayotolewa na Musky ya $54.20

    Mashitaka yaliyopenekezwayaliwasilishwa wiki iliyopitakatika Mahakama ya wilaya yaNorthern District na California na mwekezaji William Heresniak, ambaye alisemekana alikuwa anafanya hivyo "kwa niaba yake na wenzake waliowekwa katika hali kama yake".

    Mashitaka hayo yalijumuisha ujumbe ambapo Bw Musk alisema azma yake ya kuchukua kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii imesitishwa kwa muda kwasabu ya wasi wasi wake kuhusu idadi ya akaunti gushi kwenye jukwaa la Twitter.

    Ujumbe huo wa tarehe 13 Mei "ulikuwa ni mojawapo ya juhudi za njama ya kuchukua soko lote la hisa za Twitter kwani alifahamu kuhusu akaunti gushi ," yalisema mashitaka.

  5. Habari za hivi punde, Urusi na Ukraine: Urusi imepandikiza mabomu hadi 500 katika bahari nyeusi, yasema Ukraine

    Ukraine imedai kuwa Urusi imetawanya mabomu kati ya 400 na 500 ya kutegwa ya usovieti ya zamani katika barahi nyeusi , ambayo yamekuwa yakiyakisambaa wakati wa dhoruba na kufanya juhudi za uagizaji wa chakula kutoka kwenye bandari za Ukraine kushindikana.

    Msemaji wa Mtawala wa kijeshi katika jimbo la Odesa, Serhiy Bratchuk, anasema Urusi "imebuni mzozo wa chakula duniani" kwa kuzuia utendaji wa bandari, na kuongeza kuwa Urusi inatumia "taarifa potofu za kuambiwa" kwa kuilamu Ukraine kwa mzozo wa chakula.

    Bandari za Ukraine za Bahari nyeusi zimefungwa tangu mwanzoni mwa vita, tarehe 24 Februari, na kusitisha mauzo ya nje ya nafaka muhimu, na maafisa wanasema kuwa tani milioni 20 za nafaka zimekwama kwa sasa nchini humo.

    Umoja wa Mataifa unasema baadhi ya nchi zinaweza kukabiliwa na njaa ya muda mrefu iwapo mauzo ya Ukraine hayatarejeshwakwenye viwango vya kabla ya vita. Urusi ilitoa njia ya wazi kupitia Bahari nyeusi kwa ajili ya safari za meli za vyakula, na kwa kufanya hivyo ilegezewe vikwazo.

    BBC haijaweza kupata thibitisho huru la madai haya.

    Unaweza pia kusoma:

  6. Urusi na Ukraine: Mapigano makali yanaendelea viungani mwa mji ulioharibiwa wa Severodonetsk

    Kumekuwa na mapigano makali viungani mwa Severodonetsk – eneo muhimu linalolengwa na Warusi- hukju vikosi vya Urrusi vikijaribukuuteka mji huo uliopo katika jimbo la Luhansk nchini Ukraine.

    Mji huo umekuwa na mashambulio ya makombora yanayoendelea ambapo- 60% ya nyumba zimeharibiwa kabisa na 90% ya majengo yameharibiwa na yatahitaji kukarabatiwa, amesema meya wa mji huo Oleksandr Stryuk.

    Raia wanne wameuawa katika Severodonetsk Alhamisi, huku wapatao 1,500 wakiuawatangu ulipoanza uvamizi wa Urusi mwezi wa Februari na katikati mwa mji mkuu huo wa jimbo kunaharibiwa na makombora ya ardhini na anga ya urusi, mkuu wa utawala wa jeshi wa jimbo la Luhansk Regional, Serhiy Haidai anasema.

    Anasema vikosi vya Urusi vilijaribu kuingia kwa nguvu katika vikitokea miji iliyopo karibu ya Purdivka na Shchedryshcheve, na kushambulia ngome za wanajeshi wa Ukraine.

    Vikosi vya Urusi vimekuwa vikifanya mashambulio ya hapa na pale dhidi ya maeneo yenye ulinzi mkali ya Waukraine katika Donbas tangu Urusi ilipoimarisha juhudi zake za kivita pale.

    Unaweza pia kusoma:

  7. Hospitali yachunguzwa baada ya mjamzito kutolewa figo bila kujitambua

    Polisi wilayani Mubende nchini Uganda wanachunguza kuhusu madktari wasio waaminifu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa baada ya kudaiwa kutoa figo kutoka kwa mama mjamzito ambaye alikuwa hajitambui.

    Mjamzito huyo Peragiya Muragijemana, 20, ni mkazi wa Kijiji cha Lwemiggo, wilayani Mubende anaelezea jinsi alivyokimbizwa hospitalini akiwa katika hali mbaya na kuhitajika kufanyiwa upasuaji, lakini figo yake ikadaiwa kuvunwa.

    Bi Muragijemana anasema alijifungua mikononi mwa mkunga wa jadi, lakini alishindwa kutoa kondo la nyuma, na kusababisha kutokwa na damu nyingi.

    “nilipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Mubende, ambapo mume wangu, Amos Tiringanya, alitakiwa kusaini hati ya kuniruhusu kufanyiwa upasuaji,” alisema katika mahojiano na gazeti la Daily Monitor.

    Mume wake alisema kuwa madaktari walimueleza kuwa ndiyo njia pekee ya kuokoa maisha yake kwani alikuwa akivuja damu.

    “Baada ya upasuaji, mke wangu alirudishwa wodini akiwa amepoteza fahamu na aliruhusiwa baada ya siku tatu kutokana na msongamano hospitalini. Tulimpeleka nyumbani kwa mama mkwe wangu ,” alisema.

    Aliongeza: “Lakini baada ya siku tatu, nilipigiwa simu na mama mkwe akinijulisha kuwa mke wangu amepata matatizo ya tumbo. Tulienda kwa uchunguzi wa hali ya juu zaidi, ambao ulionyesha kuwa figo yake ya kulia haikuwepo. Nilitia saini tu hati inayokubali kuondolewa kwa uterasi ya mke wangu ili kuokoa maisha yake, si figo yake.”

    Mamake wa muathirika Piyera Musanabeera, alitoa taarifa kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu madaktari waliodaiwa kutoa figo ya binti yake.

    Dkt Onesmus Kibaya, msimamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mubende, alishauri familia ya Muragijemana kuwa watulivu kwani hospitali hiyo pia inafanya uchunguzi wake.

    Anaeleza kuwa mwanamke anapokuwa mjamzito, viungo vikuu hupata matatizo. Viungo hivyo ni pamoja na moyo, figo na uterasi.

    "Mbali na hilo, hospitali ya Mubende haina uwezo wa kufanya upasuaji wa figo bali hufanywa katika hospitali ya Mulago".

    Msemaji wa polisi wa mkoa wa Wamala, Rachel Kawala, alisema wamechukua taarifa za mgonjwa na uchunguzi wa kisa hicho unaendelea.

    • Madaktari Uganda wathibitisha Judith kutolewa figo akiwa kwa mwajiri wake Saudi Arabia
    • Judith Nakitu : Mwanamke wa Uganda aliyepoteza figo yake bila kujua Saudia afidiwa
  8. Matumizi ya vifaru vya zamani yanaashiria ukosefu wa vifaa vya Urusi - Uingereza

    Urusi inaaminika kutumia vifaru vya umri wa miaka 50 katika juhudi zake za kuteka eneo la kusini mwa Ukraine.

    Inayaleta magari ya T-62 ili kuimarisha Kundi lake la Kusini la Vikosi, kulingana na taarifa ya asubuhi kutoka Wizara ya Ulinzi ya Uingereza (MoD).

    Magari haya yanafikiriwa kuwa "hasa ​​yanaweza kuathiriwa na silaha za kukinga vifaru" na yanaashiria uhaba wa "vifaa vya kisasa, vilivyo tayari kupigana".

    Wizara ya ulinzi pia inasema vikosi vya Urusi vinaendelea na juhudi za kuzingira Severodonetsk na Lysychansk.

    Hivi karibuni wameteka vijiji kadhaa kaskazini-mashariki mwa Popasna - lakini upinzani wa Ukraine "unainyima Moscow udhibiti kamili" wa eneo la mashariki la Donbas, inasema MoD.

    Unaweza pia kusoma:

  9. Jeshi la DR Congo lafanikiwa kupambana na waasi wa M23

    Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limechukua tena udhibiti wa eneo la Jimbo la Kivu Kaskazini kutoka kwa waasi wa M23, moja ya makundi yenye silaha ambayo yanaendesha operesheni zao katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo yenye machafuko.

    Radio Okapi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti kwamba Vikosi vya Wanajeshi vya DR Congo vimechukua tena eneo la Kabaya, katika kundi la vijiji vya Kisigari, jana.

    Iliongeza kuwa jeshi limewarudisha nyuma waasi wa M23, ambao walikuwa wakitishia kuizingira kambi ya kijeshi ya Rumangabo, ambayo hapo awali iliripotiwa kutekwa na waasi hao.

    Mapigano yalizuka mapema wiki hii katika maeneo kadhaa huko Kivu Kaskazini, ambayo inapakana na Rwanda.

    Kufuatia uvamizi huo wa waasi, Marekani ilitoa ushauri ikiwaonya raia wake dhidi ya kusafiri katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo yenye utajiri wa madini.

    Kundi la waasi la M23 - ambalo kimsingi ni la Watutsi wa Congo - lilianza tena mapigano mwaka huu, likiituhumu serikali ya DR Congo kwa kushindwa kuheshimu makubaliano ya mwaka 2009 ambapo wapiganaji wake walipaswa kuunganishwa katika jeshi.

    Wakati huo huo DR Congo inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 Tunasubiri majibu baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Christophe Lutundula Apala Pen'Apala jana kuishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.

    "Rwanda inasonga mbele...naweza kusema bila kusita, Rwanda imeshambulia kambi ya Rumangabo huko DR Congo...narudia tena M23 wakiungwa mkono na Rwanda walishambulia wanajeshi wa kimataifa wa Monusco [Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini DR Congo]," Lutundula Pen'Apala alisema wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la AU huko Malabo, Equatorial Guinea, Mei 25.

    Uhusiano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda ulikuwa umeanza kudorora baada ya Rais Felix Tshisekedi kuchukua madaraka mwaka wa 2019, lakini kuzuka upya kwa ghasia za M23 kumeongeza hali ya wasiwasi.

    • Waasi wa M23 waingia DRC
    • Waasi wasitisha vita Msumbiji
    • DR Congo: FARDC yaishtumu Rwanda kwa kuisaidia M23
    • Je waasi wa M23 watakoma?
    • https://www.bbc.com/swahili/habari/2013/11/131105_drc_tathmini
  10. Marekani yatwaa jumba la kifahari la kiongozi wa zamani wa Gambia Jammeh lenye thamani ya $3.5m

    Wizara ya Sheria ya Marekani inasema imefanikiwa kutwaa jumba la kifahari lililonunuliwa na rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh kwa $3.5m (£2.7m) kwa madai ya mapato ya rushwa.

    Mali hiyo iliyoko Potomac, Maryland, inasemekana kupatikana kupitia wakfu ulioanzishwa na mkewe, Zineb Jammeh.

    Sasa limechukuliwa na Marekani pamoja na mapato yote ya kukodisha yanayotokana na mali hiyo tangu malalamiko yalipowasilishwa mnamo 2020, taarifa ya idara hiyo ilisema.

    "Marekani inakusudia kuuza mali hiyo, na inapendekeza kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba mapato yatokanayo na mauzo ya mali iliyotwaliwa yatumike kuwanufaisha watu wa Gambia waliodhuriwa na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ya Rais wa zamani Jammeh," idara hiyo ilisema.

    Rais huyo wa zamani anashutumiwa kwa kula njama na familia yake na washirika wake kwa kutumia makampuni ya ng'ambo na amana za ng'ambo kujipa mapato yake yanayodaiwa kuwa ya kifisadi duniani kote.

    Serikali ya Gambia wiki hii ilisema iko tayari kumfungulia mashitaka kwa kile ilichokiita "mamia ya uhalifu" aliofanya wakati wa utawala wake.

  11. Mauaji ya shule Texas: Mume wa mwalimu aliyeuawa afariki ‘kwa huzuni’

    Mume wa mmoja wa walimu waliouawa kwa kupigwa risasi Jumanne huko Uvalde, Texas, nchini Marekani ameripotiwa kufariki kutokana na mshtuko wa moyo.

    Joe Garcia alikuwa mume wa Irma Garcia, ambaye alifundisha kwa miaka 23 katika Shule ya Msingi ya Robb.

    Bi Garcia alikuwa mmoja wa walimu wawili waliouawa na kijana mwenye bunduki katika ufyatuaji risasi uliosababisha vifo vya watu 21 - wakiwemo watoto 19.

    Wawili hao - ambao walikuwa wameoana kwa miaka 24 - wameacha watoto wanne.

    Kwenye Twitter, mpwa wa Bi Garcia, John Martinez, alisema kuwa Bw Garcia "alifariki kutokana na huzuni" kufuatia mauaji ya mkewe.

    Akina Garcia wameacha watoto wanne - wavulana wawili na wasichana wawili - kuanzia miaka 12 hadi 23.

    Baada ya shambulio hilo la mauaji huko Uvalde, Bw Martinez aliambia gazeti la New York Times kwamba Bi Garcia alipatikana na maafisa "akiwa amekumbatia watoto mikononi mwake hadi pumzi yake ya mwisho".

    "Alijitolea kuwalinda watoto katika darasa lake," aliandika kwenye ukurasa wa kuchangisha pesa. "Alikuwa shujaa".

    Bi Garcia na mwalimu mwingine aliyeuawa kwa kupigwa risasi, Eva Mireles, walikuwa wakifundisha pamoja kwa miaka mitano na walikuwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 40 kati yao.

  12. Vitendo vya Urusi Donbas ni ‘mauaji ya halaiki’-Zelensky

    Mashambulio makali ya Urusi katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine yanaonyesha "sera ya wazi ya mauaji ya halaiki," Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema katika hotuba yake ya usiku wa Alhamisi.

    "Mashambulizi ya sasa ya wavamizi huko Donbas yanaweza kufanya eneo hilo kutokuwa na watu," Zelensky alisema. "Wanataka kuchoma Popasna, Bakhmut, Lyman, Lysychansk na Severodonetsk kuwa majivu.

    Kama Volnovakha, kama Mariupol."

    Katika miji iliyo karibu na mpaka wa Urusi kama Donetsk na Luhansk, vikosi vya Urusi "vinakusanya kila mtu wawezavyo ili kujaza mahali pa wale waliouawa na kujeruhiwa katika uvamizi," Zelensky alisema.

    "Yote haya, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kwa watu wetu na mauaji ya halaiki ya raia, ni sera ya wazi ya mauaji ya halaiki inayofuatiliwa na Urusi."

    Zelensky alisema kuweka shinikizo kwa Urusi "kihalisi ni suala la kuokoa maisha" na kwamba kila kucheleweshwa, mzozo au pendekezo la "kutuliza" Urusi ni kusababisha "Waukreni wapya kuuawa" na vitisho vipya kwa kila mtu katika bara.

    Unaweza pia kusoma:

  13. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Ijumaa tarehe 27 Mei 2022