Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mapigano ya Donbas yatakua kama Vita vya Pili vya Dunia, yasema Ukraine
Waziri wa mambo ya nje Dmytro Kuleba anatoa wito kwa washirika wa Nato kutoa silaha zaidi mara moja huku Urusi ikilenga vita vyake mashariki mwa nchi hiyo.
Moja kwa moja
Uingereza yakanusha ujasusi katika ubalozi wa Urusi
Mbali na Umoja wa Mataifa na Nato, mapema leo mlinzi katika ubalozi wa Uingereza mjini Berlin alikana kufanya ujasusi kwa Urusi.
Raia wa Uingereza David Smith, 57, anatuhumiwa kukusanya taarifa kutoka kwa ubalozi huo na kuzisambaza kwa mtu ambaye aliamini kuwa ni mwakilishi wa Urusi, miongoni mwa madai mengine.
Alikanusha makosa tisa chini ya Sheria ya Siri Rasmi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Westminster. Inadaiwa kuwa Smith alijaribu kuwasiliana kwa barua na Jenerali Meja Sergey Chukhurov, afisa wa jeshi la Urusi aliyeko nje ya Ubalozi wa Urusi mjini Berlin.
Pia anatuhumiwa kukusanya taarifa kuhusu mpangilio na uendeshaji wa ubalozi wa Uingereza mjini Berlin ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa taifa la Urusi.
Mauigizaji maarufu Jean-Claude van Damme awaomba wasanii nyota kutembelea DR Congo
Mauigizaji maarufu wa filamu ya Ubelgiji Jean-Claude van Damme, anayejulikana pia kama Muscles kutoka Brussels, amefurahia kupewa pasipoti ya kidiplomasia ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo - na kusema kwamba analenga kuwashawishi nyota wengine kutembelea nchi hiyo.
"Nitajaribu kuwashawishi nyota wa kimataifa kama vile Stallone, Schwarzenegger, Jacky Chan na wengine wengi,"
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 61 alisema hayo mji mkuu, Kinshasa, alipokuwa akipokea hati yake ya kusafiria na jukumu lake kama balozi wa kitamaduni, vijana na wanyamapori.
"Pia kuna waimbaji kama Jennifer Lopez na wanasoka kama Messi, Ronaldinho, Cristiano Ronaldo. Ni lazima waje nchini ili kuonyesha kwamba iko salama, ili kuonyesha kwamba DRC inaweza kuwapa ulinzi watu maarufu”
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekabiliwa na miongo kadhaa ya kukosekana kwa utulivu, huku makundi mengi yenye silaha yangali yanarandaranda katika eneo lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa nchi hiyo, yakiua, kubaka na uporaji.
Bingwa wa sanaa ya kijeshi, Van Damme aliendelea kuigiza katika filamu za kubwa za Hollywood kama vile Cyborg, Kickboxer na Universal Soldier - na hivi majuzi zaidi alionyesha Master Croc katika filamu za Kung Fu Panda.
Aliwashangaza watu katika mkutano na waandishi wa habari kwa kusema kwamba kweli alizaliwa DR Congo, akisema alikuwa "mzaliwa wa Likasi", jiji lililo kusini-mashariki mwa nchi hiyo.
Hii ingekuwa katika mwaka ambao nchi hiyo ilipata uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji.
Pia aliangazia umuhimu wa kuvutia uwekezaji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
"DR Congo ina thamani ya $36tn [£27tn] katika madini... kazi yangu ni kutafuta wawekezaji ambao wanaelewa kwamba wanapaswa kutoa kwanza kabla ya kupokea, na kuwa na uaminifu wa hali ya juu kwa Rais Félix Antoine Tshisekedi."
Hata hivyo, baadhi wamehoji pasipoti mpya ya mwigizaji huyo, kwani katiba ya DR Congo inapiga marufuku uraia wa nchi mbili.
Nato iko tayari kufanya zaidi kusaidia Ukraine
Stoltenberg anaulizwa ikiwa Nato inaharakisha uwasilishaji wake wa silaha kwa Ukraine ili kusaidia kuandaa nchi hiyo kwa mashambulio yanayotarajiwa kutoka kwa Urusi mashariki mwa Donbas.
Anasema Nato imetoa msaada mkubwa wa vifaa na imetoa mafunzo kwa makumi ya maelfu ya vikosi vya Ukraine kwa miaka mingi kabla ya uvamizi wa Urusi tarehe 24 Februari - na msaada zaidi umetolewa tangu wakati huo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine amesema nchi yake inahitaji kwa dharura hata silaha zaidi kutoka kwa washirika wake wa Magharibi ili kujilinda dhidi ya Urusi.
"Washirika wanatoa na wako tayari kufanya zaidi linapokuja suala la msaada wa kijeshi," Stoltenberg anasema.
Anaongeza kuwa kumwalika waziri wa mambo ya nje wa Ukraine kwenye mazungumzo ya Nato ni njia mojawapo ya muungano huo kuweka kile ambacho Ukraine inakihitaji.
Soma zaidi:
Ulimwengu lazima ujiandae kwa mzozo wa muda mrefu - Stoltenberg
Ulimwengu lazima uwe tayari kwa "mgogoro wa muda mrefu"na vita vya Ukraine, katibu mkuu wa Nato anaonya.
Jens Stoltenberg anasema vita vinaweza kudumu kwa wiki, miezi au hata miaka zaidi, akiongeza washirika walikuwa "wanaweka gharama kubwa" kwa Urusi kupitia vikwazo ili kusaidia kufupisha muda wa mzozo huo.
Anaongeza ikiwa vita vitadumu kwa muda mrefu, hatari iko kwa watu wa Ukraine "ambao watateseka zaidi, ambao wataona kifo na uharibifu zaidi".
toltenberg anasema: "Lakini bila shaka, maadamu vita vinaendelea, kutakuwa na hatari zaidi ya Ukraine na hilo ndilo ambalo Nato inazingatia, ili kuzuia ongezeko hilo."
Unaweza pia kusoma:
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Khashoggi: Ghadhabu baada ya mahakama ya Uturuki kusimamisha kesi ya mauaji
Kesi ya raia 26 wa Saudia wanaotuhumiwa kwa mauaji ya mpinzani Jamal Khashoggi mjini Istanbul Uturuki mwaka 2018 imesitishwa .
Jaji alisema kesi hiyo sasa itakabidhiwa kwa Saudi Arabia ambayo imekataa kuwasafirisha washukiwa hao nchini humo.
Mchumba wa Khashoggi, Hatice Cengiz, alisema ataendelea kupigana.
Mwandishi huyo wa gazeti la Washington Post aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia baada ya kukamtwa.
Mauaji yake yanayodaiwa kutekelezwa na maajenti wa Saudia yalizua ghadhabu kote duniani.
Mahakama ya Saudi iliwatia hatiani watu wanane ambao hawakutajwa majina yao kutokana na mauaji ya mwaka 2019.
Uamuzi huo wa Alhamisi unakuja baada ya waziri wa sheria wa Uturuki kukubaliana na ombi la mwendesha mashtaka la kusitisha kesi hiyo kwa madai kuwa ilitatizwa na kutokuwepo kwa washtakiwa.
Mwendesha mashtaka alisema mamlaka ya mahakama ya Saudi iliahidi kutathmini mashtaka dhidi yao.Hatua hiyo hata hivyo imekashifiwa na wanaharakati wa haki za binadamu.
Afisa wa Amnesty International wa Uturuki Milena Buyum alisema ni "uamuzi wa kutisha na wazi wa kisiasa".
Mahakama ya Kenya yawapa wanaume haki ya kulea watoto wa chini ya miaka tisa
Mahakama nchini Kenya imeamua kuwa wanaume wanaweza kupewa malezi ya watoto walio chini ya miaka tisa.
Mahakama inasema wajibu wa mzazi haufai kwenda kwa wanawake moja kwa moja ikiwa watoto wako katika umri mdogo.
Chini ya sheria ya Kenya, akina mama mara nyingi hupewa haki ya kuwalea watoto wadogo, lakini wanaweza kupoteza malezi kamili katika hali mbaya kama vile mama anaonyeshwa kuwa mzazi asiyefaa.
Habari za hivi punde kutoka Ukraine: Wito wa silaha katika kikao cha Nato
Kama ndio kwanza unajiunga na matangazo yetu mubashara, huu ndio muhtasari wa yake yanayojiri kutoka katika vita nchini Ukraine :
Wito wa silaha
- ·Mawaziri wa mambo ya kigeni wa G7 wamelaani "mauaji ya kikatili" katika ‘’vita yaukatili " ya Urusi katika Ukraine na kuyataja kama ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa
- ·Silaha zimeonekana kuwa ajenda muhimu ya leo, huku Ukraine ikitoa wito wa msada zaidi wa kijeshi kutoka kwa nato kuyanusuru Maisha ya raia dhidi ya mashambulio ya Urusi
- ·Akizungumza katika mkutano wa Nato mjini Brassels, waziri wa mambo ya nje Dmytro Kuleba alipongeza awamu mpya ya vikwazo, lakini pia akatoa wito kwa mataifa ya magharibi kuongeza juhudi na kumaliza matumizi ya mafuta na gesi ya Urusi
- ·Mawaziri wa mambo ya nje kutoka muungono wa Nato wameingia siku ya pili ya mkutano, huku majadiliano yakiangazia zaidi juu ya njia bora zaidi za kuisaidia Ukraine
Hali Ukraine kwenyewe
- Jeshi laUrusi linafanya juhudi za kufanikiwa katika jimbo la Donbas, Wizara ya ulinzi ya Uingereza inasema
- Huku vikosi vya Urusi vikiondoka kutoka kaskazini mwa Ukraine, taarifa zaidi za kusikitisha zinajitokeza
- BBC imeambiwa kwamba wanajeshi wa Urusi waliwatumia watu kama ngao za vita kujilinda na mashambulio kutoka Ukraine katika vijiji vya kaskazini mwa Ukraine kaskazini
- Waandishi wetu pia wameshuhudia maeneo ya makazi yaliyoangushwa katika Chernihiv, kuelekea kaskazini-mashariki mwa mji mkuu Kyiv
Unaweza pia kusoma:
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Kwa picha: Rais Samia katika kumbukizi ya miaka 50 ya aliyekuwa raia wa kwanza wa Zanzibar
WHO latahadharisha juu ya uchimbaji wa mafuta yenye madhara kiafya
Karibu kila mtu anavuta hewa chafu, huku magonjwa yasiyoambukiza yakiongezeka Afrika, WHO limetahadharisha.
Mabadiliko ya tabia nchi yamebainika kuwa moja ya tisho kubwa zaidi la afya ambalo binadamu wanakabiliana nalo, huku watu wapatao milioni 13 wakifariki kila mwaka kutokana na sababu za kimazingira kote duniani.
Shirika la afya duniani limetaja uchimbaji wa mafuta yatokanayo na makaa (fossil Oil) kuwa chanzo cha utoaji wa hewa chafu yenye madhara, ambayo inahusiana na magonjwa sugu. WHO limetoa wito wakuchukuliwa kwa hatua za kukabiliana na matumizi yake.
“Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, mengi ya matukio ya kiafya yamekuwa yakihusiana na mazingira, iwe ni yale yatokanayo na sababu nyingine au yatokanayo na maji machafu, ambayo watu waliyaambukizwa kutoka kwa wanyama au kutokana na majanga,” alisema Dkt Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika.
Kulingana na DKt Moeti , magonjwa yasiyaoambukizwa yanatarajiwa kuwa mengi zaidi ya magonjwa ya kuambukizwa, ya kipindi cha ujauzito na ya baada ya kujifungua, pamoja na magonjwa yatokanayo na ukosefu wa virutubisho vya mwili kwa pamoja, na hivyo kusababisha vifo ifikapo mwaka 2030.
Kenya yachunguza usalama wa kiafya wa chokoleti ya Kinder Joy
Mamlaka ya udhibiti wa viwango nchini Kenya inaripotiwa kuchunguza usalama wa kiafya wa chokoleti maarufu inayofahamika kama Kinder Joy ambayo imekuwa ikiondolewa kwenye maduka ya Ulaya kwa hofu za kiafya.
Mamlaka ya viwango nchini Kenya imeliambia gazeti Business Daily newspaper nchini humo kwamba sampuli za bidhaa hizo zilizopo kwenye soko la Kenya zitafanyiwa uchunguzi.
Shirika la viwango vya vyakula nchini Uingereza liliondoa bidhaa hizo zinazo tengenezwa nakampuni ya Italia -Ferrero – ambayo ni watengenezaji wa Kinder Joy – wiki hii kutokana na visa 63 vya bakteria aina ya Salmonella husasan ni miongoni mwa Watoto.
Ferrero ilisema kuwa hakuna bidhaa yake yoyote ya Kinder ilitotolewa kwa ajili ya mauzo iliyopatikana na salmonella baada ya kupimwa.
Salmonella ni aina ya bakteria ambayo inaweza kusababisha dalili kama vile kuendesha, kupanda kwa joto mwilini na maumivu ya tumbo.
Visa vingi vimeripotiwa Ulaya, ikiwa ni pamoja na mataifa ya Ireland, Ufaransa, Ujerumani, Sweden na Uholanzi.
Wanafunzi watatu wafariki kwa mshituko wa moyo wakati wa mtihani
Wakazi wa jimbo la Gujarat nchini India wanaendelea kupigwa na mshangao baada ya wanafunzi watatu kufariki ghafla kutokana na mshituko wa moyo kutokana na mtihani.
Jumatatu, mwanafunzi aliyetambuliwa kwa jina la Sneh alizimia ghafla wakati alipokuwa akiandika kwenye karatasi ya mtihani katika shule ya sekondari ya Limbassi, magari ya kubebea wagonjwa 108 kuokoa Maisha yake. Madaktari waliowasili katika hospitali walisema mwanafunzi huyo alikufa kutokana na mshituko wa moyo.
Awali katika eneo la Ahmedabad, mwanafunzi kwa jina Sheikh Mohammad Aman Arif aliyekuwa akifanya pia mtihani alianza kuwa na dalili za kuzorota kwa afya yake kutokana na mtihani aliokuwa akiufanya. Gari la kubebea wagonjwa liliitwa na kukimbizwa hospitalini ambako aliongezewa oksijeni lakini alifariki na madaktari walisema shinikizo la damu yake lilikuwa la kiwango cha juu .
Saw ana wenzake, Utsav Shah, mwanafunzi mwingine wa sekondari katika shule yaNavsari, alifariki kwa mshituko wa moyo kabla ya muanza kufanya mtihani. Watu wa familia yake walimkimbiza hospitalini akiwa na maumivu ya kifua, ambako madaktari walitangaza kuwa amefariki. Baba yake alisema alikuwa na mshituko wa moyo.
Kifo cha ghafla cha wanafunzi wanaofanya mtihani wa kitaifa kimewashitua wengi, kwani haijawahi kutokea miaka iliyopita.
Mahakama ya Nigeria yaidhinisha Wanawake washikilie robo ya kazi za umma
Mahakama nchini Nigeria imeagiza serikali kutekeleza sera ya usawa wa jinsia inayoleza kuwa 35% ya uteuzi wa nyadhifa katika ofisi za umma itengwe kwa ajili ya wanawake.
Uamuzi wa Jaji Donatus Okorowo umepongezwa na wanakampeni wa haki za binadamu.
Makundi ya wanawake wa Nigeria yamekuwa yakitoa wito wa uwakilishi wa wanawake katika siasa na nyadhifa za uteuzi.
Mwanaharakati Mufuliat Fijabi, ambaye alikuwepo waati uamuzi huo ulipotolewa na mahakama, ameviambia vyombo vya habarikwamba amefurahia uamuzi huo.
Hii inakuja wakati wabunge wa Nigeria wakitarajiwa kupigia kura tena miswada ya usawa wa jinsia mitatu kati ya mitano iliyokataliwa wiki hii.
Bunge lilisitisha uamuazi wake mwezi uliopita baada ya makundi ya wanawake kuandamana kote nchini.
Rais wa Somalia apinga uamuzi wa waziri mkuu wa kumtimua mwakilishi wa AU
Rais wa Somali Abdullahi Farmajo amepuuzilia mbali hatua ya waziri mkuu ya kumfukuza nchini humo, mwakilishi maalumu wa Muungano wa Afrika nchini humo.
Waziri mkuu Mohamed Hussein Roble awali alisema kuwa Francisco Madeira ni mtu asiyetakikana nchini humo kwa kujihusisha na “vitendo ambavyo haviendani na hadhi yake”.
Katika taarifa, alisema kwamba mwakili wa AU alikuwa na saa 48 za kuondoka nchini humo.
Lakini akipinga hatua hiyo, Bw Farmajo alisema serikali “haiidhinishi hatua zilizo kinyume cha sheria ” na “sera yetu ya kigeni haifuati hysia na maslahi ya kibinafsi dhidi ya Bw Madeira”.
Hatua hii ya kupingana inakuja huku kukiwa na mgawanyiko wa muda mrefu katika mahusiano baina ya rais farmajo na waziri mkuu.
Hali ya uhasama wa kisiasa baina ya viongozi hawa wawili imekuwa ikilaumiwa kwa kuchelewesha uchaguzi wa wabunge ambao umekuwa ukifanyika tangu mwezi Februari.
Bw Madeira, ambaye anatoka katika taifa la Msumbiji, aliteuliwa kuchukua wadhifa huo wa AU mwaka 2015.
Picha za vifaru vya kijeshi vya Czech vimeripotiwa kuelekea Ukraine
Televisheni ya Czech imeonyesha picha za zana za kijeshi katika treni katika kituo katika mji wa Jihlava – zilizoripotiwa kuelekea Ukraine.
Jumanne waziri wa ulinzi wa Czech Jana Cernochova alisema Jamuhuri ya Czech inatuma " vifaa muhimu vya kijeshi" nchini Ukraine.
Akizungumza huku kikao cha mawaziri wa mambo ya nje wa Nato mjini Brassels wanaojadili mzozo wa Ukraine, Katibu mkuu wa usalama wa muungano huo Jenerali Jens Stoltenberg alisema hataingia katika maelezo ya kina kuhusu ni aina gani za silaha washirika wa muungano huo wanazozitoa kwa Ukraine.
"Lakini ninaweza kusema wa ujumla kile ambacho washirika wanakifanya ni muhimuna kwamba inajumuisha pia baadhi ya mifumo mizito zaidi kwa pamoja na mifumo myepesi."
Jamuhuri ya Czech - ambayo kama sehemu ya Czechoslovakia ilikuwa katika mkataba wa Warsaw na mshirika wa Muungano wa Usovietu-ilijiunga na Nato mwaka 1999.
Vifaru vimeripotiwa kutengenezwa na Usovieti au Urusi.
Unaweza pia kusoma:
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Rais wa zamani wa Burkina Faso aachiliwa huru kutoka kizuizini
Rais aliyeng’olewa mamlakakani nchini Burkina Faso Roch Kaboré ameruhusiwa kurejea nyumbani katika mji mkuu, Ouagadougou, serikali ya kijeshi imesema katika taarifa yake.
Bw Kaboré alikuwa amefungwa kifungo cha nyumbani katika jengo la serikali katika mji mkuu tangu mwezi wa Januari katika mapinduzi yaliyoongozwa na Luteni Kanali Paul-Henri Damiba, ambaye kwa sasa ni mkuu wa nchi.
Chama chake kimeithibitishia BBC kwamba ameachiliwa huru, bila kutoa maelezo zaidi.
Tangazo la kuachiliwa huru kwake kunakuja baada ya wiki kadhaa za mashauriano.
Pia inafuatia miito ya jamii ya kimataifa ya kutaka aachiliwe.
Serikali iliongeza kwamba hatua zilikuwa zinachukuliwa kuhakikisha usalama wake.
Unaweza pia kusoma:
- Ripoti: Thomas Sankara aliuawa kinyama
- Kesi ya Thomas Sankara nchni Burkina Faso: Ni nani aliyemuua Che Guevara wa Afrika?
Mali yachunguza madai ya mauaji yaliyotekelezwa na wapiganaji wa Urusi
Mamlaka za kijeshi nchini Mali zimesema kuwa zimefungua uchunguzi kuhusu madai ya mauaji ya raia yaliyofanywa na wanajeshi wa Mali na wapiganaji wa kigeni.
Jeshi la Mali lilisema Ijumaa iliyopita kuwa limewaua zaidi ya wanamgambo 200 wa Kiislamu katika kipindi cha siku 10 za mapigano katika eneo la kati la Moura.
Lakini Marekani, EU na Umoja wa Mataifa wametaka uchunguzi huru ufanyike kuhusu ripoti kwamba mamia ya raia waliuawa na wanajeshi wa serikali na mamluki wa Urusi wanaojulikana kama kundi la Wagner.
Maelfu ya wanajeshi na raia wameuawa katika mzozo wa miaka 10 wa Mali na wanamgambo wa Kiislamu.
Marekani yaionya India dhidi ya kuungana na Urusi
Mshauri mkuu wa Rais Joe Biden wa masuala ya kiuchumi amesema kuwa Marekani iliionya India dhidi ya kushirikiana kwa karibu sana na Urusi kufuatia uvamizi wa Ukraine.
"Ujumbe wetu kwa serikali ya India ni kwamba gharama na matokeo kwao ya kuhamia katika upatanishi wa kimkakati ulio wazi zaidi na Urusi itakuwa muhimu na ya muda mrefu," Mkurugenzi wa Baraza la Kitaifa la Uchumi la White House Brian Deese aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.
"Kwa hakika kuna maeneo ambayo tumekatishwa tamaa na maamuzi ya China na India, katika muktadha wa uvamizi," aliongeza.India imekataa kuweka vikwazo dhidi ya Urusi, kama nchi zingine zilivyofanya.
Nchi hiyo, ambayo Marekani inaiona kuwa ni kinzani dhidi ya uwezo wa China barani Asia, ndiyo nchi inayoagiza zaidi silaha za Urusi kutoka nje ya nchi, kulingana na Bloomberg.Inakuja baada ya Naibu Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Daleep Singh kufanya ziara rasmi nchini India wiki iliyopita.
"Kile ambacho Daleep aliweka wazi kwa wenzake wakati wa ziara hii ni kwamba hatuamini ni kwa manufaa ya India kuharakisha au kuongeza uagizaji wa nishati ya Urusi na bidhaa nyingine," msemaji wa White House Jen Psaki alisema baada ya Bw Singh kurejea wiki hii.
Urusi yakamilisha kuyaondoa majeshi yake kutoka Kyiv na Chernihiv - Pentagon
Maafisa wa idara ya ulinzi ya Marekani wamesema kuwa hatua ya Urusi kujiondoa katika mikoa ya Kyiv na Chernihiv sasa imekamilika.
"Vikosi vya Urusi karibu na Kyiv na Chernihiv vimekamilisha kujiondoa katika eneo hilo ili kuungana tena na kurejea Belarus na Urusi," afisa wa Pentagon aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.
"Hatuonyeshi vikosi vya Urusi ndani au karibu na Kyiv au ndani au karibu na Chernihiv," msemaji wa Pentagon John Kirby baadaye aliongeza, akisema kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin "amefikia sifuri ya malengo yake ya kimkakati".
"Kwa kweli anadhibiti tu vituo vidogo vya watu .... Hawajachukua Kharkiv."
Inakuja siku chache baada ya Urusi kutangaza kwamba itaelekeza nguvu zake katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine.
Afisa mkuu wa Pentagon, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kwamba wanajeshi wa Urusi wanaweza kurudi Kyiv katika siku zijazo, na kwamba bado haijafahamika ikiwa wanajeshi wanaorejea ndio watakaotumwa tena .
Kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Vita ,vitengo vya Urusi vinavyorudi kutoka karibu na Kyiv vina uwezekano wa "kupata tena ufanisi wa vita kwa muda".
Kati ya vikosi 130 vya Urusi ambavyo vimetumwa Ukraine, zaidi ya 80 bado vimesalia nchini, afisa huyo alisema.
Shirika la habari la Associated Press, likimnukuu afisa wa ulinzi wa Marekani, akisema kwamba idadi ya wanajeshi wa Urusi walioondoka ni takriban watu 24,000.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Alhamisi tarehe 7 Aprili 2022