Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Vikwazo vipya vya Marekani vyalenga familia ya Putin

Ikulu ya White House imetangaza vikwazo vipya dhidi ya maafisa wa ngazi ya juu wa Urusi, wakiwemo mabinti wa Putin na jamaa za Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo twakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  2. Kimbieni sasa au muwe hatarini kuuawa, Ukraine yawaambia watu wa mashariki

    Watu wanaoishi mashariki mwa Ukraine wamehimizwa na serikali kuhama huku wakipata nafasi. Lakini Urusi inapanga nini katika eneo hilo?

    Moscow imewaondoa wanajeshi wake kutoka Kyiv na kuelekeza mtazamo wake kwa Donbas ya zamani ya makaa ya mawe na chuma - ambayo inajumuisha mikoa miwili mikubwa ya mashariki, Luhansk na Donetsk. Kirusi

    Kiongozi huyo wa Urusi mara kadhaa ametoa shutuma zisizo na msingi kwamba Ukraine imefanya mauaji ya halaiki mashariki mwa nchi.

    Vita vilipoanza, theluthi mbili ya mikoa ya mashariki ilikuwa mikononi mwa Ukraine. Mengine yaliendeshwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

    Rais Putin ametambua maeneo hayo mawili ya mashariki kuwa huru kutoka kwa Ukraine.

    Hatua inayofuata itakuwa kunyakua Donbas, kama vile Putin alivyofanya na Crimea baada ya kura ya maoni iliyopingwa mwaka 2014.

    Unaweza pia kusoma:

  3. Habari za hivi punde, Vikwazo vipya vya Marekani vinalenga familia ya Putin

    Marekani imeweka vikwazo dhidi ya watu wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin wakiwemo mabinti zake.

    Orodha hiyo pia inajumuisha familia ya Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov na benki kuu.

    Hatua hizo zinafuatia ufichuzi mpya wa ukatili unaofanywa na wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine, zikiwemo picha za miili ya raia iliopatikana katika mitaa ya Bucha, karibu na mji mkuu wa Kyiv.

    Urusi inasema, bila ushahidi, picha hizo zinazonyeshwa na maafisa wa Kyiv ni feki.

    Umoja wa Ulaya pia unatarajiwa kusitisha uagizaji wa makaa ya mawe kutoka nchini Urusi huku wasiwasi juu ya madai ya uhalifu wa kivita ukiongezeka.

    Kabla ya msururu mpya wa vikwazo kutangazwa mjini Washington, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema hawezi "kuvumilia hali yoyote ya kutofanya maamuzi"

    Unaweza pia kusoma:

  4. Vita vya Ukraine: Mpango wa $4bn wazinduliwa kusaidia Afrika

    Taasisi ya kifedha inayoongoza barani Afrika, Afreximbank, inasema imebuni mpango wa ufadhili wa biashara wa takriban dola bilioni nne (£3.3bn) ili kuliepusha bara hilo dhidi ya athari za vita nchini Ukraine.

    "Kwa kuzingatia umuhimu wa Urusi na Ukraine kama vyanzo vya mafuta na gesi ghafi, malighafi na nafaka, kuzuka kwa mzozo huo kuna athari kubwa zaidi kwa kiwango cha kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuathiri vibaya uchumi wa Afrika, haswa zile zinazotegemea sana nafaka, mbolea na uagizaji wa mafuta kutoka nje," ilisema katika taarifa.

    Benki hiyo ilisema tayari imepokea maombi ya ufadhili wa zaidi ya dola bilioni 15.

    "Tuanaharakisha kutimiza maombi haya ili kuepusha hali mbaya ya kijamii barani Afrika na kupunguza hatari ya kubadilika kwa hali hiyo kuwa changamoto za kisiasa," iliongeza.

    Unaweza pia kusoma:

  5. Ghadhabu yaibuka juu ya kufungwa kwa asiyeamini Mungu kwa kukufuru

    Wanaharakati wa haki za binadamu wameelezea kukasirishwa na kuhukumiwa kwa mwanaume asiyeamini Mungu kifungo cha miaka 24 jela na mahakama ya jimbo la kaskazini mwa Nigeria la kano.

    Mubarak Bala, ambaye ni rais wa shirika la Humanist Association of Nigeria, alikamatwa mwaka 20202 na Jumanne alikana mashitaka 18 ya kukufuru dhidi ya Uislamu na kutuma jumbe kwenye mitandao ya kijamii ambazo zingeweza kuchochea ghasia.

    Humanist International, shirika lililojitolea kuboresha uhuru wa kuamini kote dunia, lilielezea hukumu kama ‘’ya kukasirisha’’.

    Lilisema ni ‘’siku ya aibu kwa mamlaka za Nigeria ".

    Tume ya Marekani kuhusu Uhuru wa uhuru wa kimataifa wa kidini pia imelaani kufungwa kwa Bala.

    Kikundi chake, the Humanist Association of Nigeria, kimesema ulikuwa ‘’mshituko mkubwa’’ na ni ‘’siku ya huzuni’’ kwa utu na uhuru.

    Lakini huku ya mahakama imeafikiwa na mahakama za kaskazini mwa Nigeria- jimbo lenye Waislamu wengi – huku baadhi wakisema matendo yake yalidhalilisha dini ya wengine.

    Makundi ya haki za binadamu yamesema yataendelea kukampeinia kuachiliwa kwake.

    Bala mwenye umri wa miaka 37 ambaye hamuabudu Mungu, aliukana Uislamu mwaka 2014 na baadaye akawa rais wa shirika la utu la Nigeria-Humanist Association of Nigeria.

  6. Rais wa zamani ahukumiwa kifungo cha maisha kwa mauji ya Sankara

    Mahakama ya kijeshi nchini Burkina Faso imemuhukumu rais wa zamani Blaise Compaore kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusika katika mauaji ya mtangulizi wake thamas sankara mwaka 1987.

    Compaore, ambaye yuko uhamishoni, alihukumiwa bila kuwepo.

    Mkuu wake wa usalama, Hyacinthe Kafando, pia alihukumiwa kifungo cha Maisha jela.

    Bw Sankara, mwanamapinduzi aliyekuwa na itikadi za Kimarxist, aliuawa kwa kupigwa risasi na kundi la watu wenye silaha katika mji mkuu, Ouagadougou katika mwaka 1987.

    Baada ya mauji hayo Compaore alitawala kwa miaka 27 kabla ya kupinduliwa mwaka 2014.

    Unaweza pia kusoma:

    • Kesi ya Thomas Sankara nchni Burkina Faso: Ni nani aliyemuua Che Guevara wa Afrika?
    • Thomas Sankara na Patrice Lumumba: Mashujaa waliouawa katika hali za kutatanisha
    • B.Faso:mwili wa Thomas Sankara kufukuliwa
  7. Mapigano mapya yaibuka DRC baina ya serikali na waasi wa M23

    Mapigano mapya yameibuka mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congokatika jimbo la Kivu Kaskazini Jumatano asubuhi.

    Vyanzo vya habari vinasema kuwa vikosi vya serikali vinapigana kuchukua tena vijiji katika eneo la Rutshuru, ambalo kwa sasa linadhibitiwa na waasi wa M23.

    Mkazi wa mji wa mpakani wa Bunagana ameiambia BBC kwamba wanaweza kusikia milio ya silaha nzito kwa umbali.

    M23 walitangaza usitishaji wa mapigano tarehe 1 Aprili, ili kutoa fursa ya mazungumzo na serikali.

    Viongozi wa kikanda walitarajiwa kukutana kwa ajili ya mazungumzo ya amani mwishoni mwa juma hili.

    Unaweza pia kusoma:

    • Je waasi wa M23 watakoma?
    • Waasi wa M23 waingia DRC
  8. Ed Sheeran ashinda kesi ya hakimiliki kuhusu wimbo wa Shape of You

    Ed Sheeran ameshinda kesi kwenye mahakama ya juu zaidi juu ya hakimiliki ya wimbo wake wa mwaka 2017 uliovuma kwa jina-Shape of You.

    Jaji aliamua Jumatano kwamba mwimbaji na mwandishi huyo hakunakili wimbo huo wa mwaka 2015 unaojulikana kama Oh Why ulioimbwa na Sami Chokri.

    Chokri, ambaye ni msanii anayeimba chini ya nembo ya jina Sami Switch, alikuwa amedai kuwa "Oh I" ulijitokeza katika wimbo wa Sheeran "ukiwa unafanana sana" na wimbo wa "Oh why" ambao aliuimba mwenyewe.

    Sheeran alisema hakumbuki akisikia 'Oh Why' kabla ya kesi

    Shape of You ulikuwa ni wimbo uliouzwa zaidi nchini Uingereza mwaka 2017 na ni wimbo uliochezwa zaidi katika App ya Spotify kuwahi kushuhudiwa.

  9. Wanamgambo wa Ethiopia washutumiwa kuangamiza jamii ya Tigray

    Makundi mawili ya kutetea haki za bindamu yamevishutumu vikosi kutoka jimbo la Ethiopia la Amhara kwa kuendesha kampeni ya kuangamiza jamii dhidi ya Watigrinya.

    Katika ripoti ya pamoja, mashirika hayo, Amnesty International na Human Rights Watch (HRW) yamewashutumu maafisa wa Amhara na vikosi maalumu vya kikanda na wanamgambo wanaopigana magharibi mwa Tigray kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.

    Pia wamelishutumu jeshi la Ethiopia kwa kuhusika katika vitendo hivyo.

    Mashrika hayo ya haki za binadamu yaliwahoji zaidi ya watu 400 katika kipindi cha mwaka mmoja, na kutumia picha za setilaiti kukusanya Ushahidi kutoka kwenye jimbo hilo ambako imekuwa vigumu sana kwa waandishi wa habari, makundi ya misaa na wengine kufika.

    Makundi hayo yanasema kwamba maelfu ya Watigrinya wameendelea kufungwa kinyume cha sheria na yametoa wito waachiliwe mara moja.

    Katika barua kwa mashirika hayo, serikali ya jimbo laAmhara imezitaja shutuma katika ripoti hiyo -uongo..

    Fisseha Tekle, mtafiti wakikanda wa Amnesty International kwa ajili yae neo la upembe wa Afrika, ameiambiaBBC juu ya kile alichokielezea kama mambo ya kushtua waliyoyabaini.

    " Kampeni hii ya kuangamiza jamii ilifanyinyika kupitia msururu wa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuwafunga watu na kuwatesa, unyanyasaji wa kingono, mauaji ya kiholela, kunyima watu misaada ya kibinadamu na kuwalazimisha Watigrinya kuyahama makazi ," alisema.

    Mzozo katika Tigray umekuwa ukiendelea kwa zaisi ya mwaka mmoja,na makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema umewalazimisha mamilioni ya watu kukimbia.

    Kulingana na Umoja wa Mataifa, vita hivyo pia vimewaacha maelfu ya watu wakikumbwa na njaa.

    Wiki iliyopita, malori kadhaa yaliwasili katika mji mkuu wa Tigray kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa. Misaada hiyo ilifika huko baada ya serikali ya Ethiopia kutangaza mkataba wa kibinadamu.

    Hatahivyo, Amnesty International linasema jimbo la magharibi la Tigray bado halijapata msaada linaouhitaji.

    Unaweza pia kusoma:

    • Ethiopia: Mzozo wa Tigray ulivyogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe
    • Mzozo wa Ethiopia: Ndani ya mji wa Makelle uliotengwa na ulimwengu
    • Mzozo wa Tigray: Kufufuka kwa uasi kunamaanisha nini kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia?
  10. Ukraine: Maelfu ya wakazi wa Donbas wayakimbia mashambulizi ya Warusi

    Melfu ya wakazi wa jimbo la mashariki mwa Ukraine la Donbas wanakimbilia magharibi mwa nchi.

    Mwandishi wa BBC Jonathan Beale anasema kumekuwa na msururu mrefu wa magari wakati walipokuwa wakiwasili katika eneo hili-ambako mapigano yanaendelea.

    Ni katika mji huu ambako Urusi imeweka kambi baada ya kuondoa vikosi vyake magharibi.

    Jeshi la Ukraine linasimamia usalama katika vituo vyote vya ukaguzi katika barabara zotendani nan je ya jimbo.

    Pia wanavipanga upya vikosi vya ulinzi Pamoja na wataalamu wengine wa jesi wa Ukraine katika jimbo hilo.

    Jeshi la Ukraine limekuwa likipambana na waasi wanaoungwa mkono na Urusi kwa miaka minane katika jimbo la Donbas.

    Vikosi vya Urusi kwasasa vinadhibiti eneo kubwa la Luhansk na zaidi ya nusu ya Donetsk, huku vikijaribu kulizingira jeshi la Ukraine.

    Unaweza pia kusoma:

  11. Yanayojiri leo kuhusu vita ya Ukraine

    • Marekani na EU wako tayari kuiwekea urusi viikwzo zaidi huku kukiwa na madai ya uhalifu wa kivita katika mji wa Ukraine wa Bucha
    • Washington inaripotiwa kuangalia uwezekano wa kuchukua hatua zinazowalenga mabinti wawili wa Rais Putin na benki kubwa zaidi ya Urusi.
    • Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa hotuba kwa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa ambapo aliainisha orodha ya maafa yanayodaiwa kufanywa na Warusi.
    • ·Katika kauli kali ambayo haijawahi kutolewa tangu ilipovamiwa na Urusi, Ukraine , India imelaani maukaji katika mji wa Bucha nchini Ukraine na kuunga mkono miito ya kufanyika kwa uchunguzi huru juu ya ‘’ripoti zinazosikitisha sana’’

    Ukraine kwenyewe

    • Vikosi vya Urusi vimelenga juhudi zake operesheni ya "uchokozi" inayolenga kupata udhibiti kamili wa majimbo ya Donetsk na Luhansk,Mkuu wa majeshi ya Ukraine amesema katika taarifa za kila siku juu kuhusu mzozo wa Ukraine.
    • Mapigano makali na mashambulio ya ndege za Urusi yameendelea katika mji wa mwambao wa Mariupol, kulingana na taarifa za hivi punde za ujasusi kuka wizara ya ulinzi ya Uingereza.
    • Mawaziri wa mambo yan je wa Nato watakutana mjini Brussels baadaye leo kwa ajili ya mazungumzo ya siku mbili kujadili juu ya njia bora zaidi ya kuisaidia Ukraine katika awamu ijayo ya mzozo .

    Unaweza pia kusoma:

  12. Mtawa wa Kimarekani atekwa nyara kaskazini mwa Burkina Faso

    Mtawa wa kike mwenye umri wa miaka 83 ametekwa nyara nchini Burkina Faso Askofu wa dayosisi ya kaskazini ya Kaya amesema kuwa watu wenye silaha walimchukua kutoka kwenye makazi ya watawa ambako waliiba vitu kwenye vyumba na gari.

    Mtawa alikuwa mehudumu kwenye parokia hiyo tangu Oktoba mwaka 2014

    Msako unaendelea katika eneo hilo linalopakana na jimbo la Soum ambako mashambulio dhidi ya raia yamekuwa yakiongezeka na ambako kuna makundi ya watu wenye silaha ambayo yamekuwa yakiwashambulia watu.

    Raia wa Magharibi kadhaa wamekuwa wakitekwa nyara na wanamgambo wa Kiislamu katika Burkina Faso na maeneo mengine ya Sahel katika miaka ya hivi karibuni.

  13. Polisi Malawi yamuachilia huru mwandishi wa habari maarufu baada ya uvamizi wa ofisi

    Polisi nchini Malawi imemuachilia mwandishi wa habari za uchunguzi baada ya kumkamata kwa saa kadhaa kufuatia uvamizi katika ofisi yake.

    Gregory Gondwe ambaye ni mkuu wa jukwaa la waandishi wa habari za uchunguzi(PIJ), chapisho la uchunguzi la mtandaoni ambalo limekuwa maarufu kwa kuchapisha msururu wa ripoti zinazofichua ufisadi wa kiwango cha juu..

    Mwandishi mwenzake , Golden Matonga, alisema kuwa polisi waliidai kujua vyanzo vya baadhi ya nyaraka za serikali zilizochapishwa katika na jukwaa la PIJ.

    Maafisa wa usalama Jumanne walishikilia kompyuta na vifaa vingine mali ya Bw Gondwe na chombo chake cha habari, aliongeza.

    Polisi walikataa kutoa kauli yai kuhusu kushikiliwa kwa mwandishi huyo.

    Taasisi inayofuatilia utendaji wa vyombo vya habari nchini Malawi imelaani tuki hilo, ikisema kumlazimisha mwandishi wa habari kufichua vyjanzo vya habari kunakiuka haki ya ulinzi ya mfichuzi wa habari.

    Ubalozi wa Uingereza nchini Malawi umesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamaba ulikuwa "unatiwa hofu sana" juu ya uvamizi wa polisi:

    Ubalozi wa Uingereza nchini Malawi umeeleza kuwa umefahamu kuwa ameachiliwa huru, ubalozi hatahivyo umeitolea wito polisi kurejesha vifaa inavyovishikilia na kuheshimu usiri wa habari zilizomo ndani ya vifaa hivyo.

  14. Urusi inalenga kudhibiti Donetsk na Luhansk - jeshi la Ukraine

    Vikosi vya Urusi vimeelekeza nguvu zao kuu katika operesheni "ya uchokozi" inayolenga kuweka udhibiti kamili wa mikoa ya Donetsk na Luhansk, Mkuu wa jeshi la Ukraine amesema katika taarifa yake ya kila siku.

    Pia kumekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara katika maeneo ya mashariki mwa nchi, lakini bila mafanikio, taarifa hiyo iliongeza .

    Vikosi vya Urusi pia vinaendelea na juhudi za kuvamia Mariupol, mojawapo ya miji iliyoshambuliwa kwa mabomu na kuharibiwa vibaya zaidi nchini Ukraine.

    Wanajeshi wa Ukraine wamekuwa wakizuia mashambulizi dhidi ya jiji hilo kwa zaidi ya siku arobaini, taarifa hiyo ilisema.

    Pia inadai kuwa Urusi inaendelea kutumia kikamilifu risasi zilizopigwa marufuku na sheria za kimataifa.BBC imeshindwa kuthibitisha hili kwa njia huru

    Unaweza pia kusoma

  15. Mtaalam wa afya aliyeamua kutengeneza viti vya magurudumu

    Msichana Ornella Uwimana kutoka nchini Burundi alisomea masomo ya afya ya udaktari na kuhitimu katika chuo kikuu nchini Burundi mwaka 2020. Hatahivyo baada ya kuhutimu aliamua kufanya kazi ya kutengeneza viti kwa kutumia magurudumu ya magari.

    Kwa mara ya kwanza alitengeneza viti vya aina hii mwaka 2016 akiwa bado ni mwanafunzi

    "Nilinunua magurudumu manane kwa franga za Burundi 40,000, na ili kuniunga mkono mzazi wangu alivipenda viti vyangu na kuvinunua akaviweka kwenye veranda ya nyumba’’.

    Ujuzi aliutoa wapi?

    Ornella anasema hupenda kujifunza mambo mengi kwenye mtandao wa YouTube, ukiwemo ujuzi wa kutengeneza viti vyake.

    "Nilianza kufanyika kazi nyumbani lakini sasa ninafanyia kazi mahala ambapo ninaweza kulipia kila mwezi’’ anasema Ornella, na kuongeza kuwa ‘’nimewaajiri wafanyakazi watatu wa kudumu na wengine wanne ambao huja ninapowahitaji’’

    Ushauri kwa vijana

    Ornella Uwimana anawashauri vijana kufanya kazi yoyote ile inayoweza kuwasaidia kujiendeleza kimaisha, bila kuchagua.

    "Kuna wengi wanaoniona nikitafuta magurudumu wananishangaa. Wengine hata huninyima na kunilazimu kuwaomba mafundi wa magari…Kuna hata wanaonichekawakiniona natoboa mataili…lakini sasa baadhi wameanza kugundua kuwa nimeanza kujiendeleza kimaisha.

  16. Marekani inaweza kuwawekea vikwazo mabinti wawili wa Putin

    Marekani na Umoja wa Ulaya zinatazamiwa kuiwekea Urusi vikwazo zaidi siku ya Jumatano kujibu madai ya Ukraine kwamba wanajeshi wa Urusi walifanya uhalifu wa kivita katika mji wa Bucha.

    Katibu wa habari wa Ikulu ya White House Jen Psaki alisema Marekani itapiga marufuku uwekezaji mpya nchini Urusi na kuweka vikwazo zaidi kwa taasisi za fedha za Urusi, pamoja na maafisa wa Kremlin na familia zao.

    Gazeti la Wall Street Journal linaripoti kwamba Washington inazingatia vikwazo vya ziada dhidi ya binti wawili wa Putin na Sberbank, benki kubwa zaidi ya Urusi.

    Mabalozi wa Umoja wa Ulaya Jumatano watazingatia mipango ya kifurushi cha tano cha vikwazo, ambavyo ni pamoja na kupiga marufuku uagizaji wa makaa ya mawe ya Urusi, na kuzuia meli nyingi zinazomilikiwa na Urusi au zinazoendeshwa kutumia bandari za EU.

    Unaweza pia kusoma

  17. Ukraine kupokea vifaru vya Czech na makombora ya $100m ya Javelin kutoka Marekani

    Jamhuri ya Czech imeripotiwa kuwa nchi ya kwanza ya Umoja wa Ulaya kuipatia Ukraine moja kwa moja silaha za kivita tangu uvamizi wa Urusi uanze siku 41 zilizopita.

    Maafisa wakuu wa Czech waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba nchi hiyo imetuma vifaru vya T-72 vilivyotengenezwa na Soviet na magari ya kivita ya BVP-1 kwenda Ukraine, na kuthibitisha ripoti za vyombo vya habari vya ndani ambazo zilionyesha treni iliyosheheni vifaru vitano na magari matano ya mapigano.

    Waziri wa Ulinzi Jana Cernochova aliliambia bunge kuwa hatathibitisha au kukataa maelezo ya msaada wa Czech kwa Ukraine.

    "Nitawahakikishia tu kwamba Jamhuri ya Czech...inasaidia Ukraine kadri inavyoweza na itaendelea kusaidia kwa (kusambaza) zana za kijeshi, nyepesi na nzito," Jana Cernochova alisema.

    Inakuja huku kukiwa na ripoti kwamba serikali ya Ujerumani mapema wiki hii iliondoa pingamizi dhidi ya mfanyabiashara binafsi wa silaha wa Czech anayesafirisha magari56 ya kijeshiyaliyoundwaUjerumani Mashariki hadi Ukraine.

    Marekani yaahidi $100m nyingine katika makombora ya Javelin

    Katika duru ya hivi punde ya usaidizi wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine, maafisa wa Marekani walisema Jumanne kwamba watatoa $100m (£76m) za makombora javelin ya kukinga silaha kwa vikosi vya Ukraine.

    Hili ni kundi la sita la msaada wa vifaa vya Marekani kutolewa kwa Ukraine tangu Agosti.

    Ahadi ya hivi punde ina maana kwamba $1.7bn ya vifaa vya kijeshi imeahidiwa kwa Ukraine na Marekani pekee tangu mashambulizi ya Urusi kuanza tarehe 24 Februari, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

    Msemaji wa Pentagon ya Marekani John Kirby alisema katika taarifa yake kwamba fedha hizo mpya zilizoidhinishwa "zitakidhi hitaji la dharura la Ukraine la kuongeza mifumo ya kuzuia silaha za Javelin , ambayo Marekani imekuwa ikitoa kwa Ukraine na wamekuwa wakitumia kwa ufanisi kuilinda nchi yao. ".

    Unaweza pia kusoma

  18. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Jumatano tarehe 6 Aprili 2022