Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maelfu wakwama huku Urusi ikipuuza usitishaji mapigano- Ukraine
Uokoaji wa raia kutoka katika mji wa Mariupol umeahirishwa huku maelfu wakikwama, kulingana na baraza la jiji la Mariupol. Linasema Upande wa Urusi haujatekeleza usitishaji mapigano wa muda kama ilivyokubaliwa.
Moja kwa moja
Kuweka no-fly zone itamaanisha kujiunga na mzozo - Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema hana nia ya kuweka sheria ya kijeshi nchini kwake, lakini akatahadharisha kuwa nchi yoyote ambayo itawekano-fly zone juu ya anga ya Ukraine itachukuliwa kama imejiunga na vita nchini Ukraine.
"Kusogea kokote katika mwelekeo huu kutachukuliwa na sisi kama kushiriki katika mzozo wa silaha nan chi hiyo ," rais wa Urusi anasema.
atika dhana ya kijeshi,no-fly zone ni eneo ambako ndege zimewekwa marufuku ya kuingia ili kuzuwia mashambulizi au upelelezi. Lakini lazima itekelezwe kwa njia ya kijeshi- ikimaanisha , kunakuwa na uwezekano wa kudungua ndege.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameilaumu Nato kwa kushindwa kuwekano-fly zone Nato akisema ni "udhaifu’’ na ‘’ukosefu wa umoja".
Nato imesema kwa kufanya hivyo itasababisha vita kuwa vibaya zaidi kwa nchi nyingine nyingi zaidi.
Taarifa zaidi kuhusu mzozo wa Ukraine:
- Urusi na Ukraine: No-fly zone-Inacho maanisha na kwanini nchi za magharibi haziwezi kuchukua hatua
- Urusi na Ukraine: Nini kitatokea ikiwa Urusi itadhibiti maeneo yote ya Ukraine?
- Ukraine ilitoka vipi kuwa nchi ya tatu kwa nguvu za nyuklia duniani hadi hali yake ya sasa
Homa ya manjano yalipuka Kenya
Kenya imetangaza mlipuko wa homa ya manjano baada ya watu watatu kufariki dunia na kubainika wengine 15 wanashukiwa kuambukizwa katika kaunti ya Isiolo, kaskazini mwa nchi hiyo.
Wizara ya Afya inasema imetuma jopo la wataalamu wa kushughulikia suala hilo kwa haraka. Wizara ilisema pia kuwa itaweka kipaumbele katika utoaji wa chanjo katika kaunti nyingine zipatazo sita, zilizo jirani na Isiolo ambazo pia zinashukiwa kuwa na maambukizi.
Taarifa za vyombo vya habari nchini Kenya zinaeleza kuwa watu wa kwanza wenye maambuki ya homa ya manjano walibainika katikati mwa Januari mwaka huu katika maeneo ya Merti na Garbatullah, hivyo kuzua maswali ni kwa nini hali ya tahadhari imetolewa Jumamosi Marchi 5.
Lakini hayo ni maeneo ambayo ni vigumu kufikika ambako familia ni za wafugaji huku wakihama kutoka eneo moja hadi lingine kutafuta malisho ya mifugo na maji. Vituo vya afya vina wafanyakazi wachache na vitendea kazi vichache pia.
Homa ya manjano ni hatari inayoenezwa na mbu. Dalili zake ni pamoja na homa kali, kichwa kuuma, mdomo kuwa mchungu na wakati mwingine ini kushindwa kufanya kazi.
Pamoja na chanjo ya homa ya manjano kupatikana katika hospitali za serikali, idadi ya watu waliochanjwa ni ndogo, moja ya sababu ni gharama ya chanjo ambayo inafikia dola za Marekani 18 hadi 20, ambazo ni nyingi kwa watu wengi wa Kenya hususan wa vijijini.
Mlipuko wa mwisho wa homa ya manjano nchini Kenya ulitokea 1992/1993
Urusi inapiga makombora katika miji iliyotangaza kusitisha mapigano Ukraine
Uokoaji wa raia kutoka katika mji wa Mariupol umeahirishwa, kulingana na baraza la jiji laMariupol. Linasema Upande wa Urusi haujatekeleza usitishaji mapigano wa muda kama ilivyokubaliwa.
Linasema wakazi wanapaswa kutawanyika na kutafuta mahala pa kujificha na kwamba taarifa zaidi zitatolewa karibuni.
Dakika chache zilizopita meya wa mji huo aliiambia BBC kuwamji wa Mariupo ulikuwa ukipigwa makombora, na kuna ripoti kwamba mapigano yanaendela karibu na mwisho wa barabara ya kuwaokolea watu.
Meya Serhiy Orlov ameiambia BBC kuna ufyatuaji wa makombora unaoendelea katika Mariupol, na kwenye barabara ya uokoaji iliyokubaliwa, karibu na mji wa Orikhiv.
"Sio salama kwenda kwa barabara kwasababu ya haya mapigano," anasema.
Serikali ya Ukraine tayari inazungumza na maafisa wa Urusi kuhusu ukiukaji wa usitishaji mapigano, anasema na majadiliano yanaendelea.
Taarifa zaidi kuhusu mzozo wa Ukraine:
- Urusi na Ukraine: No-fly zone-Inacho maanisha na kwanini nchi za magharibi haziwezi kuchukua hatua
- Urusi na Ukraine: Nini kitatokea ikiwa Urusi itadhibiti maeneo yote ya Ukraine?
- Ukraine ilitoka vipi kuwa nchi ya tatu kwa nguvu za nyuklia duniani hadi hali yake ya sasa
Rais Samia: Benki Tanzania jitanueni nje ya nchi
Benki za Biashara za Tanzania zimehimizwa kuchangamkia fursa ya kufungua matawi katika nchi za nje hivyo kuendelea kushindana vilivyo na benki nyingine kubwa.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu amezimbia benki hizo kuwa anafarijika kuona benki za nchi yake zinakuwa na uwezo wa kushindana na benki nyingine za nje na kwamba anapenda kuona sekta ya benki ambayo ni kubwa imara, shindani na inayokua siku hadi siku.
‘Nawatia moyo endeni kote inapowezekana nje… wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini, wao wana kili na sisi tuna akili’ Alisema Rais Samia wakati akizindua jengo la makao mkuu ya benki ya CRDB ambayo ni moja ya kubwa za kibiashara nchini Tanzania huku akimwagisa mwenyekiti wa chama cha mabenki Tanzania kuungana kutekelza shabaha hiyo.
Japo hakufafanua, kauli ya Rais inaonesha anapenda benki za Tanzania kutanua mtandao wake kwenda nchi nyingi kuanzia za Afrika Mashariki na kwingine Afrika, na duniani kama zilivyo benki nyingine za nje zenye matawi Tanzania. CRDB ndiyo benki ya Tanzania yenye tawi nchini Burundi na inapanga kujitanua hadi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Baadhi ya benki za Afrika Mashariki zenye matawi Tanzania ni Kenya Commercial Bank (KCB) na Equity Bank pia ya Kenya. Nje ya Afrika Mashariki benki za kiafrika zenye matawi Tanzania ni pamoja na ABSA ya Afrika Kusini na BankABC ya Zimbabwe.
usitishaji mapigano wa kwanza siku 10 baada ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine
Kama tulivyoripoti hapo awali, Urusi na Ukraine zimekubaliana kusitisha mapijgano kwa muda mfupikatika miji miwili ya kusini mwa nchi ili kuwaruhusu raia kuondoka katika miji hiyo.
Urusi imesema itakuwa na ‘’ukimwa wa utawala’’ kuruhusu raia kuondoka katika miji ya Mariupol na Volnovakha iliyokumbwa na mapigano
Ni usitishaji mapigano wa kwanza wa kwanza kuafikiwa tangu Urusi ilipoivamia Ukraine siku kumi zilizopita.
Huku ikiwa ni habari njema kwa raia katika Mariupol na Volnovakha wanaotaka kuondoka, miji hii ni maeneo pekee ambako makubaliano ya usitishaji huu wa mapigano wa muda mfupi yanatekelezwa.
Wakati huo huo, miji kote nchini inaendelewa kukabiliwa na mashambulio ya mabomu.
Uokoaji unakaribia kuanza katika kipindi cha chini ya saa, kuanzia saa tano za asubuhi kwa saa za eneo.Tutaendelea kukupatia taarifa kuhusu mzozo wa Ukraine kadri tunavyozipata.
Taarifa zaidi kuhusu mzozo wa Ukraine:
- Urusi na Ukraine: No-fly zone-Inacho maanisha na kwanini nchi za magharibi haziwezi kuchukua hatua
- Urusi na Ukraine: Nini kitatokea ikiwa Urusi itadhibiti maeneo yote ya Ukraine?
- Ukraine ilitoka vipi kuwa nchi ya tatu kwa nguvu za nyuklia duniani hadi hali yake ya sasa
Rais Samia akutana na Mbowe Ikulu
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan jana usiku alikutana na kiongozi wa upinzani nchini humo, Freeman Mbowe Ikulu jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo ilikuja saa chache tu baada ya Mahakama Kuu Divisheni ya makosa ya Uhujumu Uchumi kumuachia huru Mbowe na wenzake watatu, kufuatia ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuiambia mahakama hiyo kuwa haina nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Taarifa fupi kwa vyombo vya habari kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyosambazwa mitandaoni ilieleza kuwa Rais Samia alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.
Mbowe alinukuliwa akimshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali na kwamba amekubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taifa la Tanzania ni kusimama katika haki na kwamba wawili hao walikubaliana kufanya siasa za kistaarabu na za kiungwana huku akiwa tayari kushirikiana na na serikali katika kuleta maendeleo.
Hatua ya Rais Samia kukutana na Mbowe imejadiliwa kwa kina hususan katika mitandao ya kijami. Kwa kiwango kikubwa kuna pongezi nyingi kwa Rais kufanya kikao hicho, na kutoa ishara nzuri ya mshikamano wa kitaifa kama ambavyo Rais Samia amekuwa akizungumza tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021.
Kadhalika kufutwa kwa kesi dhidi ya Mbowe kumepokewa vema kwa ujumla. Hata hivyo wapo wanaokosoa juu ya mashtaka kuwa hayakuwa na msingi ikizingatiwa kuwa mkurugenzi wa mashtaka ameondoa kesi wakati mahakama ikiwa tayari imeamua kuwa washtakiwa wote wanne wana kesi ya kujibu, kufuatia ushahidi uliowasilishwa mahakamani na upande wa mashtaka. Kisheria DPP anayo mamlaka hayo na hawajibiki kufafanua sababu zake za kuondoa kesi.
Mbowe alikuwa gerezani kwa zaidi ya siku 220 tangu alipokamatwa akiwa mjini Mwanza, mji ulio kusini mwa ziwa Victoria Julai, 2021 muda mfupi kabla ya kufanyika kongamano la kudai Katiba mpya ya Taifa. Aliunganishwa na wenzake watatu katika kesi iliyokuwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, ugaidi na kupanga kuwadhuru viongozi wa umma.
Mbowe amekuwa Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tangu mwanzoni mwa miaka 2000 na aliwahi kugombea urais wa Tanzania wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005. Pia amewahi kuwa mbunge wa Hai, Mkoani Kilimanjaro kaskazini mwa nchi hiyo kwa vipindi tofauti.
Sasa anayo kazi kubwa ya kukijenga upya chama chake kuelekea uchaguzi wa 2025 baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi wa 2020 na kupata mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa. Hata hivyo Chadema na baadhi ya vyama vya upinzani vililalamikia uchaguzi huo kuwa ulikuwa na kasoro nyingi zilizokiwezesha chama tawala, CCM kuibuka na ushindi mkubwa, huku CCM ikijibu kuwa ambaye hakuridhika na matokeo afungue kesi mahakamani.
Unaweza pia kusoma:
- Freeman Mbowe: Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema aachiwa huru
- Mahojiano Maalum na Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe hayajachochewa kisiasa
- Kukamatwa kwa Mbowe: Zitto amtaka Rais Samia kuingilia kati
Ni siku ya 10 tangu Urusi iivamie Ukraine, yapi yamejiri kwa sasa?
Ni siku ya 10 tangu Urusi iivamie Ukraine-Na haya ndio yaliyotokea hadi sasa:
- Wizara ya ulinzi ya Urusi imetangaza kipindi kifupi cha usitishaji wa mapigano na kufungua njia za misaada ya kibinadamu kwa raia kuanzia saa nne asubuhi kwa saa za Moscow saa moja asubuhi Jumamosi katika miji miwili kusini-mashariki mwa Ukraine mji wa , Mariupol na Volnovakha
- Urusi inasema imekubaliana na Ukraine kuhusu njia hizo zilizopo nje ya miji, lakini haijaona thibitisho kutoka kwa Ukraine
- Mariupol ni mji muhimu wa bandari na imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi kutoka Urusi kwa siku kadhaa. Kumekuwa na mapigano makali Volnovakha
- Mapema, meya wa Mariupol alitoa wito wa raia kuruhusiwa kuondoka huku kukiwa na kile alichokiita "kizuwizi" cha vikosi vya Urusi
- Kwingineko, mapigano yanaendela. Milipuko mingi ilisikika katika Kharkiv, Kaskazini Mashariki mwa ukraine
- Katika mji wa mashariki wa Sumy, ambao umezingirwa na vikosi vya Urusi, mashambulio ya anga yalianzakumi na moja alfajiri, kulingana na vyombo vya Habari vya Ukraine
Taarifa zaidi kuhusu mzozo wa Ukraine:
- Urusi na Ukraine: No-fly zone-Inacho maanisha na kwanini nchi za magharibi haziwezi kuchukua hatua
- Urusi na Ukraine: Nini kitatokea ikiwa Urusi itadhibiti maeneo yote ya Ukraine?
- Ukraine ilitoka vipi kuwa nchi ya tatu kwa nguvu za nyuklia duniani hadi hali yake ya sasa
Urusi yaridhia kusaidia kuwaondoa wanafunzi wa Kitanzania Ukraine
Ubalozi wa Tanzania mjini Stockholm Sweden pamoja na Ubalozi wa Tanzania ulio nchini Urusi zimesema kwamba kupitia njia za kidiplomasia, serikali ya Urusi imeridhia wanafunzi wa Kitanzania walioko Chuo Kikuu Sumy State kutoka nchini Ukraine kwa kupitia mpaka wa Urusi.
Taarifa ya Ubalozi wa Tanzania mjini Stockholm na Ubalozi wa Tanzania mjini Moscow inasema zoezi la kutoa wanafunzi kutoka Sumy hadi kwenye mpaka wa Urusi linaratibiwa na serikali ya Urusi na tayari mipango ya utekelezaji imeanza.
''Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi utawapokea kwa taratibu nyingine za kurejea nyumbani'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
'Watu wote wanaokufa wanakufa kwasababu yenu'
Akiripotiwa kuzungumza kutoka katika ofisi yake katika mji mkuu Kyiv rais wa Ukraine Zelensky amelaani kutendo cha viongozi wa Nato cha ' kukataa Ijumaa kuanzisha eneo la anga ambalo ndege hazipai -no-fly-zone juu ya nchi yake.
Zelensky alisema: "Watu wote wanaokufa wanakufa kwasababu yenu, kuanzia leo, watakufa kwasababu yenu. Kwasababu ya udhaifu wenu, kwasababu ya kutoungana."
Aliendelea kusema kuwa: " Mkutano wa Nato ulifanyika leo. Mkutano dhaifu. Mkutano uliokanganyikiwa. Mkutano unaoonyesha kwamba sio kila mtu anayechukulia mapambano kwa ajili ya uhusu kwa Ulaya kuwa lengo namba moja.
"Mashirika yote ya ujasusi yan chi za Nato yanafahamu fika kuhusu mipango ya adui. Walithibitisha kuwa Urusi inataka kuendeleza mashambulizi.
"Kwa makusudi Nato iliamua kutofunga anga juu ya Ukraine. Nchi za Nato zimebuni fikra kwamba kufunga anga za juu ya Ukraine kutakuwqa ni uchokozi wa moja kwa moja dhidi wa Urusi dhidi ya Nato.
“Haya ni mawazo ya kipekee ya wale ambao ni dhaifu, wasio jiamini, licha ya ukweli kwamba wanamiliki silaha silaha ngingi zaidi ya zile tulizo nazo."
Zelensky baadaye aliuhutubia umati mkubwa wa waandamanaji wanaoendelea kuandamana katika mataifa ya Ulaya, akiwaambia waandamanaji : " Iwapo Ukraine haitanusurika, Ulaya yote haitanusurika.
"Kama Ukraine itaanguka, badi Ulaya nzima itaanguka."
Taarifa zaidi kuhusu mzozo wa Ukraine:
- Urusi na Ukraine: No-fly zone-Inacho maanisha na kwanini nchi za magharibi haziwezi kuchukua hatua
- Urusi na Ukraine: Nini kitatokea ikiwa Urusi itadhibiti maeneo yote ya Ukraine?
- Ukraine ilitoka vipi kuwa nchi ya tatu kwa nguvu za nyuklia duniani hadi hali yake ya sasa
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo, ambapo tutakuletea taarifa kuhusu mzozo wa Ukraine kadri zinavyojiri