Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Hali ya wasiwasi yazuka kuhusu Simba walioambukizwa Corona Afrika Kusini

Simba na Puma katika mbuga ya kuhifadhia wanyamaporinchini Afrika Kusini huenda wameambukizwa virusi vya corona kutoka kwa wamiliki wao, kulingana na utafiti uliofanywa na wanasayansi katika chuo Kikuu cha Pretoria.

Moja kwa moja

  1. Miguu yao imewekewa bima ya mamilioni ya dola

    Miguu ya mwanamitindo mwenye uraia wa Marekani na Ujerumani Heidi Klum imewekewa kwenye bima ya mamilioni ya dola, ili iwe na muonekano bora wakati wote.

    Mwanamitindo huyu mwenye umri wa miaka 48 alifichua kwa mara ya kwanza mwaka 2011 kwamba miguu yake imewekewa bima ya dola milioni 2.2.

    Garama ya miguu ya Heidi hivi karibuni imekuwa mada ya kujadiliwa naada ya kushiriki kwenye mazungumzo na kipindi cha Televisheni cha cha The Ellen DeGeneres wiki hii

    Katika mazungumzo hayo alisema mguu wake mmoja ni ‘’ghali kuliko mwingine’’

    Aliliambia jarida la People Magazine mwaka 2017 kwamba mguu wake mmoja unagarimiwa dola milioni 1.2 na mwingine dola milionina ndio maana hadi sasa watu wanamtamani akiwa na miaka 40 na ushee.

    "Kila mara nafurahia kuvaa sketi fupi sana( mimi skirt) ili kuoyesha miguu yang una bado ninaipenda ,"

    Watu wengine watano maarufu walioweka bimaya juu ya miguu yao

    Taylor Swift

    Muimbaji wa muziki wa pop amekuwa akivaa mavazi ya kuonyesha miguu yake baada ya kuweka bima ya dola milioni 40 kwa ajili ya miguu yake tu(milioni $20 kwa kila mguu), alisema hayo kabla ya kuanza safari yake ya kimuziki aliyoiita 1984 Tour mwaka 2015.

    Mariah Carey

    Miguu ya Mariah Carey imewekewa bima ya dola bilioni 1.

    Pia aliweka a bima ya sauti yake ya dola milioni 35, kwa ajili yatamasha la muziki la Sweet Sweet Fantasy Tour mwaka 2011.

    Cristiano Ronaldo

    Miguu ya mchezaji wa kimataifa wa soka wa Ureno na mshambuliaji wa Man United Striker, Cristiano Ronaldo pia hayuko nyuma katika kuiweka miguu yake katika bima ya bei kali.

    Real Madrid iliweka bima ya miguu yake ili kuizuwia kupata majeraha alipojiunga na klabu hiyo 2009. Waliiwekea bima miguu ya Ronaldo ya dola milioni 144.

    Lionel Messi

    Mchezaji wa kimataifa wa Argentina wa soka, Lionel Messi analipiwa bima ghali zaidi kuliko wote kwa ajili ya miguu yake. Mguu wa Messi wa kushoto umewekewa bima ya dola milioni 900.

    Tina Turner

    Ni maarufu sawa na miguu yake pamoja na uwepo wake kwenye jukwaa. Miguu ya huyo Mmarekani huyo Mzaliwa wa Uswiss imewekewa bima ya dola milioni 3.2

  2. Yasemwayo kumuhusu muamuzi mwanamke katika michuano ya AFCON

    Baada ya mchezo uliosimamiwa na muamuzi mwanamke Salma Mukansanga, Mkufunzi wa timu ya taifa ya Zimbabwe Norman Takanyariwa Mapeza alisema kuwa 'alifanya vyema'.

    Watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wa soka waliokuwa wakishuhudia michuano ya AFCON walikuwa na shauku ya kumuona Bi Mukansanga akiandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza muamuzi katika kombe hilo la Afrika, la wanaume.

    Katika uwanja wa soka wae Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde umati wa watu ulimpigia makofi na kushangilia wakati Bi Salma Mukansanga alipopiga kipenga cha kuanzisha mechi , na mechi ilipokamilika walisifu jinsi alivyousimia, anasema Mwandishi wa BBC Yves Bucyana aliyeshuhudia mtanange huyo kati ya Warriors ya Zimbabwena Syli National ya Guinea

    Katika mazungumzo na waandishi wa habari baada ya mechi, Mkufunzi waZimbabwe alisema Mukansanga alichezesha mchezo vyema

    "Nafikiri kwamba ni hatua kubwa kwa CAF kumpatia fursa mwanamke kuongoza mchezho huu."

    Shabiki mwingine aliandika kwenye ukurasa wa Twitter kuhusu kazi aliyoifanya Bi Mukansanga alisema "… Tulishuhudia maambuzi mengi yaliyoibua maswali katika wiki mbili zilizopita…lakini sio leo !"

  3. Fanta Bility: Maafisa wa Marekani washitakiwa kwa mauaji ya mtoto

    Waendesha mashitaka wamewashitaki maafisa watatu wa polisi kwa mauaji ya mtoto msichana mwenye umri wa miaka minane, na kuondoa kesi ya mauji dhidi ya vijana wawili ambao waliwashikilia.

    Maafisa hao walifyatua risasi kwenye garilililokuwa nje ya uwanja wa soka wa shule ya sekondari karibu na Philadelphia tarehe 27 Agosti 2021, baada ya kusikia milio ya risasi kwenye jengo la gorofa lililopo karibu.

    Polisi walifikiria kuwa washukiwa walikuwa ndani ya gari, lakini alikuwa ni mtoto Fanta Bility.

    Waendesha mashitaka walidai kuwa mkasa huo ulisababishwa vijana waliofyatuliana risasi.

  4. Miili iliyotupwa mtoni Kenya kwa miaka miwili – polisi yasema

    Polisi nchini Kenya sasa imesema kwamba matukio ya miili iliyooza ya watu inayopatikana kutoka katika mto magharibi mwa Kenya yamekuwa yakiendelea kwa miaka miwili.

    Hatahivyo msemaji wa polisi Bruno Shioso ameiambia BBC kuwa uchunguzi bado haujawafichua wale waliohusika wala sababu ya mauji hayo.

    Inaonekana kuna utofauti kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.

    Jumanne , wanaharakati walikwenda katika hospitali ya Yala Sub-County iliyopo takriban kilomita 40 (24 maili) Maskazini -magharibi mwa mji wa Kisimu, na walisema wameihesabu miili ishirini iliyoopolewa kutoka katika Mto Yala, ambayo haijadaiwa na yeyote.

    Huku hospitali hiyo hutunza miili ya watu wasiotambuliwa kwa siku 90, miili hiyo imeopolewa kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

    Waandishi wa habari wa BBC wameshuhudia miili zaidi katika mto huo.

    Lakini katika taarifa Jumatano, Polisi ilisema kuwa ilikuwa na kesi ya miili 19 pekee iliyoripotiwa kwa kipindi cha miaka miwili.

    Dereva ambaye anasema amekuwa akisaidia kuopoa maiti kwa miezi sita iliyopita anaamini kuwa huenda kukawa na miili mingi zaidi katika mto.

    Famia zilizowakosa wapendwa wao zimeanza kuripoti kwa polisi, ambayo baadhi imeharibika vibaya.

    Polisi inasema timu ya uchunguzi wa miili imetumwa Yala kuharakisha utambuzi wahanga.

    Wakenya wenye wasiwasi wanataka majibu, huku tuhuma kwamba mingi kati ya miili inayoopolewa kutoka kwenye mto ikionyesha dalili za kuteswa.

  5. Comoros yaiondoa Ghana Afcon

    Ghana ilipata pigo kubwa baada ya kuondolewa katika awamu ya kimakundi ya michuano ya kombe la A frika baada ya mabingwa hao mara nne kushindwa na Comoros.

    El Fardou Ben Nabouhane aliwaweka mbele wana visiwa haomapemana baadaye Ghana wakapata pigo wakati Andrew Ayew alipopokea kadi nyekundu ya moja kwa moja.

    Ahmed Mognialiongeza uongozi huo kwa kufunga goli la pili kabla ya The Black Stars kusawazisha na kuwa 2-2.

    Hatahivyo , Mogni alifunga goli la pili katika dakika ya 85 na kuwaondoa mabingwa hao kwa mara ya kwanza tangu 2006 katika awamu ya kimakundi.

    Matokeo hayo katika kundi C yatakuwa pigo kubwa katika historia ya kombe hilo huku Comoros ikifunga katika michuano hiyo kwa mara ya kwanzakabla ya kupata ushindi huo.

    Kikosi hicho ambacho kimeorodheshwa katika nafasi 132 duniani sasa kina nafasi ya kufikia awamu za muondoanokama miongoni mwa timu 4 bora zilizomaliza katika nafasi ya tatulicha ya kupoteza mechi zake mbili za kwanza.

  6. Hali ya wasiwasi yazuka kuhusu Simba walioambukizwa Corona Afrika Kusini

    Simba na Puma katika mbuga ya kuhifadhia wanyamaporinchini Afrika Kusini huenda wameambukizwa virusi vya corona kutoka kwa wamiliki wao, kulingana na utafiti uliofanywa na wanasayansi katika chuo Kikuu cha Pretoria.

    Wanasayansi hao wameonya kuhusu hatari ya kirusi kipya kutokea iwapo virusi hivyo vitasambaa katika hifadhi nyingine za Wanyama na kusambazwa tena kwa binadamu

    Utafiti huo ulifanywa baada ya Wanyama hao kuugua na dalili ambazo zinafanana na zile za virusi vya corona kwa binadamu ikiwemo tatizo la kupumua , kutokwa na kamasi na kikohozi kikavu.

    Vipimo vilivyofanyiwa Wanyama hao vilionesha kwamba wameambukizwa corona , watafiti hao walisema , huku data zikisema kwamba waliambukizwa ugonjwa huo na wafanyakazi waliokuwa wakiwahudumia.

    Watafiti hao waliongezea kwamba wahudumu wa hifadhi hizo za Wanyama walikuwa na virusi vya corona walivyosambaziana wakati huo lakini hawakuonesha dalili zozote.

    Wamependekeza hatua kama vile kuvalia barakoa wakati wanapowahudumia Wanyama hao.

    Utafiti huo umechapishwa katika jarida la virusi la Peer Review

  7. Mamlaka ya mpito Chad yawaachilia waasi 250

    Mamlaka ya mpito nchini Chad imewaachilia wafungwa 250 ambao ni wanachama wa makundi ya wapiganaji kama ilivyoahidi kuwaachilia huru chini ya mpango wa kutoa msamaha.

    Makundi ya waasi yamealikwa kujiunga katika mazungumzo ya kitaifa ya kuleta amani ambayo yanatarajiwa kuanza mwezi ujao.

    Mmoja ya walioachiliwa huru, Samedi Torde Tanel , aliwashukuru wale waliowezesha mpango huo na kusema kwamba alitumai wengine watafaidika na mpango kama huo katika siku za baadaye.

    Mpango huo wa kusameheulipendekezwa kufuatia kifo cha rais Idriss Deby katika vita Aprili iliopita.

    Baraza la kijeshi la mpito nchini Chad linaongozwa na mwanawe Deby Mahamat Idriss Deby.

  8. Hujambo. Kama ilivyoada tutakupasha kuhusu habari tofauti duniani