Nyama ya kasa yenye sumu yaua watu 7 Zanzibar huku wengine 24 wakilazwa

Kimsingi,kasa wa baharini huliwa na watu wengi katika ufukwe wa bahari lakini inasadikiwa kuwa ule ambao wakazi wa Msuka Taponi Wilaya ya Micheweni Pemba walikula ulikuwa na sumu.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho, majaaliwa.

  2. Nick Mwendwa: Rais wa Shirikisho la soka Kenya ashitakiwa makosa manne ya ufisadi

    Mwendwa

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Nick Mwendwa ameshitakiwa kwa wizi wa takriban dola 337,200.

    Rais wa shirikisho la soka la Kenya (FKF) Nick Mwendwa ameshitakiwa makosa manne ya wizi na idara ya upelelezi wa makosa ya jinai(DCI).

    Jumla ya kiasi cha fedha ambacho Mwenda na wenzake, ambao walikuwa mahakamani, wanashutumiwa kuchukua kutoka katika FKF ni zaidi ya shilingi milioni 38 za Kenya – ambazo ni takriban dola 337,200.

    Mwendwa, ambaye awali alikana kufanya kosa lolote, alifikishwa mahakamani mjini Nairobi Jumatatu baada ya kuwa jela wikendi baada ya kukamatwa tena Ijumaa.

    Atalala tena jela, huku akisubiri kesi ya kuomba rufaa iliyopangwa kufanyika Jumanne.

    Kulingana na nyaraka za polisi makosa hayo yalifanyika kati ya tarehe 4 machi na 31 mei mwaka huu.

  3. Mashabiki wa Wizkid wawapita walinzi wa O2 Arena na kuingia ndani ya onyesho lake

    G

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mashabiki wa Muimbaji wa Nigeria Wizkid wameingia kwa nguvu katika uwanja wa O2 Arena Jumapili usiku, na kutazama onyesho lake.

    Video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha msururu wa watu wakivuka uzio wa usalama na kuingia kwa nguvu ndani ya tamasha lake la muziki.

    Wizkid ambaye alishiriki katika densi ya Drake iliyovuma na kuwa namba moja -One Dance, anacheza kwa siku tatu mjini London.

    Msemaji wa O2 Arena alisema "kuvunja uzio wa usalama katika lango la arena kulitokea" na "mashabiki wengi waliokuwa kwenye msururu wa kuingia uwanjani waliweza kuingia ndani".

  4. Mwanamke aliyepanga kusafiri Saudia kwa ajili ya Umrah akamatwa akiwa na Cocaine Abuja

    THE WAY

    Chanzo cha picha, THE WAY

    Shirika la kupambana na madawa ya kulevya nchini Nigeria (NDLEA) limesema kuwa limemkamata mwanamke aliyekuwa njiani kuelekea nchini Saudia kwa ajili ya Umrah akiwa na mifuko 80 ya cocaine katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Abuja.

    Mshukiwa, huyo Adisa Afusat Olayinka, mzaliwa wa jimbo la Kwara, ambaye amekuwa akiishi eneo la Ibafo katika eneo la ​​Ogun, alikamatwa alipokuwa ndani ya Qatar Airways flight, imesema taarifa ya NDLEA, Jumatatu.

    Mwanamke huyo amesema kuwa alianza kujihusisha na usafirishaji wa mihadarati baada ya kukutana na mwanamke mwingine katika Umrah katika mwaka 2019.

    Hatahivyo, kulingana na taarifa, mwanamke huyo alisema alikuwa anataka kuchangisha Naira milioni 7 ili kuweza kutibiwa ili apate mtoto baada ya kuolewa kwa miaka 28 bila mtoto.

  5. Wahudumu wasimamishwa kazi baada ya kuuzwa kwa panzi(Nsenene) ndani ya ndege ya Uganda

    Shirika la taifa la ndege la Uganda limepiga marufuku ya mauzo ya chakula maarufu cha senene (panzi) ndani ya ndege, tukio lililotokea mwishoni mwa juma.

    Uganda Airlines hilo lilisema mauzo ya chakula hicho, kinachofahamika kwa jina maarufu la Nsenene, ni kinyume cha ‘’maadili ya kampuni hiyo ya taifa".

    Ndege hiyo ilisema kuwa tukio hilo liliwawaonyesha baadhi katika hali ya "ukosefu wa usimamizi wa masoko masoko katika safari yao ya ndege ".

    Vyombo vya habari vimeripoti kuwa baadhi ya wafanyakazi wa ndge hiyo wamesimamishwa kazi kutokana na tukio hilo.

    Video ilisambazwa kwenye mtandao ikionyesha mwanaume mmoja akiuza Nsenene:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Ndege hiyo imesema ilitambua kwamba msisimuko wa furaha iliyokuwa ndani ya ndege ilikuwa ni kwasababu nsenene sio wengi katika msimu huu na " inaangalia uwezekano wa kuongeza chakula hicho katika menu inayotoa iwapo ombi litatolewa".

    "Hatua hii inaboreshautangazaji wa utalii na maisha ya watu katika soko la panzi siku zijazo," ilisema ndege hiyo.

  6. Italy yampatia hifadhi msichana mwenye macho ya kipekee wa Afghanstan

    Msichana

    Chanzo cha picha, DPA

    Maelezo ya picha, Mpiga picha Steve McCurry alimpiga picha Sherbat Gul alipokuwa katika kambi ya wakimbizi

    Msichana mwenye macho ya kijani iliyekuwa ishara ya madhila ya Afghanstan yanayoendelea, amewasili nchini Italia na amepewa hifadhi na serikali ya nchi hiyo.

    Msichana huyo alipata umaarufu wa kimataifa wakati chombo maarufu cha habari cha kimataifa - National Geographic kilipochapisha picha yake kwenye jarida lake mwaka huu . Msichana huyo kwa jina Sherbat Gul alikuwa na umri wa miaka 9 wakati huo.

    Ofisi ya Waziri mkuu wa Italia Mario Draghi Alhamisi ilithibitisha kuwa msichana huyo amewasili katika mji mkuu Roma.

    Mpiga picha wa msichana huyo aliyeitwa ua la sherbet alichapisha picha yake mwaka 2006, aliyopigwa akiwa mtoto na Steve McCurry, mpiga picha wa jarida la -National Geographic , na kumpatia umaarufu wa kimataifa na kumfanya kuwa mmoja wa wakimbizi maarufu zaidi wa Afghanistan.

  7. Mahakama ya Botswana yaidhinisha uamuzi wa kutowabagua wapenzi wa jinsia moja

    Wapenzi wa jinsia moja

    Chanzo cha picha, AFP

    Mahakama ya rufaa ya Botswana imeidhinisha uamuzi wa mwaka 2019 wa kutowabagua wapenzi wa jinsia moja nchini humo.

    Majaji watano wa mahakama hiyo waliiidhinisha kwa kauli moja kwamba kuwabagua watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kulikiuka haki za kikatiba za wapenzi wa jinsia moja wa kike, wakiume, wenye jinsia mbili na waliobadili jinsia zao, (LGBT)

    Mwaka 2019, mahakama ya juu nchini humo ilipinga kuwa sheria zilizoweka zinazoidhinisha hadi kifungo cha miaka saba kwa wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, ikizitaja kuwa kinyuma cha Katiba,

    Imesema pia kuwa utu wa binadamu unadhurika wakati makundi ya raia walio wachache yanapoachwa nyuma.

    Taifa lilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo, likidai kanuni ya adhabu ni zaidi ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja. Ilisema pia kwamba raia walio wengi hawakuafiki uamuazi wa mwaka 2019.

    Uamuzi wa Jumatatu unaondoa vipengele viwili vya sheria ya adhabu vilivyokiuka sheria kuhus mapenzi ya jinsia moja.

    "Vipengele hivyo viliondoa maana yake, na kuegemea utashi wa idara za utekelezi wa sheria na hivyo kuwafanya wawe watu wa kuingilia maisha ya kibinafsi ya raia ," alisema jaji wa mahakama ya rufaa, Ian Kirby, aliyeongoza mchakato wa utoaji wa hukumu hiyo.

    Sheria zinazopinga mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja zipo katika nchi nyingi kati ya nchi 54 za Afrika.

  8. Ndege ya kipekee ya vita yawauwa wapiganaji 26 Nigeria

    Ndege

    Chanzo cha picha, NIgeria army

    Ndege mpya isiyo ya kawaida ya jeshi la Nigeria aina ya Super Tucano imewauwa wapiganaji 26 wakikundi cha ISWAP na kuangamiza kabisa vifaru vyao vya kijeshi katika eneo la Borno nchini humo.

    Vyombo vya habari vya PRNigeria viliripoti kwamba waasi hao walikuwa wameingia katika mji huo huku wakiwa wamejihami kwa vifaru na kufanya mashambulizi, kisaha ndege hiyo ya kijeshi ikawasili na kumimina silaha kwenye vifau hivyo.

    PRNIGERIA

    Chanzo cha picha, PRNIGERIA

    Jeshi la Nigeria linasema kuwa limekamata silaha kadhaa wakati lilipofanya uvamizi wa anga na ardhini dhidi ya wanamgambo hao

    PRNigeria vinasema afisa wa ujasusi wa jeshi amesema miili 26 ya wanamgambo hao imepatikana baada ya shambulio la anga.

  9. Oscar Pistorius kukutana na wazazi wa mwathiriwa Reeva Steenkamp

    Mkutano huo ni sehemu ya mchakato unaweza kupelekea kuachiliwa kwake hatimaye

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Mkutano huo ni sehemu ya mchakato unaweza kupelekea kuachiliwa kwake hatimaye

    Oscar Pistorius amehamishiwa gereza tofauti kukutana na familia ya Reeva Steenkamp, mwanamke aliyemuua mwaka 2013. Idara ya magereza ya Afrika Kusini imethibitisha taarifa hiyp, ikisema ni sehemu ya mchakato wa ukarabati unaofanyika kabla ya mwanariadha huyo wa zamani wa Olimpiki ya walemavu kuzingatiwa kwa msamaha.

    Idara hiyo pia imethibitisha kwamba alihamishwa hadi katika gereza katika mji wa bandari wa Gqeberha, uliyopo Cape ya Mashariki, ili kukutana na wazazi wa Reeva Steenkamp, ​​wanaoishi karibu.

    Haijulikani ikiwa mkutano huo - au mikutano - imefanyika.

    Mapema mwaka jamaa ya Steenkamps walikiri kupokea barua kutoka kwa mwanamume aliyemuua binti yao. Lakini walidokeza kwamba majuto yake yalikuwa ya kujitakia'

    Maafisa wa Afrika Kusini hawajaonyesha dalili ya muda gani mchakato huo - unaojulikana hapa kama mazungumzo ya mwathirika-mkosaji - utaendelea. Lakini itazingatiwa wakati bodi ya msamaha itakapokutana ili kuamua ikiwa Pistorius aachiliwe kutoka gerezani.

    Reeva Steenkamp alipigwa risasi nne akiwa amejificha nyuma ya mlango wa bafuni mnamo Februari 2013.

    Awali Jaji alimpata Pistorius na hatia ya kuua bila kukusudia, ambayo ilibadilishwa na kuwa mauaji, baada ya kukata rufaa.

    Mwanariadha huyo ambaye miguu yake yote miwili ilikatwa akiwa mtoto mchanga, alisema aliamini alikuwa akimpiga risasi mvamizi.

  10. Israeli Kuruhusu Wayahudi 3,000 wa Ethiopia Kuhamia nchini humo

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Serikali ya Israel siku ya Jumapili iliidhinisha uhamiaji wa maelfu ya Wayahudi kutoka Ethiopia inayokumbwa na vita, ambao baadhi yao wamesubiri kwa miongo kadhaa kuungana na jamaa zao nchini Israel.

    Uamuzi huo ulichukua hatua kuelekea kusuluhisha suala ambalo kwa muda mrefu limetatiza uhusiano wa serikali na jamii ya Ethiopia nchini humo

    Wayahudi wa Ethiopia wapatao 140,000 wanaishi Israeli. Viongozi wa jamii wanakadiria kuwa takriban wengine 6,000 wamesalia nyuma nchini Ethiopia.

    Ingawa familia hizo ni za asili ya Kiyahudi na wengi wao ni Wayahudi, Israeli haiwaoni kuwa Wayahudi chini ya sheria za kidini. Badala yake, wamekuwa wakipigania kuingia nchini chini ya mpango wa kuunganisha familia ambao unahitaji idhini maalum ya serikali.

    Wanaharakati wa jamii wameishutumu serikali kwa kujikokota katika kutekeleza uamuzi wa 2015 wa kuwaleta Waethiopia wote waliosalia wa ukoo wa Kiyahudi nchini Israeli ndani ya miaka mitano.

  11. Nyama ya kasa yenye sumu yaua watu 7 Zanzibar huku wengine 24 wakilazwa

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Watu saba wamefariki dunia na wengine 24 wakipigania maisha yao katika hospitali moja kisiwani Pemba baada ya kula nyama ya kasa.

    Kimsingi,kasa wa baharini huliwa na watu wengi katika ufukwe wa bahari lakini inasadikiwa kuwa ule ambao wakazi wa Msuka Taponi Wilaya ya Micheweni Pemba walikula ulikuwa na sumu.

    Kamanda wa Polisi Pemba Kaskazini, Juma Sadi amepiga marufuku ulaji wa kasa baada ya kubainika kuwa nyama yake ina sumu,The Citizen imeripoti.

    Alisema watatu walikufa Ijumaa , wawili walikufa Jumamosi na vifo vingine viwili vilithibitishwa Jumapili,Novemba 28.

    Haikuwa wazi ikiwa wote saba walikuwa wa familia moja au vinginevyo.

    Katika ujumbe wake wa Twitter, Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi alituma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na kuwataka wawe na subra.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  12. Madhya Pradesh: Mume amjengea mkewe nyumba kama ya Taj Mahal

    th

    Chanzo cha picha, ANAND PRAKASH CHOUKSEY

    Mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 52 nchini India amejenga mfano mdogo wa Taj Mahal kuwa nyumba ya mke wake wa miaka 27.

    Anand Prakash Chouksey amejenga "mnara wa upendo" wake - nyumba ya vyumba vinne inayofanana na ajabu ya usanifu jwa jengola Taj mahal katika jiji la Burhanpur katikati mwa jimbo la India la Madhya Pradesh.

    "Ilikuwa zawadi kwa mke wangu lakini pia kwa mji na watu wake," Bw Chouksey aliambia BBC.

    Imewekwa ndani kabisa ya mali ya Bw Chouksey - baadhi ya ekari 40-50 za ardhi, ikiwa ni pamoja na hospitali - nyumba hiyo imekuwa ikivutia wageni wengi.

    th

    Chanzo cha picha, ANAND PRAKASH CHOUKSEY

    Watu hutembea kwenye nyasi na kupiga picha, alisema. "Watu wengi pia wameanza kupiga picha zao za kabla ya harusi hapa," Bw Chouksey aliongeza.

    "Siwazuii kwa sababu katika mji wetu, sisi ni jamii iliyoshikamana kwa karibu ambapo kila mtu anamjua mwingine. Kwa hiyo, nyumba yangu iko wazi kwa wote."

    Bw Chouksey alisema kuwa sio wageni wote wanaoruhusiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo kwa sababu " ni nyumba yetu na tunaishi humo".

    Lakini wakati mwingine, familia huwafurahisha wageni wake wanaokuja na kustaajabia mambo ya ndani ya nyumba hiyo yenye kupendeza - michoro ya maua ambayo hupamba kuta za marumaru na sakafu, na madirisha yake ya kimiani.

    th

    Chanzo cha picha, ANAND PRAKASH CHOUKSEY

    Nyumba hiyo ina vyumba viwili vikuu vya kulala ambavyo viko kwenye sakafu mbili tofauti. Pia ina maktaba na chumba cha kutafakari. Chumba cha kuchora huangazia nguzo za marumaru, ngazi zilizopinda na dari iliyopambwa.

  13. Takriban watu 22 wauawa katika shambulizi katika kambi ya DR Congo

    th

    Chanzo cha picha, AFP

    Takriban watu 22 wameuawa katika shambulizi kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika jimbo la Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Shambulio hilo limelaumiwa kwa kundi la Cooperative for the Development of the Congo (Codeco) ambalo linasemekana kufyatua risasi kwenye kambi hiyo.

    Watu 20 walizikwa mara moja katika makaburi mawili ya kawaida, huku wengine wawili wakizikwa baadaye, shirika la habari la AFP lilimnukuu afisa wa Msalaba Mwekundu akisema.

    Shambulio kwenye kambi hiyo hiyo wiki iliyopita liliua watu 29.

    Ituri na jimbo jirani la Kivu Kaskazini ziliwekwa chini ya hali ya kuzingirwa tarehe 7 Mei - kwa mamlaka kukabiliana na ukosefu wa usalama katika eneo lililosababishwa na makundi yenye silaha ikiwa ni pamoja na Codeco na Allied Democratic Forces (ADF).

    Kama sehemu ya kuzingirwa, maafisa wa kijeshi walichukua nafasi za maafisa wa kiraia waliokuwa wakisimamia utawala wa eneo hilo.

  14. Rwanda yasitisha safari za ndege kuelekea mataifa ya kusini mwa Afrika

    Serikali ya Rwanda imetangaza hatua mpya ambazo ni pamoja na kusimamisha safari za ndege kwenda na kutoka nchi za kusini mwa Afrika.

    Abiria wote wanaowasili lazima wathibitishe kutokuwa na virusi vya corona na wafanyiwe vipimo vya marudio wanapowasili .

    Karantini ya siku saba pia imerejeshwa kwa wasafiri wanaotoka nchi zilizoathiriwa hivi karibuni na mawimbi mapya.

    Wale wote wanaohudhuria mikusanyiko kama vile harusi na mazishi lazima wapate chanjo kamili.

    Kufuatia maagizo ya serikali kuhusu usafiri, shirika la ndege la Rwandair limesitisha huduma kwenda Afrika Kusini, Zimbabwe na Zambia:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Rwanda ndiyo nchi ya hivi punde zaidi kuweka marufuku ya kusafiri kwenda Afrika Kusini baada ya aina mpya ya virusi vya corona Omicron kugunduliwa nchini humo.

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema "amesikitishwa sana" na marufuku dhidi ya nchi yake na mataifa jirani ambapo kirusi hicho kimegunduliwa.

  15. Mbunge New Zealand Julie Anne Genter aendesha baiskeli kwenda hospitali kujifungua

    TH

    Chanzo cha picha, JULIE ANNE GENTER FACEBOOK

    Mbunge wa New Zealand aliendesha baiskeli hadi hospitalini akiwa katika uchungu wa kujifungua siku ya Jumapili na kujifungua baada ya saa moja tu.

    "Kwa kweli sikuwa nimepanga kuendesha baiskeli katika leba, lakini iliishia kutokea," Julie Anne Genter alisema kwenye Facebook baadaye.

    Msemaji huyo wa chama cha Green Party katika masuala ya usafiri hakuwa akifanya hivyo kwa mara ya kwanza - alikuwa waziri miaka mitatu iliyopita aliposafiri kwa njia hiyo.

    Bi Genter, mwenye umri wa miaka 41, ni mtetezi maarufu na mzungumzaji wa uendeshaji baiskeli.

    Mwanasiasa huyo mzaliwa wa Marekani alisema mikazo yake "haikuwa mbaya" wakati yeye na mumewe walipoamua kuendesha baiskeli.

    Alichapisha picha zao wakiwa kwenye maegesho ya magari ya hospitali.

  16. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hivi leo Jumatatu tarehe 29 Novemba 2021