Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mashabiki washangilia kuungana tena kwa wasanii wa P-Square Nigeria

Wawili hao - wanaojumuisha mapacha Peter na Paul Okoye - walitofautiana miaka kadhaa iliyopita kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia, na kutengana mnamo 2017.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Mtoto aokolewa na paka Mumbai

    Mtoto wa kike wa siku tano, ambaye aliokolewa kutoka kwenye shimo la maji taka alimokuwa ametupwa jijini Mumbai, India anaendelea kupata nafuu katika hospitali ya eneo hilo.

    Madaktari katika hospitali ya Rajawadi wameambia BBC kuwa "anaendelea vyema" na kwamba afya yake inafuatiliwa kwa karibu.

    Polisi wanasema wakaazi walimpata mtoto huyo baada ya kundi la paka waliokusanyika kando ya barabara na kuanza kuzua fujo - na kupiga kelele kwa sauti ya juu.

    Maafisa wanachunguza jinsi alivyoishia kwenye bomba hilo.

    Polisi hawajatoa tamko lolote kuhusiana na kile kilochochangia tukio hilo lakini matukio mengine kama hayo siku za nyuma yamehusishwa na suala la watoto wa kiume kupendelewa zaii kuliko wa kike nchini India.

    Wanawake mara nyingi wanabaguliwa kijamii na wasichana wanaonekana kama mzigo wa kifedha, haswa miongoni mwa jamii masikini.

    Uwiano wa kijinsia wa nchi ni mojawapo ya hali mbaya zaidi duniani. Na ingawa mimba zinazokadiriwa kuwa za watoto wa kike hutolewa kwa usaidizi wa kliniki haramu, visa vya watoto wa hao kuuawa au kuachwa baada ya kuzaliwa si jambo la kushangaza.

    Katika tukio la hivi punde zaidi, mtoto huyo aliokolewa na timu ya polisi inayoongozwa na wanawake kutoka kitongoji cha Mumbai siku ya Jumapili.

    Soma zaidi:

  3. Edouard Mendy alalamikia matumizi ya picha yake katika taarifa ya Benjamin Mendy

    Mlinda mlango wa Chelsea Edouard Mendy amevikosoa vyombo vya habari kwa kutumia kimakosa picha yake katika taarifa kuhusu Benjamin Mendy wa Manchester City.

    Beki wa City na Ufaransa Benjamin Mendy ameshtakiwa kwa makosa sita ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono, na anaendelea kuzuiliwa.

    Picha za Edouard Mendy na binamu yake, Ferland Mendy wa Real Madrid, zimetumiwa kuangazia taarifa hiyo.

    "Inasikitisha kufikia mwaka 2021, nchini Ufaransa na Uingereza, kwa wengine, watu weusi hawana majina wala sura tofauti," mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal aliandika kwenye Instagram.

    Soma zaidi:

    • Beki wa Manchester City Benjamin Mendy ashitakiwa kwa ubakaji
    • Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 18.11.2021: Haaland, Mbappe, De Vrij, Brozovic, Strakosha, Pogba, Olmo
  4. Kenya yakabiliwa na uhaba wa mipira ya kondomu

    Vituo kadhaa vya afya vya umma, hoteli na mikahawa nchini Kenya vinakabiliwa na uhaba wa kondomu kutokana na mvutano wa ushuru kati ya wafadhili na serikali ya Kenya, Gazeti la Daily Nation linaripoti.

    Mpango ambao hutoa kondomu za bure, sehemu muhimu ya kampeni ya Kenya ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwa( VVU), inategemea kabisa usaidizi wa wafadhili kununua bidhaa hizo.

    Serikali ya Kenya husambaza bure karibu mipira milioni 180 kila mwaka kupitia mpango ambao unaofadhiliwa na Hazina ya Kimataifa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA)

    Hata hivyo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopiti, wagonjwa walio na virusi vya HIV katika makundi tofauti yamekuwa yakilalamikia uhaba wa kondomu nchini.

    Mkurugenzi wa wakfu unaoshughulikia masuala ya UKIMWI (AIDS Healthcare Foundation) amenukuliwa na Gazeti la Nation akisema mwaka huu serikali haikununua kondomu na shehena inayosambazwa na wakfu huo kwa sasa iliwasili nchini 2019.

  5. Blinken alaani ukandamizaji dhidi ya wanaharakati wa Sudan

    Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Anthony Blinken, amelaani ghasia dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia nchini Sudan na kusisitiza wito wa kutaka waziri mkuu aliyeondolewa madarakani Abdalla Hamdok arejeshwe kazini.

    Siku ya Jumatano watu 15 waliuawa kwa kupigwa risasi na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya wakati vikosi vya usalama vilipofyatua risasi dhidi ya umati mkubwa wa watu waliokuwa wakiandamana kupinga mapinduzi ya mwezi uliopita.

    Katika mahojiano na BBC Bw Blinken, ambaye yuko katika ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu aingie madarakani, alitaka wafungwa wa kisiasa waachiliwe na kusema viongozi wa kijeshi wanahitaji kusikiliza vilio vya watu wa Sudan.

    Mazishi ya waathiriwa yanatarajiwa kufanyika saa chache zijazo.

  6. Tafiti zifanyike kubaini kwanini waathirika wa saratani kanda ya ziwa wengi ni wanawake-Rais Samia

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amehimiza kufanyika kwa tafiti kubaini ni kwanini ugonjwa wa Saratani unaathiri wanawake zaidi katika eneo la kanda ya ziwa.

    Hayo ameyasema leo alipokuwa amehudhuria sherehe za kumbukumbu ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa hospitali ya Rufaa ya kanda hiyo Bugando iliyoko jijini Mwanza.

    ''Maelekezo ya mtangulizi wangu ni kwamba Wizara ya afya kuhakikisha wanashirikiana nanyi kwenye kufanya tafiti na kubaini sababu za kuwa na kiwango kikubwa cha saratani katika kanda ya ziwa.''

    Amesema ni jambo la kusikitisha kuona idadi ya wagonjwa wa saratani imeendelea kukua ndani ya kanda ya ziwa.

    Rais Samia amesema kwa mfano mwaka 2019, hospitali ya Bugando ilipokea wagonjwa wapya 1200 waliohamasika kupima na kwa mwaka 2021 hospitali hiyo inaweza kufikisha wagonjwa 1500.

    ''Hii ni idadi kubwa sana kwa magonjwa kama haya.'' Ameeleza pia umuhimu wa tafiti ni kujikita zaidi kwenye kubaini chanzo cha saratani hizo na kwanini kanda ya ziwa inaongoza kwa waathirika wengi wa saratani ambapo wanawake ndio waathirika wakubwa wakiathiriwa na saratani ya kizazi na saratani ya matiti.

    ''Kuna sababu Kadhaa zinatolewa, wengine tunasema kwamba labda ni uchafuzi wa mazingira kutokana na uchimbaji wa kutumia Zebaki ambayo watu hufanya uchimbaji kwenye mito, maji yakisambaa watu hunywa na kueneza maradhi ya saratani kwa watu'',alisema Rais Samia.

  7. Mashabiki washangilia kuungana tena kwa bendi ya P-Square Nigeria

    Mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii alisema kwenye Instagram: "Tafadhali acha upendo na upatanisho huu udumu milele. Amina."

    "Nimejawa na hisia. Kama pacha siwezi kufikiria kutokuwa na uhusiano mzuri na pacha wangu kwa muda mrefu," mwingine alisema.

    Pia walifanya ushirikiano wa kimziki na wanamuziki wengine kama vile Diamond Platinumz wa Tanzania na nyota wa Marekani Akon.

    Walisaini lebo ya Akon ya muziki -Konvict katika mwaka 2011 na mwaka mmoja baadaye wakapata mkataba wa kusambaza muziki wao na kampuni ya Universal Music Group.

    Pamoja na kutajwa kama kikundi cha msanii wa MTV Afrika wa muongo mwaka 2015 walishinda pia tuzo ya kikundi bora mara tatu.

    Mashabiki wa kundi maarufu la muziki la P-Square nchini Nigeria wanaelezea kufurahishwa kwao na taaarifa kwamba ndugu hao walianza kuimba pamoja karibu miongo miwili na kisha kutengana wamepatana.

    Wawili hao - wanaojumuisha mapacha Peter na Paul Okoye - walitofautiana miaka kadhaa iliyopita kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia, na bendi hiyo ikatengana mnamo 2017.

    Sababu hasa ya kutengena kwao haikuwahi kutangazwa wazi kwa umma hata hivyo majaribio ya awali ya kuwaleta pamoja, yalihusisha wanasiasa, viongozi wa kidini na watu wengine mashuhuri hayakufanikiwa.

    Jumbe za mitandao mbali mbali ya kijamii ambazo walituma tangu watengane kimuziki ziliashiaria kuwa ugomvi wao ulihusisha wake zao na kaka yao mkubwa, ambaye pia alikuwa meneja wao.

    Lakini katika ujumbe wa Instagram Peter na Paul walisema "vichwa 2 ni bora kuliko 1".

    Tayari kuna taarifa kuwa wawili hao huenda walimaliza mzozo wao baada ya kila mmoja kumfuata mwingine kwenye mtadao wa Instagram. Halafu video ya wawili hao wakikumbatiana ikasambaa sa a kwenye mitandao ya kijamii Jumatano.

    Baada ya kutengana kila mmoja wao alishuka kimziki kwani iwe Mr. P (Peter) na Rudeboy (Paul) hakuna aliyefikia kiwango cha mafanikio waliyoyapata walipokuwa pamoja kama -P-Square.

    Wakiwa wawiliwalitawala katika muziki wa Nigeria kwa miaka na walikuwa ni moja ya makundi ya kuwanza kuuza miziki ya Afrobeats katika maeneo mengine ya bara

    Waliuza matamasha yao ya maonyesho ya moja kwa moja yaliyotawaliwa na densi ya ukakamavu iliyokuwa na miondoko ya break-dance

    Wawili hao - wanaojumuisha mapacha Peter na Paul Okoye - walitofautiana miaka kadhaa iliyopita kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia, na bendi hiyo ikatengana mnamo 2017.

    Ndugu hao, ambao walitimiza miaka 40 siku ya Alhamisi, walitawala tasnia ya muziki ya Nigeria kwa miaka mingi na muziki wao ulivuma chini humo na kwingineko.

    Hivi majuzi walionekana wakikumbatiana katika video iliyosambazwa sana mitandaini.

    Pulse Nigeria imeshiriki video hiyo kwenye Twitter.

    Mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii alisema kwenye Instagram: "Tafadhali acha upendo na upatanisho huu udumu milele. Amina."

    "Nimejawa na hisia. Kama pacha siwezi kufikiria kutokuwa na uhusiano mzuri na pacha wangu kwa muda mrefu," mwingine alisema.

    • Peter wa P-Square aomba radhi mashabiki
  8. Sheria mpya ya Kenya kuruhusu ujumuishaji wa wakimbizi kwa urahisi

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametia saini kuwa sheria mswada mpya wa wakimbizi unaowaruhusu wanaotafuta hifadhi kupata elimu kwa urahisi, na fursa za kujumuika na kujipatia riziki.

    Inakuja miezi sita tu kabla ya kusitishwa kwa mpango na mamlaka ya kambi mbili zinazohifadhi wakimbizi zaidi ya nusu milioni.

    Mamlaka zinasema kuwa kambi hizo zimetumika ngome za magaidi wanaolaumiwa kwa kuhusika na baadhi ya mashambulizi mabaya zaidi katika ardhi ya Kenya.

    Kenya imekuwa katika mapambano ya muda mrefu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi kuhusu mipango ya kufunga kambi za wakimbizi za Kakuma na Daadab ambazo kwa miongo kadhaa, zimekuwa makazi ya wakimbizi nusu milioni hasa kutoka Somalia na Sudan Kusini.

    Mnamo Septemba, rais alikataa mswada wa awali ambao ulitaka kulazimisha serikali kutoa makazi na huduma za kijamii kwa wakimbizi katika vituo maalum vya usafirishaji.

  9. Mkuu wa idara ya Jinai Kenya George Kinoti ahukumiwa kifungo cha miezi 4 jela kwa kukaidi mahakama

    Mkurugenzi wa idara DCI nchini Kenya George Kinoti amehukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa kukosa kutii agizo la mahakama lililomtaka kuachilia bunduki za mfanyabiashara Jimi Wanjigi.

    Kinoti anatakiwa kujisalimisha gerezani ndani ya siku saba la sivyo Inspekta mkuu wa Polisi kutekeleza hati ya kumkamata.

    Jaji wa Mahakama ya Kuu Anthony Mrima mnamo Januari 2019 aliamuru DCI, Inspekta mkuu wa Polisi na Mkurugenzi wa mashtaka ya umma kurejesha bunduki na risasi zote zilizochukuliwa kutoka kwa makazi ya Wanjigi mnamo 2017.

    Silaha zinazotafutwa ni bastola moja ya ya Smith and Wesson, bastola moja ya Glock, bunduki moja kati ya zingine.

    Mrima katika kutoa agizo hilo alisema Serikali ilikosea kuchukua bunduki za Wanjigi ilhali bado ana leseni halali.

  10. Merkel: Ujerumani inakabiliwa na maambukizi makubwa ya Covid-19

    Ujerumani iko katika mtego wa wimbi "kubwa" la nne la Covid, Kansela Angela Merkel amesema katika mkesha wa mkutano wa mgogoro na viongozi wa kanda.

    Maambukizi ya kila siku yalifikia 52,826 rekodi mpya ya Ujerumani ya siku ya Jumatano wakati serikali za Ulaya zikijizatiti kudhibiiti maambukizi ya virusi katika bara hilo.

    Ingawa jumla ya vifo vya Ujerumani ni chini sana kuliko ile ya Uingereza, vifo 294 vimerekodiwa ndani ya masaa 24 na Bi Merkel alizungumza juu ya dharura na vitanda vya wagonjwa mahututi vinavyojaa hospitalini.

    Uingereza iliripoti vifo vingine 201 ndani ya siku 28 za kupimwa kuwa na Covid mnamo Jumatano, na maambukizo zaidi 38,263.

    Ubelgiji ilitangaza msururu wa hatua katika jahudi ya kuzuia amri ya kutotoka nje.

    "Ishara zote za ni nyekundu," Waziri Mkuu Alexander De Croo alisema, alipowasihi watu kupunguza mawasiliano ya kibinafsi.

    "Ramani ya Ulaya inageuka nyekundu kwa kasi, na sisi hatujasazwa."

    Watoto wa kuanzia umri wa miaka 10 nchini Ubelgiji watalazimika kuvaa barakoa badala ya umri wa sasa wa miaka 12.

    Kufanya kazi nyumbani itakuwa lazima kwa siku nne kwa wiki kuanzia Jumamosi.

    Pasi zinazojulikana kama Tiketi za Covid Safe zitahitajika katika kumbi za sinema, na makumbusho.

    Ujerumani na Austria zimeripoti foleni katika vituo vya chanjo, lakini zina viwango vya chini zaidi vya watu waliopokea chanjo eneo la Ulaya Magharibi.

  11. Peng Shuai: Shauku yaibuka kuhusu barua pepe kutoka kwa nyota wa tenisi wa China

    Mkuu wa Chama cha Tenisi cha Wanawake (WTA) ametilia shaka barua pepe iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya China inayohusishwa na mchezaji wa tenisi Peng Shuai.

    Hakuna aliyesikia lolote kutoka kwa nyota huyo wa tenisi tangu alipotoa madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya China wiki mbili zilizopita.

    Katika barua pepe hiyo, inadaiwa Bi Peng anasema madai hayo "si ya kweli".

    Steve Simon, mwenyekiti wa WTA, alisema ujumbe huo "unaibua tu" wasiwasi wake kuhusu usalama wa Bi Peng.

    "Nina wakati mgumu kuamini kwamba Peng Shuai kweli aliandika barua pepe tuliyopokea au anaamini kile kinachohusishwa naye," alisema katika taarifa.

    Imeandikwa kwa sauti yake na kuchapishwa na shirika la habari la serikali CGTN, barua pepe hiyo inadai kwamba hajakosekana au hayuko salama, na kuongeza: "Nimekuwa nikipumzika tu nyumbani na kila kitu kiko sawa."

    BBC imeshindwa kuthibitisha barua pepe hiyo.

  12. Wakenya waguswa na sheria mpya inayolenga wapenzi wa siri

    Wakenya mitandaoni wamekaribisha kutiwa saini kwa sheria mpya inayowazuia wapenzi wa siri kurithi mali endapo wapenzi wao wataaga dunia.

    Mswada huo unaofadhiliwa na Mbunge Peter Kaluma, unaruhusu tu watoto wanaolelewa na marehemu kupata sehemu ya mali lakini inawafungia nje wapenzi ambao hawajafunga ndoa kihalali.

    Bw Kaluma alikaribisha kutiwa saini kwa mswada huo kuwa sheria, akisema kuwa marafiki wa kike ambao walikuwa wakisubiri kufaidika na mali ya familia sasa "wamezuiliwa".

    Baadhi ya Wakenya mtandaoni walisherehekea kutiwa saini kwa sheria hiyo huku mtumaji huyu wa Twitter akisema hakutakuwa na mitego tena:

    Akinyi Abong'o aliandika hakutakuwa tena na watu watakaopata utajiri wa kudandia:

  13. Ripoti yalaumu makundi ya wahifadhi Kenya kwa mizozo

    Ripoti mpya ya taasisi ya sera yenye makao yake makuu nchini Marekani inasema kuwa baadhi ya mashirika ya hifadhi nchini Kenya yanafukuza jamii kutoka katika ardhi zao na kuchochea migogoro ya kikabila kaskazini mwa nchi hiyo.

    Mwaka huu, ghasia za kijamii zinazohusisha wafugaji katika hifadhi ya wanyama zimesababisha vifo vya makumi ya watu na mamia kufurushwa makwao.

    Taasisi ya Oakland inashutumu Northern Rangelands Trust (NRT) kwa kunyang'anya jamii ardhi kwa jkisingizio cha uhifadhi, huku ikidai kuwa baadhi ya vitengo vyake vya mgambo wenye silaha vimehusika katika ukiukaji wa haki za binadamu.

    Taasisi hiyo imepinga madai hayo ikisema ripoti hiyo inatokana na imani potofu.

    NRT ni shirika tanzu la hifadhi 43 za jamii kaskazini mwa Kenya.

    Hifadhi hizi zinajieleza kuwa ni maeneo ya hifadhi yanayoendeshwa ndani kwa ajili ya ulinzi wa wanyamapori, na uhifadhi wa maeneo ya malisho na vyanzo vya maji, katika eneo la kilomita 42,000 mraba.

  14. Kampuni iliyosafirisha taka za kinyesi cha mbwa na nepi hadi China ili kuchakata yapigwa faini

    Kampuni ya uchakataji wa bidhaa kutoka Uingereza-Scotland ilitozwa faini ya £20,000 kwa kusafirisha tani 1,300 za taka za nyumbani hadi China kinyume cha sheria.

    Psycha Nature ilisafirisha nje kiasi kikubwa cha taka kama vile nepi zinazoweza kutupwa, samadi ya mbwa, na makopo ya vinywaji kutoka kiwanda chake cha North Lanarkhire kama "taka za karatasi" kwa karatasi iliyosindikwa.

    Kulingana na Wakala wa Ulinzi wa Mazingira wa Scotland (SEPA), kesi hiyo ni mojawapo ya usafirishaji haramu mkubwa wa taka nchini Scotland.

    Mkurugenzi wa SEPA Terry Eihan anadokeza kuwa ni shughuli mbaya zaidi haramu ambayo nimewahi kuona. Alionesha wasiwasi wake kwamba nyenzo zilizorejelewa zinaweza "kusababisha maswaki kwa umma" ikiwa zilisimamiwa ipasavyo.

    Saika Natur alikuwa anasafirisha taka kwenye meli kwa ajili ya kuchakatwa tena nchini China. Hapo awali, taka za karatasi zilichakatwa kwenye kiwanda huko Manchester, lakini moto mnamo Juni 2016 ilipunguza uwezo wake wa usindikaji, kwa hivyo unategemea mauzo ya nje.

    iligundua kiasi kikubwa cha taka za karatasi "za ubora duni" kwenye kiwanda. Inasemekana kwamba vipande vingi vinavyoitwa "vifuniko", ambavyo hutengenezwa kwa kubana na kufunga karatasi zilizotumika kwa ajili ya kuhifadhi na kusafirisha, vilikuwa na "kiasi kikubwa" cha taka za nyumbani kama vile nguo, plastiki, nepi za kutupwa, chuma, kioo na. chakula kilichobaki.

    SEPA ilimuagiza meneja wa kiwanda hicho kusitisha mauzo yote ya nje, pamoja na kusimamisha makontena ambayo tayari yalikuwa yamesafirishwa nje ya nchi.

    Vifuniko vya karatasi taka vilivyochunguzwa na mamlaka kati ya Septemba 2016 na Machi 2017 ni pamoja na vifaa vya kielektroniki, nepi za kutupwa na bidhaa za usafi, vyombo vilivyochafuliwa na mabaki ya chakula, chakula, kinyesi cha mbwa, mbao, nguo na viatu. Nguo, vito, makopo ya dawa, vidole, kioo, vifurushi vya chakula vya plastiki na vinywaji, makopo, nk.

    Kwa mujibu wa SEPA, idadi ndogo ya vifuniko vilifaa kwa mauzo ya nje, lakini nyingi hazikuwa za ubora wa kuuzwa nje.

    Saika Natur alikiri kukiuka kanuni za usafirishaji taka za Tume ya Ulaya mwezi Septemba mwaka huu. Sheria hii inalinda nchi zinazoendelea ambazo huagiza taka kutoka kwa nchi zilizoendelea kutoka kwa hatari za mazingira na kiafya.

    Kulingana na SEPA, kampuni inashughulikia mipango ya kuongeza uwezo wa usindikaji wa mitambo yake.

    "SEPA hairuhusu taka za Uskoti kuwa tatizo la kimazingira kwa mtu yeyote," Eihan wa SEPA alionya.

  15. 14 wauawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya Sudan - madaktari

    Madaktari nchini Sudan wanasema kuwa watu 14 wameuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama huku maelfu ya watu wakiingia barabarani kupinga unyakuzi wa kijeshi hivi majuzi.

    Wanaharakati walikuwa wameitisha maandamano makubwa kuadhimisha siku ambayo raia alitakiwa kuchukua uongozi wa Baraza Kuu la Utawala.

    Mtu aliyeongoza mapinduzi ya mwezi uliopita, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, aliifuta serikali, kukamata makumi ya wanasiasa na kujitaja kuwa mkuu wa Baraza jipya la Utawala.

    Kuna ushahidi unaoongezeka wa jinsi vikosi vya usalama vya Sudan vimekuwa na ukatili.

    Madaktari katika mji mkuu Khartoum wanasema gesi ya kutoa machozi imerushwa ndani ya majengo ya hospitali na wanajeshi wamezuia baadhi ya majeruhi kutibiwa.

    Watu wengi wamekamatwa katika vitongoji ambapo umeme ulikuwa umezimwa.

    Jenerali Burhan na wenzake walionyakua mamlaka wameazimia kusitisha maandamano ya kupinga jeshi kupata nguvu.

    Pia wanatangua maendeleo mengi yaliyopatikana baada ya Omar al-Bashir kupinduliwa.

    Washirika wake wanarejesha baadhi ya mamlaka na kuirejesha nchi katika udikteta ambao Wasudan walitdhani umetokomezwa.

  16. Marekani yaiondoa Nigeria katika orodha ya wanaokiuka dini

    Marekani imeiondoa Nigeria katika orodha ya wanaokiuka dini, kabla ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken nchini humo.

    Serikali ya Marekani mwaka jana iliiweka Nigeria katika orodha yake maalum ya waangalizi wa mataifa ambayo yaliendekeza ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa kidini.

    Nigeria haimo katika orodha ya 2021 ambayo ina Myanmar, China, Eritrea, Iran, Korea Kaskazini, Pakistan, Russia, Saudi Arabia, Tajikistan na Turkmenistan.

    Algeria, Comoro, Cuba, na Nicaragua pia zimo kwenye orodha maalum ya serikali ambazo zimekiuka uhuru wa kidini, kulingana na idara ya masuala ya kigeni ya Marekani.

    Hata hivyo, makundi ya kijihadi ya Boko Haram na Iswap linaloendesha shughuli zake kaskazini-mashariki mwa Nigeria, bado yanatia wasiwasi.

    Bw Blinken anazuru Nigeria siku ya Alhamisi katika awamu ya pili ya safari yake ya mataifa matatu ambayo ni pamoja na Kenya na Senegal.

    Anatarajiwa kukutana na Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari kujadili jinsi nchi zote mbili zinaweza kushirikiana zaidi katika afya ya kimataifa, usalama, kupanua upatikanaji wa nishati na ukuaji wa uchumi.

    Nigeria inapambana na vitisho vingi vya usalama, vikiwemo uasi wa muda mrefu wa Boko Haram, mapigano baina ya jamii na hivi karibuni, wimbi la utekaji nyara mkubwa shuleni unaofanywa na magenge yenye silaha.

    Soma:

  17. Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Alhamisi 18.11.2021