Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mume ni ‘mshukiwa’ baada ya mwanariadha wa Kenya Agnes Tirop kupatikana amefariki
Mwanariadha Agnes Tirop, aliyeiwakilisha Kenya katika mbio za mita 5000 katika Olimpiki amekutwa amefariki nyumbani kwake.
Moja kwa moja
IMF yashindwa kutoa makadirio ya pato la ndani la Ethiopia
Shirika la Fedha Duniani(IMF) limesema kuwa haliwezi kukisia kukua kwa kiwango cha Pato ndani la Ethiopia kwa kipindi cha mwaka 2022-2026 kufuatia kile wanachosema kuwa ni "kiwango cha juu cha kutokuwa na uhakika".
Hali inakuja kufuatia mzozo uliochukua miezi kumi na moja katika eneo la kaskazini la Tigray.
IMF imetoa makadirio ya uchumi ya dunia kwa kukadiria kukua kwa pato la ndani kwa nchi kuwa 2% kwa mwaka 2021, ambayo iko chini kwa 6% ya mwaka 2020.
Kwa kulinganisha, na nchi jirani ya Eritrea- ambayo pia inahusika katika mzozo huo - itaona ukuaji wa 4.8% kwa 2022-2026.
Kenya- ambayo ina uchumi mkubwa Afrika Mashariki- kwa upande mwingine, utaongezeka kwa 6% katika kipindi hicho hicho.
Katika muongo mmoja uliopita, Ethiopia ilikuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi, kwa kuongezeka hata mara mbili ya takwimu ya kiwango kilichopita.
Hata hivyo uchumi wake umeathirika kutokana na ukame, mvutano ya kikabila wakati huohuo wataalam pia wameonya juu ya kulipwa kwa deni lake la kigeni ambalo lilifadhili miradi mikubwa ya miundombinu.
Nchi zingine ambazo IMF haikutoa makadirio ni Afghanistan, Libya na Syria- na nchi zote zilizokumbwa na mizozo.
Ripoti ya IMF ilisema uchumi wa duniani unakadiriwa kukua asilimia 5.9 mnamo 2021 na asilimia 4.9 mnamo 2022, asilimia 0.1 chini kwa 2021 kuliko makadirio ya Julai.
Mlipuko wa janga la corona pia umeathiri uchumi haswa wa nchi zinazoendelea.
- Takwimu rasmi za serikali: Uchumi wa Tanzania waanza 2019 kwa kuyumba
- Uchumi wa zimbabwe unadidimia ;IMF
Kijana wa bodaboda asifiwa kwa kurudisha $ 50,000 zilizopotea
Kijana anayeendesha bodaboda Liberia amekuwa shujaa wa kitaifa baada ya kuokota dola 50,000 ambazo zilikuwa zimepotea za mwanamke mmoja ambaye ni mfanyabiashara maarufu kaskazini mashariki mwa mpaka wa Ivory Coast.
Kijana huyo mdogo, Emmanuel Tolue, alizikuta pesa zikiwa kwenye mfuko wa plastiki barabarani na alisikia tangazo kwenye radio ambapo mwenye fedha Musu Yancy,aliomba sana atakayeziona amsaidie kwa kumrudishia..
Kijana huyo alimjulisha kuwa amezipata katika ofisi za serikali ya mitaa.
Bi Yancy ameiambia BBC kuwa amemzawadia dola 1,500 (£1,100) pamoja na zawadi nyingine.
Mwanamke huyo alifurahi sana kupata taarifa ya kuwa anazipata pesa zake, alipiga kelele kumsifu Mungu mpaka sauti ilikuwa inakaribia kupotea.
Watu wengi walimsifia kijana huyo kwa kufanya usamaria mwema wa aina hiyo.
Jambo kama hilo la ambalo kijana wa bodaboda amelifanya si jambo la kawaida kutokea Liberia, mara baada ya vita.
Mume ni ‘mshukiwa’ baada ya mwanariadha wa Kenya Tirop kupatikana amefariki
Mshikilizi wa rekodi ya ulimwengu mkenya Agnes Tirop amepatikana ameuawa kwa kuchomwa kisu nyumbani kwake katika mji wa Iten magharibi mwa nchi hiyo , polisi wakimchukulia mumewe kama mshukiwa .
Mshindi huyo mara mbili wa medali ya shaba ya Mashindano ya Riadha ya Dunia, ambaye alimaliza wa nne katika fainali ya Olimpiki ya mbio za mita 5,000 miezi miwili iliyopita, alikuwa na umri wa miaka 25.
Uchunguzi wa jinai sasa unaendelea juu ya kifo chake, na polisi wanasema mumewe ametoweka.
Siku ya Jumatano, wachunguzi wa eneo la uhalifu walikuwa nyumbani kwa Tirop, ambaye polisi wanasema aliripotiwa kupotea na baba yake Jumanne usiku.
"[Polisi] walipoingia nyumbani, walimkuta Tirop kwenye kitanda na kulikuwa na damu sakafuni," Tom Makori, mkuu wa polisi wa eneo hilo, alisema.
"Waliona alikuwa amechomwa kisu shingoni, jambo lililotupelekea kuamini ni jeraha la kisu, na tunaamini kwamba ndicho kilichosababisha kifo chake.
"Mumewe bado hajulikani aliko , na uchunguzi wa awali unatuambia kuwa mumewe ni mshukiwa kwa sababu hawezi kupatikana. Polisi wanajaribu kumtafuta mumewe ili aweze kuelezea kilichomsibu Tirop."
Makori ameongeza kuwa polisi wanaamini kuwa CCTV katika nyumba hiyo inaweza kusaidia uchunguzi wao.
Tirop pia alikutwa na jeraha la kuchomwa tumboni mwake, vyanzo vimeiambia BBC.
Wabunge wanyimwa dhamana baada ya tamko la Rais Museveni
Mawakili wa wabunge wawili wa chama cha upinzani cha NUP nchini Uganda wamesema majaji wanaogoba kusikiliza maombi ya wateja wao kupewa dhamana.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Museveni kutoa tamko la kuondoa dhamana kwa watuhumiwa wa mauji na uhaini.
Wabunge hao wawili ambao ni Allan Ssewanyana na Mohamed Ssegirinya walikamtwa tangu Septemba 7 mwaka huu kwa tuhuma za mauji na Ugaidi,na jumla ya mashtaka yao kufikia saba.
Mwezi uliopita, Wabunge hao walipewa dhamana na mahakama kuu lakini walikamatwa tena na vyombo vya usalama.
Wakili wa watuhumiwa ambaye pia ni Meya wa Jiji la Kampala Erias Lukwago ameiambia BBC kuwa leo wanafikishwa tena mahakama lakini ombi lao la kupata dhamana halitasikilizwa kwa kuwa baadhi ya majaji walitakiwa kusikiliza ombi hilo wanaogopa kusikiza kutokana na tamko la Rais Museveni kutaka kuondowa dhamana.
Aidha haijulikani ni lini mahakama kuu itasikiliza ombi la dhamana ya wabunge hao kwani wana haki ya kupewa dhamana kulingana na katiba ya Uganda baada ya kutimiza vigezo vinavyotakiwa na mahakama kuu.
Tamko la Rais Museveni la kutaka kuondowa dhamana limekuwa gumzo kubwa nchini Uganda na watetezi wa haki za binadamu wakipinga pendeko za Museveni kuingilia Idara ya mahakama.
Wabunge hao wa chama NUP wanatuhumiwa kwa mauji ya mkoa wa Masaka mwezi wa Julai na Agosti ambapo watu zaidi ya 28 waliuawa kwa kukatwa mapanga na idadi kubwa yawalioua ni wazee wa miaka 60 na kuendelea.
Mwanamuziki wa Zambia ajitoa kuwania tuzo baada ya mashabiki kumpinga mtandaoni
Mwanamuziki maarufu wa Zambia Slapdee amejiondoa kuwania tuzo baada ya mashabiki kumkosoa kwa kufanya maonesho ya muziki kwa chama kilichokuwa madarakani.
Chama hicho cha Patriotic Front kilishindwa uchaguzi na hivyo kundoka madarakani mwezi Agosti.
Slapde, ambaye jina lake halisi ni Mwila Musonda, awali alitetea maamuzi yake ya kufanya maonesho kwa ajili ya maofisa kama biashara lakini inaoneka iliathiri muziki wake.
Kufuatiwa kuchaguliwa Afrimma kushiriki kuwania tuzo, Wazambia walihamasisha watu watu mtandaoni kumpigia kura mwanamuziki wa Afrika Kusini Cassper Nyovest katika kipengele alichokuwa anawania cha mwanamuziki bora wa kiume kusini mwa Afrika ambapo kulikuwa na mshiriki wa Zimbabwe Jah Prayzah naTha Dogg kutoka Namibia na wengine.
Kampeni za kumpinga Slapdee na kumuunga mkono Cassper Nyovest zilizua gumzo mtandaoni.
Mwanamuziki wa Afrika kusini aliandika kwenye twitter "kwanini anazungumziwa Zambia?" alafu akasema "Ni sawa Zambia, hii ni biashara tu"
- BET Awards 2021:Wajue wasanii waliokuwa na rekodi za makosa ya jinai, waliowahi kushinda tuzo za BET
Rais Kenyatta kuwa rais wa kwanza wa Afrika kukutana na rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atakutana na rais wa Marekani Joe Biden wakati akimaliza ziara yake ya siku mbili nchini Marekani.
Rais Kenyatta atakuwa rais wa kwanza kutoka Afrika kukutana na rais Biden tangu kiongozi huyo aapishwe mwaka huu.
Msemaji wa Ikulu ya Kenya amesema viongozi hao wawili watajadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya amani , usalama na mabadiliko ya tabia nchi.
Jumanne, Rais Kenyatta aliwaongoza viongozi wa biashara kusaini mikataba kadhaa ya uwekezaji wa biashara ndogo na wastani pamoja na miradi ya usafirishaji na nishati safi.
Marekani inaiona Kenya kuwa mshirika sahihi katika kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Mashariki mwa Afrika.
Mdogo wa rais wa zamani wa Algeria afungwa
Mdogo wa aliyekuwa rais wa Algeria hayati, Abdelaziz Bouteflika, amefungwa gerezani kwa kipindi cha miaka miwili kwa kosa la kukwamisha haki kutendeka.
Said Bouteflika alifungwa pamoja na waziri wa zamani wa haki, Tayeb Louh, pamoja na mfanyabiashara , Ali Haddad.
Bwana Louh atatumikia kifungo cha miaka sita wakati bwana Haddad atafungwa miaka miwili.
Wote watatu walikamatwa baada ya rais Bouteflika alipoondolewa madarakani kwa lazima mnamo mwaka 2019.
Rais wa zamani wa Algeria ,Bouteflika alifariki mwezi uliopita, miaka nane baada ya kuugua kwa muda mrefu.
- Abdelaziz Bouteflika: Rais wa zamani wa Algeria amefariki akiwa na miaka 84
- Rais asiyeonekana mbele za watu Abdelaziz Bouteflika atawezaje kuiongoza tena Algeria?
'Kenya haitakubali kutoa hata inchi moja ya ardhi yake kwa Somalia'
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya kuwa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa wa kuipatia Somalia eneo kubwa la bahari linalogombaniwa kutoka pwani ya nchi yao itafanya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kudorora.
Kenyatta alipinga uamuzi huo wa eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi akisema watageuza faida za kisiasa na kiuchumi, na kutishia usalama katika Pembe dhaifu la Afrika.
Amesisitiza wito wake wa kuwepo kwa suluhu ya mazungumzo katika mzozo huo.
Awali rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohammed maarufu farmajo aliitaka Kenya kuheshimu sheria ya kimataifa baada ya mahakama hiyo ya Umoja wa Kimataifa kukabidhi umiliki wa eneo kubwa linalodaiwa kuwa na mafuta na gesi katika bahari hindi kwa Somali.
Katika hotuba iliokwenda moja kwa moja katika runinga baada ya uamuzi huo, Mohamed Abdullahi Mohamed, alisema kwamba Nairobi inapaswa kuona uamuzi huo kama fursaya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Mnamo 2009, nchi hizo mbili zilikubaliana katika hati ya makubaliano, ikiungwa mkono na UN, kumaliza mzozo wa mipaka kupitia mazungumzo.
Lakini miaka mitano baadaye, Somalia ilisema mazungumzo yalishindwa na badala yake ikaenda kwa ICJ.
Mwaka 2014, Somalia iliamua kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo katika mahakama ya kimataifa ya (International Court of Justice) iliyoko Hague.
Katika ombi lake, Somalia ilisema mazungumzo ya kidiplomasia yameshindikana na sasa mahakama "iamue uratibu sahihi wa kijiografia wa mpaka mmoja wa baharini katika Bahari ya Hindi".
Lakini hayo si yote. Somalia iliitaka mahakama ya kimataifa ICJ kutangaza kuwa “Kenya… imekiuka wajibu kimataifa wa kuheshimu haki za nchi na mahakama".
Mwaka mmoja baadae , Kenya iliweka upingamizi mahakamani juu ya kesi hiyo.
- ICJ yakataa kesi ya Kenya katika mzozo wa mpaka wa baharini na Somalia
- Mgogoro wa mpaka: Kenya yamrudisha nyumbani balozi wake wa Somalia huku ikimfurusha yule wa Somalia nchini humo
- ICJ yasema kesi ya Kenya na Somalia itaendelea
- Kenya yajiondoa katika kusikilizwa kwa mzozo wake wa majini na Somalia
Jeshi lapelekwa katika shule Eswatini
Wanajeshi na polisi wamepelekwa katika shule zote katika Eswatini ambako wanafunzi wamekuwa wakifanya maandamano kwa muda wa wiki moja kudai mageuzi ya kisiasa.
Shule za msingi na sekondari katika nchi hiyo pekee ya Kiafrika inayotawaliwa Kifalme zamani ikifahamika kama Swaziland, wamekuwa wakisusia kuingia madarasani na kufanya mgomo baridi kwa mwezi mzima uliopita.
Hapo nyuma, maandamano ya wanaounga mkono demokrasia yalikuwa yakifanyika katika maeneo ya mijini, lakini katika kipindi cha mwaka hivi -maandamano hayo yamekuwa yakionekana miongoni mwa jamii za vijijini-ambako kwa kawaida wamekuwa walimuunga mkono Mfalme.
Maafisa wa usalama wamekuwa wakionekana katika miji mikuu ya Eswatini-Mbabane na Manzini.
Maafisa wanasema wamepelekwa kusaidia kuimarisha amani lakini wanafunzi waandamanaji wanaamini ni kuwatisha.
Maandamano ya wanafunzi ya wiki hii ni ya hivi karibuni katika miezi ya hivi karibuni ya ghasia katika ufalme huo mdogo.
Wanatoa wito wa hali bora za kusoma na elimu ya bure. Wanasema gharama ya elimu katika shule za taifa haipatikani kwa wengi-katika nchi ambazo karibu 25% ya watu wazima hawana ajira.
Waandamanaji, ambao wamekuwa wakikusanywa na makundi ya wanafunzi, pia wanadai kuachiliwa kwa wabunge wawili waliokamatwa wakati wa maandamano ya kudai demokrasia mapema mwaka huu.
Mfalme Mswati III aliwahi kuwashutumiwa na wanaharakati kwa kutumia ghasia kuwanyamazisha wapinzani wake wa kisiasa-baadhi wanaona kusambazwa kwa wanajeshi kama sehemu ya kutekeleza nia hiyo.
Ufalme wa Eswatini ni mojawapo ya nchi masikini zaidi barani Afrika-wakosoaji wake wanamshutumu kwa kuishi maisha ya anasa huku watu wake wakikabiliwa na njaa kila siku.
Wachambuzi wa siasa wanasema maandamano ya mara kwa mara ya upinzani ni ishara ya kutaka mabadiliko nchini-kwamba watu wanaendelea kutofurahia utawala uliopo sasa madarakani.
- Je, ni kweli usipokuwa na wake wawili eSwatini unafungwa?
Kiongozi wa zamani wa Msumbiji ahimiza amani baada kifo cha mkuu wa waasi
Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano amesema juhudi za kushirikisha kikundi kilichojitenga cha upinzani cha Renamo zinapaswa kuendelea baada ya kiongozi wake kuuawa Jumatatu.
Jenerali Mariano Nhongo aliuawa na vi vikosi vya usalama katika mkoa wa Sofala ya kati.
"Sikutaka kifo cha mtu yeyote lakini watu lazima walindwe. Na watu wakilindwa , huenda kukazuka makabiliano na maadui," alisema Bwana Chissano, aliongeza kumekuwa na nafasi ya mazungumzo na kiongozi wa waasi.
Jenerali Nhongo alipinga mmkataba wa amani ambao Renamo ilifikia na serikali mnamo 2019 na alikuwa akifanya mashambulio dhidi ya raia na vikosi vya usalama.
Karibu nusu ya wapiganaji wake watiifu 5,000 lwalikuwa wameunga mkono mkataba huo.
- Africa Eye: Kwanini Msumbiji imekuwa kitovu cha ugaidi kusini mwa Afrika?
- Mzozo wa Msumbiji: Majeshi ya Rwanda yateka ngome ya wanamgambo Msumbiji
Mali za jambazi maarufu wa Marekani Al Capone zauzwa kwa $3m
Uuzaji wa mali za jambazi maarufu wa Marekani Al Capone umekusanya jumla ya dola milioni tatu za kimarekani (£ 2.2m) kwenye mnada uliofanyika mwishoni mwa wiki huko California.
Baadhi ya vitu 174 - pamoja na silaha za moto na picha za kibinafsi pamoja na vito na samani- zimeonyeshwa.
Hafla hiyo, inayoitwa Karne ya Umaarufu: Mali ya Al Capone, ilifanyika katika kilabu cha kibinafsi na ilivutia wazabuni karibu 1,000.
Bidhaa maarufu zaidi ilikuwa bunduki inayopendwa na Capone, ambayo iliuzwa kwa $ 860,000.
Bunduki hii inaaminika ilkuwa bei ya juu zaidi ya silaha ya karne ya 20 iliyouzwa kwenye mnada, kulingana na Chicago Tribune.
Al Capone alikuwa mhalifu mkubwa Chicago aliyejulikana kama Adui Namba moja wa Umma kwa utawala wake mfupi kama kiongozi wa uhalifu miaka ya 1920.
Mali ya Al Capone ilisalia katika milki ya familia yake kwa karibu miaka 75 baada ya kifo chake mnamo 1947.
Diane Capone - mmoja wa wajukuu watatu wa Al Capone walionusurika, ambao wanaishi California - alisema uamuzi wa kuuza vitu hivyo ulitokana na yeye na dada zake kuzeeka, kulingana na taarifa za shirika la habari la Reuters.
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatano 13.10.2021.