Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kesi ya Mbowe yaahirishwa Polisi watawanya wafuasi wake mahakamani
Polisi jijini Dar es Salam wamewatawanya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wamekusanyika nje ya mahakama ya Kisutu kufuatilia kesi ya mwenye kiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Watoto watatu wauawa na Simba nchini Tanzania
Wanafunzi watatu wa ya shule moja ya msingi nchini Tanzania wameuawa baada ya kushambuliwa na Simba katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha .
Mtoto mwingine mmoja alijeruhiwa katika tukio hilo wakati walipokuwa wamekwenda porini kuwatafuta mifugo wao waliokuwa wamepotea .
Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi nchini Tanzania imewataja watoto waliouawa kama Olobiko Metui mwenye umri wa miaka 10, Ndaskoi Sangau mwenye umri wa miaka 9 na Sanka Saning’o mwenye umri wa miaka 10.
Wote walikuwa katika darasa la tatu ilhali aliyejeruhiwa ni Kiambwa Lektonyi mwenye umri wa miaka 11. Polisi imewatahadharisha wazazi wa jamii za ufugaji zinazopakana na hifadhi kuwa waangalifu wanapowatuma watoto wadogo kuchunga mifugo .
Umoja wa Afrika watangaza kuzindua chanjo milioni 400 kwa nchi wanachama
Umoja wa Afrika umetangaza kusambaza dozi milioni 400 za chanjo ya corona kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika na eneo la Caribbean.
Hii ni mara ya kwanza kwa nchi wanachama wa AU kununua chanjo kwa pamoja.
Nchi kadhaa barani Afrika zitapokea shehena za kwanza za chanjo ambazo zilinunuliwa na Jumuiya ya Afrika.
Shena ya kwanza wa chanjo zitakazonunuliwa pamoja itajumuisha usafirishaji wa kila mwezi wa chanjo ya Johnson & Johnson na dozi ya kwanza ya COVID-19.
Chini ya mpango huo unaoongozwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, nguvu ya ununuzi ya pamoja ya bara ilisababisha watengenezaji wa chanjo kukubali kutoa dozi milioni 400 katika miezi ijayo.
Hatua ya mwisho ya mchakato wa utengenezaji unafanywa nchini Afrika Kusini. Karibu dozi milioni sita zinapaswa kusambazwa kwa nchi wanachama mwishoni mwa Agosti.
Chanjo milioni 400 zinatosha kuchanja theluthi moja ya watu wa Afrika katika hatua ambayo itasaidia bara hilo kufikia lengo lake la kuchanja angalau asilimia 60 ya idadi ya watu.
Nchi nyingi za Kiafrika - kwa sasa zinakabiliwa na wimbi la tatu la virusi - zina viwango vya chini kabisa vya chanjo ya corona kwa sababu zilikabiliwa na changamoto ya kupata vifaa.
Machar awaita 'waharibifu wa amani' wale walipanga jaribio la kumuondoa
Makamu wa Rais wa Kwanza nchini Sudan Kusini Riek Machar, amelaani kundi la majenerali ndani ya mrengo wa kijeshi wa chama chake cha Sudan People's Liberation Movement upande wa upinzani (SPLM-IO), ambao walitangaza kung'olewa kwake kutoka kwa uongozi wa chama.
Siku ya Jumanne majenerali watatu walisema wamemuondoa madarakani Bw. Machar na nafasi yake kupewa mkuu wa zamani wa majeshi wa SPLA-IO, Simon Gatwech Dual, kama kiongozi wa mpito wa chama hicho na mkuu wa majeshi katika hatua ambayo imeleta mabadiliko mapya katika siasa za Sudan Kusini.
Machar alimuondoa Bw. Gatwech kutoka wadhifa wake kama mkuu wa watumishi na kupendekekeza uteuzi wake kama mshauri wa Rais wa masuala ya amani, lakini Bw. Gatwech amekataa uteuzi huo.
Soma zaidi:
- Miaka 10 ya Uhuru wa Sudan Kusini: John Garang, 'Baba wa taifa' ambaye hakuonja matunda ya uhuru wa nchi
- Miaka 10 ya Uhuru wa Sudani Kusini: Vita mbili kuu na harakati za miongo sita ya kutafuta kujitawala
- Mambo matano usiyoyajua kuhusu Sudan Kusini
Makamu wa rais alisema watu walio nyuma ya jaribio la kumuondoa madarakani ni "waharibifu wa amani" katika taarifa kwa waandishi wa habari.
Alisema hatua hiyo ilikuwa na lengo la kuhhujumu mpango wa kupelekwa kwa vikosi vya muungano baada ya bunge jipya kuapishwa.
Bwana Machar alisisitiza kujitolea kwa chama chake katika utekelezaji kamili wa makubaliano ya amani yaliyofufuliwa "kwa roho moja".
Wavuvi wa Kenya 'wavua' mabomu ziwa Victoria
Kundi la wavuvi wa Kenya waliokuwa wakivua samaki katika ziwa Victoria walipigwa na butwaa baada ya kuvua sanduku kubwa la chuma lililokuwa na mabomu sita badala ya samaki.
Wavuvi hao kutoka mji wa Mbita magharibi mwa Kenya waliodhani wamepata samaki mkubwa asubuhi ya Jumatatno, walikimbilia kufungua sanduku hilo lakini walipata mambomo yenye kutu.
Polisi wa Kenya'wamekuwa wakituma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuhusiana na tukio hilo:
Wawili kati ya wavuvi hao walipiga mbizi kwenye ziwa hilo kwa kuhofia mabomu hayo huenda yakalipuka huku wenzao watatu wakati wakiongoza boti ufuoni.
Waliripoti ugunduzi huo kwa wasimamizi wa ziwa ambao waliwajulisha polisi.
Idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya (DCI) ilisema wataalam wa utupaji mabomu walijulishwa mara moja na "wakakimbilia eneo la tukio na kuchukua sanduku hilo".
Mabomu hayo yalitarajiwa kufyatuliwa baadaye na wataalam.
Mnamo mwaka wa 2019 mabomu yaliyosadikiwa kutoka enzi ya ukoloni yalipatikana yamefichwa kwenye sanduku la zamani la mbao ndani ya ziwa.
Msaada wa chakula wa UN wawasili Tigray lakini zaidi inahitajika
Zaidi ya lori 150 zilizobeba msaada wa chakula zimewasili katika eneo la Tigray linalokabiliwa na mzozo kaskazini mwa Ethiopia. Mamilioni ya misaada zaidi inahitajika, kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.
Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema lori 175 zilizobeba na shehena za chakula zimewasili jimbo la Tigray.
Mkurugenzi mkuu wa shirika, David Beasley, ameweka ujumbe kwenye kwenye Twitter akisema tijapokuwa hii ni "hatua kubwa" zaidi ya lori 100 zinahitajika kupeleka chakula cha msaada kila siku kwa watu wanaokabiliwa na hali ngumu ya kibinadamu katika leneo hilo.
Serikali ya Ethiopia imethibitisha kuwasili kwa chakula hicho cha msaada na vifaa vingine vilivyosafirishwa na WFP a mashirika mengine ya UN.
Haya yanajiri siku moja baada ya Ethiopia kutangaza kusitisha vibali vya kufanya kazi vya mashirika matatu ya misaada, ikiyashutumu kwa ukiukaji wa kiutawala na kujihusisha na shughuli zilizo nje ya mamlaka yao.
Rais mpya wa Iran Ebrahim Raisi kuapishwa
Rais mpya wa Iran Ebrahim Raisi,anatarajiwa kuapishwa rasmi kuingia madarakani baada ya kushinda uchaguzi mwezi Juni.
Bw. Raisi, mhubiri mwenye misimamo mikali anamrithi Hassan Rouhani, alionekana na nchi za magharibu kuwa na misimamo ya kadri.
Anaingia madarakani wakati ambapo changamoto zinazoikabili Iran zinaendelea kuongezeka kutokana na vikwazo vya kimataifa vilivyolemaza uchumi wake.
Mvutano pia ulioongezeka kati ya nchi hiyo na mataifa ya kigeni ambayo yanailaumu Iran kwa shambulio baya la ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya meli ya mafuta karibu na Oman wiki iliyopita, ambayo Iran imekanusha.
Watu wawili - walinda usalama wa Uingereza na Kiromania - waliuawa wakati meli ya MV Mercer, inayomilikiwa na Israel iliposhambuliwa. Uingereza, Amerika na Israel zinailaumu Iran kwa kutekeleza shambulio hilo.
Mvutano kati ya Iran na Marekani umeongezeka tangu 2018, wakati Rais wa wakati huo Donald Trump alipoondoa nchi hiyo katika mkataba wa wa kimataifa juu ya mpango wa nyuklia wa Iran na kurudisha vikwazo.
Rais wa zamani wa Msumbiji ahimiza mazungumzo na makundi yenye silaha
Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano ametoa wito kwa serikali kutathmini uwezekano wa kujadiliana na makundi yenye silaha yanayohudumu katika eneo la Cabo Delgado linalokumbwa na mzozo.
Anasema kuna “aina flani ya ugaidi” ambao umekomeshwa kupitia majadiliano.
“Huenda pengine kiongozi wa kundi hilo naonesha ishara ya kutaka kutupatia nafasi ya majadiliano ambayo yatasaidia kumaliza” ghasia za silaha,alikiambia kituo cha Radio Mozambique kinachomilikiwa na serikali, katika mahojiano siku ya Jumatano.
Rais huyo wa zamani wa Msumbiji alisema sababu za vurugu za silaha huko Cabo Delgado lazima zichunguzwe kama njia ya kutatua mzozo wa kijeshi na kijamii katika jimbo hilo.
Bwana Chissano alikuwa rais wa Msumbiji kati ya 1986 na 2005. Aliongoza mazungumzo ya mafanikio na waasi wa zamani wa upinzani wa Msumbiji (Renamo), ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 16 mwaka 1992.
Rais wa sasa, Filipe Nyusi, ameelezea nia yake ya kujadiliana na vikundi vyenye silaha lakini amelalamika kuwa waasi hawajaonesha "ishara" ya kukaribisha mazungumzo hayo.
Mkoa wa Cabo Delgado umetumbia kwenye ghasia tangu mwaka 2017, baadhi ya mashambulio yakidaiwa kufanywa na kundi la Islamic State.
Mashambulio hayo kufikia sasa yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 na wengine zaidi ya 800,000 kufurushwa makwao.
Soma zaidi:
- Cabo Delgado: Uhusiano uliopo kati ya mali asili,uasi na mapigano nchini Msumbiji
- Msumbiji: Je, Cabo Delgado ni kituo cha wapiganaji wa Islamic State?
Habari za hivi punde, Kesi ya Mbowe yaahirishwa Polisi watawanya wafuasi wake mahakamani
Polisi jijini Dar es Salam wamewatawanya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wamekusanyika nje ya mahakama ya Kisutu kufuatilia kesi ya mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
Kesi hiyo ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa nia ya mtandao hata hivyo imeahirishwa kutokana na changamoto za kimawasiliano. Mbowe anatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho asubuhi kuendelea na kesi hiyo.
Awali wafuasi wa Chadema walionekana nje ya mahakama hiyo wakiwa na mabango yaynaosema: 'Mbowe sio gaidi’ na pia walikuwa wakipaaza sauti na kusema, ‘katiba mya sio ugaidi’.
Hata hivyo polisi waliwatawanya wafuasi hao na baadhi yao kukamatwa.
Mawakili wa Mbowe wakiongozwa na Peter Kibatala , wapo mahakamani hapo lakini mteja wao ni mahabusi katika gereza la Ukonga.
Mbowe anakabiliwa na mashtaka ya kuhujumu uchumi na kufadhili vitendo vya kigaidi.
Wakosoaji wa serikali ikiwemo Chadema pamoja na mashirika ya haki za kibinadamu wanaichukulia kesi hiyo ni ya kisiasa na kushinikiza serikali imwachie huru mwanasiasa huyo.
Hata hivyo polisi wamekanusha madai hayo na kwamba wanasema wana ushahidi wa kutosha kwamba Mbowe alitenda makosa hayo na kutaka mahakama iachwe itekeleze wajibu wake.
Soma zaidi:
- Mashirika ya kutetea haki yalaani kukamatwa kwa Mbowe
- Nini maana ya mwisho wa Uenyekiti wa Mbowe Chadema?
Ghadhabu yaibuka baada ya mbunge mwenye vitiligo kufedheheshwa
Spika wa bunge la Mauritius amekosolewa vikali kwa kumuaibisha mbunge mwenye ugonjwa w angozi wa vitiligo, hali ambayo husababisha sehemu ya ngozi kuwa nyeupe zaidi.
"Angalia uso wako!" Spika Sooroojdev Phokeer alipaza sauti akimwambia mbunge Rajesh Bhagwan mara 11.
Hii ilifuatia matamshi ambapo mbunge alimuelezea spika kama "mlevi" na "aibu"
Video ya malumbano hayo imeshirikishwa umma kwenye mtandao waTwitter:
TWEET
Vitiligo ni ugonjwa unaosababisha mtu kupoteza sehemu ya ngozi yake ya kawaida au rangi yake.
Kauli hizo zimeibua miito ya kumtaka spika ajiuzulu na zimelaaniwa kote nchini na nje ya nchi.
Baada ya malumbano hayo Bw Bhagwan alisema ilikuwa ni "jambo la aibu " kuzungumzia kuhusu afya ya mtu, akisema spika ni"fedheha kwa taifa".
Katika ujumbe wake wa Twitter kikundi cha Uingereza kinachounga mkono Vitiligo kiliita kauli ya spika "fedheha".
"Vitiligo sio maelezo ya tabia yetu," kilisema kikundi hicho, kikiongeza kuwa uso wa Bw Phokeer' haupaswi "kuonesha aibu" kwa " kumfedhehesha na kutomheshimu".
Bwana harusi na wageni wake wauawa na radi Bangladesh
Radi nchini Bangladesh imewapiga na kuwaua wageni 17 waliohudhuria sherehe ya harusi moja nchini humo.
Watu 14 wengine ikiwemo bwanaharusi , walijeruhiwa .
Wakati huo bi harusi hakuwepo katika sherehe hiyo.
Sherehe hiyo ilikuwa inafanyika katika boti moja katika mji uliopo karibu na mto wa Shigbanj, wakielekea katika nyumba ya biharusiwakati walipopigwa na radi hiyo.
Wakazi wanasema kwamba radi kadhaa zilipiga kundi hilo.
Kila mwaka mamia ya watu kusini mwa bara Asia hufariki kutokana na radi.
Mwaka 2016, Bangladesh ilitangaza radi kuwa janga wakati zaidi ya watu 200 walipofariki katika mwezi wa Mei pekee, ikiwemo watu 82 katika siku moja.
Wataalamu wanasema kwamba kukatwa kwa misitu kumesababisha ongezeko la radi kutokana na kutoweka kwa miti mingi mirefu ambayo huzuia radi.
Natumai hujambo