Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Madagascar yasema imezima njama ya kumuua rais Andry Rajoelina

Madagascar yasema imezima njama ya kumuua rais Andry Rajoelina Mamlaka nchini Madagascar zimesema washukiwa kadhaa wa "kigeni na Malagasy" walikamatwa juu ya njama ya kumuua Rais Andry Rajoelina.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja hivi leo hadi hapo kesho panapo majaaliwa

  2. Familia ya watu tisa waliozaliwa tarehe na mwezi mmoja

    Mwalimu mmoja nchini Pakistankwa jina Amir Ali, amevunja rekodi ya dunia kwa kuwa na familia yeney watu wengi waliozaliwa katika tarehe moja –ya agostimosibaada ya watu tisa wa familia moja kuzaliwa tarehe hiyo.

    Rekodi ya awali ilikuwa imeshikiliwa na familia kutoka Caymans kwa miaka tisa ambapo watoto watano walikuwa wamezaliwa tarehe 5 mwezi februarilakini miaka tofauti .

    Amir, mkazi wa Larakana , alisema alizaliwa tarehe 1 mwezi Agosti ,Mke wake alizaliwa tarehe moja mwezi Agosti , Binti yake wa kwanza Sindh alizaliwa mwanawe wa kiume wa pili Amber na wanae pacha Ammar na Ahmar, wote walizaliwa tarehe 1 Agosti .

    Amir Ali anaamini katika elimu ya nyota- nyota yake ni Asad au Zmarai na inaelezwa kuwa namba ya kwanza ya bahati, wakati alipoanza kazi tarehe 1 mwezi Agosti na kuoa tarehe 1 mwezi Agosti.

    Amir anasema familia yake yote inasheherekea siku ya kuzaliwa kwao siku moja. Bw. Amir pia anaamini katika unajimu na kuandika ushairi. Ana shahada ya uzamili kwenye masomo kadhaa, ikiwemo sayansi ya jamii, mahusiao ya kimataifa na uchumi.

    Tarehe 1 mwezi Agosti, familia yote husheherekea kwa pamoja, Bw. Amir i anasema. Anaongeza kuwa watoto wote wamezaliwa nyumbani kisha wakasajiliwa na mamlaka za manispaa.

    Aliongeza kuwa kwa ushauri wa rafiki yake, alituma maombi ya usajili kwa ajili ya kuwekwa rekodi kwenye Guiness Book of World Records.

  3. Samaki waliokutwa wamekufa ufukweni Tanzania, chanzo chake kujulikana kesho,

    Serikali ya Tanzania imesema haijafahamu mpaka sasa chanzo cha vifo vya samaki waliokutwa katika fukwe ya bahari ya Hindi katika jiji la Dar es Salaam.

    Asubuhi ya jana katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga khan palizagaa samaki wengi waliokuwa wamekufa na kuzua taharuki miongoni mwa wafanyabiashara na walaji wa samaki.

    Waziri wa Uvuvi nchini Tanzania, Mashimba Ndaki ameiambia BBC kwamba uchunguzi umeanza na sasa wanasubiri majibu kujua nini kimewaua samaki hao.

    ‘tulipelekea sampo kwa mkemia mkuu wa serikali, na sampo nyingine tulipeleka kwa maabara yetu kuu iliyoko Mwanza, na nyingine tuliwaachia Polisi wa kitengo chao kile cha uchunguzi, kwa hiyo bado hatujaelewa chanzo hasa itakuwa nini’.

    Waziri Ndaki amesema mpaka kufikia kesho Serikali itakuwa imepata majibu ya uchunguzi kutoka kwa wataalamu wake kuhusu chanzo cha vifo vya samaki hao na yatawekwa wazi kwa umma.

    Taarifa iliyotolewa awali na kitengo cha Mawasiliano Serikalini inasema Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), maofisa uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa na meneja wa soko la Magogoni Feri walikusanya samaki kiasi cha Kilogramu 164 na kufikisha Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

    “Sampuli zilichukuliwa kwa ajili ya maabara ya TAFIRI, maabara ya Taifa ya Uvuvi na Polisi Kitengo cha Sayansi ya Uchunguzi kwa ajili ya kupeleka maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,

    "kiasi cha Kilogramu 156 kilichosalia kilikabidhiwa kwa ofisa uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kuteketezwa na tukio la kuteketezwa lilishuhudiwa na maofisa wa wizara, uongozi wa Soko la Feri, ofisi ya uvuvi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,” imesema taarifa hiyo.

    Pamoja na kukutwa samaki waliokufa wamezagaa ufukweni, Waziri huyo wa uvuvi Tanzania alisesema biashara ya samaki inaendelea kama kawaida katika habari hiyo ya Hindi akisema ‘kwa sababu hali hiyo (ya samaki kufa) huwa inatokea’.

    BBC ilitaka kujua kama kuruhusu kwa biashara hiyo kuendelea bila kujua matokeo ya samaki waliokutwa wamekufa hakuwezi kuleta madhara kwa walaji? Alijibu ‘Kwa samaki ambao wanavuliwa wakikutwa wako hai na wavuvi, hatuwezi kuwa na mashaka nao sana, kwa sababu ndiyo hali halisi ya samaki baharini na hata ziwani, unawakuta samaki wakiwa wazima, unawavua, unapeleka nyumbani unawafanya kitoweo'. Alisema.

  4. Nahodha wa Ghana Andre Ayew kujiunga na Al Sadd SC ya Qatar

    Nahodha wa timu ya soka ya Ghana Andre Andreyeye yuko tayari kusaini makubaliano na klabu ya Qatar Al Sadd SC. Klabu hiyo inasema imefikia makubaliano ya kumsaini nahodha huyo wa Black Stars.

    Kijana huyo wa miaka 31 anasafiri kwenda Qatar kukamilisha kusaini mkataba.Ayew anatarajiwa huko Doha Alhamisi (leo) kufanyiwa matibabu na baadaye kutia saini makubaliano hayo.

    Ayew amekuwa hana kilabu baada ya kandarasi yake ya miaka mitatu na klabu ya Wales Swansea City kukosa kuongezwa mwishoni mwa msimu uliopita. Ilikuja wakati klabu ilikosa kupanda hadi Ligi ya Premia dhidi ya Brentford katika fainali ya mchujo.Ripoti zinaonyesha kuwa tapata zaidi ya dola laki mbili ($ 200, 0000) kwa wiki.

    Uhamaji wake ni sawa na mtangulizi wake kama nahodha wa Ghana Asamoah Gyan ambaye aliacha ligi ya Uingereza na kucheza Mashariki ya Kati wakati alihama kutoka Sunderland kwenda Al Ain huko UAE.

  5. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Tanzania, Anna Mghwira amefariki dunia

    Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo Alhamisi Julai 22, 2021 katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha alikokuwa akipatiwa matibabu. Mdogo wa Anna Mghwira na marafiki zake wa karibu wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho leo.

    "Ni kweli Mghwira amefariki mchana huu, alikuwa amezidiwa akawa amepelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)," mdogo wake aliithibitishia Mwananchi Zaidi ya wiki moja iliyopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru.

    Wakati huo huo Rais wa Tanzania Samia Suluhu ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo hicho kwa familia,ndugu, jamaa na marafiki wa Bi Anna Mughwira.

    Kulingana na taarifa ya rambi rambi hizo iliyotumwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Samia amepokea taarifa za kifo kwa majonzi na masikitiko makubwa hasa ukikumbuka mchango wake alioutoa katika ujenzi wa taifa.

    Amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea marehemu Ana Mghwira apumzike mahala pema peponi

    Bi Mghwira alikuwa mgombea pekee wa kike wakati wa kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015. Baada ya kushindwa uchaguzi, aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, hayati John Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akichukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa mkuu wa mkoa huo.

    Marehemu Bi. Mghwira alikuwa mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, chama kichanga zaidi Tanzania kilichoundwa mwaka 2014.

  6. Madagascar yasema imezima njama ya kumuua rais Andry Rajoelina

    Madagascar yasema imezima njama ya kumuua rais Andry Rajoelina Mamlaka nchini Madagascar zimesema washukiwa kadhaa wa "kigeni na Malagasy" walikamatwa juu ya njama ya kumuua Rais Andry Rajoelina.

    Mwanasheria Mkuu Berthine Razafiarivony alisema siku ya Alhamisi kwamba watu hao walikamatwa Jumanne kama sehemu ya uchunguzi "juu ya shambulio dhidi ya serikali".

    Razafiarivony, akiwahutubia waandishi wa habari, pia alisema njama hiyo iliyovunjwa ni pamoja na "mauaji na kuwaangamiza " wanasiasa wengine kando na rais.

    Hakukuwa na uthibitisho rasmi kuhusu nchi wanakotoka washukiwa wa kigeni. Ukubwa wa mpango huo au jinsi ulivyopangwa kutekelezwa bado haujafamika wazi .

    Rajoelina aliapishwa kama rais wa nchi ya kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi mnamo 2019 baada ya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali na ambao ushidni wake ulipingwa katika mahakama ya kikatiba na mpinzani wake.

    Unaweza pia kusoma:

    • Jovenel Moïse: Mwili wa rais wa Haiti 'ulichanika' kwa kumiminiwa risasi nyingi-mkewe asema
    • Jovenel Moïse: Tazama kikosi cha mamluki waliomuua rais wa Haiti-polisi
    • Jovenel Moïse: Haiti yaomba vikosi vya kigeni baada ya rais wake kuuawa
    • Kifo cha Rais wa Haiti: Hawa ni marais wengine waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani
  7. Treni yenye kasi zaidi duniani yazinduliwa China

    Treni yenye uwezo wa kusafiri kwa kasi ya kilomita 600 kwa saa imezinduliwa katika eneo la Qingdao nchini China.

    Treni hiyo ya mfumo wa Magliev iliotengenezwa na shirika la reli nchini China inadaiwa kuwa yenye kasi zaidi duniani CRRC.

    ‘’Magliev ni neno kwa ufupi lenye maana ya magnetic Levitation’’.

    Treni hiyo inaonekana kuelea angani kutokana na nguvu za umeme zinazoifanya kuonekana kuwa juu ya barabara ya reli.

    Liang Jianying, naibu meneja na muhandisi mkuu wa shirika la CRRC Sifang , aliambia vyombo vya habari nchini humo kwamba mbali na kasi yake , treni hiyo haina kelele na inahitaji uangalizi mdogo ikilinganishwa na treni zengine zenye kasi ya juu

    Mfano wa treni kama hiyo ulifichuliwa kwa vyombo vya habari mwaka 2019.

    Mwaka huohuo, China ilitangaza mipango yake ya kuanzisha uchukuzi wa saa 3 katika katika miji yake mikuu.

    Reli yenye kasi ya juu nchini China ni kipaumbele , ikiwa na lengo la kuunganisha miji yake mikuu kwa treni ili kupunguza muda na gharama za usafiri ndani ya taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu duniani.

    Kwa sasa , wastani wa kasi ya treni nchini humo ni kilomita 350 kwa saa , huku ndege zikiendeshwa katika kasi ya kati ya kilomita 800 hadi 900 kwa saa.

    Treni kama hiyo iliozinduliwa Qingdao inaweza kujaza pengo muhimu lililopo katikati.

    Hatahivyo kuna kitu kimoja muhimu ambacho ni kizuizi katika ufanisi wake - ukosefu wa reli za magliev ambazo hazijakamilishwa.

    Kwa sasa China ina reli moja pekee ya mfumo wa Magliev inayotumika kibiashara, na inaunganisha uwanja wa ndege wa Pudong huko Shanghai na kituo cha barabarani cha Longyang mjini humo.

    Safari hiyo ya kilomita 30 huchukua takriban dakika saba na nusu huku treni hiyo ikisafiri kwa kasi ya kilomita 430 kwa saa moja.

  8. Chombo cha Nasa chajiandaa kuchukua sampuli za mwamba wa sayari ya Mars

    Kifaa kidogo chenye ukubwa wa kidole cha mkono, kitafungwa kwenye mrija mdogo kwa ajili ya kurejeshwa hatimaye duniani.

    Wanasayansi wanasema ni fursa yao bora ya kubaini iwapo sayari Mars iliwahi kuhifadhi maisha viumbe ni kufanyia uchunguzi sehemu ya juu ya ardhi na miamba katika maabara za kisasa.

    Chombo hicho kinachofahamika kama Perseverance kilitua kwenye sayari nyekundu mwezi Februali, kwenye kreta yenye upana wa kilomita 45 (maili 30 ) crater called Jezero.

    Huu ni mkusanyiko wa rangi ya miamba chakavuambayo wanasayansi wanaamini kuwa inawakilisha sakafu ya kreta za sayari ya Mars zinazofahamika kama Jezero.

    Picha za setilaiti zinaonesha eneo la chini la mahala ambapo paliwahi kuwa ziwa wakati mmoja , lililojazwa kwa mto wa aina ya delta.

    Kitokana na hili, eneo hili linachukuliwa kama eneo ambalo huenda liliwahifadhi viumbe wadogo wa kale - kama walikuwepo.

    Roboti ya Nasa imejiendesha Kilomita1 (sawa na futi 3,000) kusini kutoka mahala ambapo ilitua kwa mtindo wa ajabu miezi mitano iliyopita.

    Nasa inafurahia jinsi chombo cha Perseverance kinavyofanya kazi

  9. Mapigano yarindima katika jimbo Afar nchini Ethiopia

    Mapigano makali yanaripotiwa kuendeleakatika jimbo la Afar nchini Ethiopia ambako maelfu ya watu wamesambaratishwa

    Huku mzozo wa muda mrefu ukiendelea katika jimbo la Tigray, mzozo huo una unaendelea kusambaa katika majimbo mengine ya nchi.

    Katika jimbo la Tigray, ripoti zinasema kumekuwa na mapigano makali kwa siku siku nne mfulurizo zilizopita .

    Waasi waTigray People’s Liberation Front (TPLF) wanakabiliana na vikozi vya jimbo la na washirika wake.

    Wakazi wa jimbo la Afar waliozungumza na BBC wamedai kuna majeruhi wengi katika eneo hilo kutokana na mashambulio ya wapiganaji waasi wa TPLF.

    Hatahivyo, msemaji wa TPLF alitoa taarifa kupitia mtandao wa Twitter akisema chama hicho hakiko vitani na watu wa Afar au wapiganaji, bali viongozi wa Ethiopia.

    Wanaharakati katiak jimbo la Afar wanasema msaada wa dharura w akibinadamu unahitajika kwa wakulima wa eneo hilo na watu wengine walio lazimishwa kukimbia kufuatia mapigano.

    Soma zaidi:

    • Chombo cha anga za juu cha Perseverance rover cha Nasa chatua sayari ya Mihiri.
    • Maziwa matatu yaliojificha yagunduliwa katika sayari ya Mars
  10. Zuma kuhudhuria mazishi ya kaka yake Alhamisi

    Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa ruhusa ya kuhudhuria mazaishi ya kaka yake mdogo, Michael, ambayre anapangwa kuzikwa Alhamisi mchana.

    ‘’Maombi ya Bw Zuma ya msamaha kama mfungwa wa muda mfupi, mwenye kiwango cha chini cha hatari yalishugulikiwa na kuidhinishwa ," alisema msemaji wa idara ya huduma za magereza , Singabakho Nxumalo, alisema Alhamisi.

    Bw Zuma havai sare ya wafungwa wakati wa “likizo ya msamaha ”, huku Bw Nxumalo akisema wafungwa hawahitaji kuwa wamevaa sare za jwafungwa wanapokuwa nje ya gereza .

    Rais huyo wa zamani kwa sasa anahudumia kifungo cha miezi 15 jela kwa kosa la kutoheshimu agizo la mahakama.

    Kufungwa kwake kuliibua ghasia katika jimbo la kwao la KwaZulu-Natal na Gauteng – ambako zaidi ya watu 200 waliuawa na mamia ya maduka na biashara kuporwa na kuharibiwa.

  11. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Alhamisi 22.07.2021