Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Chadema kwenda mahakamani kesho iwapo Freeman Mbowe hataachiliwa

Mkurugenzi wa mawasiliano na itifaki wa mambo ya nje wa chama cha upinzani cha Chadema John Mrema, amesema watakwenda Mahakama kuu kushinikiza Kiongozi wa chama hicho aachiliwe au ashitakiwe.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja hivi leo,hadi hapo kesho panapo majaaliwa

  2. Polisi wafisadi wakutwa na Choo cha dhahabu katika jumba lao

    Choo cha dhahabu na vitu vingine vya kifahari vimekutwa kwenye jumba lililovamiwa na wapelelezi wa Urusi , ambao wamesema walikuwa wakilifuatilia genge la polisi mafisadi.

    Tovuti ya kamati ya uchunguzi ina video inayoonesha yaliyomo ndani ya jumba hilo, miongoni mwa mali hizo ni zile zilizoporwa.

    Kanali Alexei Safonov mkuu wa polisi wa trafiki wa mkoa wa Stavropol, alikamatwa na wenzake sita.

    Polisi huyo anadaiwa kuchukua hongo ili kutoa vibali vya kughushi kwa ajili ya kufanya biashara.

    Vibali hivyo vinadaiwa kuwaruhusu madereva kupita kwenye vituo vya ukaguzi wakiwa na mizigo isiyoruhusiwa ya nafaka na vifaa vya ujenzi.

    Mtuhumiwa hajasema lolote kuhusu mashtaka yanayomkabili

    Vikosi vya polisi Caucasus Kaskazini nchini Urusi walihusika katika operesheni dhidi ya rushwa. Wapelelezi hao wamesema walifanya operesheni 80 za upekuzi- ikiwemo dhidi ya maafisa polisi wa usalama wa barabarani-na kukamata fedha nyingi, pia magari ya kifahari.

    Idara ya upelelezi ya SK inayofananishwa na FBI ya Marekani kimesema kuwa genge la Safonovo limechukua rushwa kwa miaka kadhaa, yenye thamani ya dola za Marekani 225,000.

    Safonov anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani ikiwa atakutwa na hatia. Mtangulizi wake Alexander Arzhanukhin ni miongoni mwa waliokamatwa.

    Alexander Khinshteyn, mbunge katika chama kinachounga mkono serikali, amesema zaidi ya polisi 35 wa usalama barabarani wa mkoa huo wamekamatwa.

    "Kwa asili, aina halisi ya umafia umekuwa ukifanya kazi huko Stavropol, ukifaidika na kila kitu: kutoka kwenye biashara haramu na vibali vya mizigo, hadi vya kusafirisha mchanga," aliandika kwenye programu ya ujumbe ya Telegram.

  3. Mungu alinituma niwaonye kuhusu rais Buhari’- Mhubiri wa Nigeria David Oyedepo

    Askofu avid Oyedepo, wa kanisa la Living Faith Church, kwa jina jingine Winners Chapel, amezungumzia utawala wa raisMuhammadu Buhari .

    Kiongozi huyo wa kidini amesema kwamba alikuwa amutumwa na Mungu kuwaonya raia wa igeria dhidi ya kumchagua rais Buhari mwaka wa 2015 .

    Alidai kwamba Buhari sio kiongozi ambaye anayajali maslahi ya raia wa Nigeria . Askofu huyo aliyasema hayo mwishonimwa wiki akihubiri katika katikaJimbo la Ogun kusini mwaNigeria .

    Alisema kwambawanigeria walipuuza onyo yake kuhusu kumchagua Buhari .

    ‘Wakati mwingine nabii anapozungumza ,watu wanafaa kumsikiliza ‘ alisemaOyeepo

    Alisema wakati alipotoa utabiri wake kuhusu serikali ya Buhari watu wengi walimshambulia lakini sasa yote yanayofanyka nchini humo yametimizautabiri wake .

    Oyedepoamesema aliona majanga mengi chini ya utawala wa Buhari kabla hata rais huyo hajachaguliwa kuingia madarakani

  4. Chanjo ya Corona tayari ipo nchini Tanzania, asema Waziri Mkuu Majaliwa

    Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa chanjo ya ugonjwa wa Corona ipo tayari nchini humo na amesema mwananchi yeyote anayetaka kuchanjwa akachanje kwa ajili ya kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo.

    Bw Majaliwa ameitoa kauli hiyo katika Baraza la Eid El Adha lililofanyika katika Msikiti wa Mtoro, Ilala jijini Dar es Salaam.

    "Tunao wagonjwa wachache tuendelee kuwaombea jukumu la Serikali ni kutoa huduma kwa wanaofikwa na ugonjwa huu, lakini pia tusiache kujikinga," "Tuchukue tahadhari kwa kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono, pamoja na kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko.

    Pia tuendelee kujikinga kwa kufanya mazoezi, juisi yetu ile tusiiache, lakini pia kukaa kwenye joto ambapo tuliipa jina la nyungu nayo itumike ili kupambana na ugonjwa huu," amesema.

    Kuhusu chanjo, Waziri Mkuu amesema amesema ipo na kwamba anayetaka akachanje kwani tayari hospitali zimeelezwa mahali.

  5. Nisaidieni!Tazama mwanamke alivyosombwa na mafuriko makubwa

    Mwanamke mmojaameokolewa na watu katikati mwa China baada ya kusomwa na mafuriko makubwa ambayo yameikumba nchi hiyo .

    Watu 12 wamefariki na zaii ya 100,000 kuokolewa katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa kuwahi kushuhudiwa nchini China .zaidi ya miji kumi katika mkoa wa Henan ukiwemo mji mkuu wa mkoa Zhengzhouimeathiriwa.

  6. Pogba atoa salam za Idd

    Katika mtandao wake wa Twitter kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba ameushirikisha umma wa mashabiki wake picha yake na mkewe.

    Paul Pogba ameambatanisha picha hiyo na ujumbe wa heri ya siku ya Idd akisema Eidd Mubarak kwa kaka na dada

    Waislam katika maeneo mbali mbali ya dunia waliadhimisha sherehe za Eid al-Adha huku baadhi wakiadhimisha sherehe hizo leo.

    Bw Pogba ambaye ni Muislam amekuwa akihudhuria ibada za hija mjini Mecca nchini Saudi Arabia, zinazohudhuriwa na maelfu ya Waislam kutoka maeneo mbali mbali ya dunia.

    Hatahivyo mwaka huu ibada za hija zilihudhuriwa na watu 60,000 pekee , raia na wakazi wa Saudia kufuatia hofu ya mambukizi ya virusi vya corona.

  7. Marekani yafanya shambulio la kwanza la angani chini ya Biden Somalia

    Marekani imefanya shambulio la kwanza la angani dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab mjini Galkayo, kaskazini mwa Somalia, Jumanne.

    Hili ni shambulio la kwanza la angani tangu Rais Joe Biden kuingia madarakani.

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Cindi Kingal amesema Marekani ilikuwa ikiyasaidia majeshi ya Somalia ambayo yalikuwa yakivamiwa na wanamgambo.

    Ripoti za awali zinasema kuwa raia walijeruhiwa.

    Rais Biden alidhibiti mashambulio ya angani kwa kutumia ndege zisizo na rubani nje ya Marekani.

    Mtangulizi wake Donald Trump aliongeza mashambulio ya angani nchini Somalia wakati wa utawala wake.

    Kabla tu ya kuondoka ofisini, aliamuru vikosi maalum vya wanajeshi 700 vilivyopelekwa Somalia viondolewe.

    Somalia imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama kutokana na mashambulio yanayofanywa na wanamgambo wa al-Shabab.

  8. Nigeria yawaokoa wanawake 100 na watoto waliokuwa wametekwa nyara

    Maafisa katika eneo la kaskazini-magharibi wa Nigeria wameweza kuwaokoa wanawake 100 na watoto- husuasan akina mama wanaonyonyesha watoto wachanga - waliokuwa wametekwa na majangili.

    Kundi hilo lilitekwa tarehe 8 Juni katika jimbo la Zamfara state. Watu wanee pia waliuawa wakati watukio hilo.

    Serikali ya jimbo la Zamfara limesema waliachiliwa buru bila kikombozi , lakini haikutoa maelezo zaidi.

    Kikundi hicho cha wanawake na watoto sasa kitafanyiwa vipimo vya kimatibabu na kupewa maagizo kabla ya kurejea nyumbani.

    Visa vya utekaji nyara vya mara kwa mara vimekuwa vikitokea katika eneo hilo katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.

    Tangu mwezi Disemba 2020, zaidi ya watu 1,000 wamekamatwa.

    Wengi wamekuwa wakiachiliwa huru ikiropotiwa baada ya kulipwa kwa kikombozi, lakini baadhi wamekuwa wakiuawa.

  9. Afrika Kusini yakadiria hasara baada ya vurugu zilizolenga biashara

    Mamlaka nchini Afrika Kusini bado zinakadiria gharama halisi ya kiuchumi kufuatia uporaji na ghasia zilizozoka baada ya kufungwa kwa rais wa zamani Jacob Zuma.

    Inakadiriwa kuwa athari za kiuchumi katika mkoa wa KwaZulu-Natal pekee ni ni zaidi ya dola bilioni moja za Kimarekani.

    Waziri katika ofisi ya rais amesema ghasia na uporaji uliathiri biashara 40,000 katika mkoa wa KwaZulu-Natal.

    Akinukuu data zilizotolewa na chama cha wamiliki mali nchini Afrika Kusini, Khumbudzo Ntshavheni alisema zaidi ya maduka 200 yaliporwa.

    Pia aliongeza kuwa bidhaa za thamani ya zaidi ya dola milioni moja zilipotea mjini Durban pekee.

    Mashine za 1,400 za kutoa pesa zililengwa katika uporaji huo ulisababisha kuharibiwa kwa maduka 90 ya kuuza dawa.

    Hii haijumuishi uharibifu uliofanyika Johannesburg - ambao bado unaendelea kukadiriwa.

    Umasikini na ukosefu wa ajira vimechangia pakubwa uporaji huo.

    Hali ingelikuwa mbaya zaidi laiti kazi zingeliathiriwa na vurugu hizo, anasema Waziri.

    Soma zaidi:

  10. Chadema kitakwenda mahakamani Alhamisi kushinikiza Mbowe aachiliwe au ashitakiwe

    Mkurugenzi wa mawasiliano na itifaki wa mambo ya nje wa chama cha upinzani cha Chadema John Mrema, amesema watakwenda Mahakama kuu kushinikiza Kiongozi wa chama hicho aachiliwe au ashitakiwe.

    Akizungumza na BBC Bw Mrema amethibitisha kukamatwa kwa Bw Freeman Mbowe katika chumba chake cha hoteli jijini Mwanza.

    ''Jana majira ya saa nane usiku akiwa hotelini kwake, hoteli alimofikia Mwanza, Jeshi la polisi walizingira hoteli kumtaka atoke,wakamkamata yeye pamoja na viongozi wengine 11 kwa hiyo jumla walikamatwa watu 12.Wakawekwa kwenye gari hili la kawaida la polisi wakapelekwa kwenye kituo cha polisi cha kati Mwanza, wale wengine wakashushwa wakapelekwa kwenye kituo cha polisi cha kati Mwanza, gari zilikuwa mbili za polisi za Landcruiser ila yeye hawakumshusha na badala yake wakaenda naye haijulikani amepelekwa wapi.

    Anasema Polisi hawakuripoti kumkamata Bw mbowe, ila walisema kuwa wanawashikilia watu 11 na wa kumi na mbili Mbowe hawakumtaja.

    Bw Mrema anasema kuwa Bw Mbowe hayuko kwenye kituo chochote cha polisi Mwanza na simu yake imezimwa.

    ''Taarifa iliyotolewa muda mfupi uliopita na polisi kuhusiana na watu 11 ambao imesema imewakamata wamesema

    Polisi haijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa za kukamatwa kwake.

    Maafisa kutoka chama chake wanasema kuwa hadi sasa hawajaweza kubaini anashikiliwa kwenye kituo kipi cha polisi.

    Kulingana na taarifa ya Chadema iliyotumwa kupitia akaunti yake ya Twitter, Bw Mbowe amekamatwa pamoja na wanachama wengine 10 wa chama hicho.

    Tunaendelea kufuatilia taarifa hii, hususan kauli kutoka kwa polisi juu ya taarifa za kukamatwa kwa kiongozi wa Chadema Bw freeman Mbowe

    Kauli za hivi karibuni za Bw Mbowe

    Mwanzoni mwa wiki hii kiongozi wa Chadema Freeman Mbowe alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alilalamikia kukamatwa kwa wafuasi wa chama hicho na polisi, pamoja na suala la mabadiliko ya katiba.

    Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kimesema hakitaendelea kumpigia magoti Rais wa nchi hiyo, Samia Hassan Suluhu kuhusu mustakabali wa taifa hilo, Bw Mbowe aliwaambia waandishi wa habari hivi Jumatatu.

    Mwenyekititi huyo wa CHADEMA, aliyasema hayo kufuatia Jeshi la Polisi la nchi hiyo kuwakamata viongozi, wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi wa dini 38 waliokuwa wahudhurie mkutano wa chama hicho kupitia baraza lake la vijana (BAVICHA) wenye lengo la kuhamasisha kupatikana kwa katiba mpya ya nchi hiyo.

    Mara baada ya kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu, Rais Samia alitangazia umma dhamira yake ya kukutana na wapinzani ili kuzungumzia maswala mbalimbali ikiwemo ya kisiasa na namna gani ya kuendesha shughuli za siasa.

    Licha ya kukutana na makundi mengine kama vijana, wazee na wanawake mpaka sasa Rais Samia hajakutaa na wapinzani. ‘‘Hatuwezi kuendelea na ule utaratibu wa zamani, tuna haki ya kukutana tunakamatwa, tunapigwa, tunashitakiwa, tunasoteshwa mahakamani miaka miwili miaka mitatu, kisha tunaachiwa huru, ama tunahukumiwa vifungo batili tukikata rufaa sote tunashinda’, alisema Mbowe

    Pamoja na polisi kuzuia mkutano huo uliokua ufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Boma wiki hii na kukamata watu hao 38, Kiongozi huyo wa Upinzani alisema, mkutano upo pale pale na utafanyika wiki hii na kama kukamatwa wako tayari kukamatwa wote.

    Kama wanataka kuwaweka ndani wanachadema kwenye hoja hii ya katiba, wapanue kwanza na magereza, kwa sababu tuko tayari wote tuwekwe ndani , na wala hatutaomba dhamana’ alisema Mbowe kabla ya kulaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mwanza, kuwakamata viongozi wa dini na wafuasi wa chama hicho .

  11. Morocco ilijaribu kudukua simu ya Macron

    Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinasema kuwa huduma za usalama za Morocco zilifanya udukuzi wa simu ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa kutumia waya wa udukuzi uliotengenezwa nchini Israeli -Pegasus spyware.

    Makundi ya kutetea haki za binadamu Forbidden Stories na Amnesty International yanasema kuwa Rabat ilitambua simu ambayo Rais Macron amekuwa akiitumia tangu mwaka 2017.

    Haijafahamika wazi iwapo waya huo wa Pegasus uliwahi kutumiwa.

    Mawaziri kadhaa pia walidaiwa kufuatiliwa, akiwemo waziri mkuu wa zamani Edouard Philippe.

    Namba zao za simu zilikuwa miongoni mwa namba 50,000 ambazo zilikuwa zimezoorodheshwa kati ya namba zinazoweza kudukuliwa .

    Ripoti hiyo ilisema kuwa ufuatiliaji wa kidigitali wa nyaya za udukuzi wa Pegasus ulikuwepo kwenye makumi ya nambari hizo za simu.

    Watengenezaji wa Pegasus, NSO Group, wanasema huuza kifaa hicho kwa serikali zilizochunguzwa kwa ajili kukabiliana na uhalifu na ugaidi.

  12. Rais wa Mali asema jaribio la kumuua ni ‘sehemu ya kazi yangu’

    Rais wa Mali amepuuzilia mbali jaribio la kumuua lililofanyika ndani ya Msikiti wakati wa sala ya Eid al-Adha – akisema kuwa"Ni sehemu ya kuwa kiongozi".

    "Kila kitu kiko sawa. Hakuna tatizo," Assimi Goïta aliwambia waandishi wa habari, saa kadhaa bada ya wanaume wawili kumshambulia katika msikiti mkuu wa wa Grande Mosque uliopo katika mji mkuu Bamako.

    Mmoja wa washambuliaji hao alikuwaamejihami kwa kisu, kulingana na ripoti, na alijaribu kumdunga rais.

    Hatahivyo, alishindwa kumjeruhi Kanali Goïta, ambaye aliongoza jeshi kuchukua malaka ya nchi mwezi Agosti mwkaa jana, na wakakamatwa maramoja.

    "Ni sehemu ya kuwa kiomngozi," alisema rais huyo wa mpito na kuongeza kuwa. "Kuna watu kila mara ambao hawajafurahi, kuna watu ambao wakati wowote wanaweza kujaribu kufanya mambo kuyumbisha, kujaribu kufanya vitendo tofauti.

    "Ninataka kuwahakikishia watu na kusema kuwa niko vyema, hakuna shida, hakuna aliyejeruhiwa na hali ilishugulikiwa ."

  13. Hujambo na karibu kwa matangazo haya mubashara leo Jumatano tarehe 21.07.2021