India yaripoti visa karibu 9,000 vya ugonjwa usiokuwa wa kawaida
India imeripoti zaidi ya visa 8,800 vya ugonjwa hatari wa "kuvu nyeusi" huku nchi hiyo ikikodolea macho janga la magonjwa.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Waasi washambulia Rwanda ‘kutoka Burundi’
Jeshi la Rwanda limesema waasi wa FLN wameshambulia eneo la kusini magharibi mwa nchi hiyo usiku wa Jumapili kutoka Burundi.
Katika taarifa, Jeshi la Rwanda lilisema wawili kati ya waasi hao waliuawa, na silaha pamoja na sare mbili za jeshi la Burundi kunaswa kabla “wavamizi kutorokea Burundi”.
Msemaji wa jeshi la Burundi ameiambia BBC kwamba hawezi kuangazia taarifa iliyotolewa upande wa Rwanda muda mfupi baada ya kutolewa kwake.
Shambulio hili linakuja wakati mamlaka wa nchi zote mbili zikijizatiti kurejesha uhusiano uliogubikwa na taharuki za kisiasa na makabiliano machache ya kijeshi maeneo ya mpakani tangu kutibuka kwa jaribio la mapinduzi ya mwaka 2015 nchini Burundi.
Mamlaka katika nchi zote mbili zinalaumiana kwa kuunga mkono waasi wanaotishia usalama wa kitaifa.
Mkutano wa vyama vya upinzani vilivyo na makao ya nje ya nchii, MRDC,uliwahi kusema kwamba National Liberation Front (FLN) ni mrengo wao wa kijeshi, ambao ulishambulia Rwanda mwaka 2018 na 2019.
Paul Rusesabagina, naibu rais wa MRCD, pamoja na wasemaji walili wa zamani wa FLN walikamatwa mwaka 2019 na 2020, kwa sasa wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi katika mahakama za Rwanda.
Video hizi hazionyeshi mlipuko wa Mlima Nyiragongo,
Video zisizo na uhusiano wowote na mlipuko wa Mlima Nyiragongo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimekuwa zikisambazwa sana na watu mtandaoni wakidai kimakosa kwamba zinahusiana na tukio hilo.
Moja ya video zilizosambazwa sana inaonyesha mlipuko katika Mlima Fagradalsfjall nchini Iceland miezi miwili iliyopita.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ilichukuliwa na kupakiwa mtandaoni kwenye Instagram na Joe Shutter.
Video nyingine inayoonyesha lava ikitiririka na kumwagika kupitia ua wa nyaya na kisha kwenye mwinamo kwenye ukingo wa barabara imesambazwa sana pia.
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Haihusiani na DR Congo kamwe bali inaonyesha lava kutoka volcano ya Kilauea, Hawaii ikitiririka kwenye mji wa Pahoa mwaka 2014.
Kuna picha hii ambayo imesambazwa sana, watu wakidai inaonyesha mlipuko wa mlima wa Nyiragongo na nyuma yake kwamba inaonyesha jiji la Goma.
Ruka X ujumbe, 3Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Picha hii ilipakiwa mtandaoni zaidi ya miaka mitano iliyopita na inaonyesha mlipuko katika Mlima Etna katika eneo la Sicily, Italia.
Mtandao mmoja wa habari nchini DR Congo ulitumia picha hiyo kwenye taarifa kuhusu volcano na mji wa Goma Septemba mwaka jana, lakini waliandika vyema kwamba ilikuwa picha kiashiria.
India yaripoti visa karibu 9,000 vya ugonjwa usiokuwa wa kawaida

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, India imeshuhudia maelfu ya maabukizi ya ''Black Fungi'' India imeripoti zaidi ya visa 8,800 vya ugonjwa hatari wa "kuvu nyeusi" huku nchi hiyo ikikodolea macho janga la magonjwa.
Ugonjwa huo usiokuwa wa kawaidi, unajulikana kama mucormycosis, huua hadi asilimia 50 ya wagonjwa, huku wengine wakiponea kifo baada ya kutolewa jicho moja.
Lakini katika miezi ya hivi karibuni, India imeshuhudia maelfu ya maabukizi ya ugonjwa unayowaathiri waliougua corona na wanaopona.
Madktari wanasema kuna uwezekano ugonjwa huo unatokana na dawa aina ya steroid inayotumiwa kutibu corona. Wanaougua maradhi ya kisukari wamo hatarini zaidi.
Madaktari wameiambia BBC kwamba ugonjwa huo unamshambulia mtu kati ya siku 12 hadi 18 baada ya kupona corona.
Maelezo zaidi:
Mji ambao wasioolewa wananyimwa kupangishwa nyumba

Chanzo cha picha, AYODELE JOHNSON
Wanawake wasio na waume wanabaguliwa na wamiliki wa nyumba za kupangisha mjini Lagos, lakini hakuna changamoto inayokosa ufumbuzi.Soma zaidi
Nigeria yawasaka wasafiri 90 waliokiuka masharti ya corona

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Wasafiri hao waliwasili kutoka nchi zilizowekewa vikwazo vya usafiri Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa watu 90 wanatafutwa kwa kukiuka kanuni za karantini zilizowekwa kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.
Watu hao wanajumuisha Wanigeria 63 na raia 27 wa kigeni waliongia nchini humo kati ya tarehe 8 na 15 mwezi Mei ambao wanaripotiwa kukataa kufanyiwa vipimo vya corona na uchunguzi zaidi.
Taarifa iliyotolewa na kamati iliyoteuliwa na rais kushughulikia ugonjwa wa COVID-19,inasema watuhumiwa wanakabiliwa na vikwazo, vinavyojumusha kupigwa marufuku ya usafiri kwa maka mmoja; kufutwa kwa visa zao na vibali kwa raia wa kigeni na kushtakiwa.
Iliongeza kuwa watu hao ni tisho kwa usalama wa afya ya umma kwani wamekwepa masharti ya karantini ya siku saba iliyowekwa kwa Iwatu wanaowasili kutoka nchi zilizowekewa vikwazo vya usafiri na kuwaagiza wasafiri kujiwasilisha katika vituo vya afya vya umma ndani ya saa 48 ili kufanyiwa uchunguzi haraka iwezekanavo.
Mapema mwezo huu, Kamati hiyo ya ushauri wa rais ilitoa ilani ya usafiri kwa wasafiri wanaowasili nchini Nigeria kutoka Brazil, India na Uturuki.
Wasafiri kutoka nchi hizo tatu walitakiwa kkuenda karantini ya lazima na kufanyiwa vipimo vya kubaini hawana maambukizi ya corona.
Watu 15 wathibitishwa kufariki katika mlipuko wa volkano DRC

Chanzo cha picha, AFP
Takriban watu 15 wamethibitishwa kufariki kutokana mlipuko wa volkano uliotokea katika Mlima wa Nyiragongo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) lakini huenda idadi ya vifo ikaongezeka wakati maafisa wakiyafikia maeneo yaliyoathirika zaidi.
Volkano ililipuka katika mlima Nyiragongo una kumwaga uji uji wa moto ama lava uliolifanya anga kuwa jekundu Jumamosi, lakini lava hiyo haikufika katika mji wa Goma unaokaliwa na watu milioni mbili kusini mwa mlima huo.
Wakazi wa vijiji vya karibu na mlima huo pamoja na mji Goma ambao waliyakimbia makaazi yao kwa hofu ya mlipuko huo wameanza kurejea huku wengi wao wakiwasaka jamaa zao waliopotea.

Chanzo cha picha, AFP
Watu tisa miongoni mwa waliothibitishwa kufa, walipoteza maisha katika ajali za barabarani wakati watu walipokuwa wakihaha kukimbia ili kuokoa maisha yao.
Wanne walikufa walipokuwa wakijaribu kutoroka gerezani huku wawili wakiungua hadi kufa, alisema msemaji wa serikali Patrick Muyaya Jumapili.
Zaidi ya watoto 170 wanahofiwa kupotea na wengine 150 wametengana na familia zao, kulinga na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) ambalo linasema litaweka vituo vya kuwapokea watoto watakaopatikana wakiwa peke yao.
Lava iliishia karibu na wilaya ya Buhene, viungani mwa mji wa Goma na kuangamiza mamia ya nyumba na hata majengo makubwa. Ukarabati unatarajiwa kuchukua miezi kadhaa.

Chanzo cha picha, AFP
"Nyumba zote zilizopo katika wilaya ya Buhene zimeungua," Innocent Bahala Shamavu aliliambia shirika la habari la kimataifa la Associated Press.
Kwengineko, lava ilikatiza katika moja ya barabara kuu inayounganisha Goma na mji wa Beni, ambayo ni njia muhimu ya usambazaji wa misaada.
Hata hivyo, uwanja wa ndege wa wa mji wa Goma haukuguswa na lava, kinyume na ripoti za awali kwamba uliathiriwa.
Mlima huo wa volkano uliopo kilomita 10 (maili sita) kutoka Goma, ulilipuka mara ya mwisho mwaka 2002 na kusababisha vifo vya watu250 huku watu wengine 120,000 wakiachwa bila makazi.
Mlipuko wa volkano uliosababisha vifo zaidi ulitokea mwaka 1977, ambapo watu 600 waliuawa.
- Mlima Nyiragongo: Volkano iliyolipuka yasababisha watu kukimbia makazi yao DRC
- Je ingewezekana tahadhari ya mlipuko wa volcano kutolewa mapema?
Mwanamuziki wa Rwanda Médard Jobert Ngabo maarufu Meddy apata jiko,

Chanzo cha picha, Meddy Instagram
Maelezo ya picha, Meddy na mke wake Mimi Mehfira Mwanamuziki wa Rwanda Médard Jobert Ngabo maarufu Meddy amefuinga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi Mimi Mehfira mwenye asili ya Ethiopia mwishoni mwa Juma.
Sherehe za harusi ya Meddy aliyepata umaarufu kutokana na nyimbo kama Slowly na Holly spirit zilihudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wanamuziki nyota kutoka Rwanda.
Sherehe hizo zilifanyika katika mji wa Dallas, Texas Marekani ambako Meddy na mkewe wanaishi.
Soma zaidi:

Chanzo cha picha, Meddy Instagram

Chanzo cha picha, Meddy Instagram
Maelezo ya picha, Sherehe hizo zilifanyika katika mji wa Dallas, Texas Marekani Jeshi la Msumbiji 'latibua shambulio jipya Palma'

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji wa Cabo Delgado umekumbwa na ukosefu wa utulivu kwa muda mrefu Majeshi ya Msumbiji yamezima jaribio la mashambulizi mapyakutoka kwa wanamgambo wa Kiislamu katika mji wa kaskazini wa Palma, kwa mujibu wa Rais Filipe Nyusi.
Palma iko karibu na mradi mkubwa wa gesi unaoendeshwa na kapuni kubwa ya kawi ya Total ya Ufaransa.
Mwezi Machi, mamia ya wanamgambo walio na mafungamano na kundi la Islamic State (IS) walivamia mji huo katika shambulio lililosababisha vifo vya makumi ya watu.
Rais alisema tukio la wikendi lilihusisha jaribio la wanamgambo wakijaribu kuvamia kijiji cha Lumbi, Wilaya ya Palma. Aliongeza kuwa wanamgambo hao waliwaua wenzao watano waliojaribu kujiondoa.
- Msumbiji: Je, Cabo Delgado ni kituo cha wapiganaji wa Islamic State?
- Tanzania: 'Tunapolinda mipaka yetu tusitafsiriwe kama tunawazuia wakimbizi'
Bw. Nyusi alitoa tamko hilo katika mkutano wa chama tawala cha Frelimo uliofanyika Matola, Mkoa wa Maputo.
Alisema serikali yake iki tayari kuunga mkono msaada wa kigeni kukabiliana na wanamgambo kaskazini mwa nchi hiyo "hakuna mtu anayepaswa kujiona ana kinga au anaweza kupambana na ugaidi peke yake".
Marekani yaiwekea vikwazo Ethiopia juu ya mzozo wa Tigray

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Maelfu ya watu wameuawa na wengine kadhaa kuachwa bila makao tangu mzozo ulipozuka miezi sita iliyopita. Marekani imeweka vikwazo kadhaa vya kiuchumi na usaidizi wa kiusalama dhidi ya Ethiopia kufuatia mzozo wa eneo la Tigray.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, pia ametangaza marufuku ya usafiri dhidi ya maafisa wa Ethiopia na Eritrea pamoja na wengine ambao wanatuhumiwa kufanya ukatili.
Bw. Blinken amesisitiza kuwa hatua ya kimataifa inahitajika ili kusaidia katika utatuzi wa mzozo huo na kuongeza wale waliopewa dhamana hawajachukua hatua madhubuti kukomesha ghasia.
Maelfu ya watu wameuawa na wengine kadhaa kuachwa bila makao tangu mzozo ulipozuka miezi sita iliyopita.
Pande zote mbili zimelaumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.
Mapema siku ya Jumapili serikali ya Ethiopia ilipuuzilia mbali madai kwamba raia katika Jimbo lililokumbwa na vita la Tigray, walilengwa kwa silaha za kemikali kutoka kwa majeshi ya Ethiopia au Eritrea.
Gazeti la Telegraph la Uingereza limeripoti kuwa watu kadhaa walichomeka vibaya kutokana na utumizi ya phosphorous nyeupe. Kemikali ambayo inaweza kutumika kihalalli vitani lakini ikitumiwa dhidi ya raia inasadikiwa kuwa uhalifu wa kivita.
Gazeti hilo limesema miongoni mwa waathiriwa ni mtoto wa kike wa miaka 13 ambaye alichomeka baada ya nyumba yao kushambuliwa mwezi uliopita .
Wizara ya Mambo ya nje ya Ethiopia imeelezea madai kwamba silaha za kemikali zilitumiwa dhidi ya watu wa Tigray kuwa mabaya na ya kutowajibika.
Maelezo zaidi:
- Mzozo wa Tigray: Jukumu la Eritrea katika mzozo wa Ethiopia
- Mzozo wa Tigray Ethiopia: Mataifa yenye nguvu za kiuchumi duniani yakemea 'ukiukaji wa haki za binadamu'
Hujambo na karibu katika matangazo mbashara leo Jumatatu 24.05.2021
