ICC yamhukumu kiongozi wa zamani wa LRA Dominic Ongwen kifungo cha miaka 25

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC imemhukumu kifungo cha miaka 25 kiongozi wa zamani wa waasi wa Lord's Resistance Army nchini Uganda Dominic Ongwen.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya mubashara. Hadi kesho panapo majaaliwa, asante

  2. Akanusha mashitaka ya mauaji ya kimbari ya Rwanda akidai alikuwa 'mjamzito'

    Munyeyezi

    Mwanamke aliyefukuzwa Marekani na kurejeshwa nchini mwao Rwanda, amekanusha mashitaka ya makosa ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 – akisema alipata ujauzito muda mfupi baada ya kujifungua mapacha.

    “Kuwa na mapacha na kuwa mjamzito, ningewezaje kushiriki kwenye mauaji ninayodaiwa kutekeleza?” ameiambia mahakama.

    Béatrice Munyenyezi anakabiliwa na mashitaka saba ya mauaji – yenye kuhusishwa na uhalifu kuanzia mauaji hadi ubakaji.

    Kulingana na ushahidi uliotolewa wakati wa kusikiliza kwa kesi ya mume wake na mama mkwe wake katika mahakama ya Umoja wa Mataifa huko Arusha, Tanzania, Bi. Munyenyezi alishutumiwa kwa kusimama katika vituo vya ukaguzi barabarani kubaini raia wa Kitutsi ili wauawe na kuhamasisha wanamgabo wa Kihutu kubaka wanawake kabla ya kuwaua huko Butare, mji wa kusini mwa Rwanda.

    Akishtumiwa kwa kuwa mwenye ushawishi katika mauaji ya wanafunzi wa Kitutsi mjini humo, Bi. Munyenyezi amekanusha madai hayo akisema alikuwa mgeni na hakuwa ameenda kwenye vituo vya ukaguzi barabarani.

    Anasema aliwasili Butare Julai 1993 na kuolewa akiwa na ujauzito wa miezi miwili, akajifungua mapacha na muda mfupi baada ya hapo akapata tena ujauzito mwingine.

    Wakati wa kusikilizwa kwa ombi la kuachiwa kwa dhamana Jumatano, akiwakilishwa na mawakili wawili maarufu nchini Rwanda, alikanusha madai yote, amesema mwandishi wa

    Pia alishutumu baadhi ya mashahidi katika mahakama ya Arusha kwa kusema uongo kuwa walisoma naye Chuo Cha Taifa cha Rwanda kabla ya kutokea kwa mauaji ya kimbari wakati yeye “alikuwa hata hajamaliza shule ya sekondari”.

    Mwaka 2011, Arsène Shalom Ntahobali – Mume wa Munyenyezi – na mama mkwe wake Pauline Nyiramasuhuko, aliyekuwa waziri wa masuala ya wanawake, walikuwa mwanamke wa kwanza na kijana wake kupatikana na hatia ya mauaji yaliyotekelezwa Butare wakati wa vita vya kimbari mwaka 1994.

    Wawili hao wanahudumia kifungo cha miaka 47 nchini Senegal.

    Mahakama itatoa uamuzi wake Jumatatu juu ya ombi la kuachiwa kwa dhamana lililowasilishwa na Bi. Munyenyezi.

  3. Somalia yatangaza kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Kenya,

    Rais wa Farmajo na mwenzake Uhuru wa Kenya

    Chanzo cha picha, VILLA SOMALIA

    Somalia imetengaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo mwezi Desemba mwaka jana ikiishutumuj Kenya kwa kuingilia siasa zao za ndani.

    Naibu waziri wa habari wa Somalia Abdirahman Yusuf amesema sasa mahusiano ya kati ya nchi hizo mbili yamefufuliwa akiongeza Qatar ndiyo iliyoasaidia mchakato wa upatanisho.

    Serikali ya Kenya haijatoa tamko kuhusiana na tangazo hilo la Somalia ila Ikulu ya Rais ya Nairobi iliandika katika ukurasa wa Twitter leo kuwa Rais Uhuru Kenyatta amekutana na Mfalme wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na kupokea kile kilichotajwa ujumbe maalum.

    • Uhusiano unaoundwa kati ya Kenya na Somaliland una maana gani?
    • Kenya yajiondoa katika kusikilizwa kwa mzozo wake wa majini na Somalia
  4. Wahanga wa uhalifu wa kivita wa Uganda 'wanahitaji kufanyiwa mengi zaidi'

    For some Ugandans, finding any sense of closure is still proving hard

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wakili wa masuala ya haki nchini Uganda Sarah Kihika Kasande amesema hukumu ya Alhamisi dhidi ya Dominic Ongwen imetuma ujumbe kuwa wahusika wa uhalifu watawajibishwa.

    Bi Kasande pia ameiambia kituo cha televisheni cha NBS kwamba mengi zaidi yanahitajika kufanywa kuwasaidia wahanga wa uhalifu wa kivita kaskazini mwa Uganda.

    "Wahalifu waliosalia wanastahili kuwajibishwa kitaifa au kimataifa kwasababu Ongwen hakutekeleza uhalifu huo peke yake," alisema.

  5. Kwanini jaji mmoja alitofautiana na wenzake juu ya hukumu ya Ongwen

    Dominic Ongwen.

    Mmoja wa majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC Jaji Bertram Schmitt ameelezea jinsi mahakama ilivyofikia uamuzi wa kumfunga kifungo cha miaka 25 r rebel kamanda wa waasi Dominic Ongwen.

    Amesema uamuzi huo haukuwa wa pamoja.

    Jaji Raul Cano Pangalangan alikuwa amependekeza kifungo cha miaka 30- jela, akisema mazingira ya utotoni ya Bw. Ongwen haistahili kugubika mateso waliopitia waathiriwa.

    Jaji kiongozi baadaye alisema hukumu yakifungo cha miaka 25 ilifikiwa na majaji wengi.

  6. ICC yamhukumu kiongozi wa zamani wa LRA Dominic Ongwen kifungo cha miaka 25

    Dominic Ongwen

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC imemhukumu kifungo cha miaka 25 kiongozi wa zamani wa waasi wa Lord's Resistance Army,LRA Dominic Ongwen.

    Dominic Ongwen, anayefahamika kama White Ant, alipatikana na zaidi ya makosa 60 ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

    Waendesha mashtaka wanasema kuwa Bw. Ongwen amepewa adhabu ndogo kwasababu alikuwa ametekwa na LRA akiwa mtoto mdogo.

    Kundi hilo la waasi liliundwa zaidi ya miaka 30 iliyopita ikiendesha shughuli zake nchini Uganda na mataifa jirani.

    Dominic Ogwen alizaliwa mwaka 1975

    Chanzo cha picha, AFP

    Dominic Ogwen ni nani?

    Dominic Ogwen alizaliwa mwaka 1975 katika kijiji cha Choorum wilaya ya Amuru kaskazini mwa Uganda.

    Alitekwenyara na kundi la waasi wa Josephy Kony akiwa mvulana mdogo wakati akielekea shule ya msingi Abili Koro, kulingana na maelezo yake alidai alitekwanyara mwaka 1988 akiwa na umri wa miaka 14.

    Lakini ripoti sahihi zinasemekana alitekwanyara akiwa na umri wa miaka 9 au 10.

    Kwani alibebwa katika safari yao hadi kwenye kambi ya LRA, alikuwa hawezi kutembea.

    Waasi wa LRA

    Chanzo cha picha, AFP

    Mama yake Ogwen alipofahamishwa habari za kutekanywara kwa mtoto wake aliamuwa kuwafata wafuasi hao, na badaye watu walimkuta mama huyo amefariki pamoja na mumewe.

    Baada ya muda akiwa na umri wa miaka 18, Ogwen alipewa cheo cha Brigadier wa kundi la waasi wa LRA na kuongoza kikosi cha Sinia.

    Ogwen alishirika katika matukio mbalimbali ya uhalifu wa kivita mwezi wa Mei mwaka 2004 walishambulia kambi ya ndani ya Lukodi wilayani Gulu kaskazini mwa Uganda.

    Pia alishambulia kambi nyingine za ndani ikiwemo ya Pajule, Odeke na Abok na kushiriki mauaji mbalimbali ya wanchi wasiokuwa na hatia , ubakaji na unyanyasaji wa kigono.

  7. Rais Paul Kagame azungumza na kaka wa Mahamat Idriss Déby,

    Kagame

    Chanzo cha picha, RWANDA PRESIDENCY

    Rais Paul Kagame amempokea kwa mazungumzo Abdelkerim Déby Itno kama mjumbe maalum na mkuu wa ofisi ya rais wa Baraza la Jeshi la Mpito nchini Chad, kulingana na ofisi ya Rais wa Rwanda.

    Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu mazungumzo hayo ya Jumatano jioni.

    Bwana Kagame anajulikana kama mmoja wa wale ambao walikuwa na uhusiano mzuri na makubaliano juu ya maswala yanayohusu bara la Afrika na Rais wa zamani wa Chad Idriss Déby Itno.

    Utawala wa kijeshi nchini Chad sasa unatishiwa na shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa na Jumuiya ya Afrika kutaka wanajeshi warudishe madarakani kwa raia.

    Barala kuu la kijeshi linaloongoza Chad pia liko kwenye vita na vikundi vya waasi,ikiwa ilidaiwa kuwa Rais wa zamani Idriss Deby Itno alipigwa aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akipigana kwenye vita hivyo mwezi uliopita.

    • Mfahamu Jenerali Mahamat Kaka mtoto wa Déby aliyerithi madaraka ya Chad
    • Idriss Déby: Suitafahamu yaikabili Chad baada ya rais wake kufariki vitani

    Rais Kagame alipokea ujumbe wa Chad akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Vincent Biruta na Meja Jenerali Joseph Nzabamwita, mkuu wa idara ya ujasusi (NISS).

    Kwenye mitandao ya kijamii, wengine walisema kuwa kuonekana kwa Abdelkerim Idriss Déby kama balozi wa kaka yake mkubwa Jenerali Mahamat Idriss Déby ilikuwa ishara kwamba "familia ya Déby inaendelea kuimarisha utawala wake’’ Kabla na baada ya kifo cha mzee Déby, kuliripotiwa malumbano kati wanawe kuhusu atakayemrithi.

    Abdelkerim Idriss Déby, 29, alihitimu kutoka Chuo cha Jeshi cha Marekani (USMA) huko West Point mnamo 2015. Mnamo mwaka wa 2019 aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa ikulu ya Rais wa Chad.

    Mnamo mwaka wa 2020, aliongoza ujumbe wa Chad uliokutana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kujadili "kufungua" ubalozi wa Chad mjini Jerusalem.

  8. Malkia wa Zulu kuzikwa katika sherehe ya faragha

    Zulu people in traditional attire mourned the queen

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Watu wa Zulu wakiwa wamevalia nguo za kitamaduni kumuomboleza Malkia

    Malkia wa Zulu, Mantfombi Dlamini Zulu, anatarajiwa kuzikwa katika sherehe ya faragha mkoani KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.

    Alifariki ghafla mjini Johannesburg wiki iliyopita, karibu mwezi mmoja baada ya kifo cha mume wake, Mfalme Goodwill Zwelithini.

    Familia haijatangaza hadharani chanzo cha kifo chake.

    Licha ya sherehe kubwa, wasichana wa Kizulu waliofuata na mwili wa Malkia Mantfombi kurudi ikulu yake Jumatano jioni.

    Uamuzi wa atakayeongoza ufalme wa Zulu unatarajiwa kutolewa baada ya mazishi.

    Maelezo zaidi:

  9. Watekaji nyara wawachilia wanafunzi 27 Nigeria

    Kuachiwa huru kwa wanafunzi hao kunakuja siku moja baada ya familia zao kuandamana

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Kuachiwa huru kwa wanafunzi hao kunakuja siku moja baada ya familia zao kuandamana

    Wanafuzi 27 waliokuwa wametekwa kutoka taasisi ya misitu katika Jimbo la Kaduna Kaskazini mwa Nigeria wameachiwa huru.

    Walikuwa miongoni mwa wanafunzi 39 waliyotekwa kutoka katika chumba zao za malazina genge la wahalifu waliokuwa wamejihami kwa silaha mwezi Machi.

    Mamlaka zinasema wahasiriwa walioachiwa huru siku ya Jumatano watafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu baada ya kuzuiliwa kwa muda zaidi tangu visa vya utekaji dhidi ya wanafunzi kwa lengo la kuitisha kikombozi kuongezeka katika miezi ya hivi karibuni.

    Kuachiwa huru kwa wanafunzi hao kunakuja siku moja baada ya familia zao kuandamana nje ya bunge la taifa mjini Abuja kushinikiza mamlaka kuingilia kati suala hilo.

    Kiongozi mashuhuri wa Kiislamu ambaye amekuwa akiongoza juhudi za mazungumzo na magenge ya wahalifu wenye silaha Sheikh Ahmad Gumi ameiambia BBC kwamba yeye na Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo waliingilia kati ili kuachiliwa kwa wanafunzi hao. Haijulikani ikiwa fidia ililipwa.

    Nigeria imeshuhudia ongezeko la visa vya utekaji nyara wanafunzi tangu mwezi Disemba huku hali ya usalama ikiendelea kudorora maeneo tofauti nchini.

    Zaidi ya wanafunzi 800 wametekwa huku baadhi yao wakiachiliwa huru baada ya kikombozi kulipwa.

    • Shambulio la shule Nigeria: 'Jinsi nilivyotoroka watekaji'
    • Wasichana zaidi ya 300 wa shule ya sekondari ya Zamfara watekwa nyara Nigeria
  10. Afisa wa ANC aliyefurushwa chamani 'amsimamisha kazi' Rais Ramaphosa

    ANC ilimtimua Bw Magashule siku ya Jumatatno

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, ANC ilimtimua Bw Magashule siku ya Jumatatno

    Ace Magashule, katibu mkuu wa chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini, ameJIBU hatua ya kutimuliwa kwake chamani kwa kumsimamisha kazi Rais Cyril Ramaphosa kama mkuu wa chama hicho.

    "Mimi pia, kwa kuzingatia mamlaka niliyopewa kama katibu mkuu wa ANC, na kwa kutii kikamilifu maazimio ya mkutano wa chama, namsimamisha kazi kwa muda rais wa ANC, Ndugu Cyril Ramaphosa, " Bw. Magashule alinukuliwa na vyombo vya habari akisema.

    Naibu katibu mkuu wa chama, Jessie Duarte, hata hivyo amesema Bw. Magashule hana mamlaka ya kumpatia rais barua ya kumsimamisha kazi na anaweza kufanya hivyo yeye binafsi bila uungwaji mkono wa chama.

    Bw. Magashule amesema atakata rufaa kupinga uamuzi wa kumfuza chamani "unaokiuka katiba" - na kusisitiza atasalia katika nafasi yake hadi rufaa hiyo itakapoamuliwa.

    ANC ilimtimua Bw Magashule siku ya Jumatatno na kuonya wanachama wengine wanaokabiliwa na mashtaka ya ufisadi kwamba watafuata mkondo huo endapo hawatajiuzulu ndani muda wa mwezi mmoja.

    Bw. Magashule amepinga mashtaka ya ubadhirifu, ufisadi na utakatishaji fedha yanayomkabili.

    Soma zaidi:

    • Cyril Ramaphosa - Kiongozi wa Afrika Kusini anayepania kukibakiza madarakani chama cha ANC
    • Cyril Ramaphosa ni nani?
  11. Marekani inazingatia kusambaza dawa za kupunguza makali ya Ukimwi zilizokwama Kenya

    Dawa za kupunguza makali ya Ukimwi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Marekani inapania kupeleka dawa za kupunguza makali ya Ukimwi ambazo zimekwama katika bandari ya Kenya katika nchi zingine zinazohitaji, ubalozi wake nchini Kenya unaesema.

    Dawa hizo ziliwasili nchini Kenya mwezi Januari na zimekwama katika bandari ya Mombasa kutokana na mzozo unaoendelea wa kodi na vibali.

    Ubalozi wa Marekani umesema unahofia muda wa mwisho wa matumizi ya dawa hizo,na huenda ikawa rahisi kupeleka dawa hizo katika nchi nyingine kutumika.

    Serikali ya Kenya iliondolea ushuru dawa hizo lakini afisa wa mamlaka uya ukusanyaji kodi amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema kwambabaadhi ya makontena bado zinasubiri kibali kutoka kwa shiriki la dawa.

    Afisa kutoka shirika la madawa anasema kibali kipya kinahitajika kuombwakwani ya awali inasema mpokeaji ni Shirika la Kenya la usambazaji madawa.

    Mfadhili, USAid,imepatia kampuni ya kibinafsi kusambaza dawa hiyo wakati serikali inataka shirika lake la usamazaji dawa kusimamia mpango huo.

    Zaidi ya watu milioni 1.5 wanaoishi na virusi HIV wanahitaji dawa hizo na zimekuwa zikitolewa kwa mgao katika vituo vya afya ili kikidhi mahitaji hayo kwa muda.

    • Kwa nini baadhi ya wazazi nchini Kenya huficha hali yao ya HIV?
    • Je mwanamke mjamzito mwenye virusi vya ukimwi anaweza kumnyonyesha mwanae?
  12. Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Alhamisi 06.05.2021.