Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tanzania wako huru kutumia tena twitter
Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania hii leo wanaweza kuingia katika mtandao wa Twitter bila kuruka kihunzi chochote.
Moja kwa moja
Esther Namuhisa
Rais Kenyatta awafukuza wakurugenzi wote wa bodi ya usambazaji wa dawa
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewafukuza kazi wakurugenzi wote wa bodi ya wakala wa usambazaji wa dawa.
Hatua hii imekuja baada ya KEMSA kukabiliwa na kashfa kadhaa miaka ya hivi karibuni – ikiwemo ya vifaa vya kujikinga na Covid-19.
Huku usambazaji wa dawa ukiainishwa kuwa miongoni mwa sababu zilizosababisha.
Kashfa ya hivi karibuni ilihusisha dozi elfu ishirini na nne ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi ambazo tayari zimeondolewa kwa umma.
Kenya imesitisha matumizi ya Nevirapine mwaka 2019 baada ya wagonjwa kuanza kuathirika na dawa hizo.
Wakala hao ni sehemu ya sababu ya kwanini zaidi ya dozi 200,000 za dawa ya anti-retroviral zimekwama katika ghala iliyopo Mombasa, miezi minne baada ya US-AID kutoa msaada.
Mwaka jana, KEMSA ilishutumiwa kutumia vibaya mamilioni ya dola kununua vifaa kinga vya Covid-19.
Hata hivyo wakala hao wanatarajiwa kurudisha imani kwa umma.
Na Bodi mpya inatarajiwa kuanza kazi wiki tatu zijazo.
Chuo kikuu cha Kenya chakanusha kutoa shahada ya uchawi
Chuo kikuu kimoja kilichopo mashariki mwa Kenya kimekanusha taarifa kuwa kinawaandikisha wanafunzi wa shahada ya uchawi.
Chuo kikuu cha Machakos kimesema taarifa hizo ni za uongo:
Makala iliyoandika katika blogu moja ya Kenya kuhusu kuanzishwa kwa kozi ya uchawi katika chuo hicho.
Suala hilo liliwafanya watu kuwaandikia chuo kikuu cha Machakos kutaka ufafanuzi zaidi kuhusu taarifa hiyo.
Kanisa laibiwa kengele Kenya
Kanisa moja nchini Kenya inawaomba watu kusaidia kutafuta kengele ya kanisa yenye uzito wa kilo 500 ambayo imeibiwa.
Kanisa la Bikira Maria la Orthodox lililopo Ngecha eneo la Kiambu, kaskazini mwa mji mkuu wa Kenya,Nairobi, limeviambia vyombo vya habari nchini humo pamoja na polisi kuhusu kupotea kwa kengele hiyo.
Gazeti la Kenya la Standard limeweka kwenye kurasa yake ya tweeter picha ya kengele iliyoibiwa:
Waumini wamelalamikia kuhusu marufuku ya kusitisha mikusanyiko ya kidini kwasababu ya janga la virusi vya corona kwani katazo hilo limesababisha wizi kuongezeka makanisani na kuwataka polisi kutoa ulinzi, The Standad imeripoti.
Kanisa limesema pia limepoteza chupa 10 za mvinyo , vifaa vya matangazo ya nje na vitu vingine hata kabla ya kuibiwa kwa kengele hiyo ya shaba.
Wachezaji mpira wa Zambia washambuliwa na mashabiki wa mpira wa DRC
Mchezaji mpira wa Zambia Kabaso Chongo anaugulia majeraha ya kichwa baada ya mashaiki wa timu ya DRC ya TP Mazembe kumshambulia siku ya Jumatano.
Mazembe walikuwa wanacheza na FC Sanga Balende huko Mbuji Mayi, nchini DR Congo,ambapo walipata ushindi kwa kuchelewa, jambo ambalo halikuwafurahisha mashabiki wa timu ya DRC.
Mashabiki walianza kuwapiga mawe na hivyo kuwaacha wachezaji wanne kujeruhiwa, akiwemo Chongo.
Twitter 'yafunguliwa' Tanzania
Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania hii leo wanaweza kuingia katika mtandao wa Twitter bila kuruka kihunzi chochote.
Mtandao huo ambao ulikiuwa sehemu ya mitandao ya kijamii iliyozuiliwa nchini humo muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 uliendelea kuminywa nchini humo hata baada ya mitandao mingine kufunguliwa baada ya uchaguzi.
Watu waliondelea kuutumia kwa kipindi chote cha kuminywa kwake ilibidi watumie njia ya mkato kwa kutumia programu tumishi za VPN.
Wakati Tanzania ilipochukua hatua hiyo mtandao wa Twitter uliandika kuwa "tunashuhudia mtandao wetu kuminywa Tanzania".
Twitter ilisema kufungwa kwa intaneti ni jambo lenye madhara na kuvunja haki za binadamu.
Wakati ilipofungiwa, watumiaji wengi walihusisha suala hilo la zuio la imitandao na uchaguzi mkuu.
Mpaka leo serikali ya Tanzania haikueleza kwa nini mitandao hiyo iliminywa.
Malawi kuondoa hukumu ya kifo
Mahakama kuu ya Malawi imeamua kuwa adhabu ya kifo ni kinyume cha katiba.
Mahakama imesema kuwa hukumu ya kifo ipo kinyume na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu,
Hii ikimaanisha kuwa adhabu kubwa zaidi itakayotolewa nchini Malawi itakuwa hukumu ya kifungo cha maisha.
Tume ya haki za binadamu imeelezea uamuzi huo kuwa hayo ni maendeleo.
Aidha ilibainika kuwa hakuna aliyenyongwa ncini humo tangu mwaka 1975.
Malawi sasa imekuwa nchi ya 22 ukanda wa mataifa ya -Sahara kusitisha adhabu ya kifo.
Msichana wa miaka 17 aiba mtoto kuokoa ndoa yake Tanzania
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania, msichana mmoja mkazi wa mkoa wa Geita bi. Anjelina Masumbuko mwenye umri wa miaka 17 anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga.
Inadaiwa kuwa, Anjelina aliamua kuchukua uamuzi huo ili kunusuru ndoa yake baada ya mume wake kutaka mtoto mara kwa mara na yeye kushindwa kuzaa.
Kamanda wa polisi mkoani Geita, Henry Mwaibambe ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa Anjelina alikamatwa Aprili 22, 2021 akiwa na mtoto huyo na kubainisha kuwa Machi 12, 2021 saa 2 usiku mtuhumiwa alimchukia mtoto wa Juliana Mlichades bila taarifa.
Inadaiwa baada ya Juliana kujifungua mtuhumiwa alijenga mazoea na mwanamke huyo akimsaidia shughuli mbalimbali na kwamba siku ya tukio, Juliana alimlaza mwanae ndani lakini aliporejea hakumkuta na alimtilia shaka mtuhumiwa huyo ambaye alikamatwa akiwa na mtoto huyo.
“Mtoto tulimpeleka hospitali akafanyiwa uchunguzi ana afya njema kabisa na amekabidhiwa kwa mama yake mzazi, Anjelina anaendelea mahojiano polisi na atafikishwa mahakamani wakati wowote,” amesema.
Ramaphosa: ANC ilishindwa kudhibiti rushwa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekiri kuwa chama tawala kilishindwa kudhibiti rushwa wakati wa utawala wa Jacob Zuma.
Amesema chama cha African National Congress (ANC) kingefanya zaidi kuzuia rushwa, akitoa ushuhuda wake kabla ya uchunguzi wa kisheria kufanyika juu ya madai ya rushwa ya wakati wa utawala wa bwana Zuma.
Ramaphosa amesema ANC haikuwapa raia wa Afrika Kusini kile ambacho walikuwa wanakitarajia kwa kuwajibika , wakati rushwa ilidhoofisha utawala wa sheria.
"Wote tunakubaliana kuwa taasisi ingeweza kufanya jitihada zaidi kuzuia utumiaji mbaya wa madaraka na matumizi mabaya ya rasilimali ," alisema.
Rais amezungumza kama mkuu wa tume ya ANC na anatarajia kuendelea kutoa ushahidi wake siku ya Alhamisi.
Mwanzo wa maelezo yake siku ya Jumatano, alisema ANC ingejaribu kutoa muangaza wa namna jambo hili lingechunguzwa ili wahusika wawajibike.
Bwana Zuma anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa ikiwemo ulaghai, mikataba ya uongo na utakatishaji fedha wakati akiwa madarakani kwa miaka tisa.
Ingawa alikanusha kuhusika katika madai.
Habari...Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kurasa ya BBC Swahili leo ikiwa Alhamisi tarehe 29/04/2021