Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mazishi ya kitaifa ya Rais Idris Deby yafanyika N'jamena

Mazishi ya kitaifa ya rais wa Chad Idriss Déby Itno yanafanyika Ijumaa katika mji mkuu wan chi hiyo N'Djamena kabla ya kuzikwa katika mkoa wake.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Chanjo mpya ya Malaria yaonesha ufanisi mkubwa

    Ufanisi wa chanjo mpya ya malaria iliyotengenezwa nchini Uingereza umefikia kiwango cha asailimia 77 katika kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

    Matokeo ya awali ya kipimo cha chanjo hiyo yanaonesha kuwa na ufanisi zaidi katika dozi mojaya chanjo.

    Chanjo hiyo mpya ilifanyiwa majaribio kwa watoto wachanga 450 nchini Burkina Faso.

    Kutakuwa sasa na upimaji wa watu wengi zaidi utakaowahusisha watoto takriban 5,000 kote barani Afrika.

    Mwandishi wa BBC anasema malaria huwauwa zaidi ya 400,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa ni wakazi wa maeneo ya kusini mwa jangwa la sahara.

  2. Wakenya wavamia tena mtandao wa IMF wakiilaumu kuikopesha nchi yao

    Kwa mara ya pili wiki hii, mtandao wa kijamii wa shirika la fedha duniani IMF umejipata ukivamiwa na ukosoaji kutoka kwa Wakenya,wanaolilaumu kwa kuendelea kuikopesha fedha nchi yao.

    Matangazo mubashara ya ukurasa wa Facebook ya IMFyalijazwa na maoni ya Wakenya ambao hawataki madeni Zaidi yatolewe kwa serikali, wengi wao wakisema pesa nyingi zitafanyiwa ubadhilifu nana maafisa wa taifa lao.

    Katika maoni yao, baadhi walielezea hofu kuhusumadeni ya umma ambayo yamefikia hadi dola bilioni 70 mwishoni mwa mwaka 2020.

    Matangazo hayo yaliongozwa na Kristalina Georgieva MkurugenziMkuu wa IMF Alhamisi usiku yaliyomalizika baada ya dakika 23.

  3. Kwa picha: Mazishi ya rais wa Chad katika Idris Deby

    Mazishi ya rais wa Chad idris Deby, aliyeuawa mapema wiki hii kutokanana majeraha aliyoyapata wakati wa mapigano ya waasi yanafanyika Ijumaa.

    Rais Deby, ambaye aliiongoza nchi hiyo kwa miaka 30, alifariki siku moja baada ya matiokeo ya uchaguzi kuonesha kuwa ndiye mshindi ambapo alikuwa anapanga kurejea tena madarakani kwa muhula wa sita.

    Mwanae wa kiume Mahamat Idriss Déby Itno, al maarufu Jeneral Kaka, ataongoza nchi kwa miezi 18 hadi uchaguzi utakapofanyika.

    Mazishi ya kitaifa ya hayati Deby yanafanyika katika mji mkuu N'Djamena.

  4. AU yalaani kurefushwa kwa muhula wa rais Somalia

    Muungano wa Afrika umelaani kurefushwa kwa muhula wa rais wa SomaliaMohamed Abdullahi Farmajo na unatuma mjumbe maalumu Mogadishu kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

    Baraza la Amani na Usalama la Muungano wa Afrika lilitoa tangazo lake baada ya saa kadhaa za mazungumzo ya faragha ambapo uliamua kupatanisha mzozo huo.

    Taarifa iliyotolewa baada ya kikao hicho Alhamisi ilizitaka pande zpote husika nchini Somalia "kufufua mara moja mazungumzo juu ya misingi ya makubaliano ya yaliyofikiwa Septemba 2020 ".

  5. Dkt. Agnes Kijazi: Kimbunga Jobo kinaweza kuathiri pwani ya bahari Hindi na Ziwa Victoria,

    Mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA ) na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi anasema kuwa Kimbunga Jobo kwa sasa kipo kilomita 236 kutoka kisiwa Cha mafia Mkoa wa Pwani nchini Tanzania.

    “Kimbuga hiki kwa sasa kipo kilomita 236 kutoka mashariki mwa kisiwa cha mafia, na kwa mwenendo huu kitaendelea kuja katika maeneo ya nchi yetu, mawingu yanaendelea kusogea.”

    Dkt. Kijazi ameongeza pia kwamba kimbunga hiki kinaweza kufikia ziwa victoria, kwani dalili za mawingu zimeanza kuonekana upande wa ziwa Victoria.

    Kimbunga hiki kinatarajiwa kufika maeneo ya nchi kavu au mwambao wa pwani ya bahari nchini Tanzania , kuanzia tarehe 25. Na maeneo yatakayo athiriwa ni Lindi, Mtwara, Pwani,Dar es salaam Unguja na ziwa Victoria.

    Kwa upande wa athari zitakazo tarajiwa Dkt. Kijazi amesisitiza kuwa watu wanaofanya shughuli katika bahari kama wavuvi wachukue tahadhari dhidi ya kimbunga hiko. lakini pia wakazi wa Maeneo ya pwani ya bahari, kwasababu kunatarajiwa kuwa na mvua pamoja na upepo mkali

    “Athari ambazo zinatarajiwa ni upepo mkali baharini pamoja na mawimbi makala, lakini pia kikitua nchi kavu upepo mkali utakuwepo nchi kavu, mara nyingi vimbunga kuambata na mvua kubwa, kwa hiyo mafuriko yanaweza kutokea “ anasema Dkt Kijazi.

    Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutua Tanzania tangu mwaka 1952.

    Utabiri ulionyesha kuwa kimbunga hicho kilipiata Ushelisheli Aprili tarehe 22 kikiwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa na kinatazamiwa kutua Tanzania Aprili 24 au 25.

  6. Bobi Wine atakiwa kulipa mamilioni ya fedha ili arudishiwe gali lake la kifahari linaloshikiliwa

    Mamlaka ya mapato nchini Uganda (URA), imemtaka kiongozi wa upinzani na mgombea wa uchaguzi Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, kulipa ushuru ya shilling za Uganda milioni 337 sawa na dola 166,700, ili arudishiwe gari lake la land Cruiser.

    Taarifa ya uamuzi huo kwa kiongozi wachama cha National Unity Platform (NUP) inakamilisha mchakato wa mamlaka ya forodha nchini humowa kutathmini thamani ya gari hilo linalozuia risasi, ambalo awali lililipiwa ushuru mdogo kwa kulinganishwa na gari lingine la kawaida.

    Akijibu juu ya hatua kuthamanishwa upya kwa gari lake kupitia ujumbe wake wa twitter, Bobi Wine amelalamikia hatua hiyo.

    ‘’Baada ya majaribio kadhaadhidi ya maisha yangu, baadhi ya marafiki zangu walinipatia gali linalozuia risasi. Mara ya kwanza mambo yote alikuwa mazuri kwasababu halikwa kwa jina langu. Interpol, Idara ya uchunguzi ya polisi na URA wote walilichunguza na kuliidhinisha . Ushuru unayotozwa na URA tuliilipa. Mambo yalianza kugeuka wakati walipogundua kuwa ni gari langu’’ amesema:

  7. Nigeria yaimarisha usalama kwenye mpaka wake na Chad

    Waziri wa ulinzi wa Nigeria Bashir Magashi amesema kuwa nchi yake imeimarsha usalama kwenye mpaka wake na Chad baada ya kifo cha rais wan chi hiyo.

    Waziri huyo amesema kuwa Nigeria inakabiliana na uasi ndani ya mipaka yake na inatambua tisho la vitisho kutoka nje ambavyo vinaweza kusababishwa na kuingia kwa wakimbizi.

    Ni Wanaigeria wanaoishi Chad tu ambao wataruhusiwa kuingia nchini , Shirika la Habari la Reuters limeripoti.

    Mipaka ya Nigeria na Chad ipo katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa nchi ambako wanamgambo wa Boko Haram wamekuwa wakiendesha mashambulio hivi karibuni.

    Chad inaonekana kama nchi muhimu katika juhudi za Umoja wa Mataifa za kupambana na ukosefu wa usalama Magharibi mwa Afrika

  8. Chad yajiandaa kwa mazishi ya Rais Deby huku viongozi wakiwasili

    Mazishi ya kitaifa ya rais wa Chad Idriss Déby Itno yatafanyika Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo N'Djamena kabla ya kuzikwa katika mkoa wake.

    Aliuawa Jumatatu katika eneo la mapigano dhidi ya wapiganaji wa Front for Change and Concord in Chad (Fact), kikindi cha wanajshi kilichoundwa na maafisa wa kijeshi mwaka 2016.

    Viongozi wa mataifa ya Mali na Guinea wamewasili, na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia anawasili kuelekea mjini N'Djamena licha ya onyo kutoka kwa waasi kwamba kiongozi huyo wa kigeni hapaswi kuhudhuria kwa sababu za kiusalama.

    Baada ya kutolewa kwa heshima za kijeshi na hotuba mbali mbali, sala itafanyika katika msikiti wa Grand Mosque uliopo N'Djamena.

    Baadaye , mwili wa Bw Déby's utasafirishwa kwa ndege hadi Amdjarass, kijiji kidogo kilichopo karibu na mji anakotoka wa Berdoba, uliopo zaidi ya kilomita 1000 (maili 621) kutoka mji mkuu, karibu na mpaka wa Sudan.

    Rais Déby alikuwa mtu muhimu katika mkakati wa usalama katika kanda ya Sahel.

    Baraza la kijeshi linaloongozwa na mwanae, Jeneral Mahamat Idriss lilichukua madara baada ya kifo chake naanaungwa mkono kwa kiasi kidogo na jeshi lakini anauungwa mkono na mtawala wa Ufaransa.

    Generali Déby, 37, amesema jeshi litafanya uchaguzi wa kidemokrasia katika kipindi cha miezi 18 ijayo, lakini viongozi wa upinzani wamelaani hatua yake ya kuchukua mamlaka na kuitaja kama mapinduzi na jenerali wa kijeshi amesema maafisa wengi wanapinga uongozi wake wa mpito.

    Ni mpango ambao pia waasi waliupinga huku pia wakionya kuwa watasitisha kipindi kidogo kilichokuwepo cha usitishaji mpigano.

    Mgawanyiko ndani ya jeshi na upinzani vinamaanisha kuwepo kwa ukosefu mkubwa wa usalama huku kukiwa piwa nma changamoto za kiuchumi wakati Chad inaingia katika kipindi cha mpito .

  9. Hujambo na karibu tena kwa matangazo haya Mubashara ya leo Ijumaa tarahe 23.04.2021