Ndege za kampuni 3 za Kenya zazuiwa kuingia Tanzania

Tanzania imezuwia kampuni tatu za ndege za Kenya kuingia nchini Tanzania kufuatia masharti ya kukabiliana na janga la korona

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja ...Tukutane tena kesho

    Tunakuaga kwa taarifa hii ya kisa cha kusikitisha cha muhifadhi wa wanyamapori aliyeuawa na Simba nchini Afrika Kusini.

  2. Muhifadhi wa wanyamapori afariki baada ya kujeruhiwa na simba wawili

    West Mathewson aliishi na simba hao tangu walipokua wadogo

    Chanzo cha picha, MATHEWSON FAMILY

    Maelezo ya picha, West Mathewson aliishi na simba hao tangu walipokua wadogo

    Muhifadhi wa wanyamapori maarufu nchini Afrika Kusini amefariki baada ya kuraruriwa na simba wawili weupe alipokuwa akitembea nao

    Mke wake West Mathewson, ambaye alimfuata nyumakwa gari, alijaribu kuwazuwia simba hao lakini hakufanikiwa.

    West Mathewson anamiliki hoteli maarufu zenye malazi ya wageni za safari lodge, na Lion Tree Top Lodge, katika jimbo la Limpopo.

    Simba hao wa kike kwa sasa wamehamishiwa katikahoteli nyingine iliyopo kwenye mbugaya wanyama ili baadae waachiliwe na kwenda katika mbuga ya wanyama.

    Simba hao walianza kugomba na ghafla wakamgeukia mpenzi huyo wa wanyamapori anayefahamika kwa jina maarufu "Uncle West", anasema mwandishi wa BBC aliyeko Johannesburg Nomsa Maseko.

  3. Pogba apatikana na virusi vya corona

    Paul Pogba

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amepatikana na virusi vya corona, amesema kocha Mfaransa Didier Deschamps. Fuatilia taarifa hii zaidi katika mtandao wetu

  4. Mamlaka ya mawasiliano Tanzania yazuia kwa muda matangazo ya redio na TV

    Mamlaka ya mawasiliano Tanzania

    Chanzo cha picha, TCRA TANZANIA/TWITTER

    Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA imepiga marufuku matangazo ya redio na televisheni za kampuni ya Clouds, Clauds TV na Clouds FM kwa siku saba.

    Maafisa wa mamlaka hiyo wamesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa kituo hicho kimepigwa marufuku baada ya kutangaza takwimu za matokeo ya uchaguzi ambazo hazikuidhinishwa na Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC).

    Jumatano NEC ilisema kuwa kituo hicho kilitangaza kwamba wagombea fulani wa wamepita bila kupingwa baada ya wapinzani wao kushindwa kufikia vigezo vya uteuzi katika majimbo fulani.

    Mapema mwezi huu TCRA ilipiga marufuku kipindi cha redio (Jahazi) cha kituo hicho kwa madai kwa ukiukaji wa maadili.

    Katika taarifa yake ya Jumatano TCRA iliviasa vyombo vya habari kuzingatia sheria na maadili yao na kuonya kuwa itachukua hatua kali za kisheria kwa chombo chochote kitakachoonekana kwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi nchini humo.

  5. Viongozi wa mapinduzi Mali 'wanataka mamlaka kwa miaka mitatu'

    Wanajeshi walimg'oa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Mapinduzi yaliyoongozwa na jeshi yalimg'oa mamlakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta, mwenye umri wa miaka 75

    Wapatanishi wa Afrika Magharibi wanasema kuwa viongozi wa mapinduzi nchini Mali wanataka kubakia madarakani kwa miaka mitatu ya kipindi cha mpito.

    Lakini ujumbe wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi Ecowas unasema umewaambia viongozi wa mapinduzi kwamba serikali ya mpito, itakayoongozwa na raia au afisa mstaafu wa jeshi inapaswa kudumu kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

    Wapatanishi hao wanaongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan.

    Haijawa wazi iwapo kuwekewa vikwazo na kuwaondolea uanachama kwa muda kutawaathiri vyovyote viongozi wa mapinduziambao awali walisema hawataki madaraka.

  6. Ni nani kati ya hawa atakayekuwa Mkurugenzi mpya wa WTO?

    Maelezo ya video, Watu 8 wameteuliwa kuwania wadhfa wa mkurugenzi mpya wa Shirika la biashara Duniani WTO
  7. Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya njaa na utapiamlo Afrika Mashariki

    Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) limesema kuwa njaa kubwa na utapiamlo vinawakabili mamilioni ya wakimbizi walioko mashariki mwa Afrika mashariki wanaoishi kwa kutegemeamsaada kutoka kwa shirika hilo la chakula.

    Limesema kuwa athari za kijamii na kiuchumi za janga Covid-19 zimepunguza msaada muhimu kutoka kwa wahisani.

    WFP tayari liimepunguza usambazaji wa chakula au utoaji wa pesa kwa kiwango cha hadi 30% kwa zaidi ya wakimbizi milioni 2.7 waliopo katika mataifa ya Ethiopia, Uganda, Kenya, Sudan Kusini, na Djibouti, limesema.

    "Wakimbizi wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na maambukizi ya Covid-19 kwasababu ya kukaa pamoja wakiwa wengi katika kambi, huku wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa maji na usafi duni ," amesema Mkurugenzi wa WFP kanda ya Afrika Mashariki Michael Dunford.

  8. Maduka kuendesha biashara kwa zamu Rwanda ili kudhibiti corona

    Soko la Rwanada

    Chanzo cha picha, UKWEZI

    Maelezo ya picha, Masoko kama hili ni mojawapo ya maeneo ambayo yamepatikana na maambukizi mapya ya corona

    Masoko na majumba makubwa ya biashara katika mji mkuu wa Kigali Rwanda yameagizwa kuendesha biashara kwa kiwango cha 50% huku yakipokezana, kama mojawapo ya hatua mpya za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

    Agizo hilo lililoidhinishwa na kikao cha baraza la mawaziri limekuja kufuatia kupanda zaidi kwa idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya corona kwa siku hivi karibuni.

    Visa vipya vya watu waliopata maambukizi imefikia karibu 1000 katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

    Maduka yatatakuwa kuendesha biashara kwa awamu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Maduka yatatakuwa kuendesha biashara kwa awamu

    Wengi kati ya watu waliopata maambukizi walikuwa ni kutoka kwenye masoko ya mji mkuu Kigali.

    Usafiri wa umma kati ya mji mkuu na mikoa mingine umezuiwa, hukumarufuku ya kutotembea usiku kote nchini ikiendelea kati ya saa moja jioni na saa kumi na moja alfajiri.

    Watu wengi wamekuwa wakipelekwa kukaa usiku kucha kwenye viwanja vya michezo kwa kukiuka marufuku hiyo baada ya saa tatu usiku.

    Hadi sasa Rwanda imerekodi visa 3,625 vya Covid-19 na vifo ni 15.

  9. Pingamizi la Lissu dhidi ya rais Magufuli na professa Lipumba lashindwa kufurukuta

    Mgombea wa urais nchini Tanzania kupitia chama cha upinzani cha CHADEMA Tundu Lissu ameshindwa kuwazuia wapinzani wake katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka huu kuondolewa katika orodha ya watakaogombea wadhfa huo.

  10. Barcelona yapanga kujenga timu nyuma ya Messi

    Lionel Messi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Messi anashikilia nafasi ya kwanza ya Barca ya mchezaji aliyefunga mabao mengi kwa kutikisa wavu mara 634

    Barcelona bado inapanga kujenga timu kwa kumtumia Lionel Messi na wanajaribu kumshawishi aendelee kubakia katika klabu hiyo, anasema Mkurugenzi wa mchezo Ramon Planes.

    Messi mwenye umri wa miaka 33-anayecheza katika safu ya mashambulizi kutoka Argentina aliiambia klabu hiyo kuwa anataka kutekeleza kipengele cha mkataba wake kinachomruhusu kuondoka bila malipo.

    Mshindi huyo wa mara sita wa tuzo ya Ballon d'Or ndiye anayeshikilia nafasi ya kwanza ya Barca ya mchezaji aliyefunga mabao mengi kwa kutikisa wavu mara 634.

    "Kile kilichotokea kimetokea na wazo letu ni kuijenga timu kwa kumtumia mchezaji muhimu duniani ," anasema Planes.

    "Tunataka kujenga msururu mwingine wa ushindi ukiongozwa na mchezaji bora duniani, bora katika historia.

    "Barca na Leo ni kama ndoa, kwani wote wamejitolea sana miongoni mwao, na wameleta furaha sana kwa mashabiki. Ninadhani hali ya baadae ni nzuri. Nina matumaini."

    Messi - anataka kuondoka Barcelona baada ya timu hiyo kushindwa kujipatia taji katika msimu uliomalizika kwa kuchapwa 8-2 na Bayern Munich katika michuano ya robo fainali ya kuwania kombe la Ulaya.

  11. Wanajeshi wa Rwanda na Burundi wakutana kujadili mzozo baina ya nchi zao

    Wanajeshi wa Rwanda na Burundi wakizungumza

    Chanzo cha picha, THENEWTIMES

    Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Burundi (katikati)wakizungumza na manajeshi wa Rwanda (kushoto) pamoja na mwakilishi wa ICGLR (kushoto) katika mpaka wa Nemba

    Katibu wa Jumuiya ya nchi za maziwa (ICGLR) amesema kuwa mkutano wa kwanza unaowashirikisha wakuu wa upelelezi wa majeshi ya Rwanda na Burundi ni mwanzo mzuri na fursa kubwa ya mataifa hayo kutatua mzozo baina yao.

    Ujumbe wa Burundi ukiongozwa na Kanali Ernest Musaba na ule wa Rwanda ukiongozwa na Brigadia Jenerali Vincent Nyakarundi umekutana kwenye mpaka wa nchi hizo mbili katika kikao kinachoongozwa na muwakilishi kutoka ICGLR Leon Mahoungou.

    Katibu Mkuu wa ICGLR Zakary Muburi-Muita ameiambia BBC kuwa mkutano huo unalenga kuwezesha nchi hizo kurejesha uhusiano mwema wa kijeshi na baadae kisiasa.

    "Mnafahamu kuwa nchi hizi mbili zimekuwa na uhusiano mbaya wa kisiasa na kijeshi kwa muda mrefu " Mubur Muita, aliiambia BBC.

    Uhusiano baina ya nchi hizi mbili umekua mbaya tangu mwaka 2015, na mwezi Mei kulikuwa na mapigano baina ya majeshi ya pande mbili karibu na mpaka wa nchi mbili eneo la ziwa Rweru.

    Kila upande umekuwa ukiulaumu mwingine kuwaunga mkono waasi wa mwenzake na kuyumbisha usalama.

  12. Wafuasi wa Laurent Gbagbo wasema atagombea urais

    Laurent Gbagbo alikuwa rais kuanzia mwaka 2000 hadi 2011

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Laurent Gbagbo alikuwa rais kuanzia mwaka 2000 hadi 2011

    Wafuasi wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, wanasema kuwa watawasilisha fomu zake za kugombea uraiskatika uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba hata kama mahakama iliamua kuwa hawezi kugombea kwasababu alipatikana na hatia awali.

    Taifa hilo lilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe bada ya uchaguzi wa mwaka 2010 , wakati Bwana Gbagbo alipokataa kuondoka madarakani na kukabidhi mamkala ya nchi kwa mshindi Alassane Ouattara.

    Mwaka jana aliondolewa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu na mahakama ya kimataifa ya jinai ICCna tangu wakati huo amekuwa akiishi nchini Ubelgiji akisubiri uwezekano wa kesi ya rufaa kuwasilishwa na upande wa waendesha mashitaka.

    Alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kuipora benki ya jimbo wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010. Hahakuwepo mahakama wakati wa hukumu yake.

  13. Kampuni za ndege za Kenya zazuiwa kuingiza ndege zake Tanzania

    Fly540

    Chanzo cha picha, Fly540

    Maelezo ya picha, Fly540 ni moja ya makampuni ya ndege ya Kenya yaliyozuiwa kuingia Tanzania

    Kampuni tatu za ndege za Kenya zimezuiwa kuingia nchini Tanzania kufuatia hatua za kudhibiti janga la korona.

    Mamlaka ya safari za anga ya Tanzania imezizuwia kampuni za AirKenya, Fly540 na Safarilink Aviation zote kutoka Nairobi.

    Ndege za makampuni hayo kwa kawaida huwasafirisha watalii kila siku kuelekea katika Kilimanjaro na Zanzibar.

    Mkurugenzi wa TCAA, Hamza Johari amethibitisha katika mahojiano na gazeti la Citizen nchini humo. Nchi hizi mbili za Afrika Mashariki zipo kwenye mzozo wa kutokukubaliana juu ya namna zinavyokabiliana na janga la virusi vya corona.

    Mwezi huu Kenya ilitoa orodha ya nchi 130 ambazo wasafiri wake hawatawekwa karantini watakapoingia nchini Kenya, Tanzania haikuwemo.

    Kampuni ya ndege ya Kenya -Kenya Airways pia iliwekewa marufuku ya kuingia Tanzania baada serikali ya Kenya mapema mwezi Agosti kuiondoa katika orodha ya nchi 19 zikiwemo za Afrika mashariki, ambazo raia wake hawatalazimika kuwekwa karantini kwa siku 14 watakapoingia nchini humo.

  14. Karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Alhamisi tarehe 27.08.2020