Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Miili 53 yazikwa katika makaburi ya pamoja Morogoro Tanzania
Watu 71 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kulipuka katika eneo la Msamvu mjini Morogogoro, Mashariki mwa Tanzania.
Moja kwa moja
Ajali ya Morogoro: Bendera zote nusu mlingoti Tanzania
Utambulisho wa miili
Miili ikipelekwa makaburini
Watanzania waomboleza
Mazishi ya waathiriwa wa mkasa wa Morogoro wazikwa
Majeneza yakipelekwa katika makaburi ya pamoja
Habari za hivi punde, Majeruhi watatu wa mkasa wa Morogoro waaga dunia
Majeruhi watatu kati ya 46 waliohamishwa katika hospitali ya Muhimbili wafariki.
Walikuwa wamehamishwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu zaidi.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa awatembelea manusura
Baadhi ya matukio ya mikasa ya malori ya mafuta Afrika
- January 31 2009 Kenya: Moto uliwachoma watu waliokuwa wakifyonza mafuta wakati lori la mafuta lilipoanguka huko Molo kaskazini mwa mji wa Nairobi na kuwaoa watu 122.
- Julai 2, 2010, DR Congo: Takriban watu 292 waliuawa wakati lori la mafuta lilipolipuka mashariki mwa kijiji cha Sange. Baadhi ya waathiriwa walikuwa wakijaribu kuiba mafuta baada ya ajali hiyo huku wengine wakitazama mechi ya kombe la dunia.
- Oktoba 6, 2018 DR Congo: Takriban watu 53 waliuawa baada ya lori la mafuta kugongana na gari jingine na kushika moto katika barabara kuu ya mji mkuu wa Kinshasa
- Septemba 16 2015 Sudan Kusini: Watu 203 walifariki na wengine 150 kujeruhiwa wakati watu walipokuwa wakijaribu kuiba mafuta.
- Novemba 17 2016 Msumbiji: Takriban watu 93 waliuawa wakati lori la mafuta lililokuwa likibeba petroli lilipolipuka magharibi mwa taifa hilo . Mamia walikuwa wakijaribu kufyonza mafuta kutoka katika gari hilo.
- Julai 12 2012, Nigeria: Takriban watu 104 walifariki walipokuwa wakijaribu kuchukua mafuta kutoka kwa lori la mafuta baada ya kuanguka kusini mwa jimbo la River State.
- Oktoba 9 2009 , Nigeria: Takriban watu 70 walifariki kusini mashariki mwa jimbo la Anambra baada ya lori la mafuta kulipuka huku moto ikichoma magari kadhaa.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa awajulia hali walionusurika
Majeneza yapangwa katika uwanja wa shule ya Morogoro
Kassim Majaliwa: Wengine wameungua kutoweza kutambulika
Magufuli: Sio wote walikuwa wameenda kupora mafuta
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewataka raia nchini humo kutowahukumu waaathirika wa mkasa wa moto uliosababisha vifo vya watu 69 mjini Morogoro siku ya Jumamosi.
Akizungumza baada ya kuwasili katika hospitali ya kitaifa ya Muhimbili ili kuwajulia hali majeruhi, Magufuli amesema kuwa baadhi ya walioathirika na mkasa huo walikuwa wamekwenda eneo la tukio ili kutoa msaada huku wengine wakiwa wapita njia.
Rais huyo amesema kwamba huu sio muda wa kulaumiana na badala yake akawashukuru baadhi ya Watanzania waliojitolea kuokoa maisha ya watu.
''Naona watu wanasema kwamba hawa wote walienda kuiba , tusiwe majaji wengine walienda kusaidia huku w engine wakiwa wapita njia , Mwengine alikuwa safarini kuelekea Mtwara.
Amesema kwamba serikali yake itauvalia njuga mkasa huo na kuwalipia gharama zote za matibabu waliojeruhiwa.
Amewataka raia wa taifa hilo kuendelea kuwaomboa walioathirika huku akitoa shilingi lakini tano kwa kila majeruhi.
Idadi ya waliojeruhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ni watu 43 huku wengine wakiwa wamejeruhiwa kwa asilimia 80.
Majeruhi waliowasili katika hospitali hiyo ni 46 huku watatu wakifariki. Katika Hospitali ya mkoa ya Morogoro ni majeraha 15 pekee waliosalia .
Hatua hiyo inajiri baada ya Jukwaa la Wahariri nchini Tanzania kusema kwamba vifo hivyo vimetokana na tabia mbaya miongoni mwa watu wanaochukulia ajali kama fursa ya kujipatia mali kwa njia haramu ilioanza katika miaka ya hivi karibuni.
Mwenyekiti wa wahariri nchini humo aliitaka serikali kuwafungulia mashtaka walionusurika mkasa huo akidai kwamba walikuwa na nia ya kupora.
Jinsi magazeti yalivyoripoti Tanzania
Wakaazi waelekea kutambua miili ya wapendwa wao
Wahariri wataka walionusurika ajali ya Morogoro kushtakiwa
Jukwaa la Wahariri nchini Tanzania limeelezea kushtushwa na taarifa za vifo vya Watanzania 69 walioungua moto wakati wakichota mafuta kutoka katika lori lililopata ajali katika eneo la Msamvu , Morogoro siku ya Jumamosi.
Katika taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari siku ya Jumamosi , kulingana na gazeti la mwananchi Tanzania, mwenyekiti wa jukwaa hilo Deodatus Balile amesema kwamba vifo hivyo vimetokana na tabia mbaya miongoni mwa watu wanaochukulia ajali kama fursa ya kujipatia mali kwa njia haramu ilioanza katika miaka ya hivi karibuni.
''Tumeshuhudia picha za watu waliofariki kwa kuungua moto zikirushwa kwenye mitandao ya kijamii kinyume cha maadili na taaluma ya uandishi wa habari, tunakemea tabia hii na kuitaka jamii iache mara moja tabia hii ya kinyama isio na utu'', alisema Balile.
Vilevile mwenyekiti huyo alizungumzia kuhusu watu 70 waliojeruhiwa akisema kwamba watakapopona wanafaa kujiepusha na tabia hiyo ya uporaji.
Ikilazimu watu watakaopona katika ajali hii wanafaa kushtakiwa kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwao na wengine kuwa ikitokea ajali tunapaswa kusaidia majeruhi na kuokoa mali zao badala ya kupora'', alisema.
''Tunaomba viongozi wa dini , wazazi, viongozi wa kisiasa na jamii kutumia ajali hii kufundisha watoto na vijana maadili mema ya kuwa watu wa msaada mtu anapopata ajali kusaidia majeruhi na kuokoa mali za waliopata ajali badala ya kuwapora'', aliongezea.
Miili ya waathiriwa wa ajali ya Morogoro yawasili
Waziri mkuu wa Tanzania ajiunga na waombolezaji Tanzania
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaaliwa na viongozi wengine na wakazi wa mji wa Morogoro wamejitokeza asubuhi hii katka viwanja Shule ya Sekondari ya Morogoro kwa ajili ya kuaga baadhi ya miili ya waliopoteza maisha katika ajali ya moto ya lori la mafuta iliyotokea jana mkoani humo.
Habari za hivi punde, Magufuli atoa siku tatu za maombolezo Tanzania
Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza siku tatu za maombolezo ya Kitaifa kuanzia leo Jumamosi kufuatia vifo vya zaidi ya watu 60 vilivyosababishwa na ajali ya kuungua kwa moto.
Marehemu walikuwa wakichota mafuta yaliomwagika baada ya lori la mafuta kupinduka mjini Morogoro.
Takriban watu 70 waliojeruhiwa kufuatia kisa hicho wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya mkoa ya Morogoro na ile ya kitaifa ya Muhimbili iliopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waliofariki wanatarajiwa kuzikwa leso siku ya Jumapili. Katika kipindi chote cha maombolezo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.