Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jeshi lachukuwa uongozi wa nchi Sudan
Maandamano ya kumpinga Bashir yalianza mwezi Disemba 2018
Moja kwa moja
Omar al-Bashir ni mmojawapo wa viongozi waliohudumu kwa muda mrefu duniani
Je Omar al-Bashir yuko wapi?
Mapema Luteni jenerali Auf alitangaza kwamba rais wa Sudan Omar al bashir atakamatwa na kupelekwa katika eneo salama.
Lakini hatujui kulew aliko kwa sasa.
Mara ya mwisho, chombo cha habari cha serikali kiliripoti akihudhuria fafla ya kiserikali nchini humo. Ilikuwa siku ya Jumatatu , kulingana na BBC Moses Rono wa BBC Monitoring.
Kule aliko ni swala ambalo limejaa uvumi mwingi. Siku ya Jumatatu shirika la habari la Suna liliripotoi kwamba yupo afisini mwake.
Je ni nani aliyesoma taarifa ya kuondolewa madarakani?
Taarifa iliotangaza kung'atuliwa madarakani kwa rais Omar al Bashir ilisomwa na naibu wake na waziri wa ulinzi Awad Mohamad Ahmed ibn Auf.
Luteni jenerali Auf mwenye umri wa miaka 65, ni mwanajeshi wa siku nyingi ambaye awali aliwahi kuhudumu kama mwenyekiti mkuu wa wafanyikazi wa umma.
Wakati wa uongozi wake kama waziri wa ulinzi, jeshi la Sudan liliimarisha mfumo wake wa zana za kijeshi. Awali alikuwa amehudumu kama kiongozi wa idara ya ujasusi wa jeshi.
Uzoefu wake wa kijeshi kidiplomasia na ule wa kisiasa unamuweka katika hali nzuri ya kumrithi Bashir ama hata kushawishi urithi wake.
Ni miongoni mwa watu waliowekewa vikwazo na Marekani kuhusu mzozo wa Darfur.
Marekani imemshutumu kwa kuwa kiunganishi cha serikali ya Sudan na wapiganaji wa Janjaweed wanaoungwa mkono na serikali.
Ripoti ya Umoja wa mataifa ilimuorodhesha luteni jenerali ibn Auf katika orodha ya wale waliohusika kwa hali mbaya ya Darfur. Kutokana na hilo Marekani imefungia mali yake tangu mwezi Mei 2007
Ujumbe haikuafikia matakwa ya raia
Waandamanaji hawatatoshekwa na tangazo la jeshi kulingana na mwandishi Reem Abbas mjini Khartoum aliezungumnza na BBC.
Alisema kuwa waziri wa ulinzi hakutaja serikali ya mpito ya raia badala yake ameongea kuhusu baraza la mpito.
''Ujumbe huo haukuwafurahisha raia'', alisema.
Na anadhania kwamba waandamanaji watasalia barabarani.
Wachanganuzi wa Sudan wapinga taarifa ya jeshi
Taarifa ya waziri wa ulinzi Ibn Auf imepokelewa na hisia tofauti miongoni mwa baadhi ya wachanganuzi wa kisiasa nchini humo ambao mara kwa mara huwa katika mtandao wa Twitter.
Wanadai kwamba taarifa hiyo haikuafikia matakwa ya waandamanaji kwa kuwa uongozi huo wa jeshi unamuondoa kiongozi wake Omar Bashir huku ukilidhibiti taifa hilo.
Jinsi kuondelewa kwa Omar al Bashir kulivyojadiliwa mitandaoni
Hali ya tahadhari yatangazwa Sudan
Habari za hivi punde, Mambo muhimu yaliotangazwa na jeshi Sudan
Mambo makuu katika taarifa ya jeshi iliyotangazwa kwenye televisheni muda mfupi uliopita:
- Rais Omar al-Bashir atakamatwa na atapelekwa mahala salama.
- Miezi mitatu ya hali ya dharura imetangazwa nchini.
- Jeshi litasimamia kipindi cha miaka miwili cha serikali ya mpito.
- Baraza lampito litaidhinihswa kusimamia kipindi cha mpito, taarifa kuhusu majukumu ya baraza itatolewa baadaye.
- Katiba ya mwaka 2005 itafutiliwa mbali.
- Zaidi ya hayo waziri wa ulinzi Awad Mohamed Ahmed Ibn Auf amesisitiza kwamba haki za binaadamu zitaheshimiwa na kutoa wito kwa raia wote wavumilie hatua za kiusalama zitakazoidhinishwa.
Habari za hivi punde, Waziri wa ulinzi atangaza Bashir ameondolewa madarakani
Waziri wa ulinzi Sudan ametangaza katika televisheni kwamba rais Omar al Bashir ameondolewa madarakani na anazuiliwa mahali salama.
Ametangaza serikali ya mpito ya miaka miwili. kadhalika ameeleza kuwa mipaka yote imefungwa na ofisi ya waziri mkuu, bunge na usalama wa kitaifa zote zimevunjiliwa mbali.
Biashara zasimama Khartoum
Rashid Mohammed raia wa Kenya ambaye ni mwanafunzi nchini Sudan tangu 2013 ameileza BBC Swahili kwamba tangu asubuhi barabara za mji wa Khartoum zimejaa raia wanaoelekea katika makao makuu ya kijeshi.
Hali Sudan yajadiliwa katika mitandao ya kijamii
Baadhi kama huyu wakitathmini uwezekano wa Bashir kuondoka madarakani na maana yake katika utawala wa baadhi ya viongozi Afrika ambao wamelazimika kuondoka madarakani kupitia ima ni kupitia maandamano, hatua ya kijeshi, umri mkubwa au kutokana na kuugua.
Omar al-Bashir ni nani?, Utawala wa miaka 30 wa Omar al-Bashir Sudan
Utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir umegubikwa na mapigano.
Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na ameiongoza taifa hilo kubwa zaidi Afrika kwa mkono wa chuma hadi mwaka 2011.
Alipochukua madaraka, Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini.
Tuhuma dhidi ya Omar al-Bashir
Mauaji ya kimbari
- Kuwaua watu wa jamii ya Fur, Masalit na Zaghawa
- Kuwasababishia mafadhaiko makubwa ya kimwili na kiakili
- Kuwaweka katika hali ngumu kwa kuwaharibia makaazi yao
Uhalifu dhidi ya binadamu
- Mauaji
- Kumpoteza mtu
- Kuwahamisha watu kwa nguvu
- Ubakaji
- Mateso
Uhalifu wa kivita
- Kushambulia raia katika jimbo la Darfur
- Kuiba mali katika miji na vijiji
Kwa taarifa zaidi: Soma hapa
Kwa picha: Waandamanaji na Wanajeshi Khartoum
Uhusiano kati ya waandamanaji na jeshi huenda ukabaini hatma ya maandamano ya dhidi ya rais Omar al-Bashir.
Picha hizi kutoka mitaa ya mji mkuu wa Khartoum yanatoa taswira kuhusu uhusiano huo.
Hapa, wanajeshi na waandamanji wanaonekana wakiwa karibu wakiwa nje ya makao rasmi. Na hakuna hisia ya uhasama baina yao.
Jeshi bado li kimya Sudan,
Hakujukuwa na kauli yoyote mpaka sasa kutoka kwa jeshi nchini Sudan
Shirika la habari la Reuters kwa kutotaja duru, limeripoti kwamba rais Omar al-Bashir amejiuzulu na mashauriano yanaendelea kuunda baraza la mpito.
Tangu asubuhi jeshi limetarajiwa kutoa tangazo muhimu wakati maandamano yakirindima kwa siku ya sita mtawalia kumshinikiza rais Omar al Bashir ajiuzulu.
Umati mkubwa wa watu umekusanyika nje ya makao makuu ya jeshi katika mji mkuu Khartoum na waandamanaji wameapa kuondoka tu iwapo rais atajiuzulu.
Nyimbo za uzalendo zimekuwa zikichezwa katika redio ya taifa na uwanja mkuu wa kimataifa umefungwa sasa.
Shinikizo limeongezeka kutaka mageuzi ya kisiasa nchini .
Watu wamekuwa wakishereheka katika mji mkuu Khartoum na wito umetolewa kwa raia zaidi kujiunga katika maandamano hayo nje ya makao makuu hayo ya jeshi.
Waandamanaji Khartoum 'waimba utawala umeanguka'
Picha kutoka eneo kuu la maandamano
Benjamin Strick, ni mwandishi wa BBC Africa Eye, amekuwa akitumia teknolojia kutambua uhalisi wa matukio katika maeneo katika kuthibitisha au kuhakiki picha zinazosemekana kutoka kwa waandamanaji Sudan.
Video hizi zinatoa taswira ya ukubwa wa hisia miongoni mwa waliokusanyika.
Wasubiri kwa hamu kubwa Sudan huku uvumi ukienea
Raia nchini Sudan wanasubiri kwa hamu kile ambacho vyombo vya hanari vya kitaifa vinaeleza kuwa ni tangazo muhimu kutoka kwa jeshi.
Kumeshuhudiwa maandamano ya miezi kadhaa ya umma ya kumshinikiza rais al-Bashir ajiuzulu.
Uvumi umeenea kwamba huenda Omar al Bashir akajiuzulu, lakini hakujakuwa na taarifa rasmi mpaka sasa.
Huku maelfu ya waandamanaji wakikusanyika katika mji mkuu Khartoum, magari ya jeshi yanaripotiwa kuzifunga barabara kuu na matangazo ya redio yamekatizwa badala yake kumewekwa nyimbo za uzalendo.
Waandalizi wa maandamano wametoa wito kwa raia wasalie mitaani; wandishi habari wanasema wengi wataridhika tu iwapo serikali nzima ya Sudan itaondolewa, na sio rais tu.
Shauku ya mapinduzi ya kijeshi yatanda Sudan
Jeshi la Sudan limetangaza kuwa litatoa taarifa muhimu hivi karibuni, hali inayohisiwa kuwa utawala wa Rais Omar al-Bashir huenda ukafikia kikomo hivi karibuni.
Wanajeshi wametanda katika makazi rasmi ya rais mapema asubuhi ya leo, shirika la Habari la kimataifa la AFP linaripoti.
Jeshi pia limezingira njia zote muhimu za kuingia na kutoka mji mkuu wa Khartoum.
Zaidi: Soma Hapa
Jeshi: Muelekazaji mkuu katika historia ya Sudan, Ahmed Mohamed Abdi BBC Monitoring
Jeshi la Sudan limekuwa na jukumu kuu katika siasa za nchi hiyo tangu lilipojinyakulia uhuru mnamo 1956. Jeshi limeshutumiwa kwa kutumia vibaya malalamiko yanayowasilishwa kujipatia madaraka na alafu kuidhinisha utawala wa kukandamiza unoishia kugeuka matakwa ya raia.
Mnamo 1958, miaka miwili baada ya uhuru, mkuu wa majeshi Meja Jenerali Ibrahim Abboud alichukua uongozi katika mapinduzi ambayo hayakukumbwa na umwagikaji damu. Vuguvugu lililokuwa maarufu lilishinikiza jeshi kuachia madaraka mnamo 1964.
Jeshi baadaye lilirudi uongozini katika mapinduzi mengine mnamo 1969 yalioongozwa na Kanali Jaafar el-Nimeiri. Nimeiri mwenyewe aliidhinisha majaribio kadhaa ya mapinduzi na vuguvugu dhidi ya utawala.
Mnamo 1985, Luteni - Jenerali Abdel Rahman Swar al-Dhahab aliongoza kundi la maafisa wa jeshi katika kumpindua el-Nimeiri.
Mwaka mmoja baadaye, al-Dhahab alikabidhi madaraka kwa serikali iliyochaguliwa, ya waziri mkuu al-Sadiq al-Mahdi.
Lakini miaka mitatu baadaye, mnamo 1989, maafisa wa kijeshi wenye itikadi kali za dini ya kiislamu walioongozwa na Brigedia Omar al-Bashir waliupindua utawala ambao haukuwa imara wa Al-Mahdi.
Miaka 30 baadaye hii leo, Bashir amesalia uongozini, akiwa amekabiliwa na changamoto si haba katika utawala wake.